Magufuli alipunguza mishahara mikubwa ili wagawiwe wenye mishahara midogo?

Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,987
3,450
Hii kiki ilitrend sana,kwamba haiwezekani mtu mmoja analipwa mil 30 huku mwingine analipwa 150,000!Akasemq atapunguza hiyo mil 30 na kuigawa ili kuwaongezea hawa wa chini!!Watu wakashangilia kama kawaida halafu baada ya muda wanasahau!

Vipi jamani, ni muda sasa umepita kimya! Hatusikii chochote juu ya hilo! Kuna mtu kapunguzwa mshahara? Kuna mtu kaongezwa mshahara? Annual increment yenyewe ni mgogoro, tokea jamaa ameingia hakuna mfanyakazi amepanda ngazi au kupata ongezeko la kila mwaka la mshahara ambali lipo kisheria!

Ngosha vipi?Wale washangiliaji mpo?
 
Msiwe na wasiwasi...

Pesa iliyotokana na watu kuwapunguzia mishahara tumeipeleka kwenye ujenzi wa Chato International Airport!!

Pesa ambayo ingetumika kuongeza mishahara, kupandisha watumishi madaraja na hatimae kuajiri watumishi wapya; hiyo tumeipeleka kwenye Bombardiers & Boeing!!

In fact, tupo mbali sana kufikia malengo, kwahiyo wazalendo tunawaomba mvute subira... mambo mazuri hayahitaji haraka!

Sema AMEEEEN!
 
Ni Kweli inauma sana aisee alituahidi watumishi wanaolipwa mishahara ya chini watalipwa mishahara inayopunguza ukali wa maisha.lakini hakuna chochote hadi Leo Maanake nini hatuelewi watumishi vipi! viongozi wa vyama vya wafanyakazi VIP!? Yani ni mbaya sana kubaguliwa sisi watumishi wa umma.
 
Waungwana
Kwanza naomba tuvumiliane
Tunajua yote mnayopitia ndugu zetu Watumishi
...kuhusu kupunguza kiwango cha juu cha mshahara hilo tumetekeleza hadi 15M.
Kwa sasa mvumilie wakati tunaweka sawa mambo
Ni matarajio yetu mda si mrefu mtaona Matunda yake
 
Atawale milele
 
Anayeziamini ahadi za Mr.Makinikia kwa siku hizi huyo ni pungu-two.
Kwa hakika mtumishi kama unaweza kujiongezea kipato hapo kazini ni bora ujiongezee kwa njia uipendayo.
Kwakuwa wananchi wa kawaida ni wengi kuliko watumishi wa umma na wengi ameshawateka kwa maigizo feki yamakinikia na wafanyakazi hewa basi kawateka akili wanaomba aongezewe muda.
Hapa watumishi wa umma tusahau ashawapata wa kumpa kura 2020 .
 
Subirini 2020 mtakapopewa mshahara mara mbili.
Ila sahivi endeleeni kusota.
 
Waungwana
Kwanza naomba tuvumiliane
Tunajua yote mnayopitia ndugu zetu Watumishi
...kuhusu kupunguza kiwango cha juu cha mshahara hilo tumetekeleza hadi 15M.
Kwa sasa mvumilie wakati tunaweka sawa mambo
Ni matarajio yetu mda si mrefu mtaona Matunda yake
Umeandika kama kiongozi wa serikali hii.
Kama kweli ni kiongozi wa hii serikali naomba utolee ufanunuzi wa mambo yafuatayo

1/ Kwa nini mliongeza 15% ya makato ya mishahara kinyume na mkataba? ili hali mnajua kabisa mishahara ya wafanyakazi ni modogo sana hasa walimu.

2/ kwa nini mmezuia hata lile ongezeko la mshahara la kila mwaka , ambalo lipo pale kisheria wala halihitaji mjadala.

3/ Ni lini wafanyakazi wataongezewa mshahara pamoja na kupandishwa vyeo?

Nasubiri maelezo yako mkuu.
 
hakuna chochote zaidi ya blah blah. watumishi wenyewe wamechoka balaa hawajaongezewa hata senti. nashangaa watu wanaandaa maandamano feki ya kumpongeza....
 
Hii kiki ilitrend sana,kwamba haiwezekani mtu mmoja analipwa mil 30 huku mwingine analipwa 150,000!Akasemq atapunguza hiyo mil 30 na kuigawa ili kuwaongezea hawa wa chini!!Watu wakashangilia kama kawaida halafu baada ya muda wanasahau!

Vipi jamani, ni muda sasa umepita kimya! Hatusikii chochote juu ya hilo! Kuna mtu kapunguzwa mshahara? Kuna mtu kaongezwa mshahara? Annual increment yenyewe ni mgogoro, tokea jamaa ameingia hakuna mfanyakazi amepanda ngazi au kupata ongezeko la kila mwaka la mshahara ambali lipo kisheria!

Ngosha vipi?Wale washangiliaji mpo?
Hiyo mishahara mikubwa aliyopunguza hizo hela kwa akili yako zingelipa nyongeza kwa wafanyakazi wa chini senti ngapi kwa kila mmoja? Si mtumiage hata akili zenu kidogo? Hizo hela zitakuwa zimekununulia ARV na vitu vingine.
 
Msiwe na wasiwasi...

Pesa iliyotokana na watu kuwapunguzia mishahara tumeipeleka kwenye ujenzi wa Chato International Airport!!

Pesa ambayo ingetumika kuongeza mishahara, kupandisha watumishi madaraja na hatimae kuajiri watumishi wapya; hiyo tumeipeleka kwenye Bombardiers & Boeing!!

In fact, tupo mbali sana kufikia malengo, kwahiyo wazalendo tunawaomba mvute subira... mambo mazuri hayahitaji haraka!

Sema AMEEEEN!
Amen mkuu
 
rais anaweza kuamua jambo kwa kauli tu...ni kweli.
lakin suala la kupunguza mishahara ya watumishi haliwezi kufanyika kwa kauli moja tu (ya rais)
hii ni ishu ya kisheria, mshahara haupandishwi kwa matamko na wala haupunguzwi kwa matamko...ni lazima sheria ibadilishwe kwanza ili jambo hilo lifanyike.

sasa tujiulize, lini bunge lilirekebisha hiyo sheria???

hata ile ishu ya kusema anajipunguzia mshahara, halipo. maana katiba inasema (kifungu sikumbuki) "..raisi hatopunguziwa mshahara na malipo yake mengine kwa muda wote ataokuwa madarakani. na hakuna sheria ya kubadili hiyo.."
wafuatiliaji wa katiba wataleta hiyo article
 
Hiki ulichokisema mkuu ni kweli kabisa. Haya mambo yote ni ya kisheria.

Lakini mara ngapi tumeona katika awamu hii sheria zinakiukwa mchana kweupe?

Mara ngapi katiba imevunjwa mchana wa jua kali?

Kwa awamu hii lolote laweza kufanywa kinyume kabisa na sheria na bado watanzania wakashangilia tu.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom