Magufuli akiri matibabu nje ni kupoteza pesa za umma........................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli akiri matibabu nje ni kupoteza pesa za umma...........................

Discussion in 'Jamii Photos' started by Rutashubanyuma, Apr 2, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  <table class="contentpaneopen" border="0"><tbody><tr><td class="contentheading" width="100%">Magufuli apeleka Sh1bn Loliondo </td> <td class="buttonheading" align="right" width="100%"> Send to a friend </td> </tr> </tbody></table> <table class="contentpaneopen"> <tbody><tr> <td class="createdate" valign="top"> Thursday, 31 March 2011 21:56 </td> </tr> <tr> <td valign="top">

  [​IMG]Waziri wa ujenzi John Magufuli akinywa dawa kwa Mchungaji Ambilikile Masapila katika kijiji cha Samunge, Loliondo mkoani Arusha

  Neville Meena na Mussa Juma, Samunge
  WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli, jana aliingia katika Kijijini Samunge kwa mchungaji Ambilikile Masapila na kupata kikombe cha dawa, kisha kutangaza neema ya kujengwa kwa barabara kuu inayoingia kijijini hapo.

  Magufuli aliuambia umati wa watu uliokuwa ukisubiri zamu yao kunywa dawa kuwa, Serikali itatumia Sh1.05 bilioni kwa ajili kutengenenza barabara hiyo ili iweze kupitika wakati wote kwa lengo la kuwarahisishia usafiri wanaokwenda kunywa dawa kwa Babu Masapila.

  Barabara inayoingia katika kijiji hicho ambacho kimeshuhudia maelfu ya magari yakiingia kila siku tofauti na ilivyokuwa awali, ipo katika hali mbaya kiasi cha baadhi ya maneo kutoruhusu magari kupishana.

  Kwa mujibu wa Magufuli, Serikali ilikwishatoa Sh500/-milioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kuanzia Mto wa Mbu eneo la Kigongoni, Ngaresero, Samunge hadi kuungana na barabara ya kutoka mkoani Mara.

  Dk Magufuli alisema jana ndio aliuagiza uongozi wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Makao Makuu kutuma Sh500 milioni ili kuharakisha ujenzi huo.

  "Tayari fedha hizo zimeshatumwa Tanroads mkoani Arusha na Meneja wa Mkoa, Kakoko (Deodatus), niko naye hapa hivyo kazi itakwenda haraka ili watu wanaokuja kwa mchungaji kunywa dawa wasiendelee kuteseka," alisema Dk Magufuli huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuwa wakimsikiliza.

  Waziri pia huyo alisema kwa mamlaka aliyonayo, atawasiliana na uongozi wa Mfuko wa Barabara ili utume fedha za dharura kiasi cha Sh50 milioni kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorogoro kwa ajili ya kufanya matenegenezo mengine ya barabara, wilayani humo.

  Alisema fedha zilizotengwa kwa ajilii ya barabara za nchi nzima kupitia mfuko huo zinafikia Sh286 bilioni katika bajeti ya mwaka 2010/11, na kwamba upo uwezekano mkubwa wa fedha za dharura kupatikana kwa ajili ya matenegenezo ya barabara ya Samunge.

  Matengenezo
  Kwa mujibu wa Magufuli, matengenezo ya barabara hiyo ni muhimu sana kwani awali barabara hiyo kuanzia Mto wa Mbu ilikuwa ikipitisha magari kati ya 20 na 25 kwa siku lakini, sasa yameongezeka hadi 3,500 kwa siku.

  "Nasema barabara hii ni muhimu sana hivyo nakuagiza Meneja wa Tanroads mkoa wa Arusha kuhakikisha mkandarasi aliyepewa kazi ya kutengeneza barabara hii anafanya kazi usiku na mchana ili ikamilike, akizembea fukuza," alisema Magufuli na kuongeza:

  "Sheria namba 17 ya mwaka 1997 na vifungu vyake inatoa mamlaka ya kuondolewa kwa mkadarasi anayezembea. Pia sheria inaelekeza kufikishwa mahakamani kwa wakandarasi wa aina hiyo, na
  akitiwa hatiani na anaweza kufungwa miaka mitano. Hivyo basi sheria ipo na pale tutakapolazimika tutaitumia".

  Magufuli aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya Ngorogoro kuwasilisha maombi ya dharura ya fedha za matengenezo ya barabara katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ili kuwezesha matengenezo ya barabara nyingine kufanyika.

  "Tukiacha barabara ya kuja huku, nimetembelea barabara zenu katika wilaya ya Ngorongoro, kwa kweli ni mbaya sana hivyo zinahitaji matengenezo,"alisisitiza.

  Juzi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Eliasi Ngorisa, aliliambia Mwananchi kwamba halmashauri yake ilikuwa imeomba kiasi cha Sh400 milioni kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kuifanyia matengenezo ya dharura barabara zinazoingia kijijini Samunge.

  Dk Magufuli pia alimwelekeza Meneja wa Tanroads mkoani Arusha kuandaa mpango wa matengenezo ya barabara za Ngorongoro na kuwasilisha mapendelezo yake serikalini kwa ajili ya utekelezaji wake.

