Magufuli alitakiwa kumteua Damus katika safu ya uongozi wake kuongoza nchi hii

Giro

JF-Expert Member
Feb 9, 2009
359
24
Maswali haya pamoja na mengine mengi, yanavuta hisia zangu kufanya nipende kupitia na kuchambua utabiri wa mnajimu mashuhuri wa Ufaransa, Nostra Damus

Utabiri wa Nostra Damus juu ya mambo ya kimataifa ulianzia na nchi yake, Ufaransa. Alitabiri mapinduzi ya Ufaransa ya 1789.

Serikali ya Ufaransa tangu utawala wa Mfalme Louis wa XVI, ilijengeka juu ya mhimili wa udikteta wa kifalme (absolute monarch). Licha ya kuenea kwa mawazo mapya ya kimapinduzi yaliyopendwa na wengi juu ya kupunguzwa kwa mamlaka ya watawala kwa njia ya mgawanyo wa madaraka, haki za asili na utawala kwa misingi ya utashi wa walio wengi, mfalme aliendelea kuwa mhimili wa madaraka yote na asiyehojika.

Kama walivyokuwa wafalme Belshaza wa Babeli na Julius Kaizari wa Roma ya kale, mfalme Louis alilewa madaraka kiasi cha kujiona kuwa mtu asiyeweza kutishwa wala kuguswa na kitu chochote chini ya mbingu. Mfalme huyo alizoea kusema "mimi ndiye taifa la Ufaransa na taifa ndilo mimi."

Udikteta huo ulizua manung`uniko katika jamii yake, hasa kutoka kwa wanyonge juu ya haki za msingi za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria, hali iliyojenga chuki kubwa dhidi ya tabaka la watawala.

Nostra Damus zaidi ya miaka 160 kabla ya mapinduzi ya 1789 alitabiri uasi dhidi ya mfalme kwa sababu hizo akisema: "Mume (mfalme) akiwa mwenye huzuni pekee atatawazwa na kuondolewa. Mgogoro utaanzia kwenye kiwanda cha vigae na watu 500. Muasi mmoja atavikwa taji.

Huu ulikuwa utabiri sahihi na wa kweli kwani maasi ya 1789 dhidi ya utawala wa Mfalme Louis wa XVI yalianza na walala hoi 515 kwenye kiwanda cha kutengeneza vigae na matofali. Na mapinduzi yalipoanza, yalikuwa mapinduzi ya wanyonge dhidi ya marupurupu ya watawala.

Na pale Mfalme Louis alipoita jeshi kwa ushauri wa mkewe, mama Marie Antoniette kuwatawanya walala hoi waliozingira majengo ya bunge, ni Count Mirrebeau (muasi), msemaji wa walala hoi aliyeunguruma akisema: "Tupo hapa kwa ridhaa ya watu, hatuondoki hata kama ni kwa mtutu wa bunduki mpaka hapo tutakapoipatia ufaransa katiba yake halali."

Mfalme Louis alisalimu amri kwa madai ya wanyonge na kufungua njia ya mapinduzi ya taifa hilo.
 
Wale wa upande wetu kuja kuelewa kilichoandikwa humu it will take some hours.
 
Madaraka ya Rais katika nchi yetu ni makubwa mno, kiasi kwamba, hauwezi kutofautisha kati ya Rais na Mfalme.
Katiba mpya ije (ile ya Warioba), ili nchi iongozwe kwa Mamlaka kamili ya watu.
 
hakuna marefu yasiyo na ncha, mbadala wa ccm uko ktk generation hii hii either from within or outside.. si kwa kumwaga damu kama Wafaransa na bisu la guillotine la hasha bali kwa demokrasia hij hii inayominywa kila uchao.. time will tell #2020anotherchance
 
Katiba yetu imefanya raisi kuwa na kinga kuliko malaika tumeona mifano ya maraisi waliopita tena wengine wakijuta hadharani kwa maamuzi waliyo yafanya kipindi cha uongozi wao.

Katiba ya nchi hii inajenga matabaka ubinafsi mwingi ndani ya jamii nakufanya atakaye pata anafaidika yeye na familia yake kwa rasilimali za watanzania wote lazima kuwe na mabaadiliko ya dhati sio mabadiliko ndani ya chama kimoja.
 
hakuna haki inayoletwa mezani mtu akapewa kama chakula labda kwa busara za allah..
 
Back
Top Bottom