Magufuli anaonyesha dalili ya kiongozi mzuri zaidi kutokea Tanzania

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
KUNA baadhi ya watu kati yetu ambao wanaonesha shaka juu ya uwezo na mvuto wa Rais John Magufuli nchini. Ndugu zetu hawa –wengine wasomi (elite) – ambao wanaangalia kwa mwanga elimu na kuamua kulalamika kuwa yumkini Magufuli ni kiongozi mbaya au hafai. Wapo wengine ndani ya miezi sita tu hii wameanza kutukumbusha Rais Kikwete na wengine wanatamani hata kurudi zama zile! Naomba kuwapa taarifa mbaya kwao hawa na kwa wale wenzangu na miye iwe taarifa nzuri – kuna uwezekano Rais Magufuli akawa ni kiongozi mzuri kabisa kutoka Tanzania na labda Afrika nzima katika mwanzo huu wa karne ya ishirini na moja.

Maneno haya yanaweza kuonekana kwa baadhi ya watu ya ushabiki uliopitiliza; wanaweza kudhani kuwa nasema hivi bila kufikiria sana ninachokisema. Lakini ndugu zangu naomba niwahakikishie kabisa kuwa uongozi huu wa Magufuli una mwelekeo wa kuinua aina ya uongozi wetu kwa kiwango ambacho viongozi wengine wajao watapimwa nacho.

Sifa moja ya kiongozi mzuri na tena mzuri sana ni yule ambaye hajihisi anawiwa na vikundi vya watu au watu fulani fulani tu zaidi ya umma anaoutumikia. Kwamba, maslahi na kanuni zinazomuongoza ni zile zenye kuzingatia maslahi makubwa kabisa ya umma kuliko maslahi ya watu wachache au kikundi cha watu wachache. Kwa namna nyingine kiongozi wa aina hiyo ni kiongozi ambaye ni lazima awe mahali anajijua na anajikuta yuko peke na mpweke (alone and lonely).

Ninaposema kuwa ni “peke na mpweke” nina maana ya kwamba, siku ile anapokula kiapo cha kuwa Rais wa Tanzania maslahi ya ndugu zake, rafiki zake, jamaa zake, washirika wake yanaisha na siku ile anakula kiapo cha kutumikia maslahi ya Watanzania wote. Maslahi ya watu wa makabila yote, dini zote, rangi zote na wa hali zote.

Katika makala yangu moja ya mwaka 2012 (Toleo la 263 la Oktoba 17) nilikuwa najadili hotuba ya kusisimua ya Esther Wassira. Nilionesha jinsi gani nimefurahishwa na kupewa matumaini kuwa kuna hewa mpya imeingia katika siasa za Tanzania. Nilimnukuu Bi. Wassira akisema kitu ambacho mimi mwenyewe nilikuwa nakiamini kabla kwamba “kipo cha kujifunza, nacho ni kwamba moja ya nguzo muhimu ya uongozi ni kukubali kujitoa kwa ajili ya jamii hata kama wewe hufaidiki na uongozi wako moja kwa moja”

Nikitolea maoni kauli yake hiyo nilisema hivi wakati ule; “Mojawapo ya shida kubwa ambayo tunaweza kuwa tunaiona na inatusumbua sana ni maamuzi ambayo yanatolewa kwa misingi ya kuwanufaisha wale wanaotoa maamuzi hayo. Kwamba tunafanya vitu kwa ajili yetu sisi wenyewe kwanza”

Kwa muda mrefu uongozi wetu ulikuwa wa aina hii; uongozi wa “kishkaji”. Na hili sizungumzii kwenye siasa tu hata kwenye ajira za umma na inawezekana hata kwenye sekta binafsi. Tuliangalia nani “mwenzetu” au nani ndugu yetu wa karibu na huyo akapewa nafasi au ndiye ambaye tukaona tupigane dili la maisha. Hata ilipofika wakati wa kuchukuliana nidhamu kazini inabidi tujiulize matokeo yake kama kumsimamisha au kumfukuza mtu kazi yawezekana ukaleta matatizo kwa wakwe, binadamu, wapwa n.k

Magufuli anapoingia na kuonekana kama kichaa aliyepewa rungu sokoni watu wanaanza kuwa na wasiwasi; wanaanza kuwa na shaka, wanaanza kupoteza ule uhodhi wao wa vitu mbalimbali. Walikuwa na uhakika wa kufanya mambo fulani lakini sasa uhakika huo haupo tena (the certainty is gone). Unaweza kujikuta unampigia simu mtu ajaribu kukuunganisha au kukusaidia jambo fulani na akakuambia “we hunipendi wewe unataka nitumbuliwe mimi!” na huyo alikuwa ni mtu wako wa karibu!

Nilisema hivi kwenye makala ile; “Mwanamapinduzi yeyote ni lazima afike mahali awe mpweke; ajitoe na kukubali kuwa yuko sahihi hata kama wengine hawakubali hivyo.” Ndugu zangu naamini ukimsikiliza Magufuli na ukamwelewa utaelewa kuwa anavyosema ameamua “kujitoa muhanga” anasema kitu ambacho ndio msingi wa mabadiliko ya kweli; ya mwamko ambao unaweza kusababisha watu kukumbatia na kumfuata kiongozi nyuma wakiamini anaenda kuwaongoza vizuri.

Magufuli ameelewa na anaonekana kuelewa tatizo kubwa la msingi la taifa letu ni nini na kwa namna gani amejitolea kulishughulikia tatizo hilo. Upinzani ambao anaupata sasa hivi ni ishara tu kuwa mabadiliko haya hayawezi kuwa rahisi hata kidogo. Hakuna kiongozi yeyote wa mabadiliko ya kweli aliyekubalika au kukumbatiwa hasa na wale ambao wanaenda kupoteza nafasi zao au ile hali yao ya kuwa wao ni maalumu.

Kuanzia wabunge, mawaziri, watendaji wakuu na watu wengi ambao wamekuwa wanufaika wakubwa wa mfumo huu uliopita ni hawa hawa ndio ambao wanaongoza na sitoshangaa kwa muda mrefu ujao wataongoza upinzani dhidi ya Magufuli na wengine wakitumia nafasi zao kumpinga waziwazi; hawa hawanishangazi kwa sababu mti unapoanguka hupiga kelele!

Jambo kubwa la msingi kwa Magufuli na ni la muhimu sana kwa viongozi wengine ni kuhakikisha kuwa hawako tayari kumfurahisha mtu awaje yote. Wawe tayari kuhakikisha kuwa wanaongozwa na maslahi makubwa ya umma kuliko maslahi ya mtu mmoja mmoja au kikundi kimoja kimoja.

Waondokane na mazoea ya kuwaangalia watu usoni na kujiuliza kama huyo anaweza kuwa ni “mtoto wa mjomba!”. Polisi wakimkamata mtu haijalishi ni nani ni lazima wamsimamie kwa mujibu wa sheria; hospitali mtu akienda kupata huduma akakuta watu wengine pale asikubaliwe kupita mstari ati kwa vile yeye ni “fulani”

Watanzania hawa ambao walitamani mabadiliko ya kweli, waliotamani kuheshimiwa katika nchi; wale mamilioni ambao walikuwa wanataka kuona utu wao nao unathaminiwa kama wa akina fulani leo hii wanaanza kuinua vichwa vyao juu na kujiona kuwa na wao wanaheshimiwa. Wale ambao wanafikiri kuwa walikuwa peke yao wanastahili kuheshimiwa na kutambuliwa wanaanza kupata shaka.

Hii ni dalili njema kwa taifa, Magufuli akiendelea kusimamia maslahi makubwa ya nchi yetu na wananchi wake nina uhakika kabisa huu upinzani utakufa kifo chake cha asili na kuwa yale matumaini ambayo yalipotea sasa yatarejea na kuwa nchi yetu inaelekea neema. Ugumu wa sasa ambao wengine wanaanza kuona ni wa lazima kwani hata mgonjwa ili apone wakati mwingine inabidi aende hospitali, alazwe na hata kufanyiwa upasuaji mkubwa. Na wagonjwa wengi hata katika tiba wanaweza kujikuta wanapoteza uzito na hata hamu ya kula.
Kila mmoja kwa nafasi yake ampe Magufuli ushirikiano ili taifa letu lipone

Raia Mwema
 
Mtafute Pasco,kuna kitu anafundisha kinaitwa "Astral Projection" na "Lucid dreaming". Atakusaidia maana umeanza kuonesha hizo dalili..!
 
Back
Top Bottom