G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Akiwa kwenye kampeni leo, mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM John Magufuli ameendelea kuwanadi wagombea ubunge wa chama hicho.
Akiwa Bariadi leo amemnadi mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi mashariki Andrew Chenge kwa kumuita shujaa wa mabadiliko baada ya kile alichodai kuiandika katiba mpya kwa ueledi mkubwa. Magufuli amesema kuwa Chenge aliitendea vyema taaluma yake kwa kuwaandikia watanzania katiba iliyo bora.
Katika hatua nyingine aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Joseph Sinde Warioba ameonyesha waziwazi kuiunga mkono katiba ya Samweli Sitta aliyekuwa mwenyekiti wa bunge maalum la katiba.
Warioba amewashambulia UKAWA huku akidai kuwa hawakuwa sahihi kuususia mchakato wa kuandaa katiba mpya. Warioba amedai kuwa UKAWA walisusia bunge maalum la katiba huku wakiwa na ajenda ya siri ya kuuvunja muungano wa Tanzania.