Magufuli alikoroga, Maandamano makubwa kumpinga leo

Jamani tuseme ukweli viongozi wa CCM ni sawa na maji ambayo haya sahau ubaridi hata ungeyapasha 100C mwisho wa siku yatapoa tu
 
Tatizo si Uwaziri Mkuu, sasa tatizo ni Urais 2015. Nauli zimepanda kila mahali hatujaona wabunge wakiongoza maandamano. Nauli ya Kivuko cha cha Mto Kilombero ni kubwa kuliko Kigamboni. Magufuli mbona hajatangaza kugombea urais?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mnang'ang'ania nini uko kigamboni? kwanza kumeshauzwa na mnatakiwa kuhama, akufukuzae hakwambii toka kaka, chura upenda maji lakini c ya moto! jifunzeni kuogelea, mia mbili mnaandamana? hacheni upuuzi, mbona watu toka mbezi ya kimara mpaka town wanalipa nauli ya 1000 na watu wamekaa kimya? kivuko cha misungwi watu wanalipa nauli ya 300, kamanga sh 800 mpaka 1000, kupandishiwa mia tu mnapiga makeleleeee! kama vp amieni masaki au upanga. mkiandamana tu virungu na mtakomaje!
Ingekuwa arusha kidogo ningeweza kuamini hayo maandamano ila dar mM. Mafisiii
 
Magufuli alikoroga
• Maandamano makubwa kumpinga leo

na Abdallah Khamis na Chalila Kibuda

amka2.gif
Maandamano ya kumpinga leo
Wakati hayo yakijiri, taarifa zimebainisha kuwa maandamano makubwa ya kumpinga Waziri Magufuli yatafanyika leo na kuwashirikisha wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kikiwemo Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya chuo hicho zimesema kuwa tayari jeshi la polisi limearifiwa juu ya kuwepo kwa maandamano hayo na tayari wanafunzi wa vyuo, sekondari na wale wa shule za msingi ambao bado wako majumbani, wamekwishatangaziwa kushiriki maandamano hayo.
Hata hivyo, juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kuthibitisha kama wameruhusu maandamano hayo, hazikufanikiwa baada ya simu yake ya kiganjani kuita muda mrefu bila kupokelewa.

Tuombe taarifa za tishio la Al-shabab zisimfikikie Kamanda Kova la sivyo hakuna maandanano
 
Mnang'ang'ania nini uko kigamboni? kwanza kumeshauzwa na mnatakiwa kuhama, akufukuzae hakwambii toka kaka, chura upenda maji lakini c ya moto! jifunzeni kuogelea, mia mbili mnaandamana? hacheni upuuzi, mbona watu toka mbezi ya kimara mpaka town wanalipa nauli ya 1000 na watu wamekaa kimya? kivuko cha misungwi watu wanalipa nauli ya 300, kamanga sh 800 mpaka 1000, kupandishiwa mia tu mnapiga makeleleeee! kama vp amieni masaki au upanga. mkiandamana tu virungu na mtakomaje!

Mkuu nadhani hujasoma vizuri malalamiko ya watu wa kigamboni, na kama umeyasoma hujayaelewa.
Pamoja na kulipa 200 ya kivuko bado wanalipa nauli za mabasi kwenda sehemu mbalimbali, na hata huyo wa kimara kama anafanya kazi kigamboni atalipia kivuko.

Ukilinganisha nauli ya kamanga ferry na kigamboni usisahau kutaja na urefu(umbali) wa kusafiri vivuko hivyo viwili.

Usisahau kuna issue ya ubadhirifu wa fedha za vivuko, kama hali ingedhibitiwa hizo gharama za uendeshaji unaotajwa ungekuwa ndani ya uwezo wao.

Lakini angalia na hili, nauli ya guta na bajaji kupanda toka sh.300 hadi sh.1,800 wakati gari ndogo nauli imepanda toka sh.1,000 hadi sh.1,500 hapo kuna uwiano sawa?
 
mimi hapo naona waheshimiwa wabunge wetu wa dar wanatafuta pa kutokea au cheap popularity,naomba ni wachallenge je kwanini wasitoe pendekezo la kutoa sehemu ya posho zao za ubunge kama ruzuku ya kufidia ongezeko hilo la nauli ya kivuko kama kweli wana huruma na wanachi wa dar es salaam lengo likiwa ni kuwapunguzia mzigo wananchi at the same time kuchangia gharama za uendeshaji wa kivuko?

hebu just imagine nauli ya sh.100 pale kivukoni imedumu kwa miaka mingapi bila kupanda huku serikali ikijifunga mkanda kuboresha huduma pale ikiwamo kununua kivuko kipya kile kikubwa,leo kuomba wananchi wachangie sh 200 wala sio 500 wabunge wanakuja juu wakati wao wanapokea mamilioni ya posho!!!! magufuli ningekua mimi ningekomaa tu acha waandamane na hao wabunge wenye matumbo makubwa mpaka yanataka kupasuka na hawaridhiki kutwaa kudai posho wanazitumia wapi?

I support you Romantic! this is real a cheap polarity seeking! I hope JJM is one of them, it is not up to his standards! yaani 200/= watu waandamane? aibu tupu!
 
Mnang'ang'ania nini uko kigamboni? kwanza kumeshauzwa na mnatakiwa kuhama, akufukuzae hakwambii toka kaka, chura upenda maji lakini c ya moto! jifunzeni kuogelea, mia mbili mnaandamana? hacheni upuuzi, mbona watu toka mbezi ya kimara mpaka town wanalipa nauli ya 1000 na watu wamekaa kimya? kivuko cha misungwi watu wanalipa nauli ya 300, kamanga sh 800 mpaka 1000, kupandishiwa mia tu mnapiga makeleleeee! kama vp amieni masaki au upanga. mkiandamana tu virungu na mtakomaje!

Inaonekeana wewe ndio Masufuri ooh sory Magufuli,jitete haraka watu tuna hasira na wewe.
 
kutopoka kwingine hakusaidii kabisa..........sasa ngoja akione
 
Hizi kauli za kukurupuka, na kuropoka ukifikiria kila kitu ni sawa ndio maana nchi zingine viongozi kama Magufuli wanaishia kupigwa risasi na watu wenye hasira au wanawajibishwa lakini too bad Bongo kila kitu kinaonekana sawa tu hata kama ikiwa ni dharau kwa wananchi.
 
Siasa kitu cha ajabu sana......

Yaani nauli kuongezwa sh 200 tu wabunge(tena ni wa CCM watupu) wanajifanya wana machungu na wananchi wao na kutishia kuandamana......

Binafsi naona hawa wabunge wanajitafutia 'umaarufu' tu na kutaka kuonekana wanatetea maslahi ya wananchi wao(kwa sh 200 ya kivuko!!!!!!!!!!!!).....
 
sina uhakika sana lakini nadhani wanaotoa tender pale ni watu wa city ambamo wabunge nao wamo kwenye vikao vya halamashauri kama madiwani,naomba kusahihishwa kama kama tender haitolewi na halmashauri ya jiji..magufuli yeye analia na vivuko vyake ambavyo havikununuliwa na jiji na wala hawaujui uchungu wake..vimenunuliwa na serikali kuu na viko chini ya wizara yake!watu wakizama leo pale kwa ubovu wa kivuko atakae takiwa kuwajibika ni yeye bwana pombe,sasa kwanini asichukue tahadhari ya kuwataka mchangie gharama za kukihudumia iko kivuko kinachowasidia nyinyi wenyewe!

Kwakuwa umeanza kwa kukiri kwamba huna uhakika basi hukuwa na sababu za kutoa comment kama vile una uhakika.

Vivuko viko chini ya TEMESA ambayo ni agency chini ya wizara ya ujenzi, kwahiyo madiwani(city council) hawahusiki katika tender za kukusanya ushuru katika vivuko. Hapa wahusika ni TEMESA wenyewe pamoja na wizara ya ujenzi.
 
Siasa kitu cha ajabu sana......

Yaani nauli kuongezwa sh 200 tu wabunge(tena ni wa CCM watupu) wanajifanya wana machungu na wananchi wao na kutishia kuandamana......

Binafsi naona hawa wabunge wanajitafutia 'umaarufu' tu na kutaka kuonekana wanatetea maslahi ya wananchi wao(kwa sh 200 ya kivuko!!!!!!!!!!!!).....

wabunge wanatumika na wanaouwania urais 2015
wameona hii ndo golden oppurtunity ya 'kumuua magufuli' moja kwa moja......
Magufuli ni 'mbumbu wa michezo ya kisiasa'
na sasa wamemaliza....
 
kumbe sisiem wanajua maandamano yanasaidia as pressure mechanism, lakini kwa hili wamechemka
 
I support you Romantic! this is real a cheap polarity seeking! I hope JJM is one of them, it is not up to his standards! yaani 200/= watu waandamane? aibu tupu!

Kama ungesoma vizuri malalamiko ya watu wa kigamboni sidhani kama ungeandika hivi.
Kuna watu wameng'ang'ania nauli ya abiria kutoka 100 hadi 200 na kusahau kwamba kuna guta, bajaji, pikipiki na baiskeli.

Fikiria nauli ya guta na bajaji kuwa sh.1300 huku wenye magari madogo wakilipa sh.1500 hapo huoni kuna mushkeli? Hapa kuna kundi kubwa sana la wananchi watakaoathirika moja kwa moja.

Ongezeko la nauli kwa maguta yanayotumika kuvusha vyakula toka kariakoo kwenda kigamboni litalipwa na mlaji kwa bei ya bidhaa kupandishwa bei ili kufidia nauli. Kwahiyo hili suala ukiliangalia katika wider perspective ndipo utaona mantiki ya malalamiko haya.
 
Hawa wabunge wa Dar ama wanatafuta umaarufu au wametumwa. Yes, maneno ya Magufuli siyo mazuri lakini hii ni mara ya kwanza kusikia kiongozi akitoa kauli za kuudhi? Miezi michache iliyopita wabunge hawa walitukanwa matusi ya nguoni na Meya wa Dar - Dr. Masaburi ,wamemfanya nini hadi sasa? Wamempeleka mahakamani?

Pili, vivuko vingine vilivyo nje Dar i.e kando ya ziwa victoria na kule Morogoro, nauli ni zaidi ya shs 100, sasa huko wananchi wana kipato kikubwa kushinda wa kigamboni? Nauli ya kivuko hiki cha Kigamboni haijabadilika kwa zaidi ya miaka 5 sasa, kwa nini wasiwe wakweli hawa wabunge? Na kwa nini hawa wabunge kama kweli ni waastarabu wasingeomba kukutana na Magufuli na kujadili hali halisi badala ya kushambuliana kwenye vyombo vya habari?

Mimi nahisi Magufuli anatafutwa na kwa bahati mbaya katoa kauli tata, sasa wabunge hawa wanatumia mwanya huu kummaliza kisiasa kwa sababu wanazojua wao wenyewe.

Huko nyuma tulishudia waziri mkuu Pinda akipanda ndege kwenda nyumbani kwa Magufuli na kutoa kauli za 'kumzima' Sasa wabunge wa Dar wanaonekana kuwa kwenye mkakati mwingine. Tangu lini watu kama Zungu wakasimamia kauli zao? Si ndiyo huyu huyu Zungu alisema atajiuzulu kama watu wa mabondeni watahamishwa? Matokeo yake watu wamekufa kutokana na mafuruko. Kama wangefuata maagizo ya serikali huko nyuma na kuhama penginge wengi wao wangekuwa hai, lakini waliendelea kuishi kwenye haya mabande hatari wakiamini wana mtetezi!. Kigamboni nao watendelea kuwasikiliza hawa wanasiasa hadi siku moja watakapojikuta kivuko kimekaa juu ya mawe!

Mnyika hata wewe?
 
Siasa kitu cha ajabu sana......

Yaani nauli kuongezwa sh 200 tu wabunge(tena ni wa CCM watupu) wanajifanya wana machungu na wananchi wao na kutishia kuandamana......

Binafsi naona hawa wabunge wanajitafutia 'umaarufu' tu na kutaka kuonekana wanatetea maslahi ya wananchi wao(kwa sh 200 ya kivuko!!!!!!!!!!!!).....

Mkuu, msome Zungu vizuri hapa:

Mbunge wa Ilala Musa Azzan ”Zungu” alisema lengo la serikali ni kusaidia wajasiriamali wadogo hivyo kuwapandishia gharama hizo kutaathiri mfumo mzima wa maisha yao kwa kile alichoeleza kila inapoongezeka gharama ya aina yoyote katika maisha ya kawaida anayeathiriwa ni mtumiaji wa mwisho ambaye ni mlalahoi.
Alisema katika mtazamo wa kawaida watu watafikiri kuwa kinachopingwa ni ongezeko la sh 200 toka 100, pasipo kuangalia athari la tukio zima kwa kuwa hata mwendesha guta itambidi aongeze nauli ya kusafirishia mizigo ya wafanyabiashara ambao nao wataongeza bei itakakayomgusa moja kwa moja mtumiaji wa bidhaa hizo.

Tusisahanu pia wapo wananchi wanaoishi kigamboni na kufanya kazi huku 'bara' au wanaishi huku 'bara' na kufanya kazi kigamboni na wengi tu wana magari, baiskeli na pikipiki ambazo zote zimepandishiwa nauli. Kwa hiyo pressure haitokani na hiyo 200 peke yake!

Hata hivyo sikatai kwamba hawa wote mwisho wa siku na 'wafanyasiasa' tu!
 
Back
Top Bottom