Magufuli aige mfano wa serikali ya Uingereza kuwapa msaada wa pesa wananchi wanapopatwa na majanga

Mra Eliphas

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
266
250
Tarehe 13 June saa 01.00 BST kwa saa za uingereza, huko London jengo la gorofa 24 liitwalo Grenfell Tower liliungua moto na watu 79 wanasadikiwa walikufa kwa moto huo ulioteketeza jengo hilo.

Familia nyingi zilizokumbwa na mkasa huo zilipoteza zaidi ya mwanafamilia mmoja.

Baada ya janga hilo kutokea , serikali ya Uingereza ilipeleka timu ya wataalamu kusaidia juhudi za uokozi.

Jumapili tarehe 18 June , Siku 5 baada ya janga hilo la moto kutokea, waziri mkuu was Uingereza Theresa May alitangaza kutoa msaada wa pound za kiingereza milioni 5 ambazo ni sawa na Tsh.14,241,860,500/= ( bilioni kumi na nne ,mia mbili harobaini na moja milioni, mia nane sitini elfu na mia tano) kusaidia watu waliopatwa na janga hilo.

Kila familia iliyopoteza makazi itapokea cash pound 500 sawa na Tsh1,424,186/= na pound 5,000 sawa na Tsh 14,241,860/= zitawekwa kwenye akaunti yake binafsi. Ndio kusema kila familia iliyoathirika itapokea jumla ya pound 5,500 sawa na Tsh 15,666,046.55 (milioni kumi na tano laki sita sitini na sita elfu na harobaini na sita na senti hamsini na tano.)

Vile vile msaada huo uliotolewa na serikali ya Uingereza utasaidia kuweka waathirika ktk makazi ya muda ( temporary accommodation) , garama za mazishi, na utasaidia ktk hatua za kisheria kwa waathirika watakaofungua mashauri mahakamani. Kiasi kingine cha pesa pound 1.5 milioni sawa na 4.27b za kitanzania zitatumika kulipia garama za matibabu kwa walioathirika kiakili.(mental affected)

Hata hivyo baadhi ya viongozi wamelaumiwa kwa namna walivyoshughulikia mkasa huo akiwemo waziri mkuu Theresa May, kwamba alishindwa kufika kwenye mkasa huo kuwaona waliopona Mara tu lilipotokea janga hilo.Baraza la miji la Kensington na Chelsea pia wamelaumiwa.Nb,fedha zote zilizotolewa kwa waathirika hao ni mfuko wa maafa wa serikali ya Uingereza na sio michango ya watu.

JANGA LA TETEMEKO LA ARDHI BUKOKAA TANZANIA.

Mfuko wa maafa wa serikali upo, watu walichanga mabilioni, nchi nyingi zilitoa michango, lakini hakuna muathirika hata mmoja aliyepata senti moja!. Pesa zote zilitaifishwa na serikali na raisi Magufuli akasikika akisema na kukebehi waathirika wa TETEMEKO lille kwamba eti duniani kote hakuna nchi inayotoa pesa cash kuwapa waathirika wa majanga!.

Raisi Magufuli sasa ajifunze hapa kwa Waingereza, ikiwa litatokea janga lingine basi waathirika wasaidiwe kwa namna hiyo kama waliivyofanya Waingereza. Na ajifunze kwenda kuwafariji wafiwa watakaokuwa wameumia na sio kuwakejeli na kuwatolea maneno yasiyofaa.
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,412
2,000
Ni kwasababu ni Kagera ..subiri ikitokea kwao huone kama hatowasaidia. Na mbona kwao tayari anawasaidia, rejea safari yake alivyoenda vijiweni kwa washona viatu
 

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,595
2,000
Aige ili iweje? Akili ya Kitanzania!!!!!

Wewe mtoto wako unampa nini ukitoka kazini? Unafikiri unafanya kama mtoto wa Manji au MO anavyomlea mtoto?

Iga ufe!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom