Magufuli amshauri Museveni kuifumua Mamlaka ya Mapato Uganda (URA)

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Messages
492
Points
500

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined May 23, 2019
492 500
Rais Magufuli amemtaka Rais Yoweri Museven wa Uganda kuwa mkali kwa watendaji wake ambao wanakwamisha kuanza kwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini humo mpaka Tanga, Tanzania.

Magufuli ametoa mfano wakati alipoingia madarakani Novemba 5, 2015 alibadilisha makamishna wakuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watano lengo ni kuongeza ufanisi katika mamlaka hiyo.

“Leo niwape siri, nilikuwa namuuliza Rais Museveni mbona unachelewesha hili bomba, kwa sababu ya kodi ya huko ambayo umekataa kuikubali ya Dola 600 wakati utakuwa unatengeneza Dola bilioni 800 jitolee hii kodi kidogo utengeneze ajira na utakuwa unapata fedha kwa muda mrefu watu wako wa TRA wasikucheleweshe, sisi tulitaka hilo bomba liitwe Kaguta Pipeline siku tunapozindua, hao wasikucheleweshe.

“Simfundishi mzee, lakini nilipoingia madarakani nimebadilisha makamishna watano kwa miaka mitatu na nusu, si suala la kujidai lakini ni baya. Nikamwambia wewe umeng’ang’ania huyo wa kwako wa nini huko, tunatakiwa twende mbele, katika biashara kuna kupata na kukosa unatakiwa utoe ili upate zaidi.

“Kwanini ucheleweshwe na watendaji, kaka naona umekuwa mpole kabla ya wakati ule ulipopigana ulikwa mkali sasa uongeze, ongeza ukali kwenye hili.

“Nimeona nilizungumze hili sitaki kuwa mnafiki, I wish (natamani) hawa watendaji wangehamia Tanzania na wa Tanzania waende Uganda nideal (nishughulike) nao kwa mwezi mmoja tu,” amesema Rais Magufuli.
 
balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
4,651
Points
2,000

balimar

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
4,651 2,000
Magufuli ni mjamaa kwelikweli
Yeye kupitia kichwa cha mtu ili mambo yaende sio tatizo
Eventually, we need such the leader tumelegea sana
 
Samwel Ngulinzira

Verified Member
Joined
Aug 5, 2017
Messages
1,490
Points
2,000

Samwel Ngulinzira

Verified Member
Joined Aug 5, 2017
1,490 2,000
Leo niwape siri, nilikuwa namuuliza Rais Museveni mbona unachelewesha hili bomba, kwa sababu ya kodi ya huko ambayo umekataa kuikubali ya Dola 600 wakati utakuwa unatengeneza Dola bilioni 800 jitolee hii kodi kidogo utengeneze ajira na utakuwa unapata fedha kwa muda mrefu watu wako wa TRA wasikucheleweshe, sisi tulitaka hilo bomba liitwe Kaguta Pipeline siku tuna
Hapa kaongea point muhimu sana. Mtizamo kama huu ukifuatwa na TRA pia tutafika mbali. Wanaweka kodi kubwa mfano VAT na PAYE ambayo inasababisha waajiri kushindwa kuwapa wafanyakazi mikataba.
Inabidi watumishi wa mamlaka za mapato wa Afrika wabadilike ili Afrika ijikwamue kiuchumi
 
Msengapavi

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2008
Messages
8,181
Points
2,000

Msengapavi

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2008
8,181 2,000
Mi mwenyewe ni eona hiyo figure nikasema hiii!!!! Hizo figure zote mbili ni feki tupu. Dola 600 na dola bilioni 800?
Dola bilioni 800? Mtoa mada uko sahihi kweli kwenye hio nukuu maana kibongo hio ni zaidi ya trillion 1600. Kwa hali hii basi Uganda itaongoza kiuchumi Africa kwa mbali.
 
unprejudiced

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2017
Messages
2,055
Points
2,000

unprejudiced

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2017
2,055 2,000
Magufuli bana, anamwambia Museveni ashushe kodi ili bomba liijengwe hilo ni sawa, lakini huku nyumbani yeye kashindwa kushusha kodi mpaka biashara nyingi zinafungwa!
Kuwa mkweli. Tuko njia ya mpito kutoka Mission town na biashara ya kweli. Kodi ya huko bado rafiki sema mazoea
 
Mkirindi

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2011
Messages
5,687
Points
2,000

Mkirindi

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2011
5,687 2,000
Dola bilioni 800? Mtoa mada uko sahihi kweli kwenye hio nukuu maana kibongo hio ni zaidi ya trillion 1600. Kwa hali hii basi Uganda itaongoza kiuchumi Africa kwa mbali.
Raisi alikosea na kujisahihisha, lakini mleta mada katumia lile kosa la kwanza kwa nia zake anazozijua. Raisi alisahihisha na kusema mapato yatakuwa B 80 tuu.
 
Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2017
Messages
8,052
Points
2,000

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2017
8,052 2,000
Rais Magufuli amemtaka Rais Yoweri Museven wa Uganda kuwa mkali kwa watendaji wake ambao wanakwamisha kuanza kwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini humo mpaka Tanga, Tanzania.
Magufuli ametoa mfano wakati alipoingia madarakani Novemba 5, 2015 alibadilisha makamishna wakuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watano lengo ni kuongeza ufanisi katika mamlaka hiyo.
“Leo niwape siri, nilikuwa namuuliza Rais Museveni mbona unachelewesha hili bomba, kwa sababu ya kodi ya huko ambayo umekataa kuikubali ya Dola 600 wakati utakuwa unatengeneza Dola bilioni 800 jitolee hii kodi kidogo utengeneze ajira na utakuwa unapata fedha kwa muda mrefu watu wako wa TRA wasikucheleweshe, sisi tulitaka hilo bomba liitwe Kaguta Pipeline siku tunapozindua, hao wasikucheleweshe.

“Simfundishi mzee, lakini nilipoingia madarakani nimebadilisha makamishna watano kwa miaka mitatu na nusu, si suala la kujidai lakini ni baya. Nikamwambia wewe umeng’ang’ania huyo wa kwako wa nini huko, tunatakiwa twende mbele, katika biashara kuna kupata na kukosa unatakiwa utoe ili upate zaidi.
“Kwanini ucheleweshwe na watendaji, kaka naona umekuwa mpole kabla ya wakati ule ulipopigana ulikwa mkali sasa uongeze, ongeza ukali kwenye hili.
“Nimeona nilizungumze hili sitaki kuwa mnafiki, I wish (natamani) hawa watendaji wangehamia Tanzania na wa Tanzania waende Uganda nideal (nishughulike) nao kwa mwezi mmoja tu,” amesema Rais Magufuli.
kipofu anamuelekeza kipofu mwenzie njia!

Jiwe anapendaga kujipa cheo asichokua nacho!

Yeye kama nani kuwaelekeza Waganda cha kufanya?

Nchi yake ni shithole,anaenda kuwaelekeza wenzie cha kufanya!

Waganda hawajamuajiri kutoa his consultation services to begin with!

Aigeuze hii nchi iwe first world country ndio anaweza waelekeza wenzake cha kufanya!

Hapa EA anaeweza waelekeza wenzake cha kufanya walao ni Uhuru na Kagame,wengine wa-shup up their butts!
 
Pohamba

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2015
Messages
21,873
Points
2,000

Pohamba

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2015
21,873 2,000
Mzee alikuwa anasema ‘TRA ya Uganda ‘ ..’ USA Dola..’ akarudia Mara kadhaa hayo maneno

Hata mie huwa nasema Tanesco ya Zambia

Pengine kuna mwingine anasemaga Dawasco ya Rwanda

Cha msingi tunaelewa

Tff ya Kenya n.k

TCRA ya Malawi

Kanyaga kanyaga
 
Forum statistics

Threads 1,389,661
Members 527,997
Posts 34,031,397
Top