Elections 2015 Magufuli anaweza akawa Deng Xiaoping wa Tanzania ya leo?

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
AGOSTI 22, mwaka 1904, katika kijiji cha Xiexing Guang'an Jimbo la Sichuani nchini China, katika ukoo wa Hakka Han, mke wa pili kati ya wake wanne wa mzee Deng Wenming, siku hiyo alibarikiwa kujifungua mtoto wa kiume ambaye baadaye alimpatia jina la Deng Xiaoping.

Deng Xiaoping huyu anatajwa kama shujaa muhimu sana katika mashujaa waliochangia maendeleo ya China tunayoiona leo kama taifa lenye nguvu duniani.

Mwishoni mwa miaka ya 1970 China ilikuwa imeanza kuyumba kabisa katika masuala ya uchumi. Nyanja nyingi za uchumi kama vile kilimo, viwanda, elimu na nyinginezo zilikuwa zimekwama, ilikuwa katika hali mbaya ambayo haikuwahi kutokea tangu Mapinduzi ya Mao. Wao walikuwa wameng'ang'ania ukomunisti tu, hawakutaka kusikia chochote kile chenye chembechembe za ubepari hata kama kitu hicho kingewasaidia, hawakutaka kutega sikio lolote juu ya jambo ambalo sio la kiongozi Komredi Mao.

Sera za Mao kama ile ya "Great Leap Forward" ya mwaka 1958 iliyokuwa inalenga mapinduzi ya kilimo na viwanda zilikuwa zimeshindwa kabisa, Mao alikuwa tayari kutofautiana hadharani na afisa wake yeyote yule ambaye angeonekana kwa namna moja ama nyingine kuonyesha chembechembe za mapenzi na sera yoyote ya ubepari na mbaya zaidi alikuwa yuko juu ya chama!

Ni kipindi ambacho nchi hiyo ilikuwa na uhasama mkubwa sana na nchi za jirani, ndicho kipindi ambacho Umoja wa nchi za Soviet (USSR) na China walikuwa katika mgogoro mkubwa, mgogoro uliojulikana kama ‘The Sao – Soviet Split". China ilikuwa hovyo sana katika sera za mambo ya nje hasa hasa mataifa ya magharibi yaliyokuwa vinara wa sera za ubepari. China ilikuwa imekwama, imesimama, imedumaa na haijui nini cha kufanya katika teknolojia, elimu, kilimo, viwanda na ulinzi.

Baada ya kifo cha mwasisi au Baba wa Taifa wa nchi hiyo Mao Zedong mwaka 1976, miaka miwili baadaye, 1978 kada wa siku nyingi wa CCP Komredi Deng Xiaoping alikabidhiwa rasmi mikoba ya kukiongoza chama cha CCP pamoja na Serikali ya Watu wa China.

Xiaoping alikuwa adui na rafiki wa Mao kwa sababu kuna kipindi walikijenga chama na nchi pamoja, na kuna kipindi walitofautiana na kuonana maadui hasa baada ya kauli tata ya Deng Xiaoping mwaka 1961 pale aliposema "haijalishi paka ni mweupe au mweusi kikubwa ni kukamata panya tu", kauli hiyo ilichukuliwa au kutafsiriwa vibaya na Mao kwani alijua fika kuwa Deng alimaanisha sera za kibepari kuwa haijalishi ni za namna gani, lakini kikubwa ni maendeleo.

Baada ya kupewa madaraka Deng Xiaoping aliamua kuanza na kitu alichokuwa akikiamini na kukitamani kwa siku nyingi sana cha kuibadilisha China na kuwa na uchumi wa kisasa unaoendana na dunia ya kisasa, alikuwa na nia ya kuifanya

China ishindane kiuchumi na nchi za magharibi jambo ambalo lilikuwa tamanio lake la muda mrefu. Deng alianza na sera aliyoiita usasa wa mambo manne, yaani "Four Modernizations" sera iliyolenga kuboresha mambo manne ambavyo ni kilimo, viwanda, ulinzi pamoja na sayansi na teknolojia.

Ni sera hiyo ya "Four Modernizations" iliyomfanya Deng mwaka 1978 kuanzisha sera kama ya "Reform and Opennes" ambayo ilijikita katika maendeleo na ujamaa wa kisasa, juhudi za Deng katika kusimamia sera zake zilipeleka mapinduzi makubwa sana ya uchumi wa kisasa kwa taifa hilo ambalo lilikuwa linaelekea kushindwa kwa sera zake za ujamaa wa kizamani. Deng hakuona shida kuiga mataifa ya magharibi, hakuona shida kuiga adui zake na hakuona shida kuiga kitu chochote kilichokuwa kinaonekana kina tija katika ustawi wa taifa la China.

Ingawa yeye alisoma na kufanya kazi Ufaransa lakini ilikuwa ni nadra sana kwa Wachina kusoma nchi za kibepari katika kipindi cha Mao, lakini katika kipindi chake Deng alianzisha programu maalumu ya kupeleka Wachina kusoma nje ya nchi hasa hasa Ulaya ili waweze kupata ujuzi na teknolojia ya kisasa kabisa, alianzisha mifumo ya kusaidia kuuza bidhaa nje ya nchi, ni katika kipindi chake ambapo "special economic zones" kama ya Shenzhen ilitengenezwa, alianza kushughulikia uhusiano na mataifa jirani, na ni katika kipindi chake ambapo ustawi wa uhusiano na Urusi ulianza rasmi.

Deng aliyafanya yote hayo katika msingi wa kwanza kabisa aliouweka wa kutofautisha chama na serikali, alihakikisha hakuna mtu atakayekuwa juu zaidi ya chama kama alivyokuwa Mao Zedong, aliweka maslahi ya nchi kwanza kabla ya chama, na maslahi ya nchi yalikuwa yanajaliwa sana, alitaka China ishindane kiuchumi, kiteknolojia, na nchi za magharibi kweli kweli na pamoja na yote alihakikisha kamwe nchi yake haiachi au kusahau misingi ya ukomunisti na hakika alimaanisha kile alichokisema.

Deng aliisoma vizuri Serikali ya China na akaelewa kabisa kuwa mifumo yote imeshindwa na inaelekea kufa. Na huo ukawa mwanzo wa taifa la China kuanza kuwa na nguvu ya kiuchumi duniani na kuwa China hii tunayoiona na kuitamani mpaka leo.

Nimeamua kuanzia mbali kidogo na historia ya Deng Xiaoping na mapinduzi ya uchumi wa China kwa sababu moja kubwa, kwa sasa taifa letu limekwama, limedumaa na linayumba katika nyanja nyingi sana. Mifumo (system) yote ya taifa letu imekwama kama China iliyokuwa chini ya Mao.

Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, mwaka ambao tunaliweka taifa katika uongozi mpya wa miaka mitano ijayo, tutachagua madiwani, wabunge na rais atakayempokea Jakaya Kikwete anayemaliza kipindi chake cha miaka kumi.

Katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu mambo matatu huweza kutokea, si hapa Tanzania tu lakini katika chaguzi kuu nyingi duniani mambo hayo huweza kutokea, kuna baadhi ya nchi nyingi tu yametokea na yanaendela kutokea.

Jambo la kwanza ni madhara yatakayotokana na Uchaguzi Mkuu. Hili ndilo la kuliangalia kwa ukaribu kabisa katika nchi yetu, madhara hayo huwa pamoja na watu kugawanyika, vita na jamii kupoteza amani. Zipo nchi nyingi sana ambazo zimeingia vitani baada ya Uchaguzi Mkuu, mfano wa jirani zetu Kenya walivyoingia kwenye machafuko mwaka 2007 baada ya Uchaguzi Mkuu, kutokana na tume ya uchaguzi iliyokuwa chini ya Jaji Samwel Kivuitu kumtangaza Mwai Kibaki kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi ule. Kutangazwa kwa matokeo hayo kuliliacha taifa la Kenya katika machafuko makubwa, ikikadiriwa watu zaidi ya 1,000 walipoteza maisha.

