Magufuli anamwiga Lee Kuan Yew wa Singapore, kuifanya Tanzania ya ufanisi mkubwa lakini sawa na mke kuwa na mume tajiri bila furaha

Ndugu synthesizee,
Asante sana kwa mfano mzuri, kwa wale waliofika Singapore, watajua unalosema.

Kubadilisha mind set ya watanzania wengi ambao hawana sense ya responsibility na Nationalistic, tunahitaji kiongozi mkali
Mkuu Mkirindi, mie nilikuwa mtu wa kwanza labda kusema Tanzania ilifikia mahali pabaya sana na ilihitaji kiongozi mkali.

Lakini nitakuwa wa kwanza pia kusema ukali wa Raisi Magufuli kwa sehemu kubwa unaelekezwa sehemu zisizostahili, kwa hiyo unakuwa haufai katika sehemu nyingi.

Nyerere alikuwa mkali sana, rushwa, ufisadi, uzembe nk. Lakini bado alikuwa ni dear leader. Sasa ukali wa Magufuli kwa kina Tundu Lisu, Ben Saanane, unasaidia nini?

Afanye ukali na mawaziri, ufisadi, uzembe, utawala wa sheria nk. Sio kufanya ukali kwa yeye kuwa kinara wa kuvunja katiba na kuja na majibu yeboyebo anapokumbushwa.
 
Lakini kwa bwana Lee hazikupotea 1.5 Trillion kwenye mazingira ya kutatanisha. Au na hiyo ameiga?
Kwa kiasi fulani Mkuu - kama zilitumika kwa manufaa ya taifa sio kuwapa Usalama wa Taifa wadhibiti watu wanaomkosoa Magufuli
 
Mkuu umesema huyo rais wa Singapore pia ametengeneza international airport nyumbani kwake na alinunua ndege 7 hata kama hakuna mahitaji kama hapa kwa wadanganyika? Sijakupata vizuri hiyo Aya ya mwisho umetumia lugha ya wakoloni naomba unitafasirie tafadhali!
Hapana sijasema hivyo.

Ila huyu jamaa wa Singapore alianzisha shirika la ndege ambalo ni mojawapo ya mashirika makubwa duniani - Singapore Airlines.

Hakuwa na ubinafsi wa kujenga airport kwake au kujinufaisha. Alikuwa mzalendo na mwenye uwazi. Kama akichukua Tshs 1.5b za serikali bila ruhu8sa ya Bunge alisema alitaka zifanye nini sio kuwapa watu wa Usalama wa Taifa kisiri.
 
Kweli lakini huwezi kufanya fair comparison ya Singapore yenye 100% wana elimu na ujuzi idadi yao ni watu5.5m na Tz ya watu 55m 20% ndowenye elimu ya ujuzi 50 wanajua kusoma na kuandika ila hawaelewi (can't analyse) tena zaidi ya 70% ya biashara Singapore ni private sector western investiment ( so called Mabeberu)... sisi hatuwataki tunawafukuza na private sector tunahakikisha inakufa....kwahiyo ni rahisi Yesu kurudi sasa hivi kuliko Tz kua katika middle class income by 2020....hi miaka yote ya JPM ni potea

Sent using Jamii Forums mobile app

MKuu hujaelewa. Singapore walikuwa masikini hohehahe. Hayo unayosema ni matokeo ya alichofanya LKY. Na idadi ya watu sio tatizo - la sivyo China wangekuwa masikini wa mwisho duniani.

Masuala ya private sector yalikuzwa baadaye baada ya uchumi na miundo mbinu kuimarika. Mwanzoni ilikuwa serkali inasimamia karibu kila kitu.Kwa mfano, huwezi kubinafsisha Tanesco wakati bado wananchi hawana umeme, kwa kuwa kampuni binafsi haitapeleka umemem vijijini ambako hakuna watumiaji wakubwa.

Ila ninachosema ni kwamba, Magufuli anafanya vema kujaribu kumuiga LKY, ila ana mihasira na ukali mwingi sehemu zisizostali na anaishia kuvuruga sana japo ana nia nzuri. Hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kufeli
 
Sawa mkuu nakuelewa ila JPM wako hana political agenda wala economic focus anafanya 'try and error' model ndomaana hana mpango wakuita press conference kueleza economic policy yake na wapi tunaelekea lakini anatumia pesa za umma kuitisha kikao cha wakuu wa dini ambao hawajui mambo ya uchumi zaidi ya kusifia tu. Model za uchumi na siasa inajulikana aseme anafuata ipi? Market economy? mixed economy? socialism? Au communism? Sio kubahatisha

Mkuu, ukianza kuongea economy models na Magufuli ni sawa na kumwambia Diamond awatumbuize mbuzi. Yeye ni mtu wa Sodium chloride. Ila pamoja na hayo, anaona anajua what is best for Tanzania and everyone.
 
Sawa kama anajua what's better for Tz ila lazma kiwe organised and systematic ili viongozi wengine weweze kuendeleza akitoka na pia nivizuri tujue defined destination (goals to be achieved)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siwezi kupinga kwamba Raisi Magufuli ana nia nzuri tu na Tanzania hii - kama vile tu ilivyokuwa kwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Singapore, Lee Kuan Yew, kuanzia mwaka 1965, akaitoa Singapore katika umasikini mkubwa na kuifanya moja ya maifa tajiri duniani leo hii.

