Magufuli alitoa amri inayokinzana na sheria? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli alitoa amri inayokinzana na sheria?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 25, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,972
  Trophy Points: 280
  Jumanne Januari 25, 2011
  Makala

  Matuta barabarani yataondoka sheria zikiimarishwa

  Imeandikwa na Judicate R. Shoo; Tarehe: 24th January 2011 @ 23:59


  AMRI iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli ya kuondoa matuta katika barabara nchini, inaweza kutafsiriwa vibaya badala ya kuisifiwa, ikionekana ya uonevu na kwamba serikali haiwatakii usalama watu wake wanaoishi kando kando ya barabara.

  Katika kipindi cha upanuzi wa barabara ya Morogoro kutoka makutano ya Barabara za Sam Nujoma na Mandela eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam, kuwa njia mbili, kulikuweko ‘vuta nikuvute’ kati ya serikali chini ya Waziri Magufuli, na wenye viwanja waliokataa kuvunjiwa nyumba zao kupisha upanuzi huo, wakitaka fidia ya uharibifu wa mali zao, huku serikali ikisimama kidete kuona kuwa uvunjaji huo unakamilika, tena bila fidia!!

  Kimsingi, wananchi walitaka fidia kwa madai ya ujenzi wao kuwa ndani ya mashamba yao, huku serikali ikisema ujenzi ulikiuka sheria ya ujenzi katika hifadhi ya barabara.

  Baada ya zoezi hilo kufaulu, biashara nyingi katika maeneo ya hifadhi, zilifungwa na mpya kutoonekana, huku TANROADS ikielekeza wote waliojenga maeneo ya hifadhi kukaa mkao wa dharura, bila ruhusa ya kuongeza ujenzi wa aina yeyote zaidi ya uliokuweko.

  Serikali pia iliweka mabango – eneo la jiji la Dar es Salaam – na mawe mapya ya mipaka mwisho wa maeneo yote ya hifadhi katika barabara kuu zote, kuimarisha sheria hiyo.

  Lakini mara baada ya Dk. Magufuli kuondolewa katika wizara hiyo, tumeshuhudia madudu ya kila aina, kibaya zaidi wananchi kutambua udhaifu uliokuweko hata kudiriki kulala barabarani - kufunga barabara kudai kuwekewa matuta - hadi muda wa saa nne bila magari kupita, hadi
  kutimuliwa na mabomu ya polisi.

  Isitoshe, ujenzi holela maeneo ya hifadhi ya barabara kuu, umerudi na kupamba moto kwa kasi ya ajabu, hadi kusababisha migogoro baina ya wavamizi wa maeneo ya hifadhi na
  TANROADS.

  Mfano, mgogoro wa mamlaka moja ya serikali ya mtaa katika maeneo ya Kimara/Temboni, uliozuka baada ya TANROADS kusimamisha ujenzi wa ofisi za serikali hiyo katika hifadhi ya barabara.

  Licha ya kasi ya uvamizi ilio kuweko na kupelekea sekeseke la Temboni, ufumbuzi ulifikiwa kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka jana, ambapo licha ya ujenzi wa visehemu vya biashara, kasi ya ujenzi wa vizimba vya matawi ya wakereketwa umepamba moto huku uchukuaji sheria mkononi huo ukihalalishwa kwa upandishaji bendera za chama— kwanza kwenye sehemu ya ofisi ya mtendaji mtaa ambayo ujenzi wake ulisimamishwa na kwenye mashina ya wakereketwa.

  Ili kuondoa kadhia ya watu kulala barabarani, kudai matuta serikali iimarishe sheria kuzuia shughuli zote za kibinadamu katika hifadhi ya barabara. Na utekelezaji wake ufanywe misili ya operesheni ili kusiweko baadhi ya viongozi wa TANROADS watakaorudi nyuma kutaka ‘chochote’ na kuzorotesha utekelezaji wake.

  Zoezi hilo likifaulu, vitongoji vingi vilivyoibuka kando kando ya barabara kuu vitakufa na watu
  watakuwa na nidhamu ya matumizi ya barabara kwa kuvuka katika maeneo ya waenda kwa miguu – zebra crossing—kwenda kwenye makazi yao au maeneo ya biashara nje ya maeneo ya hifadhi ya barabara.

  Wakazi wa Kimara/Stop Over, Suca, Temboni, Mbezi na maeneo mengineyo ni mashahidi wa biashara za kibabe – hasa maeneo ya Mbezi- Mwisho, ambako baadhi ya wachuuzi hupanga bidhaa zao kukaribia katikati ya barabara kuu ya Dar- Morogoro.

  Na ubabe huu wa wachuuzi, na ufumbiaji macho ukiukwaji sheria wa TANROADS, ulishaleta maafa makubwa hapo Mbezi, hata baadhi ya wachuuzi kupoteza maisha.

  Ni Tanzania, na hasa katika jiji la Dar es Salaam, ndiko kumejaa uozo huu wa kutojali utekelezaji wa sheria ya matumizi ya hifadhi ya barabara kwa manufaa binafsi, kiasi cha serikali ya mtaa kudiriki kuwa na haki ya kuvunja sheria ya serikali kuu ya kujenga ofisi ndani ya hifadhi ya barabara.

  Wakati umefika maeneo yote ya hifadhi ya barabara kusafishwa, ambapo kwa kufanya hivyo kutazuia vioski kuendelea kuota usiku na mchana (mithili ya uyoga) kando kando ya barabara; na badala yake vijengwe mbali na barabara.

  Kwa kufanikisha hilo, TANROADS haitakuwa tena hatiani, kusababisha watu kulala barabarani kudai ujenzi wa matuta, bali mandhari ya barabara zetu yatapendeza, na wageni watakapokuwa wanaingia au kutoka katika miji na majiji yetu, wataona fahari kubwa.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,972
  Trophy Points: 280
  Is Magufuli indispensable.................Is the author suggesting without magufuli the nation is doomed?

  Well give us a break.....................before and after Magufuli the nation will thrive on...................
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,972
  Trophy Points: 280
  Nionavyo mimi matuta barabarani ni haki ya kimsingi ya kumlinda mwanadamu dhidi ya uendeshaji holela uliokithiri hapa nchini.............na kuhatarisha maisha ya mwanadamu...............................
   
Loading...