Ivory Coast mwaka 2010 Rais wa wakati huo, Profesa Laurent Gbagbo, aligoma kumwachia madaraka mshindi halali Alassane Ouattara, hali iliyosababisha nchi hiyo kuwa katika machafuko na raia wasio na hatia wakamwaga damu. Inakadiriwa watu zaidi ya 3,000 walipoteza maisha.

Jambo la pili kwenye Uchaguzi Mkuu ni kwamba kutakuwapo na wale walioshindwa, ambao watabaki na huzuni, maumivu na pengine hasira zitakazotokana na kupotea kwa rasilimali zao. Hawa mara nyingi ndio huwa wanasababisha hilo la kwanza nililolitaja hapo juu kwa kutokubali matokeo.

Wao inawapasa kukubali matokeo kwa maslahi ya taifa letu na kujipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi unaofuatia yaani baada ya miaka mitano ambayo itakuwa mwaka 2020.

Jambo la mwisho katika Uchaguzi Mkuu ambalo limenifanya nimkumbuke Deng Xiaoping ni kwamba kutakuwepo na wale walioshinda, hawa ni wale waliopewa ridhaa ya wananchi kuliongoza taifa la Tanzania kwa muda wa miaka mitano, hawa ni wale waliopakwa mafuta na wananchi kwa ajili ya kulipitisha taifa katika safari nyingine ya miaka mitano, na serikali itakuwa inatekeleza kwa umakini ilani yao ya uchaguzi ambayo ndiyo itakuwa dira mpya ya maendeleo ya taifa letu katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Rais atakayekuwa amechaguliwa anapaswa kusimamia kwa umakini mkubwa mambo muhimu ya taifa letu huku akiweka misingi ya utaifa mbele pamoja na vipaumbele vya Watanzania. Tunamhitaji Deng Xiaoping wa Tanzania, ambaye atakuwa tayari kutuletea vipaumbele vitakavyolisaidia taifa kuondoka katika mdororo mkubwa wa uchumi na kuwa katika ustawi wa hali ya juu.

Ni lazima awe mtu wa kuchukia rushwa, rushwa ndio adui mkubwa wa Tanzania. Siku zote watu wanaimba ufisadi, wanataja mafisadi, wanaonyesha mafisadi lakini kutokana na rushwa hakuna chochote kinachofanyika, rushwa huleta vifo, rushwa huongeza yatima, rushwa huleta umasikini, rushwa huleta machafuko, rushwa huwapokonya wanyonge haki zao, na rushwa huleta kila aina ya uovu katika jamii. Watanzania tunazidi kuchanganyikiwa na hali halisi ya mambo yanavyoendelea katika nchi yetu.

Zamani tulikuwa tunalia na rushwa ya wagombea wa vyama tofauti katika Uchaguzi Mkuu lakini leo tunalia na rushwa katika kura za maoni ndani ya vyama, Chadema Jimbo la Segerea wanalia na rushwa katika uchaguzi wa kumpata mgombea wao wa ubunge, CCM Iramba Magharibi wanalia na rushwa hata kabla ya kura kupigwa, kote ni kilio, waliokuwa wanalia na CCM sasa wanalia na vyama vyao, kila sehemu ni rushwa rushwa rushwa, imekuwa ni wimbo sasa.

Siwezi kuitupia lawama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) maana hata wao pia wanazidiwa kama watu wengine wanavyozidiwa na kazi zao, watamkamata nani na wamuache nani. Tanzania ya leo tuna kila aina ya rasilimali na kila siku rasilimali zetu zinaongezeka, zamani hatukuwa na gesi leo tuna gesi kesho tutakuwa na nyingine nyingi, ila rasilimali haziwezi kutumika ipasavyo, Watanzania hawawezi kujivunia rasilimali hizo kwa sababu haziendani na kasi ya umasikini.

