Magufuli alikuwa muongo sana

witnessj

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
24,245
2,000
Unapenda sana haka ka songi inaonekana alikua anakukosha akikaimba....

Hii thread nimecheka sana
Asee acha EVE...yaan kuna kipindi alikuwa huko Mwanza na JK, basi akazungumzia miradi yakee weee....badae ndo akaanza " aliseremaa seremaaa Mwanza seremaaa serema

Yaan anaimba lyric na chorus anajijib mwenyewe asee siku hiyo niliangua kicheko sio cha nchi hii
 

Ahmad Abdurahman

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
2,003
2,000
Kuna siku alienda Kilosa jimbo la Kabudi akaanza kuwananga wanachi kua wanapata shida kwa sababu wanachagua upinzani. Baadae akawauliza jina la mbunge wao...wakajibu "Kabudiiii"...akawauliza tena "Chama gani"....wakajibu "SISIEMUUUUU".

Katika hali isiyotarajiwa akajibu kwa aibu na kujichekesha "Najua anafanya kazi nzuri...naomba mtuamini"
 

Attachments

  • File size
    6.5 MB
    Views
    0

Njilembera

JF-Expert Member
May 10, 2008
1,493
2,000
Kwenye medani ya uongo na uzandiki mbona hana mpinzani huyo. Anapita bila kupingwa wala hafanyi hata kampeni (CV yake inambeba kishenz).

Ndugu mwenyekiti,

Na huu ndio wasifu wa marehemu katika sekta tofauti tofauti alizowahi kusikika nchini, file lake tunaomba iundwe "TUME HURU MAALUM YA MALAIKA WALIO BOBEA KATIKA KUGAWA DOZI" waweze kulipitia tena file kwa umakini; Naomba niwasilishe,


● Marehemu aliwahi kuokota vichwa vya treni.

● Alituambia tuwachange bukoba wahanga wa tetemeko waliovunjiwa nyumba zao. Tukajikaza kiaskari na kujibana watanzania kuwachangia. Waulize kama waliona hata Sh 100 ya ujenzi wa nyumba zao.

● Alituambia kila mwalimu atapewa Laptop. Waulize kama amepewa hata mmoja.

● Alituambia kila kijiji atawapa Millioni 50 kwaajili ya kufanya maendeleo na uchumi. Waulize kama waliiona hio hela.

● Alituambia wafanyakazi sekta za umma/walimu, wataongezewa mishahara na madaraja kabla hajaondoka. Waulize kama wameongezewa hizo nyongeza za mishahara na madaraja (Labda madaraja ya ubungo na mfugale ndio wameyaona).

● Alituambia tutalipwa hela ndefu kwenye fidia ya makinikia. Kila raia noah moja moja. Waulize kama mabeberu walitoa hio hela.

● Alituambia Tanzania tutatoa misaada kwa wazungu, sisi ni "DONA KANTRI". Hakuna cha donna wala sembe, ni mwendo wa hali ngumu mpaka skin tight kupwaya mitaani.

● Alituambia, ATCL inapata faida kwa miaka 5 na akatengeneza sinema za serikali kupewa gawio la faida. CAG akawekwa mambo hadharani kwamba ATCL imeendeshwa kwa hasara ya Sh Billion 60 kwa miaka 5.

● Alituambia, uchumi wa Tanzania unakua kwa zaidi ya Asilimia 7%, uchumi wa kati, ila akatengeneza sheria za katuzuia tusifuatilie takwimu kujua ukweli.

● Alituambia serikali yake kutakua hakuna wizi wala ufisadi, na atakefanya ufisadi wa hela basi zitamtokea tundu lolote. Mbona yeye na kina Ole Sabaaya na Makonda walifisadi nchi na kuiba.

● Kwenye kutupa idadi za samaki, watoto wa samaki pamoja na mayai yao kwenye Ziwa Victoria na Baharini. Wala tusipagusie kabisa, tuache hio issue siku ingine.

● Haya mengine ya bomba la mafuta la kutoka Uganda mpaka Tanga, yanajieleza yenyewe kwenye huu uzi.


Yule mzee sio kabisa. Siku alivyofukiwa mpaka malaika watoa kichapo waliokua likizo, ilibidi waitwe kazini kwa dharura kumpokea.

NASEMA UONGO NDUGU ZANGUUUUUUU!!! MSEMA KWERI NI MPENZI WA MUNGU!!!!
Duh! Sasa na wakati mwingine uache tu kumchambua Marehemu! Huu uchambuzi fikirisha sana- umefanya kazi nzuri,ila mwache apumzike popote alipo! Imetosha!
 

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,933
2,000
Since Mkapa hadi mwendazake, mishahara ya wafanyakazi wa serikali imekua ikilipwa on time, hata mimi nilivyo msikia mara ya kwanza nilistuka sana. Eti hata ndege tulikua tunapanda kwa milioni; hivi kuna shirika la ndege lilikua na ndege za bei nafuu kuizidi FastJet!? Nimewahi kusafiri Dar to Mwanza, go and return kwa Tsh 85k tu, halafu mwamba alivyokua anaielezea ATCL, khaa. Anyway, maisha ya mwanadamu ni mafupi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom