Magufuli, ajaye ataweza wewe ukijenga taasisi imara za kisheria na kikatiba

Mh. Rais pole na majukumu na pole kwa kazi kubwa unayoifanya iliyo ngumu na nzito ya kuliletea taifa hili maendeleo. Mh nimekusikia ukilalamika kwa kazi nzito unayokumbana nayo kama kiongozi wa nchi.

Naomba kutumia uelewa wangu kwenye masuala ya utawala na sheria kukushauri jambo ili uache "Legacy" kubwa kwenye hili taifa labda kuliko hata legacy ya nyerere "JENGA TAASISI IMARA ZENYE NGUVU KIKATIBA NA KISHERIA" hata huyo anaekuja itabidi azitatue hizo changamoto unazoona au kuhisi haziwezi tatuliwa, Ukiacha taasisi imara zitamlazimisha rais na mtu yeyote yule chini ya jamhuri kutii sheria, kanuni, taratibu, utamaduni na kuongeza uzalendo kwa taifa.

Mh. Rais ni ngumu sana kwenye utawala wa nchi wewe kama binadamu kutatuwa matatizo mbalimbali kwa nguvu zako mwenyewe. Kwa mfano suala la rushwa. Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa labda iende ikaige huko "South Korea" au "Malaysia" ambapo hizo taasisi zimeweza kuwachukulia hatua hadi maraisi kwa kujihusisha na rushwa.

Hamna sababu kila rais ajaye tuwe tunaombea kupata a " strong man" kama wewe, hata ikitokea bahati mbaya tumebugi kama taifa tukapata rais dhaifu au mpigaji basi tutamuwa na amani kama taifa sababu tunauhakika kuna taasisi zitamdhibiti.

Nakuomba na kukusihi mh. Rais kama unauzalendo na kulipenda taifa lako na kuiangalia Tanzania miaka 100 ijayo ambapo sisi hatutakuwepo basi tuachie katiba bora kabisa yenye uwezo mkubwa wa kuiendesha nchi na kuondoa kabisa dhana ya "strong man". Kati ya vitu vilivyofanya wazungu waendelee ni kuwa na taasisi imara.

KATIBA, KATIBA, KATIBA MPYA na itakayotengenezwa sio kwa maslahi ya wanasiasa bali inayoangalia maslahi ya taifa ndio mwiba utaomchuma huyo Rais ajaye atakayeshindwa kutatua hizo changamoto.

Naomba kuwasilisha.
Hebu fafanua, ni ATAWEZA (CAN) au HATAWEZA (CANNOT)!
Samahani watu wa pwani hawapendi kutumia (h), huku hataweza ni ataweza na ataweza ni ataweza.
 
Back
Top Bottom