Taifa letu sasa limepasuka katika vipande vipande hata asiye na akili na mwenye akili anaona, taifa lina wenye nacho na wasio nacho, taifa letu limegawanyika katika vipande vya udini, hilo liko wazi kabisa, tunamshukuru Mungu hatujagawanyika katika vipande vya ukabila lakini taifa letu limegawanyika katika vipande vya ukanda, wapo wa ukanda wa kaskazini, kanda ya kati, kanda ya kusini, na wengine wa kanda ya ziwa.

Hili si jambo la kuficha, tena liko wazi kabisa, Watanzania wameanza kugawanyika katika kanda zao, anayeonekana fisadi kwa Kanda ya Kaskazini anaonekana msafi kwa Kanda ya Kati, Kusini au Kanda ya Ziwa, na anayeonekana msafi kwa Kanda ya Ziwa anaonekana fisadi kwa Kanda ya Kati, Kusini au Kaskazini, tunabaguana kwa ukanda. Hili sio jambo la kufumbia macho wala kulificha ni jambo ambalo lipo wazi kabisa.

Zamani tuliimba shuleni na kuelewa kuwa kilimo ni uti wa mgongo lakini leo hii hatujui ni kitu gani ambacho ni uti wa mgongo, hatujui kama viongozi wetu bado wanaamini kwenye kilimo na kama wanaamini, hatuoni juhudi zinazoendana na ukweli kwamba kilimo ni uti wa mgongo. Kama isingekuwa juhudi za wakulima wadogo wadogo vijijini nchi yetu ingekwa katika janga la njaa kubwa sana. Hakuna juhudi zinazofanywa na serikali katika kilimo, nchi yenye eneo kubwa na zuri lenye rutuba kama yetu ilipaswa tuone mapinduzi makubwa sana ya kilimo.

Niliwahi kusafiri na rafiki yangu Mkenya maeneo mbalimbali ya Tanzania aliishia kucheka tu kwa utajiri wa ardhi tuliyonayo lakini hakubahatika kuona shamba kubwa na la kisasa zaidi ya kuona vijishamba vya wakulima wadogo, tena ni kwa juhudi tu za wakulima wenyewe. Je, viko wapi viwanda? Hakuna kitu kinachogawa ajira duniani kama kilimo na viwanda, kilimo na viwanda huenda sambamba, kilimo kikiimarishwa basi viwanda hustawi kwa kupata malighafi, lakini tujiulize kuna viwanda vingapi nchi hii? Je, vinafanya kazi kama inavyotakiwa? Na kama havifanyi kazi inavyotakiwa, ni kwa nini? Jibu lake hatulijui maana hata vipaumbele vyetu bado hatuvijui.

Tanzania yangu ya leo hatujui tuko kwenye ujamaa au ubepari, katiba yetu ya mwaka 1977 inatamka kuwa nchi hii ni ya ujamaa lakini, je, ni kweli Tanzania ni nchi ya kijamaa? Hata viongozi walioapa kwa katiba hiyo inayotamka hii ni nchi ya kijamaa bado ukiwauliza hilo swali sidhani kama watakujibu zaidi ya kigugumizi na kama watajibu kuwa ni nchi ya kijamaa basi hawajui maana ya neno ujamaa. Ukiwauliza je ni nchi ya kibepari bado hawatakujibu kama ni ya kibepari ingawa kwa ushahidi wa mambo yanayotendeka na tunavyoyaona Tanzania iko karibu sana na ubepari kuliko ujamaa.

