Magufuli ameukinai uwaziri..sasa apumzike

Status
Not open for further replies.
tanzania bila mchaka mchaka mambo hayaendi
namsifu magufuli kwa kuanika uozo wa wenzie hadharani
nini cha kuficha hapa? kama ni wazembe na ndio wanaokwamisha mradi
kwanini asiwaseme hadharani??? bravo magufuli mawaziri wengine waige mfano wake
ntashangaa leo kama JK hatambakisha.
 
Magufuri ni kiongozi bora, huwezi kumlinganisha na baadhi ya mawaziri wa TZ. Mwache achape kazi
 
Pamoja na John Obhwarwa Magufuli kuonekana kama waziri pekee wa ccm mchapakazi,lakini kuna kitu kinachomfanya uchapakazi wake uonekane sio lolote.kitu hicho ni dharau.huyu bwana ana dharau ya hali ya juu.sijui kwa kuwa amekuwa waziri kwa muda mrefu sana takribani miaka 17 au sijui kwa kuwa tunamsifu sana ndo maana anakuwa hivi sipati jibu.juzi wakati naangalia TB-CCM1 wakati huyu bwana akitembelea barabara zinazojengwa dar alikaripia vikali mamlaka zingine za serikali zinazokwamisha ujenzi huo zikiwemo tanesco na dawasco.akamwagiza mfugale afuatilie mamlaka hizo na kama wakisuasua ataonana na mawaziri wa mashirika hayo..na kama hiyo haitoshi akasema kama mawaziri hao pia watasuasua ataenda kwa JK moja kwa moja kuwashtakia...lol!!niliduwaa!!

haya ni mambo ya kuongelea hukoo kwenye vikao vyao vya ndani (inter-ministrial meetings) sio kwenye vyombo vya habari bwana magufuli.sasa kama kuna waziri mhusika alikuwa anaangalia taarifa ile ya habari unadhani atakupa ushirikiano?atakukwepa tu.mimi nadhani this is too much for magufuli.anaropoka tu hadharani.hana busara hata kidogo.pamoja na uchapa kazi wake lakini bila busara ktk kutekeleza majukumu yake ni kazi bure. ndio kuna mambo ya sheria zaidi,lakini kuna mengine hayahusu sheria.atulize jazba.achape kazi.lakini pia kuna kitu najiuliza,kuugua kwa huyu bwana malaria ya mara kwa mara ndo yamemfanya hivi?yamechukua sehemu ya ufahamu wake?mi nadhani akili zake zimezidi sana kiasi kwamba anaonekana kuchanganyikiwa...

Apumzike sasa.aachie wengine waongoze.pamoja na uchapa kazi wake lakini hafai kuwa kiongozi.
WEWE UMETUMWA AU? HIVI HIVYO VIKAO VYA BARAZA UMEWAHI KUINGIA AU UNAKISIA KISIA TU. BARAZA LA MAWAZIRI HALIENDESHWI KAMA BUNGE PALE KUNA ALIYETEUA NA WALIOTEULIWA KWAHIYO UKIONA HIVYO SIYO KWAMBA MAGUFULI NI MJINGA ANAFANYA HIVYO ILI NGUVU IWE SHUHUDA WA UKINYONGA WA KIKWETE ANAYEWAUZA. USIKUTE HATA HILI BARAZA LA MAWAZIRI LENYEWE AMEKWAMA KWASABABU WATU HAWATAKI KUSINGIZIWA NA ****** AMBAYE YUKO TAYARI KUKUANGAMIZA WEWE ILI YEYE AONEKANE ANAFANYA KAZI VIZURI .TUMIA AKILI YAKO VIZURI OTHERWISE WEWE NI KAMA MCHEKECHEA AU UNALENGA KUMCHAFUA MAGUFULI ANYEONEKANA ANAFAA KUTEULIWA KUWA MGOMBEA WA URAIS MWAKA 2015
 
wimbo wa mabata madogo madogo umenikumbusha mbaaaaali,enzi za uzalendo na uaminifu uliotukuka..!
 
Maguufuli ndio anatufanya tuamini kwamba kumbe mawaziri nao wanakazi ya kufanya..mwacheni afanye kazi yake kwa uhuru.
 
Chuki binafsi? vp nawe ni mmoja wapo wa Tanesco, Dawasco waliosemwa na Magufuli? Big up Magufuli, akiongea kwenye vikao vyao ss tutajuaje haya, tutazidi kumlaumu Magufuli pale mambo yatapo kwama bila kujua ukweli wa mambo. Tuwe wakweli...
 
CDM nimegundua mnaona wivu,Magufuli ni jembe la CCM mnahofia anaweza kuwa mgombea 2015 mkatoka na mbunge mmoja au wawili tu Tz nzima.Endelea hivyo magufuli kipenzi cha watanzania.
 
Lets call a spade a spade,pa1 na kwamba CCM hopeless lkn kwa upande wake Magufuri anajitahidi sana,hakuna aliyekamilika,hata wwe yamkini u'r worse 1000 times than Magufuli,ila anafanya kazi na anadeserve cridit zake,mbona wapinzani wanakemea na we see em heroes! Media ni sehemu ya kufikisha ujumbe kwa wananchi,ile barabara sio yake ila ni yawalipa kodi Watanzania. Mbona ripoti ya CAG Wizara ya magufuli iko poa! Big up Magufuri
 
Naona upo sahihi, lakini nahisi unaprejudice na Magufuli ambazo zinakusukuma kuichukia kazi yake ya haki. Magufuli si malaika, lakini wote ni mashahidi kwamba Magufuli anafanya kazi nzuri na isio acha maswali.

Unapomtukana huyu mzee kwa kusimamia kwa nguvu utekelezaji wa malengo yake kwa manufaa ya umma unanifnya masikio kope ziwashe ninapokusoma.

Kuchukia watu wanaosimamia kazi na kutekeleza majukumu yao kwa bidii ni kitu cha kawaida Tanzania. Hata huku maofisini, ukifanya kazi zako kwa bidii, utaambiwa unajipendekeza, na utachukiwa. Ukitaka watu wakupendeze we fanya uzembe, masyala na ufisadi kazini ndo utaonekana mtu wa maana wakati hovyo.

Magesa, jipime na ikiwezekana u-edit thread yako. Usipo fanya hivyo utaaibika kwani Maguli si muda mrefu atakuthibitishia kwamba he is the of the leader needed by Tanzanians.

Safi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Kaka mwambie huyo Magesa akawaambie na wajinga wenzake waliomtuma akidhani tutamuunga mkono. Magufuli Ni MTAMBO WA SHGHULI HAHITAJI HISANI WALA HURUMA BALI HAKI TUPU LONG LIVE OPERATION COMMANDER DR JOHN POMBE MAGUFULI.
 
Magufuli is the best wanaompiga wote ni mafisadi msije mka mmwakyembe ndio zenu mkishindwa hoja mnakwenda kwenye cosanostra:angry:
 
Hao wanaosema magufuli ana visasi wao ndio wenye visasi tena wazi ..magufuli ni waziri anaefata sheria na katiba ya nchi...mie natokea kijijin sana musoma vijijin,,lakin wanchi wanamkubali magufuli zaidi ya mtu yeyote katika serikali ya tz..so mr.Magesa acha kufikir kwa kutumia Masaburi na achana na majungu ya jamaa zako wanasiasa wenye wivu km wewe hauna wivu
 
kweli nimeamini bora umasikini wa mali kuliko umasikini wa kichwani.
hapo ndipo wakenya na sisi tunapotofautiana
 
Pamoja na John Obhwarwa Magufuli kuonekana kama waziri pekee wa ccm mchapakazi,lakini kuna kitu kinachomfanya uchapakazi wake uonekane sio lolote.kitu hicho ni dharau.huyu bwana ana dharau ya hali ya juu.sijui kwa kuwa amekuwa waziri kwa muda mrefu sana takribani miaka 17 au sijui kwa kuwa tunamsifu sana ndo maana anakuwa hivi sipati jibu.juzi wakati naangalia TB-CCM1 wakati huyu bwana akitembelea barabara zinazojengwa dar alikaripia vikali mamlaka zingine za serikali zinazokwamisha ujenzi huo zikiwemo tanesco na dawasco.akamwagiza mfugale afuatilie mamlaka hizo na kama wakisuasua ataonana na mawaziri wa mashirika hayo..na kama hiyo haitoshi akasema kama mawaziri hao pia watasuasua ataenda kwa JK moja kwa moja kuwashtakia...lol!!niliduwaa!!

haya ni mambo ya kuongelea hukoo kwenye vikao vyao vya ndani (inter-ministrial meetings) sio kwenye vyombo vya habari bwana magufuli.sasa kama kuna waziri mhusika alikuwa anaangalia taarifa ile ya habari unadhani atakupa ushirikiano?atakukwepa tu.mimi nadhani this is too much for magufuli.anaropoka tu hadharani.hana busara hata kidogo.pamoja na uchapa kazi wake lakini bila busara ktk kutekeleza majukumu yake ni kazi bure. ndio kuna mambo ya sheria zaidi,lakini kuna mengine hayahusu sheria.atulize jazba.achape kazi.lakini pia kuna kitu najiuliza,kuugua kwa huyu bwana malaria ya mara kwa mara ndo yamemfanya hivi?yamechukua sehemu ya ufahamu wake?mi nadhani akili zake zimezidi sana kiasi kwamba anaonekana kuchanganyikiwa...

Apumzike sasa.aachie wengine waongoze.pamoja na uchapa kazi wake lakini hafai kuwa kiongozi.

Bora kama amewaamsha usingizini,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom