Magufuli amefuta usemi wa 'Tatizo ni Mfumo'

1468007333465.jpg
 
Thibitisha mawazo yako kwa data mkuu..kumbuka kuwa kwa watanzania waliopo wengi wao ni wanachama wa CCM toka enzi na enzi ingawa hawakuwa ni active politicians!
Ndo maana nchi yetu imedumaa,niambie vision ya nchi yetu ni ipi?Nchi inapata viongozi wake kwa kutegemea fikra za mtu mmoja,utaratibu huu wale tunaoenda kuwaomba misaada kila siku wameshauacha maana hauna tija,sisi hata tukisema tukopy tunacopy ujinga mazuri tunayaacha,si unakumbuka kuna mheshimiwa alienda uingereza zuri pekee aliloliona huko ni bunge lao kutokuoneshwa live,nchi itafika wapi kwa mambo haya? Nchi yenye watu wa akili za aina ya akina jingalao ndio wanaamini wachina watakuja kujenga viwanda nchini mwao ili kumaliza au kupunguza tatizo la ajira nchini kwao,kwamba china wao hawana tatizo la ajira ndo maana wanakuja kutusaidia na sisi.any way nisamehe bure kujadiriana na wewe ni kujishushia hadhi yangu bure
 
Kwa hiyo tatizo ni katiba?sio mfumo?
Hii ni ajenda ya kipekee
jingalao? Kwani kwako wewe mfumo au system ni nin?wewe ungekuwa ndugu yangu ningekuwa nimeshakuwekea sumu kwenye chakula maana inaonekana huna faida kabisa
 
Wasalaam!

Kuna msemo maarufu hapa JF wa CCM ni ile ile wakimaanisha kuwa mfumo wa serikali na utendaji wake utabaki kuwa ule ule despite kwamba kuna Rais mpya aliyeingia madarakani tena kwa sera ambazo mwanzoni wapinzani walizisema kuwa ni sera zao.

Wengi wa wadau hasa hasa wa upinzani waliamini na kutuaminisha kuwa Magufuli ni sehemu ya mfumo uliokuwepo na angeendelea kuuabudu na kuutumia mfumo ule ule.

Hivi karibuni tumeshuhudua utumbuaji majipu ambao kwa sasa umeenda hatua ya pili na kuitwa uteuzi.

Tumeshuhudia mabadiliko makubwa haswa katika kutemwa kwa watendaji au waliokuwa na vyeo kuachwa na uteuliwa wapya kwa wingi wa zaidi ya asilimia 70.

Kwa maoni yangu ni wazi kuwa kile kilichoitwa mfumo au CCM ile ile kimemalizwa rasmi kwa utumbuaji uliokithiri na uteuzi mpya uliofanyika.

Swali langu linarudi kwetu wanaJF je bado tunahisi tatizo litakuwa ni mfumo au CCM ni ile ile? Au sasa msimamo wetu utabadilika na kuanzisha hoja mpya?
ni mapema mno kusema amefuta mfumo, hebu jiulize amefutaje mfumo wakati utawala wakebumeanza kwa kuwaziba midomo wapinzani? unadhani tutaendelea kusikia maovu ya serikali ya ccm ambayo mengi yaliibuliwa na upinzani mfano hivi tungejua richmond,escrow bila upinzani? sasa kama uzuia mikutano ya upinzan tu unakuwa una ajenda gani ya siri? hivi wananchi wakiaminishwa kuwa unalenga kuficha maovu na udhaifu wako utakataa? bunge live ilipigwa marufuku tafakari kwa mapana,
 
Acha upofu wewe. Mabadiliko ya mfumo maana yake ni mabadiliko ya kisheria, taratibu na uwajibikaji katika taasisi mbalimbali za nchi. Si mabadiliko ya watendaji pekee kama unavyotaka kutuaminisha. Na haya yanawezekana tu kupitia mabadiliko ya sheria mama ambayo ni katiba ya nchi.
 
Wasalaam!

Kuna msemo maarufu hapa JF wa CCM ni ile ile wakimaanisha kuwa mfumo wa serikali na utendaji wake utabaki kuwa ule ule despite kwamba kuna Rais mpya aliyeingia madarakani tena kwa sera ambazo mwanzoni wapinzani walizisema kuwa ni sera zao.

Wengi wa wadau hasa hasa wa upinzani waliamini na kutuaminisha kuwa Magufuli ni sehemu ya mfumo uliokuwepo na angeendelea kuuabudu na kuutumia mfumo ule ule.

Hivi karibuni tumeshuhudua utumbuaji majipu ambao kwa sasa umeenda hatua ya pili na kuitwa uteuzi.

Tumeshuhudia mabadiliko makubwa haswa katika kutemwa kwa watendaji au waliokuwa na vyeo kuachwa na uteuliwa wapya kwa wingi wa zaidi ya asilimia 70.

Kwa maoni yangu ni wazi kuwa kile kilichoitwa mfumo au CCM ile ile kimemalizwa rasmi kwa utumbuaji uliokithiri na uteuzi mpya uliofanyika.

Swali langu linarudi kwetu wanaJF je bado tunahisi tatizo litakuwa ni mfumo au CCM ni ile ile? Au sasa msimamo wetu utabadilika na kuanzisha hoja mpya?
Mfumo au structure maana yake ni muundo. Muundo huo huanishwa kwenye katiba cha chama au serikali husika.

Katika vyama vya siasa tulivyo navyo nchini CCM ndicho chama cha siasa chenye the best and most elaborate structure kuanzia ubalozi wa nyumba kumi kumi hadi ngazi ya taifa, namna viongozi wake wanavyopatikana au kutolewa kwenye uongozi, kanuni, na taratibu za uendeshaji nk nk.

CCM haijabadilisha mfumo / structure yake ambayo ni nzuri sana hivyo lazima iwaambie wafuasi wake kwamba CCM ni ile ile wasidanganyike. Ni ile ile ya tangu enzi za Mwalimu. Lazima ijivune kwamba ni ile ile original, sera zake nzuri ni zile zile haijabadilika.

Sasa vyama vingine vinapolalamika kwamba 'ona CCM ni ile ile' mimi huwa nawashangaa. Kumbe wao siyo wale wale wa mwaka jana? Yaani CDM ya mwaka huu siye ile ya mwaka jana? Wamebadilisha lini muundo / mfumo wao na kwa idhini ya nani?

Mfumo wa serikali ni ule ule wa mwaka 1977. Tulitaka kuubadilisha kwa kutengeneza katiba mpya, wapinzani wakaweka ngumu. Kwa hiyo serikali ni ile ile na CCM ni ile ile. Nadhani hata CDM na CUF ni wale wale.
 
Yes, bado ukweli utabaki hivyo. JPM amefumua timu ya JK, anajenga yake. Na utaratibu ni ule ule tu, wala hakuna kilichobadilika. Hata uteuzi umefuata misingi ile ile, ni sura pekee ndizo zimebadilishwa.

hata mzee wenu angechukua nchi mambo yangekuwa ni yaleyale.
 
90% ya wanaosema tatizo ni mfumo wamekaririshwa,ukiwauliza mfumo ni nini hawajui cha zaidi watakwambia ni katiba ya Warioba.
Ukiwa bavicha shida sana
 
Wasalaam!

Kuna msemo maarufu hapa JF wa CCM ni ile ile wakimaanisha kuwa mfumo wa serikali na utendaji wake utabaki kuwa ule ule despite kwamba kuna Rais mpya aliyeingia madarakani tena kwa sera ambazo mwanzoni wapinzani walizisema kuwa ni sera zao.

Wengi wa wadau hasa hasa wa upinzani waliamini na kutuaminisha kuwa Magufuli ni sehemu ya mfumo uliokuwepo na angeendelea kuuabudu na kuutumia mfumo ule ule.

Hivi karibuni tumeshuhudua utumbuaji majipu ambao kwa sasa umeenda hatua ya pili na kuitwa uteuzi.

Tumeshuhudia mabadiliko makubwa haswa katika kutemwa kwa watendaji au waliokuwa na vyeo kuachwa na uteuliwa wapya kwa wingi wa zaidi ya asilimia 70.

Kwa maoni yangu ni wazi kuwa kile kilichoitwa mfumo au CCM ile ile kimemalizwa rasmi kwa utumbuaji uliokithiri na uteuzi mpya uliofanyika.

Swali langu linarudi kwetu wanaJF je bado tunahisi tatizo litakuwa ni mfumo au CCM ni ile ile? Au sasa msimamo wetu utabadilika na kuanzisha hoja mpya?
Mfumo umeanza kunyooka. Wanajf kwa sasa tutoe ushauri wa kuboresha tu. Mambo ya kulaumu tuache. Pia tutoe taarifa za majipu na wakwepa kodi na nchi ya neema ileee!
 
Thibitisha mawazo yako kwa data mkuu..kumbuka kuwa kwa watanzania waliopo wengi wao ni wanachama wa CCM toka enzi na enzi ingawa hawakuwa ni active politicians!
Ujinga mtupu, ujinga mzigo. Toka lini Watanzania wengi wakawa wanachama wa vyama vya siasa? Unajua maana ya kuwa mwanachama wa chama cha siasa? Tatizo lenu malimbukeni hamjui tofauti kati ya chama na serikali. Kwa akili zenu fupi mngependa kuona wafanya kazi wote serikalini ni wana CCM, siyo? Na bila shaka haingeishia serikalini tu, mngependa wafanya kazi wote wa mashirika ya Umma wawe wana CCM, siyo?

Je unajua kwa nini akili zenu zinawatuma hivyo? Ni mfumo uliotengenezwa na CCM na katu si mtu. Imefikia hadi kwa vyombo vya Usalama, vimeaminishwa kwamba kazi yao kubwa ni kukilinda chama tawala, viongozi wake na wanachama wake. Utadhani mzalendo pekee wa taifa hili ni mwana CCM na kwamba ukiwa mpinzani wa CCM, huitakii mema nchi yetu. Ngoja nikukumbushe kwamba hata Magufuli ni uzao wa huo mfumo.

Kusema kweli hali kama hii inawezekana tu ndani ya taifa la kinafiki kama Jamhuri ya Tanzania. Wastaarabu wana kitu kinaitwa Katiba ya nchi na katiba haimbagui raia kiitikadi, kikabila, kirangi, kijinsia wala kidini kwani ndiyo sheria mama. Lakini sisi tumejengewa mfumo ambao Katiba si lolote si chochote. Katika mfumo wetu huu itikadi ndiyo inaamua nani ateuliwe kiongozi wa wilaya, mkoa, idara ya serikali na mkuu wa taasisi.

Tofauti na waliomtangulia, Magufuli amefaulu kulinda mfumo kwa silimia 100% kwa kuwagawa Watanzania kiitikadi kiasi kwamba sifa kuu ya teuzi zake ni ukada. Ameenda mbali kwa kuhakikisha kwamba waliokuwa wanalalamikiwa na wananchi au wale waliokataliwa na wananchi anawateua kuwaongoza wananchi wale wale waliowakataa. Ujeuri wa Magufuli katika hili hauna mfano katika historia ya taifa hili.

Amefanikiwa katika kuhakikisha kuwa hoja pinzani hazisikiki ama ndani ya Bunge au nje ya Bunge. Alianza kwa kupiga marufuku Bunge kuonekana live, akaamuru jeshi la polisi kuwakamata wakosoaji wa utawala wake na sasa maDC na maRC, makada aliowateua, wanapigana vikumbo yupi atatoa tamko kali la kupiga marufuku mikutano ya wapinzani. Wakati huo huo Wabunge wa Upinzani wakizidi kufukuzwa Bungeni.

Kila kada aliyeteuliwa ndiye mbabe katika eneo lake; atapiga marufuku, atafukuza, atakamata na kusweka ndani bila kujali Katiba inasemaje, bila kujali taratibu, kanuni na sheria zinasemaje na bila kuzingatia kwamba mhusika ni mwakilishi wa eneo husika aliyechaguliwa na wananchi kuwatumikia. Kwa wana CCM, mfumo huo ndio wanaoufahamu, wamezaliwa humo, wakakulia humo, wakakomaa humo, naam, CM ndio baba na mama.

Hiyo ndio Tanzania, taifa la wadanganyika, wanafiki na walafi.
 
Mfumo, hakuna sababu nyingine. Tunahitaji mfumo ambao kutakuwa na separation of powers, madaraka ya rais yaliyopunguzwa, kuepuka nafasi za teuzi bali kazi zitangazwe na wenye sifa waombe, hatutaki mfumo wa kuteua hadi madas, mfumo wa viongozi wa nchi kuwa na sifa ya kusoma na kuandika...
 
Utumbuaji ni sehemu ndogo tu ktk dhana pana ya mfumo.
Mtumo upo tena mkubwa. Kuja kwake ni kubadili chupa huku ladha ya mvinyo ikibakia ile ile!
 
Yan kuna wachangiaji zaid watatu wametoa tafsr tofaut juu ya neno mfumo. Hii kuoneha kuwa ndugu zetu walikuwa wamemzeshwa.
Ili kuhakikisha hilo kiurahisi tafuta sampuli ya wale wanaotaka kwenda dodoma ku andamana tarehe 23 halafu muulize mmoja mmoja nin maana ya mfumo wliokuwa wanaumaanisha utachoka na majibu yao yanavyokinzana. Halafu hawa jamaa kipindi cha kampeni walituaminisha kwamba mgombea wa ccm c tatizo ila tatizo ni mfumo leo wamekuwa na ugomvi zaid na mgombea huyoo kumuita majina ya ajabu wakiaahau kwamba walituambia tatizo siyo yeye ila ni mfumo. IKIWA MUONGO USIWE MSAHAULIFU
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom