Magufuli akutana na nguvu ya umma Mbeya, azomewa, aambiwa wanamtaka Lowassa

L

laki si pesa.

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Messages
10,043
Points
2,000
L

laki si pesa.

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2015
10,043 2,000
wangempopoa mawe kabisa.. nyambaf
 
Paul Alex

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Messages
3,612
Points
2,000
Paul Alex

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2012
3,612 2,000
Mbarali. Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli jana alikabiliana na wafuasi wa Chadema katika ziara yake ya kampeni, akawaahidi mabadiliko wanayohitaji ya kuufanya Mkoa wa Mbeya kuwa kitovu cha mabadiliko.

Magufuli aliyewasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, mkoani Mbeya saa tatu asubuhi na kuanza safari ya kwenda Mbarali, alisema hayo aliposimama katika eneo la Soweto na Uyole na kuzungumza na wananchi, wakiwamo wafuasi wa CCM na Chadema.

Miongoni mwa watu hao, wafuasi wa Chadema walikuwa wakimshangilia mgombea huyo kwa kuonyesha vidole viwili juu, huku wengine wakizungusha mikono kama ishara ya mabadiliko inayotumiwa na chama hicho na kuimba Lowassa! Lowassa! Lowassa!

Baada ya kuona hivyo, Dk Magufuli aliwaomba wana-Chadema hao wamchague ili afanye mabadiliko bila kujali itikadi za vyama vyao.

Alisema akichaguliwa kuwa rais ataufanyia mabadiliko mji wa Mbeya kuwa M4C, "Sasa itakuwa Mbeya for Change kuwa kituo cha mabadiliko"

"Nikiwa rais, nitakuwa rais wa wote, nitakuwa Rais wa CCM, CUF, Chadema na hata wasio na vyama.

"Chadema oyeeeee, people,s...." Dk Magufuli aliwasalimia wananchi hao kwa salamu inayotumiwa na Chadema, nao wakamwitikia kwa sauti ya juu, ‘power'.

Alisema anatambua kuwa Mbeya kuna wafuasi wa Chadema na kuwataka wafuasi hao kumpa kura ili awaletee maendeleo. Alisisitiza kuwa Serikali yake itahakikisha vijana wote wanapata ajira ili waweze kujitegemea.

"Chadema mnasema people's power, basi mnipe hiyo power ili niwaletee maendeleo," alisema mgombea huyo na kuendelea na safari yake kwenda Mbarali, eneo ambalo lilisalia wakati alipofanya ziara katika mkoa wa Mbeya kwa mara ya kwanza.

Mgombea ubunge wa jimbo la Mbarali, Haroon Primohamed alimwomba Dk Magufuli kutatua mgogoro wa ardhi uliopo katika eneo hilo na kushughulikia kwa haraka mgogoro kati ya wananchi wa vijiji 21 na Tanapa.

Malecela aibuka Mbarali

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu wa zamani, John Malecela jana aliibukia katika Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya na kumwombea kura mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli ili awe rais wa awamu ya tano.

Malecela ambaye pia ni makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, alisema wapinzani ni walaghai na wameshindwa katika uchaguzi wa miaka ya nyuma kutokana na kutokuwa na sera imara zenye mwelekeo wa kuwakomboa wananchi kutoka katika umaskini.

Aliwataka wakazi wa Mbarali kuichagua CCM ili kuwadhihirishia wapinzani kwamba CCM aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere bado iko imara na mwaka huu itashinda.

"Upinzani unaundwa na makundi mawili, kuna kundi la wapinzani tunaowafahamu na walioshindwa tangu mwaka 1992 na kundi la waasi na waroho wa madaraka waliotoka CCM. Wote hawa ni walaghai msiwachague," alisema Malecela.

Alisisitiza kuwa Dk Magufuli ndiye aliyeshinda kwenye kura za maoni ndani ya CCM, lakini wenye uchu wa madaraka waliona wameonewa wakakihama chama.

"Mimi pia niliwahi kugombea urais, sikuchaguliwa. Lakini sijawahi kufikiria kukihama chama kwa sababu najua utaratibu," alisema Malecela.

Mgogoro wa ardhi

Akihutubia wakazi hao, Dk Magufuli aliahidi kurudisha ekari 1,800 za ardhi alizopewa mwekezaji kinyume cha taratibu ili kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa mashamba ya Kapunga yaliyopo wilayani humo.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa Igulusi, Chimala na Rujewa, jimbo la Mbarali, Dk Magufuli alisema anaufahamu mgogoro huo ambao unamhusisha mwekezaji aliyepewa ekari 6,800 badala ya ekari 5,000 alizotakiwa kupewa.

"Ninaifahamu sheria ya vijiji, namba 5 ya mwaka 1999, ninaifahamu sheria ya ardhi, namba 4 ya 1999 na sheria ya matumizi bora ya ardhi ya mwaka 2007. Ninaomba mnichague niwe rais ili nimalize tatizo hili kwa sababu ardhi ni miliki ya rais, siwezi kushindwa," alisema.

