Magufuli anajua hesabu, atazame namba hizi za kwenye vitalu

Tina

JF-Expert Member
Jul 9, 2007
572
581
LABDA nianze kwa kutoa maelezo kidogo.

Luxembourg ni nchi ya nane kwa udogo barani Ulaya. Ina ukubwa wa takribani kilomita za mraba 2,586. Hapa Tanzania, kampuni za uwindaji wanyama zinaweza kupewa leseni za kuwinda kwa kilomita za mraba mpaka 1,000.

Hii maana yake ni kwamba, mtu mmoja (kampuni moja) anaweza kupewa eneo lenye ukubwa sawa na nusu ya nchi ya Luxembourg awinde wanyama kwa tozo ya kati ya dola 5,000 (Sh. milioni 10) hadi dola 60,000 (Sh. milioni 120) kwa muda wa miaka mitano!

Zaidi ya kuua wanyama, mtu huyo anatakiwa pia kuhakikisha kwamba eneo alilopewa analihifadhi vizuri, anawinda wanyama kwa kiwango kinachokubalika na anaishi vizuri na jamii inayomzunguka.

Mimi nafahamu baadhi ya nyumba zilizopo hapa Dar es Salaam ambazo mtu anakodi kwa gharama ya dola 3,000 hadi 5,000 kwa mwaka. Hii ni gharama ya kuishi katika nyumba moja tu.

Lakini kwenye uwindaji, mtu anapewa eneo lenye wanyama, maji, miti na uoto mwingine wa asili kwa thamani ya dola 5,000 kwa miaka mitano!

Rais John Magufuli ni mwanasayansi na bila shaka hesabu hazimpigi chenga. Je, kimahesabu, eneo la ukubwa wa nusu ya nchi lenye utajiri wa rasilimali, linakodishwaje kwa shilingi- hata tuseme milioni 120, kwa muda wa miaka mitano?

Gharama ya kupanga nyumba kwa mwaka katika jengo la Viva Towers jijini Dar es Salaam ni takribani dola 400,000 (Sh. milioni 800).

Iweje mtu aue, avune miti na afanye anavyotaka katika eneo tajiri la nchi kwa kulipa Sh. milioni 120 kwa miaka mitano?

Ukitaka kujua Tanzania ‘inaliwa’ katika eneo hili, unahitaji kusoma kitabu kilichoandikwa na Profesa Craig Packer wa Marekani kiitwacho Lions in the Balance: Man-Eaters, Manes and Men with Guns na upate mchapo mmoja wa kusisimua kuhusu jambo hilo.

Kuna sehemu anazungumzia kuhusu tukio moja la kushangaza. Kuelekea mwaka 2010, Idara ya Wanyamapori iliitaka kampuni moja kutoa kitalu chake kimojawapo kwa chuo cha Tawiri kwa ajili ya shughuli za kitafiti.

Baadaye, kitabu hicho kinaeleza, Idara hiyo ilitoa nusu ya kitalu chake kwa mojawapo ya kampuni zinazoongozwa na mdau maarufu wa sekta ya uwindaji na utalii hapa nchini, Sheni Lalji.

Kwa kupewa kitalu hicho, Sheni alilipia leseni ya kiasi cha dola 12,000 (sawa na takribani Sh. milioni 25). Baadaye, kampuni hiyo walikuwa wanakihitaji kitalu hicho kwa sababu Tawiri wala hawakuwa wanakihitaji.

Kitabu kinaeleza kuwa mabosi wa Idara ya Wanyamapori waliwaambia kuwa kama wanakitaka kitalu hicho, wanatakiwa waende kuzungumza na Sheni mwenyewe.

Sheni akakubali kuwapa kitalu hicho kama watamlipa kiasi cha dola 600,000 (sawa na shilingi bilioni 1.2). Yeye alikuwa tayari kuilipa serikali kiasi cha Sh. milioni 25 lakini yeye anajua kuwa thamani ya eneo lile ni Shilingi bilioni 1.2.