  "Kaandike mpango huo sasa na ulete ili tuone jinsi ya kufanya, kama hujui kuandika tafuta watu wakusaidie," alisema Magufuli na kusababisha umati wa watu
  kuagua kicheko.

  Waomba msaada
  Tofauti na viongozi wengine waliowahi kufika kwa mchungaji Mwasapila, Waziri Magufuli aliruhusu maswali kutoka kwa wananchi waliokuwa wakimsikiliza.

  Wengi wao walilalamikia hali mbaya ya mazingira. "...pamoja na kwamba wewe si Waziri wa Afya, lakini tunajua unatoka Serikalini, tunaomba utusadie maana afya zetu zipo hatarini. Huwezi kuamini kwani huko barabarani unakuta mtu anajisaidia haja kubwa hapo,na mtu mwingine anakula chakula, kwa kweli hali ni mbaya tunaomba msaada,"alisema Nicholas Mwangoka.

  Akijibu hoja hiyo, Waziri Magufuli alisema atawasilisha taarifa yake kwa Waziri Mkuu ambaye yupo mkoani Arusha na kwamba anaamini kupitia njia hiyo waziri wa sekta ya afya atafikishiwa ujumbe ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

  Mapema mchungaji Mwasapila kupitia kwa msaidizi wake, aliomba Serikali ijenge daraja katika mto wa Samunge ambao umekuwa kikwazo cha magari kuingia kijijini hapo kwani hufurika kila mvua zinaponyesha.

  Pia mchungaji huyo alimshukuru Waziri huyo kwa ahadi aliyoitoa akisema kuwa hatua hiyo inamtia moyo kuendelea kutoa tiba kwa wagonjwa wanaofika nyumbani kwake.

  "Nakushukuru sana kwa ujio wako na yale uliyoyasema, unatupa matumaini,unatupa moyo, asante tunashukuru sana," alisema Masapila.

  Foleni yapungua Samunge
  Katika hatua nyingine, foleni ya magari ambayo ilikuwa zaidi ya kilometa 30 kutoka eneo analotolea tiba mchungaji Masapila sasa imepungua.

  Kupungua kwa foleni hiyo kumetokana na utaratibu mpya wa kuingiza magari katika kijiji cha Samunge ambao unatarajiwa kuanza leo, pia kutokana na kasi ya mchungaji huyo katika kugawa dawa.

  Tacaids yawaasa wagonjwa
  Ellen Manyangu anaripoti kutoka Dar es Salaam kuwa, Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), imewataka wagonjwa waliokunywa dawa ya Mchungaji Masapila kutoacha kuendelea na dozi walizopewa hospitalini kwa kuwa dawa hiyo haijathibitika kutibu Ukimwi.

  Mratibu wa tume hiyo Dk Bwijo Bwijo alisema jana kuwa utafiti bado unaendelea kujua endapo kikombe hicho cha babu, kinaweza kutibu magoonjwa yanayoelezwa.

  Alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mjadala ulioandaliwa na Kituo cha Radio Clouds FM na kufanyika katika hoteli ya Kempisky jijini Dar es Salaam jana asubuhi.

  Akizungumza katika mjadala huo, Dk Bwijo alisema dawa ya Mchungaji Masapila bado inafanyiwa utafiti ili kuthibitisha kama inatibu, hivyo wananchi hawapaswi kuacha kutumia dawa za kitabibu ghafla.

  Kwa mujibu wa Bwijo, jitihada za kuthibitisha ubora wa dawa hiyo bado zinaendelea kwa ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti Ukimwi (UNAIDS).

  "Wagojwa wote walioko kwenye matibabu ya dawa za kitaalamu na wamekunywa kikombe cha dawa ya babu wasiache kutumia dawa zao mpaka itakapothibitishwa kuwa dawa hiyo ni halali na inatibu," alisema Dk Bwijo.

  Mwenyekiti Mstaafu wa Mtandao wa Wanaoishi na Ukimwi Afrika (TANEPHA), Alex Margery, alisema suala la Loliondo limejaa sura ya Ukimwi na kutahadharisha kuwa watu wasiache kutumia dawa za kitaalamu kwa kuwa dawa ya babu bado haijathibitishwa.

  Alisema walishajitokeza watu mbalimbali katika nchi za Kenya na Afrika Kusini na kutoa dawa zilizoaminika kuwa zinatibu maradhi sugu ikiwemo ukimwi, lakini baadaye zilisababisha watu wengi kufa kutokana na kuacha kutumia dawa za kitaalamu kwa imani kuwa wamepona.

  "Hili ni jambo la hatari sana hasa kwa jamii yetu kwani wagonjwa wanaacha kutumia dawa za kisayansi zilizothibitishwa kutibu, au kupunguza makali ya maradhi waliyonayo kwa imani kikombe cha dawa wanachopewa Loliondo kinawaponyesha&#8230;, "alitahadharisha Margery.

  Aliongeza dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ARV zilikuwa katika dozi kubwa ya vidonge 14 kwa siku moja, lakini kadri siku zinavyoongezeka dozi hiyo inapungua na hivi sasa ni kidonge kimoja kwa siku.
  Mtaalam wa Afya ya Jamii na Ukimwi, Dk Bennect Fimbo, alisema awali ugonjwa wa Ukimwi ulikuwa tishio kwa jamii kwa vile hawakuwa na uhakika wa mtu kuishi nao muda mrefu lakini, hivi sasa mtu anaweza kuishi nao kwa muda wa miaka 20.