Mgombea huyo alisema aliyechelewesha mashamba hayo kurudishwa kwa wananchi ni aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Modestus Kilufi kwa sababu alishindwa kusimamia kikamilifu mchakato wa kumaliza mgogoro huo.

Kilufi ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM, alikihama chama chake na kwenda ACT - Wazalendo. Anagombea ubunge tena katika jimbo la Mbarali kupitia chama chake kipya.

"Mbunge wenu ndiyo alikuwa kikwazo, akiambiwa peleka ‘document' (nyaraka) wizara ya ardhi, yeye anakaa nazo. Safari hii msifanye makosa kumchagua tena, mchagueni Haroon Primohamed kwa sababu ni mchapakazi," alisema Dk Magufuli.

Dk Magufuli ambaye baadaye alifanya mkutano Mafinga, mkoani Iringa aliwaomba wananchi wa Mbarali wamwamini kwa sababu anakusudia kumaliza matatizo ya ardhi nchini, pamoja na matatizo mengine yanayowakabili Watanzania.

"Nikiwa Rais sitawabagua watu, hizo bendera ni rangi tu, kwangu ni kazi tu," alisema Dk Magufuli wakati akizungumza na wananchi wa Chimala, eneo lililokuwa na bendera za CCM na Chadema.

Katika mkutano wake rasmi uliofanyika Rujewa, Dk Magufuli aliwaambia wakazi wa eneo hilo kwamba atahakikisha pia vijiji 21 vilivyochukuliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) kwenye hifadhi ya Ruaha, vinabaki kwa wananchi.

"Mtu yoyote asiwasumbue wananchi wanaoishi kwenye vijiji 21 vilivyochukuliwa na Tanapa. Atakayethubutu kuwasumbua, nikichaguliwa kuwa Rais hana kazi," alisisitiza mgombea huyo huku akishangiliwa na wananchi.

"Dk Magufuli ameniahidi kwamba akishinda urais atarudisha zile ekari zilizochukuliwa na mwekezaji. Ninawaomba mumchague ili amalize tatizo hili, nadhani mnajua jinsi alivyo mchapakazi," alibainisha mgombea ubunge Primohamed.

Mkazi wa Rujewa, Augustino Mwambela aliiitaka Serikali kuboresha scheme za umwagiliaji ili waweze kuzalisha kwa wingi. Alisema wanazalisha kidogo kwa sababu maji kwa ajili ya kilimo cha mpunga bado ni tatizo.

"Tunaomba Magufuli atusaidie kupata mashamba yetu aliyopewa mwekezaji. Pia, kilimo cha umwagiliaji ni muhimu kwa sababu scheme tunazotumia hazina maji ya kutosha," alisema mkulima huyo.

Chanzo: Mwananchi
 
S

Sometimes

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2010
Messages
4,562
Points
1,500
S

Sometimes

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2010
4,562 1,500
Inawezekana ww kuna mbinu chafu unazozijua mtatumia ccm mpate ushindi.lkn huko site watu wanasema ccm ikae pembeni ijipange upya. Watu wameichka ccm.
Viongozi wenu wote wanatoa sababu za kujihami! #Hapakazitu
 
Mapirobe

Mapirobe

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Messages
683
Points
195
Mapirobe

Mapirobe

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2015
683 195

Hapa ni Kazi tu.
 
Mapirobe

Mapirobe

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Messages
683
Points
195
Mapirobe

Mapirobe

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2015
683 195
CCM inasonga mbele, wapinzani wapo kulalamika kama kawaida yao.
 
S

sawabho

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Messages
5,237
Points
2,000
S

sawabho

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2011
5,237 2,000
Sio tabia nzuri ya kuzomea zomea, washaurini wafuasi wa vyama waiche. Ina maana Mgombea akienda sehemu ambayo hakubaliki azomewe ? Unaweza kuta wanazomewa nchi nzima !!
 
M

mmasala

Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
14
Points
20
M

mmasala

Member
Joined Jul 28, 2015
14 20
Sio tabia nzuri ya kuzomea zomea, washaurini wafuasi wa vyama waiche. Ina maana Mgombea akienda sehemu ambayo hakubaliki azomewe ? Unaweza kuta wanazomewa nchi nzima !!
Atazomewa tuuu kipendacho roho ni Lowasaaa..... Aende gym kufanya mazoezi ya u bodyguard Lowasa ni Raisiiii tuuuu peopleeeees poweeeer
 
S

sawabho

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Messages
5,237
Points
2,000
S

sawabho

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2011
5,237 2,000
Atazomewa tuuu kipendacho roho ni Lowasaaa..... Aende gym kufanya mazoezi ya u bodyguard Lowasa ni Raisiiii tuuuu peopleeeees poweeeer
Bado nasisitiza sio tabia nzuri ya kuzomea wagombea, awe Lowasa au Magufuli.
 