Ni wazi kwamba hapa kuna tatizo.

Tatizo kubwa zaidi

Tatizo kubwa zaidi ni kwamba upo ushahidi kuwa matajiri wanaojihusisha na uwindaji, ndiyo vinara pia wa uharibifu wa mazingira.

Kwa mfano, pamoja na matajiri kupewa vitalu kwa ajili ya kuviendeleza, yapo maeneo ambako walipewa kuyaendeleza na sasa yamekuwa mabaya kuliko walivyokabidhiwa.

Ushahidi wa hili ni namna ambavyo idadi ya wanyama waliokuwa wengi inavyozidi kupukutika. Kuna kampuni zilipewa vitalu kwa ajili ya kuwinda na kuhifadhi lakini si kwamba wamemaliza wanyama wote, lakini wamevuna hadi miti waliyoikuta.

Ndiyo sababu, Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009, ikaweka masharti yanayotakiwa kufuatwa kabla ya waombaji wa leseni za uwindaji hawajapewa leseni zao.

Kuna Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji yenye kumshauri waziri kuhusu masuala ya ugawaji wa vitalu. Kamati hii hupitia maombi ya watu wanaotaka leseni mpya au kuongezewa muda kwa leseni za zamani.

Hupitia maombi hayo kwa kutazama kama vigezo vyote vimetimizwa. Kwa kampuni ambazo zinataka kuongezewa muda, kamati ina wajibu wa kutazama kama kwenye leseni ya awali ilitimiza masharti yote.

Kwa kufanya hivi, serikali ilikuwa imejiwekea mazingira ya kuhakikisha kwamba wanaopewa leseni mpya au wanaoongezewa muda ni wale tu wenye sifa tu.

Kamati hii ingesaidia kubaini wawindaji wenye tabia mbaya na isiyofaa. Kamati hii ingesaidia kupunguza uharibifu wa maliasili ya taifa letu ambayo kimsingi ni ya vizazi vyote vya Tanzania na si kizazi kilichopo sasa pekee.

Ajabu ni hii

Wiki iliyopita, Raia Mwema liliripoti kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, amedaiwa kuongeza muda wa leseni za vitalu vya uwindaji kwa makampuni kinyume na taratibu.

Waziri huyo ameongeza muda wa uwindaji kwa wamiliki wa awali wa vitalu hivyo kwa muda wa miaka mitano; kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2022.

Katika barua pepe iliyotumwa kwa wanachama wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Uwindaji wa Kitalii Tanzania (TAHOA) Januari 19 mwaka huu, wamiliki hao walitakiwa waende kwenye ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii kuchukua leseni zao zilizoongezewa muda.

"Barua za kila kampuni kujua kama imeongezewa muda au la, kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Wanyamapori, zitakabidhiwa mkononi kwa mwakilishi wa kampuni atakayekwenda wizarani kuchukua barua hiyo," ilieleza sehemu ya barua pepe hiyo iliyoandikwa na Sheni Lalji," majira ya saa nane mchana, Januari 19 mwaka huu.

Wizara ilitoa majibu ya habari hiyo ya gazeti hili kwa kusema kwamba taratibu zote zilifuatwa na kwamba habari hiyo ilikuwa na lengo la kupotosha.

Kwa mfano, wizara inasema kwamba kamati ya kumshauri waziri ipo na iliundwa mwaka 2013. Kwa mujibu wa sheria, kamati hiyo hukaa kwa muda wa miaka mitatu na hivyo ilitakiwa kumaliza muda wake tangu mwaka 2016.

Hivyo, kisheria, hiyo kamati inayozungumziwa imemaliza muda wake.

Lakini, kuna uharaka gani wa kutoa leseni sasa bila ya kufuata taratibu? Kwanini vitalu vipya na vya zamani havikutolewa tangazo katika magazeti kama sheria inavyotaka na badala yake wadau wameambiwa ghafla tu bila ya kutarajiwa?

Kwa shida ya kifedha ambayo Tanzania inayo kwa sasa, zoezi la ugawaji wa vitalu lingeweza kuwa chanzo kizuri cha mapato. Njia nzuri zaidi ni ile ya kufanya kama wanavyofanya wenzetu wa Zimbabwe.

Wao wanatangaza kuwepo kwa vitalu na wenye fedha wanajitokeza. Yule atakayekuja na fedha nzuri zaidi ndiye atapewa kitalu. Taarifa zipo za wawekezaji walio tayari kulipia leseni zao hadi kwa dola milioni moja (zaidi ya shilingi bilioni mbili) kwa kitalu.

Siri ya kufanikiwa katika hili ni kuondoa mfumo wa kugawa vitalu kwa kuwekea madaraja. Kwamba vile vyenye wanyama na mazingira mazuri zaidi ndiyo vinakuwa vya bei ya juu na vile visivyo na wanyama wengi vinapewa bei ya chini.

Kazi ya serikali inatakiwa kuwa ni kutangaza vitalu vyote. Hivi, ni mwindaji gani atakuja kuleta fedha wakati wewe umeshatangaza kuwa kitalu hicho ni cha daraja la chini na hakuna wanyama?

Kwa kutumia mfumo wa mnada, Tanzania kwa idadi ya vitalu vyake takribani 150 vilivyopo, ingeweza kukusanya mabilioni ya shilingi.

Lakini, kwa haraka haraka hii, ya wawindaji kuitwa wizarani kwenda kuchukua barua zao ‘ kwa mkono’ za kuongeza muda wao wa kuwinda pasipo kuwepo kisheria kwa kamati ile ya kushauri, hapa ipo namna.

Hawa watu wamekwenda kuongezewa muda wa leseni zao za kuwinda bure. Lakini sharti walilopewa ni kwenda kuchukua barua zao mkononi kulekule wizarani.

Kuna msemo maarufu wa Kiswahili unaosema; “ Kusoma hujui, hata Picha Huioni?”

Source: Raia Mwema
 
Hii habari ni njema kwa wale wanaopigania maslahi ya taifa la kesho, lakini ni habari mbaya mno kwa watu wanaojijali wao na familia zao tuu. hapa hakuna pakutokea isipokua mungu atupe tuu maarifa wakati fulani haya yatakuja kuwa ni historia
 
hizo mambo ni za wana ccm. wacha ccm wale nchi. na juzi kwenye uchaguzi wa studio wameshinda kwa kishindo.
 
Najua utakuwa unajua IMLA naomba ufanye kitu kwenye tapiko lako ili niweze kuelewa
 
nchi hii ilikuwa inaliwa sana. tuendelee kufichua maovu kama ulivyo fanya mleta mada. na sisi wasomaji tupige kelele kwa kuchangia sana uzi wako huu ili wakubwa wasikie
 
Tanzania simama nishuke.. Sio kwa kodi za kukomoana kwenye salary wakati wahuni wachache wanajichotea ukwasi wa kutosha katika sekta ya uwindaji na madini!!
 
Kwenye makala kuna taarifa za upotoshaji. Kwanza kwa sasa minimum block fee ni $ 30,000 max ni $60,000 kutegemeana na grade ya kitalu.

Pili block fee hulipwa kwa mwaka, siyo miaka 5. Ownership ni miaka 5 lakini fee ni kila mwaka. Pia block fee siyo ada pekee inayolipwa. Kuna ada nyingine lukuki.

Maeneo mengi yamepoteza hadhi ya kuwa vitalu vya uwindaji kutokana na mifugo na ujangili. Ngombe wameingia kila mahali, wanyama wamepungua sana.
 
Hao wanyama wameyeyuka au wamemalizwa na wenye vitalu?
 
Back
Top Bottom