jepro
Member
- Oct 28, 2011
- 90
- 6
1. Kwanza awezeshe kuwa na uhuru wa Vyombo vya Habari.
2. Demokrasia ni jambo muhimu awape wapinzani uhuru wa kuikosoa serikali kwa kuwa hakuna aliyekamilika duniani kila mtu hutenda makosa na kukosolewa ndo njia pekee ya kujifunza ulipokosea na ukajirekebisha na mambo yakaendelea kama ilivyo ada.
3. Afanye uchunguzi yakinifu kwa habari anazoletewa na watendaji wake kabla ya kuziwasilisha kwa wananchi.
4. Aweze kusikiliza malalamiko ya wananchi kwa kuwa hawa ndio waliomchagua na akumbuke sauti ya wengi ni sauti ya Mungu asitie pamba masikioni kwa malalamiko ya wengi pindi jambo Fulani linapozungumziwa au kuhitaji ufafanuzi wa kina kutoka kwake au Mamlaka husika.
5. Azingatie sheria, kanuni na taratibu zinazotumika kuliongoza hili Taifa namaanisha aongoze Taifa kwa kufuata nini Katiba inavoelekeza
Nadhani kwa kuyafuata hayo mambo matano pamoja na uchapakazi wake mahiri hili Taifa naliona lina bright future katika ukuaji kiuchumi vinginevyo tutajikuta tunarudi nyuma miaka Zaidi ya 50
Ni hayo Tuu