Magufuli alikuwa sahihi kuhusu mabwawa?

Mwanagenzi

JF-Expert Member
Sep 11, 2006
724
249
Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana, aliyekuwa mgombea wa CCM ambaye kwa sasa ni rais, John Pombe Magufuli aliwahi kutamka kuwa kuna watumishi wa TANESCO kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme ambao hufanya njama kufungulia maji yatoke bwawani na hivyo kufanya mabwawa yasiwe na kina kinachotakiwa, kwa maslahi yao binafsi. Aliahidi kuwashughulikia endapo angefanikiwa kuwa rais.

Alipokuwa akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa mitambo ya umeme wa gesi, Kinyerezi, JPM, kwa mara nyingine aliwaonya watumishi wa kwenye mabwawa kuacha hujuma za kufungulia maji kiasi cha kufanya daima kuwe na upungufu wa maji kwenye mitambo ya kuzalisha umeme licha ya kuwepo kwa mvua za kutosha.

Hivi karibuni, na tumeambiwa ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2007, TANESCO wameamua kuruhusu maji yatoke (Kidatu) kwenye mabwawa kwa kile kilichoelezwa kuwa maji yamekuwa mengi kuliko uwezo wa mabwawa kuhimili maji hayo, kutokana na mvua nyingi.

Je, ni kweli kuwa tangu mwaka 2007 hapajakuwa na mvua nyingi katika maeneo yanayopeleka maji kwenye mabwawa kama mwaka au msimu huu? Kiasi cha mabwawa kuzidiwa na maji na hivyo kulazimika kuyafungulia?
Je, yawezekana ni kweli watumishi waliyaruhusu maji yatoke kama rais alivyodai, kwa kuzingatia makandokando mengi yenye sura ya ufisadi kwenye sekta ya nishati?

Inawezekana watumishi hawa wameogopa kutumbuliwa kama ulivo msemo maarufu kwa sasa hapa mjini?
 
Walikuwa wanaruhusu Maji yatoke ili Mgao upambe Moto watu waitose CCM kumbe mtoto wa kikwere walipolalia ma Engineer ndipo alipoamkia! Aksante Comrade Ndugu Magufuli!
 
wakati akihojiwa na Makwaya wa kipindi cha Je tutafika leo channel 10, mkurugenzi wa Tanesco, amesema, kabla ya kukamilika bomba la gesi kutoka Mtwara Tanesco ilikuwa inazalisha Megawatts 280 za umeme baada ya kukamilika sasa Tanesco inaweza kuzalisha megawatts karibu 700. kipindi cha nyuma mabwawa ya mtera na kidatu walilazimika kuyafunga kutokana na kukosa maji. lakini baada ya kupatikana neema ya mvua sasa mabwawa yote yanafanya kazi vizuri.
sasa kutokana na maelezo ya mkurugenzi amua mwenyewe kipi ni sahihi! !!
 
Back
Top Bottom