Magufuli alikoroga, Maandamano makubwa kumpinga leo

ina maana hao wabunge pamoja na hao wanaotaka kuandamana wanaamini hiyo sh 100 ambayo imekuwa ikilipwa kwa miaka nenda rudi pale kivukoni ndio iliyoiwezesha serikali kuweza kuboresha huduma pale kwa kununua kile kivuko kikubwa?sasa kwa nini kuambiwa wachangie kidogo gharama za uendeshaji iwe iwe nongwa?wabongo tupunguze stress za maisha kuna mambo kama tunaendelea kuishi hayakwepeki...
 
  • Thanks
Reactions: FJM
keshajiharibia tayari

Ngoja tusubiri kuona kama ataendeleza ubabe au atajirudi na kutoa kauli ya kwamba kauli yake ya , "watakaoshindwa kulipa nauli mpya ya Sh200 kuvuka Kigamboni ni vyema wakapiga mbizi kuvuka bahari." ilikuwa na mushkeli.
 
Acheni wakomae kwa maandamano kwa vile wananchi waishio Kigamboni pia wana haki ya kujengewa daraja kama ilivyo kwa watanzania wenzao. Serikali imekuwa ikiwaahidi uongo kila unapofika wakati wa kampeni kwamba watajengewa daraja na hela wameshatenga kumbe huwa ni gea za kupatia kura na baada ya hapo kimya!
Suala la wenzao wa vivuko vingine kutozwa zaidi na kutolalamika haliwahusu kwani na wao wana akili ya kupima na kuchukua hatua wakiona ni lazima.
 
Serikali inatakiwa kuweka mfumo wa nauli nafuu ya mwezi kwa wakazi ambao hulazimika kupanda kivuko na usafiri wao mwengine kama pikipiki ama gari.

Iwepo pass maalum kwa abiria wa kudumu
 
Hawana lolote hao waheshimiwa wanatafuta cheap popularity tu kama wana uchungu kweli wananchi kwa nini wasitoe sehemu ya mamilioni yao ya posho kufidia ongezeko hilo?
wabunge hao ni wanafiki kwani ndo vinara wa kupitisha sheria mbovu bungen zenye -ve economic impact kwa mwananchi huyo huyo ambaye leo wanajifanya kumtetea kwa ongezeko la sh.100. Hao hao ndo waunga mikono bajeti za kupand kodi za bidhaa muhimu pamoja na kuunga mikono sheria za misama kodi kwa wawekezaji wakubwa kwa maslai ya chama chao. Huruma iyo ni ya kinafiki! 2me 200/= fare ni reasonable
 
Hivi hapa kigezo kinachotumika ni hali mbaya ya wananchi au ni gharama za uendeshaji wa kivuko? Hao wabunge kama wanawaonea huruma wananchi basi waibane serikali ya ccm iache kusamehe kodi kwenye migodi iliyotapakaa nchi nzima, waibane serikali iache kutumia hovyo mapato yake finyu, wambane raia kikwete aache kuzurura hovyo nchi za watu na kutumia kiasi kikubwa cha fedha ya walipa kodi. Wakitimiza wajibu wao huo, maisha ya wapiga kura wao yataboreka na nauli ya Sh. 200 itakuwa si lolote si chochote. Vibginevyo, namuunga mkono Dr. Pombe Magufuli kwa asilimia 100 na namsihi akaze buti mpaka kieleweke.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
umeandika vizuri,maneno yako yanavutia kuyasoma lakini hujatuambia unadhani nini kifanyike kama mbadala wa kupandisha nauli kufidia gharama za uendeshaji wa kivuko chenyewe na shughuli zinazoendelea pale kivukoni kila siku..

Wabunge wamedai kwamba, "wao wakipewa kazi ya kukusanya nauli pale Kivukoni wanaweza kukusanya twice as much". Sasa Kama wanaweza kukusanya twice as much, na wao wako tayari kuonyesha kwamba kuna uzembe wa kukusanya mapato, kwanini hiyo tenda ya wiki mbili wasipewe ili tujue nani mkweli na nani muongo.

Sometimes hizi tenda za kukusanya ushuru/mapato zina mambo mengi sana ndani yake. Ndio maana zama zile za Ubungo Bus Terminal, Mzee Kingunge alitemeshwa ulaji ivi ivi kwa kuwa wakusanyaji wakati mwingine huwa wanakusanya zaidi kuliko kile wanachoripoti kwamba wamekusanya.

So, kuna options 2, moja, wawape wabunge wasimamie kazi ya kukusanya mapato kwa wiki 2. Mbili, wamuombe Dr. Ndugulile findings za uchunguzi wake ambao ulimuonyesha kwamba around 40% ya makusanyo ya kwenye hicho kivuko hayaendi serikalini huwa yanaishia kwenye mifuko ya watu. Swala la ulaji kwenye hicho kivuko hayajaanza leo, hata Dr. Mwakyembe kuna kipindi alifuatilia na kuhoji, lakini sijui aliishia wapi.

Hoja ya Dr. Pombe Magufuli kwamba vivuko vya mikoani vinatoza nauli kubwa, haina mashiko. Kwenye vivuko vya mikoani abiria ni wachache sana ukilinganisha na abiria wa hapo Kivukoni. Ni nadra kukuta Kivuko cha MV Kigamboni au Alina kinaenda na abiria chini ya 50 au magari 5. Kitu ambacho kwa vivuko vya mikoani ni swala la kawaida sana na hivyo kuwa-charge nauli kubwa ni pamoja na kufidia gharama za kuvusha watu 20 na gari, wakati kivuko kina uwezo wa kubeba magari 10 au zaidi na abiria zaidi ya 100.

Kwa hiyo, nina mashaka kwamba wabunge wanaweza kuwa na hoja kwamba fuko la kukusanyia mapato limeliwa na panya na hivyo some of the ngawiras huwa zinadondoka chini na kuingia kwenye mifuko ya watu binafsi au kutunisha viriba tumbo vya wanaokusanya mapato hayo.
 
Hawana lolote hao waheshimiwa wanatafuta cheap popularity tu kama wana uchungu kweli wananchi kwa nini wasitoe sehemu ya mamilioni yao ya posho kufidia ongezeko hilo?

naomba usilete utani kwenye issue za kitaifa. utanipa ban.
 
DR Magu(mash)fuli jirekebishe,hata unapokabidhi vivuko mikoani umekuwa ukitoa Lugha za kebehi,kejeli na Dharau,Mfano Mzuri ni pale ulipokabidhi kivuko cha MV Ujenzi,ulitoa Lugha mbaya kana kwamba kivuko kimetengenezwa kwa fedha za Ruzuku za CCM,Lugha zako zinawaudhi walio wengi,ni Muda wako wa kuwa Mwangalifu kwa kuchunga Mdomo wako,hasa ukizingatia wewe ndo Fisadi uliye bakiza chembechembe za Imani kwa watanzania walio wavivu wa Kufikiri,najua utapita humu na kusoma hapa....Mungu akutie adabu na akupe ujasiri wa kuijirekebisha
 
Yaani shs 200 tu watu wanallalam ikaaaa

Hacha kuongea pumba kwenye issue za maana,kivuko kimepanda sana bei gari dogo ilikua unavusha kwa sh 800 bila abilia sasa ivi tunavusha kwa 1500 sasa ni ndogo hiyo?guta linavushwa kwa 1300 kwa nini wananchi tusilalamike?
 
Wabunge wamedai kwamba, "wao wakipewa kazi ya kukusanya nauli pale Kivukoni wanaweza kukusanya twice as much". Sasa Kama wanaweza kukusanya twice as much, na wao wako tayari kuonyesha kwamba kuna uzembe wa kukusanya mapato, kwanini hiyo tenda ya wiki mbili wasipewe ili tujue nani mkweli na nani muongo.

Sometimes hizi tenda za kukusanya ushuru/mapato zina mambo mengi sana ndani yake. Ndio maana zama zile za Ubungo Bus Terminal, Mzee Kingunge alitemeshwa ulaji ivi ivi kwa kuwa wakusanyaji wakati mwingine huwa wanakusanya zaidi kuliko kile wanachoripoti kwamba wamekusanya.

So, kuna options 2, moja, wawape wabunge wasimamie kazi ya kukusanya mapato kwa wiki 2. Mbili, wamuombe Dr. Ndugulile findings za uchunguzi wake ambao ulimuonyesha kwamba around 40% ya makusanyo ya kwenye hicho kivuko hayaendi serikalini huwa yanaishia kwenye mifuko ya watu. Swala la ulaji kwenye hicho kivuko hayajaanza leo, hata Dr. Mwakyembe kuna kipindi alifuatilia na kuhoji, lakini sijui aliishia wapi.

Hoja ya Dr. Pombe Magufuli kwamba vivuko vya mikoani vinatoza nauli kubwa, haina mashiko. Kwenye vivuko vya mikoani abiria ni wachache sana ukilinganisha na abiria wa hapo Kivukoni. Ni nadra kukuta Kivuko cha MV Kigamboni au Alina kinaenda na abiria chini ya 50 au magari 5. Kitu ambacho kwa vivuko vya mikoani ni swala la kawaida sana na hivyo kuwa-charge nauli kubwa ni pamoja na kufidia gharama za kuvusha watu 20 na gari, wakati kivuko kina uwezo wa kubeba magari 10 au zaidi na abiria zaidi ya 100.

