Muwindaji
JF-Expert Member
- Feb 28, 2015
- 245
- 206
Mfumo ni muunganiko wa muundo, njia zilizowekwa na watu(au sheria) katika kutatua shughuli flani, kufanya kazi fulani na kuhakikisha jambo fulani linafanyika kama linavyotakiwa lifanyike.
Mfumo unabeba watendaji, wasimamizi na viongozi ambao kazi yao inakua ni kuhakikisha mambo yanakwenda sawa kama yalivyowekwa.
Mfumo unaweza ukawa halali au sio halali.
Kitendo cha watendaji fulani, kutengeneza mfumo wa kujinufaisha wao kinaweza kuhesabika kwamba watendaji hao wametengeneza mfumo usio wa halali.
Kipindi cha kampeni, kundi fulani la upinzani(UKAWA) walisikika wakisema kua, hata aingie nani hatoweza kuleta mabadiliko kwasababu hatoweza kubadilisha mfumo uliokuwepo(Mfumo usio wa halali).
Inakua ngumu kukataa kwamba kuna udhaifu mwingine wa kimfumo unasababishwa na kuwepo kwa sheria zenye utata, yaani zinazoshindwa kutibu matatizo yaliyopo sasa, na hata Katiba ya sasa ni chanzo cha baadhi ya mfumo mbovu mfano: kama pale waziri anapoteuliwa kutoka kwenye ubunge na hii inaharibu mfumo mzima wa kazi ya bunge kuisimamia serikali ipasavyo, ni mfano.
Wapinzani walijisahau kwamba mfumo ambao wanauona hauwezi kutoa raisi mzuri kwa asilimia kubwa ni mifumo isiyo ya halali, na inaweza kutibika barabara.
Na hivyo wakawaaminisha watanzania kwamba, hata Magufuli akiingia hatofanya lolote kwasababu ya mfumo uliokuwepo umeoza. Na wakasahau kwamba mfumo unajieleza vizuri, isipokua mfumo ulikosa msimamizi mzuri wa kuufanya ulete tija kwa wananchi.
Magufuli endelea kufanya kazi, endelea kutoa tiba kwa mfumo uliokuwepo na kukata mifumo yote haramu iliyotengenezwa ndani ya mifumo halali.
Tatizo lilikua ni mtu, na sio mfumo.