Triplets

Triplets

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2007
Messages
1,114
Points
1,225
Triplets

Triplets

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2007
1,114 1,225
[9/27, 13:58] Zawadi Beatus: Sasa hii ajabu yaani Mh Magufuli amezomewa na vijana wa mjini kijiweni waliochoka na ahadi za mama kuku mwanangu utanyonya kesho mnaanza kutafuta mchawi upinzani. Hao vijana ukiwafuatilia utakuta hawana kadi za chama chochote si chadema wala ccm ni watanzania. Badala ya kukaa chini kujitafakari kwanini vijana hawa makapuku, masulupwete wavaa malapulapu wanatuzomea mjirekebishe mnaanza kuwanyooshea vidole wapinzani, jeshi mnalo, taasisi za utafiti mnazo mngewaomba hata twaweza wafanye utafiti kwanini mnazomewa basi, serikali ipo chini yenu, kodi zote mnakusanya nyie, bajeti mnapanga nyie. Hivi hao vijana wangekuwa wamepewa ajira some where kwenye kiwanda wangeacha kazi kuja kuwazomea? Tujitafakari!!!!
[9/27, 14:03] Zawadi Beatus: Mimi nashangaa hivi mfanyakazi wa benki kwa mfano anapata wapi muda wa kwenda kumzomea Magufuli? Vijana watafutiwe suluhisho kikwete aliwaahidi ajira angetekeleza angeona kama Magufuli angekuwa anapata tabu
Ajira za vibarua viwandani wamewapa wachina ukienda viwanda vya saruji kuanzia Dongote , mbeya cement hadi tanga cement, vibarua wachina ndio wameajiriwa kwa mamia kule. Kazi hizi wangewapa hawa vijana nani angekuwapo barabarani kuwazomea?
 
Abdul Mohammed

Abdul Mohammed

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2013
Messages
1,334
Points
0
Abdul Mohammed

Abdul Mohammed

JF-Expert Member
Joined May 26, 2013
1,334 0
Hicho ni kikundi cha wahuni kimepangwa kwa shughuli hiyo ujaona wanavyohangaika kuchukuwa video clips wawapelekee waliowatuma.
Ongezea na hii

Last edited by a moderator:
Brodre

Brodre

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Messages
2,123
Points
1,500
Brodre

Brodre

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2012
2,123 1,500
JPM ndo rais maana ndani ya dk 3 aliweza konga moyo ya walokua wanamzomea mbeya wakageuka kumshangilia hii inaonesha anauwezo sana wa kubadili na kuunganisha watanzania hapakazitu
 
M

moto wa kifuu

Senior Member
Joined
Sep 17, 2015
Messages
156
Points
170
Age
57
M

moto wa kifuu

Senior Member
Joined Sep 17, 2015
156 170
Kama ni kweli walimzuia.Ni kosa kisheria.Anayeamua mtu kuwa raisi ni mpiga kura.Huwezi zuia mgombea wa chama kingine na kumwambia tunamtaka mgombea wetu.Inaelekea hao waliozuia hawajui sheria wala chochote.Hivi magari ya washawasha yangewamwagia maji na wakawapiga virungui wangesema wanaonewa?

Huwezi zuia msafara wa chama kisicho chako au kuuingilia msafara wa chama kingine.CHADEMA elimisheni hao wahuni weni na wanywa viroba.CCM ikiamua kumfanyizia huyo mtu wenu msije piga yowe.

Jeshi la polisi nalo likakamae lisiachie ujinga kama huo ujirudie tena
Huo ulikuwa mtihani mwingine nao pia kafaulu. Walikuwa wanampima uvumilivu, ustaarabu na mambo kama hayo.
 
M

moto wa kifuu

Senior Member
Joined
Sep 17, 2015
Messages
156
Points
170
Age
57
M

moto wa kifuu

Senior Member
Joined Sep 17, 2015
156 170
babu atawaua maccm
Mbona umemhangaisha mzee wa watu? Kama sio babu yako utakiona cha mtema kuni kumnanga babu wa wa watu. Hatujaona nyuma ya pazia (behind the scene). Umechukua masaa mangapi kumkaririsha?
 
Abou Saydou

Abou Saydou

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Messages
2,549
Points
1,250
Abou Saydou

Abou Saydou

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2014
2,549 1,250
Mbona umemhangaisha mzee wa watu? Kama sio babu yako utakiona cha mtema kuni kumnanga babu wa wa watu. Hatujaona nyuma ya pazia (behind the scene). Umechukua masaa mangapi kumkaririsha?
Sijamkaririsha

Kayaongea mwenyewe
 
Forum statistics

Threads 1,284,194
Members 493,978
Posts 30,816,820
Top