Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 653
- 1,058
Inawezekana nawe umegundua trend hii. Kila JPM akiongea kuelezea yaliyofanyika anaelezea kana kwamba yamefanyika kwake. Amekuwa hata akidiriki kutumia maneno mabaya kwa waliomtangulia mfano "uchumi ulikuwa mikononi wa majizi", "Waliishi kama malaika sasa wataishi kama mashetani", "mimi huwa sipangiwi (kama waliopita - may be!)" , "mimi ni Rais kwelikweli" (sio kama wengine may be!) n.k. Mfano mwingine ni kuonesha kuwa zoezi la kuhamia Dodoma lilikuwa limesimama tangu Mwalimu Nyerere aondoke mdarakani.
Kwa kuona hali hiyo JK kila akipata nafasi kwenye kadamnasi anaonesha kuwa hii mipango yote ilikuwepo na imekuwa ikitekelezwa karibu katika kila awamu ya uongozi. Wengi mtakumbuka kwa mfano, siku ya uzinduzi wa Ikulu ya Chamwino, alivyoelezea zoezi la kuhamia Dodoma lilivyotekelezwa katika awamu karibia zote. Alielezea yaliyofanywa kipindi cha Mkapa., aliyoyafanya yeye ikiwa ni pamoja na kuamua mahali pa kujengwa Ikulu. Hivi karibuni JK alielezea vizuri sana namna Hayati Bw Mkapa alivyoasisi mpango wa uchumi ambao unatarajiwa kufikia Mwaka 2025 pato la kila MTZ liwe dola elfu tatu.
Ukifuatilia kwa makini JK amekuwa akijaribu kumkumbusha JPM kuwa anayoyafanya leo ni vizuri kuelezea yalianzia wapi ili hata kama yamekosewa asionekane yeye JPM kakosea peke yake. Pamoja na ufafanuzi wa JK bado watendaji wa JPM hawafurahii ufafanuzi huo kw sababu wanataka tu kumpamba JPM aonekana e amekwa akitekeleza yote yeye tu - kama utakumbuka yule Msemaji wa Serikali alitaka kuanza kukanusha kuhusu pato la dola elfu tatu kufikia 2025 - akapingwa vikali sana. Yote aliyokusudia kuyafanya ilikuwa ni kujipendekeza tu.
Sasa hivi ametokwa mtetezi wa JPM - yaani Tundu Lissu. Huyu amekuwa akielezea kwa ufasaha yale yaliyofanywa na JPM na kuonesha yale ambayo yamekuwa yakifanyika awamu zote. Tundu Lissu ameonesha kwa ufasaha sana sana. Mf. ameonesha kuwa JPM amejenga kiwanja cha ndege Chato wakati waliomtangulia hawakujenga viwanja vya ndege vijijini kwao. Ameonesha jinsi JPM ambavyo mara zote anatumia lugha ambazo kwa kiasi fulani hazina staha na zinazalilisha utu na hasa jinsia wakati watangulizi wake hawakuwa wakifanya hayo mambo.
Ninachojiuliza - maneno ya Tundu Lissu ya ukweli yamekuwa yakiwaumiza wanaCCM hata humu JF - sasa wanataka waelezwe nini? Je Tundu Lissu anaongea uwongo kwani? Mbona anafafanua tu ukweli? Kwani ni kweli kuwa ndege zimeanza kununuliwa kipindi chake tu? Kwani ni kweli madaraja yameanza kujengwa kipindi chake tu? Kwani ni kweli kuwa bwawa la umeme tunalitegemea ni hili tu analojenga yeye? Ninakumbuka sisi Shinyanga miaka ya nyuma tulikuwa tunatumia umeme wa jenereta - lakini baadaye nafikiri miaka ya themanini na usheee kuelekea miaka ya 90 ndiyo tukapata umeme - nafikiri wa Kidatu au Mtera (sikna kumbukumbu nzuri).
Angalia pia suala la elimu ya msingi na sekondari bure - hili suala halikuanza kwa JPM - elimu ya msingi bure imeanza siku nyingi. Tena kuna wakati hata chakula cha bure wanafunzi walipewa. Rungwe mwenyewe ninavyofikiri anakumbuka enzi hizo ndiyo maana kaja na sera hiyo ya lishe ya ubwabwa!
Nina mengi ya kuandika - lakini ngoja niache kwanza nitafute wateja asubuhi hii ili leo niiongize hata elfu ishirini tu!
Karibuni Idukilo - Kishapu - Shinyanga ndiyo kwetu, tulewe Tila Lila!