Kitu alichofanya Lee Kuan Yew kwa Singapore ni namna ya "hapa kazi tu" ya Magufuli. Hakujali kelele za wananchi au vyama vya upinzani. Aliua siasa za upinzani na kuanzia 1972 - 1991 chama chake cha siasa kilishinda viti vyote isipokuwa viwili tu (1984) vilivyoenda upinzani, na kufanya Singapore iendeshwe kama nchi ya chama kimoja cha PAP katika mfumo wa vyama vingi.

Lee Kuan Yew alikuwa mbabe kwelikweli na alipingwa na kukosolewa kila siku lakini hakujali. Alidhibiti vyombo vya habari, hakuruhusu mandamano na aliwatia kizuizini wapinzani. Alidai kwamba ili nchi iendelee lazima hayo yafanyike ili nchi iwe na nidhamu (kuinyoosha nchi).

Lee Kuan Yew alikuwa akitamka hadharani kwamba hakuwa mtu wa kuchezewa (sijaribiwi). Alisema "mtu yeyote anaetaka kunijaribu lazima avae vyuma mkononi. Na kama unafikiri unaweza kuniumiza mimi zaidi ya mimi ninavyoweza kukuumiza wewe, basi jaribu uone".

Lee Kuan Yew alikufa mwaka 2015, akiwa na miaka 91, na kufanikiwa kufanya Singapore taifa tajiri duniani. Mwaka huo, 2015, Raisi Magufuli alishika madaraka, ikawa kama Lee Kuan Yew wa Singapore kazaliwa upya Tanzania!

Ni kweli Singapore iliendelea sana. Wananchi walivunjiwa nyumba zao bila fidia ili kupisha miradi ya maendeleo nk. Serikali ilishika miradi mikubwa yote ya nchi na sekta binafsi haikupewa kipao mbele kikubwa. Singapore ilibadilika katika kipindi cha Lee Kuan Yew na kuwa yenye ufanisi wa juu duniani, ndani ya kipindi cha chini ya miaka 20.

Ila sasa, pamoja na ufanini wote uliofikiwa na Singapore, ni nchi ambayo wananchi wake wanajulikana duniani kwa kuwa na stresss ya kiwango cha juu sana, na kusababisha matukio mengi sana ya kujiua. Wananchi wa Singapore tajiri sana hawana furaha kabisa. Ni kosa kubwa kuikosoa serikali au uongozi nchini Singapore.

Hii imenifanya nijiulize, hivi ni wanawake wangapi duniani watakuwa tayari kuolewa na mwanaume tajiri sana, wakaishi ndani ya utajiri na minyanyaso bila furaha, kwa kuwa tu wanafurahia kuishi katika utajiri? Je, hiyo ndio aina ya Tanzania tunayoitaka? Kupanga ni kuchagua.
singapore ni kosa kubwa kukosoa serikali? hapo tu umeshanidanganya pia soma vitabu vya huyo mzee ndio utajua alikuwa na vision gan.
 
Ndugu synthesizee,
Asante sana kwa mfano mzuri, kwa wale waliofika Singapore, watajua unalosema. Nadhani Singapore sio nchi kubwa zaidi ya mkoa wa Dar ama mikoa mingi ya TZ. Lakini ni nchi iliyoendelea na ni dunia ya kwanza.

Nchi nyingine za mfano ni kama Spain under Franco, South Korea, China.

Kubadilisha mind set ya watanzania wengi fuliambao hawana sense ya responsibility na Nationalistic, tunahitaji kiongozi mkali .

Sent using Jamii Forums mobile app
Magufuli hana uwezo huo, tutapoteza muda wa miaka 10
 
Watazania tujenge taifa lisilokuwa na ubaguzi apo tutafika lakini tuache kujenga tabaka ambazo zitatuangamiza huko tuendako
 
Mkuu Mkirindi, mie nilikuwa mtu wa kwanza labda kusema Tanzania ilifikia mahali pabaya sana na ilihitaji kiongozi mkali.

Lakini nitakuwa wa kwanza pia kusema ukali wa Raisi Magufuli kwa sehemu kubwa unaelekezwa sehemu zisizostahili, kwa hiyo unakuwa haufai katika sehemu nyingi.

Nyerere alikuwa mkali sana, rushwa, ufisadi, uzembe nk. Lakini bado alikuwa ni dear leader. Sasa ukali wa Magufuli kwa kina Tundu Lisu, Ben Saanane, unasaidia nini?

Afanye ukali na mawaziri, ufisadi, uzembe, utawala wa sheria nk. Sio kufanya ukali kwa yeye kuwa kinara wa kuvunja katiba na kuja na majibu yeboyebo anapokumbushwa.
Ukali wake unachagua.
Mkolomije, Cheupe kwa upendo na kutabasamu, hawasemwi,hawamo.
Kwenye barabara wa ku Ngw'anza hawaguswi.
Nadhani wake ni ukorofi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom