Elections 2015 Magufuli amshushia tuhuma Job Ndugai, amtahadharisha kuunga mkono kauli za Lowassa

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ndugu John Pombe Magufuli leo ameshusha lundo la tuhuma kwa naibu spika wa bunge na mgombea ubunge wa jimbo la Kongwa kwa tiketi ya CCM ndugu Job Ndugai, imethibitishwa.

Magufuli amemtuhumu Job Ndugai kwa kitendo chake cha kueleza hadharani kuwa anaiunga mkono kauli ya Edward Lowassa ya kuunda tume maalum kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji jimboni humo.

Magufuli amesema kuwa kitendo hicho kinaonyesha jinsi ambavyo Job Ndugai asivyo na imani naye kama mgombea wa urais kupitia chama chake na wala asisingizie migogoro.

Aidha habari za ndani zilizopatikana jimboni humo ni kuwa Job Ndugai alikuwa miongoni mwa wana CCM walio na imani kubwa na Edward Lowassa ingawa kwa sasa hajaeleza msimamo wake baada ya Lowassa kuitosa CCM.
..................
Mimi nipo na timu ya watu wa ndani kabisa wa John Magufuli mikoani.
 
Magufuli ni mamluki wa Lowassa ndani ya CCM. Ushahidi namba moja ni kwamba alipita kwa kura za maoni za hasira za wanaCCM walokuwa wamejiandaa kumpa Lowassa. Mbili ni kwamba Magufuli mwenyewe alijiandaa kumpigia kura Lowassa.

Sasa, Magufuli ndio mamluki namba moja ndani ya CCM. NDUNGAI na wengine wanafuata.
 
Duh na kura ya urais ya ndugai kwa namna hii atampa lowasa ..thank you sasa hakikisha na wanaccm wote wanaoku support mpwapwa kura wanampa lowasa..wewe ndugai unajua kuwa magufuli hawezi urais.. uliona hata kwa lamati zenu za kuitetea ccm alivyokuwa anahamaki..mtashirikianaje nae huyu..makinda anaelewa mlivyo mhukumu lowasa bila kosa ndo maana katulia tuli mama wa watu
 
Magufuli ni mamluki wa Lowassa ndani ya CCM. Ushahidi namba moja ni kwamba alipita kwa kura za maoni za hasira za wanaCCM walokuwa wamejiandaa kumpa Lowassa. Mbili ni kwamba Magufuli mwenyewe alijiandaa kumpigia kura Lowassa.

Sasa, Magufuli ndio mamluki namba moja ndani ya CCM. NDUNGAI na wengine wanafuata.
Bila kura za hasira za kumkomoa membe leo hii magufuli asingekuwa mgombea wa Urais kupitia ccm, wafuasi wa Lowasa Ndiyo waliochagua magufuli na pia magufuli na yeye ni mfuasi wa Lowasa.
 
Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ndugu John Pombe Magufuli leo ameshusha lundo la tuhuma kwa naibu spika wa bunge na mgombea ubunge wa jimbo la Kongwa kwa tiketi ya CCM ndugu Job Ndugai, imethibitishwa.

Magufuli amemtuhumu Job Ndugai kwa kitendo chake cha kueleza hadharani kuwa anaiunga mkono kauli ya Edward Lowassa ya kuunda tume maalum kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji jimboni humo.

Magufuli amesema kuwa kitendo hicho kinaonyesha jinsi ambavyo Job Ndugai asivyo na imani naye kama mgombea wa urais kupitia chama chake na wala asisingizie migogoro.

Aidha habari za ndani zilizopatikana jimboni humo ni kuwa Job Ndugai alikuwa miongoni mwa wana CCM walio na imani kubwa na Edward Lowassa ingawa kwa sasa hajaeleza msimamo wake baada ya Lowassa kuitosa CCM.
..................
Mimi nipo na timu ya watu wa ndani kabisa wa John Magufuli mikoani.

acha urofa na ujinga wa kibavicha ndani ya ccm wewe hujui lolote
 
Mm kuna taarifa nimeipata magufuli huenda akaja rasmi ukawa baada ya wiki moja.na alimuomba lowasa amuache kwenye wizara ya ujenzi
 
OOhhh, hawana taratibu za kuwekana sawa ndani ya chama??

Kwa Magufuli habari za kuwekana sawa hilo wasahau na wanajua halipo.

Mtu mbishi, hataki kushaurika, analolijua yeye ndilo hilo, hajui kwamba hajui, hajawahi kuwa team player hata siku moja, akisema amesema hata kama ni SADDAM RAISI WA KUWAIT wengine mseme ndiyo!. Mtu wa hamaki na papara, anayedhani kasoma bila kujua kasoma nini!. Huyu mtu mnawekana sawa wakati gani?

Kwanza kina Ndungai, na wote anaowabwatukia bwatukia wakati wa uchumba, wajiandae. Hii ni honey moon ya ccm na magufli. Atakapokuwa mwenyekiti wao wa chama, wajiandae namna ya kutoka salama.
 
Back
Top Bottom