Uchaguzi 2020 Magufuli akiwa Songwe: Msipomchagua Silinde sileti maji Tunduma

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918

Kuna methali ya kiswahili inasema mfupa wa kulazimisha ukivunja chungu. Kwa kila aliyefatilia hotuba ya Dr. Magufuli pale Tunduma atagundua kuwa CCM haikubaliki kama Chadema, mbaya zaidi ni kutokana na mgombea CCM inayomnadi, maana haaminiki tena kwa wananchi wa Tunduma, kwa tabia yake ya usaliti.

Ndio maana kwenye kura za maoni ndani ya chama wajumbe walimpiga chini. Sasa Dr. Magufuli analazimisha wananchi wamchague mtu ambaye siyo chague lake. Inawezekana mzee Magu anampango wa kumpa uwaziri au unaibu kama wote wawili watapita maana bado ni kitendawili.

Sasa kwa tabia ile ya kulazimisha wananchi wamchague Silinde itachochea uvunjifu wa amani maana wananchi hawatamchagua, na kwa kuwa yeye anamtaka, itabidi vyombo vya dola vilazimishe kama kawaida, hapo ndio hofu yangu kuwa kunaweza kutokea uvunjifu wa amani.

Mh. Magufuli kama unataka nchi yetu ibaki salama uwe makini kwa kauli zako na pia acha kulazimisha ili wananchi wafanye maamuzi yao.

Maendeleo yanachama kwa mtazamo wa DR Magufuli.

======

DKT. MAGUFULI: MKINICHANGANYIA SILETI MRADI WA MAJI

Dkt. John Magufuli, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM amesema katika muhula ujao ameshaweka mipango ya kupeleka maji Ireje yaweze kufika Tunduma.

Amesema wakimchanganyia wabunge, yaani wakimchagua mbunge asiye wa CCM basi hatopeleka miradi ya maji Tunduma.

Amesema miaka mitano iliyopita aliwabembeleza na hii ni mara ya mwisho yeye kuwaomba watu wa Tunduma. Amesema hawatishi ila moyo unauma kuona wanamchanganyia.

Amesema ili wapate maji ni lazima wamchague David Silinde, mgombea ubunge wa Tunduma kwa tiketi ya CCM ambaye ni mbunge wa Momba anayemaliza muda wake kwa tiketi ya CHADEMA.
 
Kwa nini suala la kuhama chama Chadema wanasumbuka sana wakati CCM ni kawaida tuu? Katika majimbo karibu yote, Mgombea wa Chadema akishinda lazima wana CCM wamepigia kura, sababu CCM ni wengi.
 
Jamani hivi hizi ahadi na maamuzi ndani ya kipindi cha kampeni sio rushwa??NEC Njooni msikilize mzee baba mmemkaza Lissu lakini huyu bado hana namna anaona asipofanya hivyo maji yamezidi unga :D:D
Yeye ni Raisi bado anapokea kero toka kwa wanachi akiwemo Lisu na kuzifanyia kazi

Kuna kero ingine? mwambieni Lisu aendelee kuzitoa ili Raisi aliyeko madarakani azifanyie kazi
 
'Ninafamu kuna kero moja kwa kinamama inaitwa kampeni ya mama kamandoo ambapo wamama wanapochelewa kwenda kliniki wanatozwa 50,000. Naifuta leo moja kwa moja hiyo tozo.'

Wawarudishie pesa zao wakinamama waliokiwashatozwa pesa hio.
 
'Lakini msinichanganyie, mkiniletea hao, nasema maji hamyapati. Lazima tuambizane ukweli na mimi nazungumzaga ukweli.'

Na anasema maendeleo hayana Chama
 
DKT. MAGUFULI: MKINICHANGANYIA SILETI MRADI WA MAJI

Dkt. John Magufuli, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM amesema katika muhula ujao ameshaweka mipango ya kupeleka maji Ireje yaweze kufika Tunduma.

Amesema wakimchanganyia wabunge, yaani wakimchagua mbunge asiye wa CCM basi hatopeleka miradi ya maji Tunduma.

Amesema miaka mitano iliyopita aliwabembeleza na hii ni mara ya mwisho yeye kuwaomba watu wa Tunduma. Amesema hawatishi ila moyo unauma kuona wanamchanganyia.

Amesema ili wapate maji ni lazima wamchague David Silinde, mgombea ubunge wa Tunduma kwa tiketi ya CCM ambaye ni mbunge wa Momba anayemaliza muda wake kwa tiketi ya CHADEMA.
 
Dr Magufuli amesema ili kuleta maendeleo ya haraka ni lazima wachaguliwe wabunge na madiwani anaoweza kuwawajibisha moja kwa moja ambao wanatoka CCM.

Dr Magufuli amemwombea kura David Silinde na kuwaambia wapiga kura wa Tunduma kuwa hii ni mara ya mwisho kuwaomba kwani amevumilia hadi moyo umeuma.

Source EATV

My take; Ni muhimu kuchagua mafiga matatu ili chungu kikae vizuri

Maendeleo hayana vyama!
 
CHADEMA mnadaiwa 2.5billion za miradi ya maji, hatuwezi kuendelea kupoteza pesa za umma kwa kupalilia majizi.

Tumbua CHADEMA lete SILINDE ili tuweke maendeleo zaidi. Msema kweli mpenzi wa Mungu, Tunduma wameamua kuokoka, leo wamebatizwa kwa moto na wamepokea upako. Wewe unadai wamefokewa hahahahah tulia ubatizo uzame.
 
Back
Top Bottom