Magufuli ametumbua watanzania wote!

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,771
7,138
Wana JF,

Heshima kwake Mh. Rais D.K. John pombe Magufuri kwa kazi tuliokupa ya kuiongoza tanzania, na baada ya kupewa mkuki kama ishara ya kuilinda nchi yako, hakika umeilinda ipasavyo kiasi kwamba watanzania ambao walikuwa wakichekelea kutumbuliwa kwa waliojifanya kuwa juu ya sheria kwa kutafuna fedha za walala pwii , sasa kibao kimegeuka kwani tumijikuta watanzania tumetumbuliwa wote. Hii tumbua itarudisha heshima ya kazi, itaondoa omba omba, heshima ya fedha isharudi, siku hizi kukopeshana , kuazimana fedha hakuna, mtu anagoma kwani anaona mwelekeo wa kumpa pesa wakati mashimo yote ya panya yamezibwa kwa simenti kali hakupi, wale waliozoea kulewa mpaka saa nane , hakuna tena, baa sasa zimeanza kufunga mapema tu.

Magufuri tayari tushanyoooka sasa, umetutumbua vilivyo, basi rejea kutujenga afya kwani tulishaathirika na ulevi, madawa, sasa tunanyemelewa na magonjwa ya lishe, Mheshimiwa basi hamlisha wakuu wa mikoa wafukunyue wale wote wanaoficha vyakula kwenye magodowni ili wavipandishe mara tatu. Ni kweli umekomesha sukari holela , nao basi wabane wazalishaji wa ndani waongeze kilimo hiki cha miwa sukari iwe nyingi badala ya pombe tunywe chai.

Tayari SBL Serengeti imeshaliona hilo, imepunguza Priziner imara kama Yanga ali maarufu kama (UKAWA) kutoka tshs 2300/= kwenda 1500/= angalau wale wa castal wanaweza kusave mkate kwa buku na mia mbili inayobaki, Tayari Pepsi imepunguza mia 2 angalau tunajipoza koo.
Hili la mafuta ya petrol umeliona, bado la nauli, bado mabasi yako mwendo kasi yamewekewa tail fupi hayawezi kutembea mpaka ufike janguani. Mheshimiwa rais. kwakweli ugali na dagaa umetuumiza kinywa kwani maharage siku hizi kuyapata ni sherehe.
 
Duu!!!. Huyu ndiye Magu aka Tingatinga. Wote kimya hapa ni mwendo wa kusoma namba ya Kirumi si mchezo. Watz tutanyoka tu.

Kuzungusha meza itabaki historia, Magu amefanya ndoa za watu ziimalike maana michepuko sio deal tena, kumwaga pesa kwenye harambee kanisani imekuwa historia. Tips kwa bar maid hakuna tena.

Nidhamu ya fedha naiona inakuja kwa mbali!!!.

Viva Magufuli!!!
 
Back
Top Bottom