  Aliongeza kuwa mti wa Mugariga unaotumiwa na babu kama dawa umefanyiwa utafiti kwa muda mrefu, hivyo inapaswa uchunguzi wa ziada ufanyike ili kubaini mti huo unatibu magonjwa yapi na dozi yake.

  Kandoro aweka udhibiti
  Kutoka Mwanza Frederick Katulanda na Sheila Sezy wanaripoti kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, amewaagiza wasafirishaji wa watu wanaokwenda kutibiwa kwa Mchungaji Masapila kuwaorodhesha watu wote ili kuweka kumbukumbu.

  Akizungumza jana katika kikao chake na wamiliki a mabasi, Kandoro alisema Serikali imepanga utaratibu maalum ikiwa ni pamoja na kuweka vizuizi kwa lengo la kupunguza msongamano na kuwezesha wagonjwa kumfikia babu haraka zaidi.

  Alisema Serikali imetambua kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaoenda Loliondo kwa ajili ya matibabu hayo hivyo utaratibu huo mpya utasaidia kupunguza msongamano.

  Alifahamisha kuwa kuanzia sasa magari yote yanayotoka Mwanza na Kagera na wageni kutoka nchi za Rwanda, Uganda na Burundi kwenda Loliondo, wanapaswa kujiandikisha jijini Mwanza na kuacha majini yao katika kizuizi cha Magu.

  Magari yatakayoruhusiwa kuondoka na kupita katika vizuizi ni yale yenye nguvu maalumu (four wheel drive) na mbasi. Malori ya aina yote hayaruhusiwi kwenda huko, alisema.

  Akizungumzia suala la nauli kuwa juu, Kandro alisema serikali haitaingilia utozaji wa nauli bali kuhakikisha inaboresha mazingira ya Loliondo na kwamba nauli zitashuka zenyewe.

  </td> </tr> <tr> <td class="modifydate"> Last Updated on Friday, 01 April 2011 09:01 </td> </tr> </tbody></table> Comments

  <center>1234567
  </center>

  0 #99 CAROLINE 2011-04-02 04:28 HAKUNA BINADAMU MZIMA KWA ASILIMIA MIA MOJA. WOTE TUNAYO MATATIZO LAKINI YANAZIDIANA KWA KIASI FULANI.MAKAMBA KANYWE DAWA USAFISHE UBONGO.WENZAKO WOTE NAWASIKIA WAMEKUNYWA WEWE UNASUBIRI NINI ILE DAWA INAREKEBISHA UBONGO PIA.DAWA YA MCHUNGAJI NI SALAMA KULIKO HAYA MADAWA YANATOKA ULAYA.KWANZA WAZUNGU HAWATUPENDI TUTAKUWA NA IMANI NA DAWA ZAO KIVIPI?.BORA DAWA YA BABU NI MWENZETU TENA KAOTESHWA NA MWENYEZI MUNGU.TUTUMIENI DAWA ZETU ZA ASILI TUSIWATAJIRISHE WAZUNGU. KWANZA BABU APEWE ULINZI KWANI KWA JINSI WATU WANAVYOENDA LOLIONDO KUNA WATU HAWAMPENDI TENA. AMEWAHARIBIA DEAL ZAO ZA KUDANGANYA WATU. UTAPONA LEO, UTAPONA KESHO HUKU UNATOA PESA.BABU MIA TANO TU MCHEZO UMEKWISHA.
  Quote

  0 #98 mpopo 2011-04-02 02:50 Namaanisha mgonjwa, wrong spelling, hehehe.
  Halafu naomba kuwe na orodha ya wagonjwa waliopona ikwahusisha mawaziri na watu mashuhuri waliotibiwa na babu.
  Utafiti wa kisasa hufanya kama ilivyo kwa babu ila watu hawafahamu. Hapa thailand watu wengi sana wamekuwa wakijitolea kwenye utafiti ikiwa ni kunywa dawa kwa mara ya kwanza. Hivyo iwe nzuri au uongo dawa hiyo yote ni one step ahead kwa taifa. Kama ushirikina basi wazungu walikuwa washirikina sana zamani kuliko sisi ila sisi tunaenda slow sana. Ili tufikie sayansi tuna hitaji experience, understanding ili tufike kweny judgment.... So naunga mkono babu na kuwataka tuwe makini zaidi na kufanya utafiti zaidi kuliko kupinga bila hoja maalum. kwani fact ni kuwa watu wanateseka sana, na wanasayansi hawalali nasi kwa nini tulale?
  Quote

  0 #97 mpopo 2011-04-02 02:42 Hivi kumbe tuna mawaziri wagonjwa wengi hivi? ndiyo maana wengi wana hasira kwaniugonjwa kama wa kisukari unatupa hasira kubwa pia uvivu wa kfanya kazi. Ndiyo maana mambo mengi hayaendi serikalini hahehe!
  Halafu kama wewe ni mganjwa kazi ya uwaziri ni ngumu kwani i ya kuzunguka nchi nzima, waachie wazima wachape mzigo upewe kazi nyingine.
  Quote

  0 #96 Juma 2011-04-02 00:27 Hizo Hela za serekali zinatumika kishirikina, serekali haiamini uchawi wala dini, sasa hiyo barabara inajengwa kwa mising ipi?
  Quote

  0 #95 kipara 2011-04-01 21:01 kama serikali imeridhia kwamba dawa ya babu ni mjarrada basi wamuhamishe huyo babu na kumuweka katika mazingara ya usalama wa kiafya na kutoa huduma bila ya usumbufu.ikiwa sharti ya hizo dawa zake ni lazima zitolewe pahala ambapo SHETANI anamuamrisha basi serikali yetu inaubia na shetani
  Quote

  +1 #94 MGAYA,Zahran 2011-04-01 20:53 Nahoji,hivi kama babu asingetokea katika zama hizi barabara ya Loliondo ikejengwa lini?.Kila kitu ni siasa nchi hii.
  Quote

  +1 #93 joseph madeu 2011-04-01 18:19 babu fanya mambo dunia nzima ije kwako!
  Quote

  0 #92 msema kweli 2011-04-01 17:50 Ma[NENO BAYA] Day niliiona tangu usiku sana hapa kwa wabeba maboxi
  Quote

  +1 #91 kamakabuzi 2011-04-01 17:19 wanapaswa kujiandikisha jijini Mwanza na kuacha majini yao katika kizuizi cha Magu.

  Mwanza ni kubwa; ataje ofisi itakayohusika na ahakikishe kuwa hapatakuwepo vitendo vya rushwa.
  Quote

  0 #90 Shamte 2011-04-01 16:39 Ni jambo la kusikitika kuwa kuwa wachangia mada katika jukwaa hili hawalitumii kama ilivyo kusudiwa badala yake wanalitumia kama kukashfiana. Ieleweke wazi kwamba imani ya kupona hutoka kwenye moyo wa mgonjwa. Endapo utaamini kuwa maji yaliyonuizwa na Sheikh au padri yatakuponya basi kweli itatokea. Na hata hiyo dawa ya Babu kama utainywa kwa kujaribu na sio kudhamiria kuinywa ili upone, basi kwako itakuwa haifai. Isipokuwa tu ningependa nianishe kuhusu maono ya Babu na wengineo. Nijuavyo mimi, Mwenye-enz-Mungu huweza kumpa maono mja wake akiwa macho na siyo usingizini. Niliwahi kumsikiliza mtaalam mmoja akitoa mada juu ya aina za tiba mbadala. Akaainisha tiba mbadala kwa makundi manne, lakini moja ambalo limenigusa ni lile aloliita tiba kupitia viumbe vya Mungu. Kwa mfano Mtu huweza kuingiwa na Jini na akaamrishwa afanye tiba kwa masharti mbali mbali kama vile kugawa kiasi cha fedha kwa makundi ya watu kadhaa wasiojiweza, misikitini, makanisani n.k. Hawa majini humjia mwanaadamu akiwa usingizini. Kwa hivyo, nawaomba wasomi waliobobea katika masuala ya dini walichanganue hili, ili kuweza kujua kati ya maono na ndoto. Hiyo ndio "homework" ninayo wapa, lakini kama nilivyokwisha sema hapo awali kwamba kupona kwa mtu kunatokana na imani ya tiba anayopewa kwa wakati ule akiwa mgonjwa. Na kutopona pia husababishwa na imani hiyo hiyo. Haya kazi kwenu.

  Ibn Saidi.
  Quote

  -1 #89 Mimi 2011-04-01 16:32 Quoting adili ignas:
  waheshimiwa ndugu watanzania tumwombe mungu wasije wakamuua babu maana dawa zao zi[NENO BAYA]sa bei​

  Hakuna anayeweza kuua nafsi ya mtu kama Mwenyezi Mungu mwenyewe hajataka.
  Hayo ni mawazo finyu.
  Quote

  +1 #88 Mimi 2011-04-01 16:28 Quoting RAIA MAKINI:
  KWA KUSEMA UKWELI LAZIMA TUTAMKUMBUKA BABA WA TAIFA KWA MAMBO MENGI SANA. IKIWAMO KUWAJENGEA WANANCHI WAKE KUTEMBEA MBELE KIFUA MBELE NA KURINGIA UFAHAMU WETU,KUJIAMINI NA KUTOKUENDEKEZA UMASKINI WA MAWAZO ULIOKITHIRI,TUL IONAO SASA.SIANA SABABU YA KUINGILIA MIPANGO YA MUNGU SIPO KATIKA NAFASI HIYO.ILA MUNGU PIA ANAWAHESHIMU WATU KAMA AKINA TOMASO.KWA SABABU NI YEYE HUYO HUYO ALIYETUKANYA KWAMBA TUSIPEPETWE NA KILA AINA YA UPEPO.KUTOKUJIAMINI KWETU NDIKO KUNAKOTUPELEKEA KUTEGA MASIKIO YETU PANDE MBALI MBALI ZA NCHI KUTAKA KUSIKIA NANI KAJA NA DAWA MPYA,BILA KUWA NA UHAKIKA KAMA IMETOKA KWA MUNGU KWELI.BABU SIJAMPINGA BADO IJAPOKUWA SIMWUNGI MKONO KWA ASILIA ZOTE.ILA HAWA WASANII WENGINE WALIOIBUKA NI JUKUMU LAKO KUWAUNGA MKONO KUENDELEA KUJIYUMBISHA.​

  WOTE SAWA TU, HAKUNA WA AFADHALI HATA MMOJA, YAANI SIO BABU WALA BIBI!! WOTE WANATAKA KUDHULUMU NAFSI ZA WATU KWA KUWAPELEKA KWA SHETANI.
  Quote

  0 #87 RAIA MAKINI 2011-04-01 16:22 KWA KUSEMA UKWELI LAZIMA TUTAMKUMBUKA BABA WA TAIFA KWA MAMBO MENGI SANA. IKIWAMO KUWAJENGEA WANANCHI WAKE KUTEMBEA MBELE KIFUA MBELE NA KURINGIA UFAHAMU WETU,KUJIAMINI NA KUTOKUENDEKEZA UMASKINI WA MAWAZO ULIOKITHIRI,TUL IONAO SASA.SIANA SABABU YA KUINGILIA MIPANGO YA MUNGU SIPO KATIKA NAFASI HIYO.ILA MUNGU PIA ANAWAHESHIMU WATU KAMA AKINA TOMASO.KWA SABABU NI YEYE HUYO HUYO ALIYETUKANYA KWAMBA TUSIPEPETWE NA KILA AINA YA UPEPO.KUTOKUJIAMINI KWETU NDIKO KUNAKOTUPELEKEA KUTEGA MASIKIO YETU PANDE MBALI MBALI ZA NCHI KUTAKA KUSIKIA NANI KAJA NA DAWA MPYA,BILA KUWA NA UHAKIKA KAMA IMETOKA KWA MUNGU KWELI.BABU SIJAMPINGA BADO IJAPOKUWA SIMWUNGI MKONO KWA ASILIA ZOTE.ILA HAWA WASANII WENGINE WALIOIBUKA NI JUKUMU LAKO KUWAUNGA MKONO KUENDELEA KUJIYUMBISHA.
  Quote

  +1 #86 Mimi 2011-04-01 15:53 Quoting fadhili:
  Hii inaonesha jinsi watz walivyo washirikina wakubwa. Wote waliokwenda kwa Babu wangeweza kwenda kwa waganga wa kiejyeji wanaotumia tunguri pia!Yote haya ni kwasababu ya u[NENO BAYA] uliokomaa na utegemezi wa miujiza kupata kila kitu na hii ndio imekuwa sababu kubwa ya inchii kutoendelea na kama tutakwenda kwa mwendo huu ipi siku akaja mtu akawafunga kamba Wabongo wote kama mbuzi na kuwapeleka machinjioni. Ni watu wachache tu watasalimika siku hiyo!​

  Nashukuru sana ndugu yangu, yaani unaonyesha jinsi gani ulivyo na upeo wa kuweza kukaa na kutafakari na kujua lipi JEMA na lipi BAYA.
  Quote

  +3 #85 fadhili 2011-04-01 15:47 Hii inaonesha jinsi watz walivyo washirikina wakubwa. Wote waliokwenda kwa Babu wangeweza kwenda kwa waganga wa kiejyeji wanaotumia tunguri pia!Yote haya ni kwasababu ya u[NENO BAYA] uliokomaa na utegemezi wa miujiza kupata kila kitu na hii ndio imekuwa sababu kubwa ya inchii kutoendelea na kama tutakwenda kwa mwendo huu ipi siku akaja mtu akawafunga kamba Wabongo wote kama mbuzi na kuwapeleka machinjioni. Ni watu wachache tu watasalimika siku hiyo!
  Quote  <center>1234567
  </center> Refresh comments list
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3

  “Wagojwa wote walioko kwenye matibabu ya dawa za kitaalamu na wamekunywa kikombe cha dawa ya babu wasiache kutumia dawa zao mpaka itakapothibitishwa kuwa dawa hiyo ni halali na inatibu,” alisema Dk Bwijo.

  Mwenyekiti Mstaafu wa Mtandao wa Wanaoishi na Ukimwi Afrika (TANEPHA), Alex Margery, alisema suala la Loliondo limejaa sura ya Ukimwi na kutahadharisha kuwa watu wasiache kutumia dawa za kitaalamu kwa kuwa dawa ya babu bado haijathibitishwa.

  Alisema walishajitokeza watu mbalimbali katika nchi za Kenya na Afrika Kusini na kutoa dawa zilizoaminika kuwa zinatibu maradhi sugu ikiwemo ukimwi, lakini baadaye zilisababisha watu wengi kufa kutokana na kuacha kutumia dawa za kitaalamu kwa imani kuwa wamepona.

  “Hili ni jambo la hatari sana hasa kwa jamii yetu kwani wagonjwa wanaacha kutumia dawa za kisayansi zilizothibitishwa kutibu, au kupunguza makali ya maradhi waliyonayo kwa imani kikombe cha dawa wanachopewa Loliondo kinawaponyesha…, "alitahadharisha Margery.

  Aliongeza dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ARV zilikuwa katika dozi kubwa ya vidonge 14 kwa siku moja, lakini kadri siku zinavyoongezeka dozi hiyo inapungua na hivi sasa ni kidonge kimoja kwa siku.
  Mtaalam wa Afya ya Jamii na Ukimwi, Dk Bennect Fimbo, alisema awali ugonjwa wa Ukimwi ulikuwa tishio kwa jamii kwa vile hawakuwa na uhakika wa mtu kuishi nao muda mrefu lakini, hivi sasa mtu anaweza kuishi nao kwa muda wa miaka 20.

  Aliongeza kuwa mti wa Mugariga unaotumiwa na babu kama dawa umefanyiwa utafiti kwa muda mrefu, hivyo inapaswa uchunguzi wa ziada ufanyike ili kubaini mti huo unatibu magonjwa yapi na dozi yake.

  Kandoro aweka udhibiti
  Kutoka Mwanza Frederick Katulanda na Sheila Sezy wanaripoti kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, amewaagiza wasafirishaji wa watu wanaokwenda kutibiwa kwa Mchungaji Masapila kuwaorodhesha watu wote ili kuweka kumbukumbu.

  Akizungumza jana katika kikao chake na wamiliki a mabasi, Kandoro alisema Serikali imepanga utaratibu maalum ikiwa ni pamoja na kuweka vizuizi kwa lengo la kupunguza msongamano na kuwezesha wagonjwa kumfikia babu haraka zaidi.

  Alisema Serikali imetambua kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaoenda Loliondo kwa ajili ya matibabu hayo hivyo utaratibu huo mpya utasaidia kupunguza msongamano.

  Alifahamisha kuwa kuanzia sasa magari yote yanayotoka Mwanza na Kagera na wageni kutoka nchi za Rwanda, Uganda na Burundi kwenda Loliondo, wanapaswa kujiandikisha jijini Mwanza na kuacha majini yao katika kizuizi cha Magu.

  Magari yatakayoruhusiwa kuondoka na kupita katika vizuizi ni yale yenye nguvu maalumu (four wheel drive) na mbasi. Malori ya aina yote hayaruhusiwi kwenda huko, alisema.

  Akizungumzia suala la nauli kuwa juu, Kandro alisema serikali haitaingilia utozaji wa nauli bali kuhakikisha inaboresha mazingira ya Loliondo na kwamba nauli zitashuka zenyewe.

  </td> </tr> <tr> <td class="modifydate"> Last Updated on Friday, 01 April 2011 09:01 </td> </tr> </tbody></table> Comments

  <center>1234567
  </center>

  0 #99 CAROLINE 2011-04-02 04:28 HAKUNA BINADAMU MZIMA KWA ASILIMIA MIA MOJA. WOTE TUNAYO MATATIZO LAKINI YANAZIDIANA KWA KIASI FULANI.MAKAMBA KANYWE DAWA USAFISHE UBONGO.WENZAKO WOTE NAWASIKIA WAMEKUNYWA WEWE UNASUBIRI NINI ILE DAWA INAREKEBISHA UBONGO PIA.DAWA YA MCHUNGAJI NI SALAMA KULIKO HAYA MADAWA YANATOKA ULAYA.KWANZA WAZUNGU HAWATUPENDI TUTAKUWA NA IMANI NA DAWA ZAO KIVIPI?.BORA DAWA YA BABU NI MWENZETU TENA KAOTESHWA NA MWENYEZI MUNGU.TUTUMIENI DAWA ZETU ZA ASILI TUSIWATAJIRISHE WAZUNGU. KWANZA BABU APEWE ULINZI KWANI KWA JINSI WATU WANAVYOENDA LOLIONDO KUNA WATU HAWAMPENDI TENA. AMEWAHARIBIA DEAL ZAO ZA KUDANGANYA WATU. UTAPONA LEO, UTAPONA KESHO HUKU UNATOA PESA.BABU MIA TANO TU MCHEZO UMEKWISHA.
  Quote

  0 #98 mpopo 2011-04-02 02:50 Namaanisha mgonjwa, wrong spelling, hehehe.
  Halafu naomba kuwe na orodha ya wagonjwa waliopona ikwahusisha mawaziri na watu mashuhuri waliotibiwa na babu.
  Utafiti wa kisasa hufanya kama ilivyo kwa babu ila watu hawafahamu. Hapa thailand watu wengi sana wamekuwa wakijitolea kwenye utafiti ikiwa ni kunywa dawa kwa mara ya kwanza. Hivyo iwe nzuri au uongo dawa hiyo yote ni one step ahead kwa taifa. Kama ushirikina basi wazungu walikuwa washirikina sana zamani kuliko sisi ila sisi tunaenda slow sana. Ili tufikie sayansi tuna hitaji experience, understanding ili tufike kweny judgment.... So naunga mkono babu na kuwataka tuwe makini zaidi na kufanya utafiti zaidi kuliko kupinga bila hoja maalum. kwani fact ni kuwa watu wanateseka sana, na wanasayansi hawalali nasi kwa nini tulale?
  Quote

  0 #97 mpopo 2011-04-02 02:42 Hivi kumbe tuna mawaziri wagonjwa wengi hivi? ndiyo maana wengi wana hasira kwaniugonjwa kama wa kisukari unatupa hasira kubwa pia uvivu wa kfanya kazi. Ndiyo maana mambo mengi hayaendi serikalini hahehe!
  Halafu kama wewe ni mganjwa kazi ya uwaziri ni ngumu kwani i ya kuzunguka nchi nzima, waachie wazima wachape mzigo upewe kazi nyingine.
  Quote

  0 #96 Juma 2011-04-02 00:27 Hizo Hela za serekali zinatumika kishirikina, serekali haiamini uchawi wala dini, sasa hiyo barabara inajengwa kwa mising ipi?
  Quote

  0 #95 kipara 2011-04-01 21:01 kama serikali imeridhia kwamba dawa ya babu ni mjarrada basi wamuhamishe huyo babu na kumuweka katika mazingara ya usalama wa kiafya na kutoa huduma bila ya usumbufu.ikiwa sharti ya hizo dawa zake ni lazima zitolewe pahala ambapo SHETANI anamuamrisha basi serikali yetu inaubia na shetani
  Quote

  +1 #94 MGAYA,Zahran 2011-04-01 20:53 Nahoji,hivi kama babu asingetokea katika zama hizi barabara ya Loliondo ikejengwa lini?.Kila kitu ni siasa nchi hii.
  Quote

  +1 #93 joseph madeu 2011-04-01 18:19 babu fanya mambo dunia nzima ije kwako!
  Quote

  0 #92 msema kweli 2011-04-01 17:50 Ma[NENO BAYA] Day niliiona tangu usiku sana hapa kwa wabeba maboxi
  Quote

  +1 #91 kamakabuzi 2011-04-01 17:19 wanapaswa kujiandikisha jijini Mwanza na kuacha majini yao katika kizuizi cha Magu.

  Mwanza ni kubwa; ataje ofisi itakayohusika na ahakikishe kuwa hapatakuwepo vitendo vya rushwa.
  Quote

  0 #90 Shamte 2011-04-01 16:39 Ni jambo la kusikitika kuwa kuwa wachangia mada katika jukwaa hili hawalitumii kama ilivyo kusudiwa badala yake wanalitumia kama kukashfiana. Ieleweke wazi kwamba imani ya kupona hutoka kwenye moyo wa mgonjwa. Endapo utaamini kuwa maji yaliyonuizwa na Sheikh au padri yatakuponya basi kweli itatokea. Na hata hiyo dawa ya Babu kama utainywa kwa kujaribu na sio kudhamiria kuinywa ili upone, basi kwako itakuwa haifai. Isipokuwa tu ningependa nianishe kuhusu maono ya Babu na wengineo. Nijuavyo mimi, Mwenye-enz-Mungu huweza kumpa maono mja wake akiwa macho na siyo usingizini. Niliwahi kumsikiliza mtaalam mmoja akitoa mada juu ya aina za tiba mbadala. Akaainisha tiba mbadala kwa makundi manne, lakini moja ambalo limenigusa ni lile aloliita tiba kupitia viumbe vya Mungu. Kwa mfano Mtu huweza kuingiwa na Jini na akaamrishwa afanye tiba kwa masharti mbali mbali kama vile kugawa kiasi cha fedha kwa makundi ya watu kadhaa wasiojiweza, misikitini, makanisani n.k. Hawa majini humjia mwanaadamu akiwa usingizini. Kwa hivyo, nawaomba wasomi waliobobea katika masuala ya dini walichanganue hili, ili kuweza kujua kati ya maono na ndoto. Hiyo ndio "homework" ninayo wapa, lakini kama nilivyokwisha sema hapo awali kwamba kupona kwa mtu kunatokana na imani ya tiba anayopewa kwa wakati ule akiwa mgonjwa. Na kutopona pia husababishwa na imani hiyo hiyo. Haya kazi kwenu.

  Ibn Saidi.
  Quote

  -1 #89 Mimi 2011-04-01 16:32 Quoting adili ignas:
  waheshimiwa ndugu watanzania tumwombe mungu wasije wakamuua babu maana dawa zao zi[NENO BAYA]sa bei​
  Hakuna anayeweza kuua nafsi ya mtu kama Mwenyezi Mungu mwenyewe hajataka.
  Hayo ni mawazo finyu.
  Quote

  +1 #88 Mimi 2011-04-01 16:28 Quoting RAIA MAKINI:
  KWA KUSEMA UKWELI LAZIMA TUTAMKUMBUKA BABA WA TAIFA KWA MAMBO MENGI SANA. IKIWAMO KUWAJENGEA WANANCHI WAKE KUTEMBEA MBELE KIFUA MBELE NA KURINGIA UFAHAMU WETU,KUJIAMINI NA KUTOKUENDEKEZA UMASKINI WA MAWAZO ULIOKITHIRI,TUL IONAO SASA.SIANA SABABU YA KUINGILIA MIPANGO YA MUNGU SIPO KATIKA NAFASI HIYO.ILA MUNGU PIA ANAWAHESHIMU WATU KAMA AKINA TOMASO.KWA SABABU NI YEYE HUYO HUYO ALIYETUKANYA KWAMBA TUSIPEPETWE NA KILA AINA YA UPEPO.KUTOKUJIAMINI KWETU NDIKO KUNAKOTUPELEKEA KUTEGA MASIKIO YETU PANDE MBALI MBALI ZA NCHI KUTAKA KUSIKIA NANI KAJA NA DAWA MPYA,BILA KUWA NA UHAKIKA KAMA IMETOKA KWA MUNGU KWELI.BABU SIJAMPINGA BADO IJAPOKUWA SIMWUNGI MKONO KWA ASILIA ZOTE.ILA HAWA WASANII WENGINE WALIOIBUKA NI JUKUMU LAKO KUWAUNGA MKONO KUENDELEA KUJIYUMBISHA.​
  WOTE SAWA TU, HAKUNA WA AFADHALI HATA MMOJA, YAANI SIO BABU WALA BIBI!! WOTE WANATAKA KUDHULUMU NAFSI ZA WATU KWA KUWAPELEKA KWA SHETANI.
  Quote

  0 #87 RAIA MAKINI 2011-04-01 16:22 KWA KUSEMA UKWELI LAZIMA TUTAMKUMBUKA BABA WA TAIFA KWA MAMBO MENGI SANA. IKIWAMO KUWAJENGEA WANANCHI WAKE KUTEMBEA MBELE KIFUA MBELE NA KURINGIA UFAHAMU WETU,KUJIAMINI NA KUTOKUENDEKEZA UMASKINI WA MAWAZO ULIOKITHIRI,TUL IONAO SASA.SIANA SABABU YA KUINGILIA MIPANGO YA MUNGU SIPO KATIKA NAFASI HIYO.ILA MUNGU PIA ANAWAHESHIMU WATU KAMA AKINA TOMASO.KWA SABABU NI YEYE HUYO HUYO ALIYETUKANYA KWAMBA TUSIPEPETWE NA KILA AINA YA UPEPO.KUTOKUJIAMINI KWETU NDIKO KUNAKOTUPELEKEA KUTEGA MASIKIO YETU PANDE MBALI MBALI ZA NCHI KUTAKA KUSIKIA NANI KAJA NA DAWA MPYA,BILA KUWA NA UHAKIKA KAMA IMETOKA KWA MUNGU KWELI.BABU SIJAMPINGA BADO IJAPOKUWA SIMWUNGI MKONO KWA ASILIA ZOTE.ILA HAWA WASANII WENGINE WALIOIBUKA NI JUKUMU LAKO KUWAUNGA MKONO KUENDELEA KUJIYUMBISHA.
  Quote

  +1 #86 Mimi 2011-04-01 15:53 Quoting fadhili:
  Hii inaonesha jinsi watz walivyo washirikina wakubwa. Wote waliokwenda kwa Babu wangeweza kwenda kwa waganga wa kiejyeji wanaotumia tunguri pia!Yote haya ni kwasababu ya u[NENO BAYA] uliokomaa na utegemezi wa miujiza kupata kila kitu na hii ndio imekuwa sababu kubwa ya inchii kutoendelea na kama tutakwenda kwa mwendo huu ipi siku akaja mtu akawafunga kamba Wabongo wote kama mbuzi na kuwapeleka machinjioni. Ni watu wachache tu watasalimika siku hiyo!​
  Nashukuru sana ndugu yangu, yaani unaonyesha jinsi gani ulivyo na upeo wa kuweza kukaa na kutafakari na kujua lipi JEMA na lipi BAYA.
  Quote

  +3 #85 fadhili 2011-04-01 15:47 Hii inaonesha jinsi watz walivyo washirikina wakubwa. Wote waliokwenda kwa Babu wangeweza kwenda kwa waganga wa kiejyeji wanaotumia tunguri pia!Yote haya ni kwasababu ya u[NENO BAYA] uliokomaa na utegemezi wa miujiza kupata kila kitu na hii ndio imekuwa sababu kubwa ya inchii kutoendelea na kama tutakwenda kwa mwendo huu ipi siku akaja mtu akawafunga kamba Wabongo wote kama mbuzi na kuwapeleka machinjioni. Ni watu wachache tu watasalimika siku hiyo!
  Quote  <center>1234567
  </center> Refresh comments list
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kama viongozi wenyewe tulio nao ndo hawa, basi tusahau maendeleo hadi kizazi kipya kishike madaraka.

  yaani barabara ijengwe kwa ajili ya biashara ya mganga wa tiba za jadi/asili mmoja tu? tena aliye mwanadamu kama mimi na wewe, akifa kesho (siombei), hizo pesa zitarudishwa hazina, au bado barabara itaendelea kujengwa? hizo pesa zilitengwa kwenye bajeti au ni mtindo uleule wa zimamoto?

  lini nchi yetu itakuwa na mipango na bajeti inayoeleweka ya maendeleo?

  sasa naamini kuwa asilimia kubwa ya viongozi tulionao ni washirikina. yaani hawa ndio ingetegemewa wawaongoze watanzania kupevuka kifikra, kumbe ndio wameganda kabisa kifikra katika masuala ya ushirikina!

  sio nyinyi mlionileta misri,
  bali Mungu alinipeleka mbele yenu ili kuwahifadhia masazo
  kwa ukombozi ulio mkuu
   
Loading...