Tanzania yangu leo maadili hakuna kabisa, neno maadili ni msamiati kwa Mtanzania wa leo, si kwa vijana tu mpaka wazee, sio kwa viongozi wa kisiasa bali mpaka kwa baadhi ya viongozi wa dini, zamani tulizoea viongozi wa kisiasa wakirushiana matusi, hatukuona ajabu sana kwa sababu tunajua siasa ni mchezo mchafu na kila anayecheza huwa amejiandaa kuchafuka lakini sasa Tanzania hii Askofu anamtukana Askofu mwenzake huku waumini ambao ni Watanzania wakishangilia, Mchungaji anamtukana Mchungaji, tena Kanisani! Mpaka sasa hatujui ni nani wa kumkanya mwenzake.

Vijana mpaka wazee hawachagui nguo za kuvaa, nguo ya usiku wanaivaa mchana, ya chumbani wanaivaa hadharani, ni vurugu katika jamii. Tumekwama Watanzania, tunaelekea kupotea kabisa, tamaduni zetu zimeingiliwa na kile wanachokiita usasa au utandawazi (ila sidhani kama ndo huu utandawazi ambao mzee Mkapa aliumanisha).

Tulipofika, sasa Watanzania tunahitaji mtu, tunahitaji rais wa kutatua matatizo ya Watanzania, tunamhitaji rais mtendaji na sio mtendewaji, tunamhitaji atakayeleta mapinduzi katika mifumo na sera zilizoshindwa au zilizozorota. Tunahitaji maendeleo katika kilimo, viwanda, elimu na twende sambamba na dunia ya leo. Tunahitaji rais ambaye atasimamia kile anachokisema jukwaani asiye mbabaishaji katika matatizo yetu, na mwenye dhamira thabiti.

Tunamhita Deng Xiaoping atakayeamsha mifumo iliyolala, atakayefufua vilivyokufa, mchambuzi nguli wa masuala ya kisiasa na kijamii wa gazeti hili la Raia Mwema, Joseph Mihangwa anasema; "John Pombe Magufuli kula pombe na bangi uokoe taifa" na mimi nasema anywe na avute tu maana hamna namna nyingine, awe kichaa, dikteta mzalendo, awe mtu wa kufukuza, asiyeombeka misamaha ya makosa ya uzembe na akamate na kufilisi mafisadi. Mungu atusaidie taifa letu livuke katika hali hii tuliyonayo na tumpate Deng Xiaoping atutengenezee Tanzania ya miaka 100 ijayo.

Mungu ibariki Tanzania

Raia Mwema
 
Ndoto za mchana hizo! Kama vile unaota UNAFUKUZWA NA NGURUWE!!! Hivi anapo sema atafuata nyayo za watangulizi wake, ana maana gani?

Si tumemsikia Mkulu akisema, "ALIANZA NA MGAWO WA UMEME NA SASA ANAMALIZA NA MGAWO WA UMEME"? Hivi miaka 10 ya uongozi ana jivunia nini?

Barabara zote zimekuwa kama BULLISH kwa kubonyea. Wakati wenzetu wakiweka angalau malengo ya kujenga kilometa 50 za reli ya kisasa kwa mwaka, sisi tunatambia kuongeza mgawo wa jezi za kijani na manjano kila baada ya miaka 5. SHAME!!
 
Hakika nimefurahi sana kwa makala hii, naamini Magufuri wetu ni next Den X
 
Hakika nimefurahi sana kwa makala hii, naamini Magufuri wetu ni next Deng X
 
Hata kama usingeposti hizo mara mbilimbili tungekuelewa tu! Safi sana kwa kupenda makala ambayo maudhui yake ni kuwa Magufuli atakuwa Deng xiaoping wa tanzania, lakini kiuhalisia HAIWEZEKANI. Hayo mambo yaliwezekana China kwa sababu Mao aliweka misingi ya kutii mamlaka hataka kama inakosea, hapa demokrasia imetamalaki na hatutarudi nyuma tena!
 
Deng' watannnzania bado hajazaliwa. Umenikimbusha mwalimu wangu wa China foreign trade..daah! Prof. Wang.
 
Wewe uliyeomba hili ulijibiwa vema. Paragraph ya mwisho imetisha sana.
 
Back
Top Bottom