Kwa hiyo, nina mashaka kwamba wabunge wanaweza kuwa na hoja kwamba fuko la kukusanyia mapato limeliwa na panya na hivyo some of the ngawiras huwa zinadondoka chini na kuingia kwenye mifuko ya watu binafsi au kutunisha viriba tumbo vya wanaokusanya mapato hayo.

sina uhakika sana lakini nadhani wanaotoa tender pale ni watu wa city ambamo wabunge nao wamo kwenye vikao vya halamashauri kama madiwani,naomba kusahihishwa kama kama tender haitolewi na halmashauri ya jiji..magufuli yeye analia na vivuko vyake ambavyo havikununuliwa na jiji na wala hawaujui uchungu wake..vimenunuliwa na serikali kuu na viko chini ya wizara yake!watu wakizama leo pale kwa ubovu wa kivuko atakae takiwa kuwajibika ni yeye bwana pombe,sasa kwanini asichukue tahadhari ya kuwataka mchangie gharama za kukihudumia iko kivuko kinachowasidia nyinyi wenyewe!
 
wabunge hao ni wanafiki kwani ndo vinara wa kupitisha sheria mbovu bungen zenye -ve economic impact kwa mwananchi huyo huyo ambaye leo wanajifanya kumtetea kwa ongezeko la sh.100. Hao hao ndo waunga mikono bajeti za kupand kodi za bidhaa muhimu pamoja na kuunga mikono sheria za misama kodi kwa wawekezaji wakubwa kwa maslai ya chama chao. Huruma iyo ni ya kinafiki! 2me 200/= fare ni reasonable

Umeeleza vzr lakini ume-luz track hapo ulipodharau hilo ongezeko la 200, usiichukulie 200/400 kama 'static' figure.
 
sina uhakika sana lakini nadhani wanaotoa tender pale ni watu wa city ambamo wabunge nao wamo kwenye vikao vya halamashauri kama madiwani,naomba kusahihishwa kama kama tender haitolewi na halmashauri ya jiji..magufuli yeye analia na vivuko vyake ambavyo havikununuliwa na jiji na wala hawaujui uchungu wake..vimenunuliwa na serikali kuu na viko chini ya wizara yake!watu wakizama leo pale kwa ubovu wa kivuko atakae takiwa kuwajibika ni yeye bwana pombe,sasa kwanini asichukue tahadhari ya kuwataka mchangie gharama za kukihudumia iko kivuko kinachowasidia nyinyi wenyewe!
Pale ferry kwa 100% wanahusika wenyewe wizara ya miundombinu, idara ya Temesa. hakuna Jiji wala Manispaa inayohusika kwa lolote pale Ferry.
Je una point nyingine labda!?
 
naomba usilete utani kwenye issue za kitaifa. Utanipa ban.

habari ndio hiyo mheshimiwa,toeni sehemu ya posho muwape ruzuku ya kivuko wapiga kura wenu,serikali haina hela ya kukihudumia kivuko,imeshawanunulia kazi ya kukihidumia ni yenu mnaokitumia!
 
THE ROMANTIC Umenena mkuu, Magufuli akomae ili mjitu ya Dar es Salaam iamke tikiyaaambia ccm inayakamua bira huruma hayatuelewi! Sasa kwa kauli ya Magufuli yawe tayari kukamuliwa la sivyo yajifunze kupiga mbizi ndipo yatakapoa jifunza kuwa kuipenda ccm ni mzigo na ghalama kubwa.

Asante Mkuu!
Kwa ufupi wakazi wa jiji ni moja kati ya wananchi walio hovyo na kimsingi wao ndio wanaochelewesha maendeleo ya nchi yetu. Wao ndio wakwanza kulia linapotokea tatizo. Angalia tv, sikiliza redio, wanaharakati. Ni walalamikaji wazuri. Halafu ni wote, hadi wabunge wao! Inapofika uchaguzi, wao ndio wanaipendezesha na kuichagua ccm. Acha watukanwe labda watapata akili. Wabunge wao walisha ambiwa wanatumia makalio kufikiri. Labda matusi na kudhalilishwa ndio kutawafungua macho. Hovyo kabisa!
 
Pale ferry kwa 100% wanahusika wenyewe wizara ya miundombinu, idara ya Temesa. hakuna Jiji wala Manispaa inayohusika kwa lolote pale Ferry.
Je una point nyingine labda!?

la hasha bali kuwataka tu mkubali kuchangia gharama mpya za uendeshaji kivuko sasa
 
Back
Top Bottom