Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,691
- 149,915
Gazeti la Nipashe la jana tarehe 01/04/2016, liliripoti kuwa,kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ibara ya 43-(2), mshahara wa Raisi na malipo mengine anayopata hayawezi kushushwa wakati Raisi anapokuwa madarakani.
- Sasa kama hali ndio hio na mshahara wa Raisi kwa mujibu wa Katiba(katiba haitaji mshahara wa Raisi bali inatoa mashariti ya kupatikana/kubadilisha mshahara wa raisi,mashariti ambayo sidhani kama Raisi Magufuli ameyafuata katika kushusha mshahara wake) ni huu wa milioni 34 aliouacha Jk,hii si ina maana kuwa kikatiba mshahara wa Raisi mpaka sasa bado ni huo wa milioni 34?
- Maana kama Katiba haijabadilishwa ila ni Raisi Magufuli tu kwa mapenzi yake ndio ameamua kupunguza mshahara wake, hii si ina maana mshahara wa Raisi unaotambulika Kikatiba bado ni huo wa milionin 34?
- Akija Raisi mwingine si anaweza tu kuendelea na huo mshahara wa milioni 34 na akawa yuko sahihi kikatiba?
- Kwa mtazamo wangu ili kweli kushusha mshshara wa raisi kwa mujibu wa katiba na sheria, inabidi Bunge ndio lifanye hiyo kazi kwani ndio lina mamlaka hayo kwa mujibu wa Katiba ibara 43-(1).