Magufuli alimlenga nani kusema "hata Obama yuko kimya, haongei ongei"

Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,987
3,450
Hiyo nimeisikia akiwa anazungumza na viongozi wastaafu!Anasema hata huko duniani wanamuacha Rais anaongoza anavyotaka,kwamba atakuja kuhukumiwa baadae!

Akatolea mfano Obama,kwamba yuko kimya kamuacha Trump aongoze kivyake!

Kauli hizi zimenishtua sana,kwamba JPM anataka aachiwe nchi aongoze kivyake,daaaah kwani nchi ni Mali ya familia?

Na je,alilengwa nani kwa mfano ule wa Obama?Au ni yule aliyeingia mitini mwaliko wa wazee ikulu?
 
Huyu jamaa haelewi anaenda au anarudi.

Mkapa alishasema wastaafu wasisumbuliwe, mpaka kwenye mambo makubwa.

Yeye mwenyewe anawatekenya, anawaomba ushauri, halafu wakicheka anawasema vibaya.

Haeleweki kama anataka kuachiwa nchi aiendeshe anavyotaka, au anataka ushauri wa wastaafu!
 
Huyu jamaahaelewi anaenda au anarudi.

Mkapa alishasema wastaafu wasisumbuliwe, mpaka kwenye mambo makubwa.

Yeye mwenyewe anawatekenya, anawaomba ushauri, halafu wakicheka anawasema vibaya.

Haeleweki kama anataka kuachiwa nchi aiendeshe anavyotaka,au anataka ushauri wa wstaafu!
Yaani hata Mimi nimeshindwa kumuelewa!
 
Hiyo nimeisikia akiwa anazungumza na viongozi wastaafu!Anasema hata huko duniani wanamuacha Rais anaongoza anavyotaka,kwamba atakuja kuhukumiwa baadae!
Akatolea mfano Obama,kwamba yuko kimya kamuacha Trump aongoze kivyake!

Kauli hizi zimenishtua sana,kwamba JPM anataka aachiwe nchi aongoze kivyake,daaaah kwani nchi ni Mali ya familia?

Na je,alilengwa nani kwa mfano ule wa Obama?Au ni yule aliyeingia mitini mwaliko wa wazee ikulu?

ebo, kwani humfahamu Obama na Trump! sasa wewe unataka amlenge nani? ok, ...alikulenga ww basi, umerizika?
 
Kama anaongoza familia yake ya kina mama Jesca hatuwezi muuliza kitu......

Na anaweza iongoza hiyo familia yake atakavyo

Lakini kama anaongoza Taifa la Tanzania la watu zaidi ya milioni 55, ni lazima tukosoe pale tunapoona haaendi vizuri
 
Sio kosa lako,uko kwenye lile kundi walilolitaja Twaweza!
kundi langu nalijuwa mimi mwenyewe sihitaji kuambiwa na mtu, kawaambie hao wasiojijua kundi lao!Huhitaji akili ya ziada kujua alichokua anaongelea mh. rais wetu! Usimuwekee maneno yako kwa kujidai unajua saana...kumbe upuuzi tu!
 
Haya yanaitwa mahaba Niue!
 
Huyu jamaa anachekesha sana.

Anataka aongoze anavyotaka hata akikosea asiambiwe chochote.

Tumsubirie mpaka amalize ndo tuanze kuuliza au kumkosoa wakati anajua kabisa katiba yetu inamkingia kifua rais pindi atokapo madarakani asiguswe kwa lolote.
.
Hovyo sana huyu jamaa.
 
Hiyo nimeisikia akiwa anazungumza na viongozi wastaafu!Anasema hata huko duniani wanamuacha Rais anaongoza anavyotaka,kwamba atakuja kuhukumiwa baadae!
Akatolea mfano Obama,kwamba yuko kimya kamuacha Trump aongoze kivyake!

Kauli hizi zimenishtua sana,kwamba JPM anataka aachiwe nchi aongoze kivyake,daaaah kwani nchi ni Mali ya familia?

Na je,alilengwa nani kwa mfano ule wa Obama?Au ni yule aliyeingia mitini mwaliko wa wazee ikulu?

Tatizo hapa ni kuwa mkuu wa kaya haoni tofauti ya demokrasia inavyoendeshwa huko Marekani na kwetu hapa. Tusimlaumu, pengine huko nyuma hakuona umuhimu wa kujua tofauti. Tujilaumu waTanzania tuliomuingiza ikulu kwa kishindo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom