Magufuli aanza kazi J2 kwa vitisho......Kweli aanza vibaya......

Taarifa ya habari ya saa moja jioni ya leo ya TBC1, Waziri wa Miundo mbinu Dr. Magufuli amesambaza Ilani ya uchaguzi za CCM kwa watendaji Wizarani kwake katika hali inayoonyesha anachapa siasa zaidi na kuwataka watendaji wote kwenye Wizara yake kuisoma, kuielewa na kuifuata..................au vinginevyo waache kazi au wataondolewa.....................

Vile vile amesimamisha zoezi la ajira mpya TANROADS katika hali inayoonyesha mwingiliano kati ya Bodi ya Wakurugenzi na Wizara Mama.............Kiutaratibu Wizara Mama haipaswi kujiingiza katika shughuli za kiutendaji za TANROADS..........Hayo ni majukumu ya Bodi na Menejimenti.......

La kusikitisha zaidi ni sababu alizozitumia katika kuhalalisha Uongozi wa Wizara kuingilia zoezi la ajira mpya za Wahandisi wa Mikoa wa TANROADS............alidai wao wanataka barabara zijengwe tu..........kama vile waliopo kazi hiyo huifanya kwa ufanisi wakati sivyo hata kidogo..................

Magufuli anashindwa kuelewa ya kuwa ni sera ya TANROADS ili kuimarisha ufanisi ajira ni za mikataba na kama watendaji wataelewa ajira ni za kudumu hawatakuwa na motisha wa kuongeza ufanisi...............................Pia TANROADS ina kashfa nyingi za matengenezo bomu ya barabara ikilinganishwa na fedha ambazo serikali hutumiwa kwenye shughuli hizo zikiongeza kasi ya umuhimu wa kuubadilisha uongozi mzima wa TANROADS....................

Mbaya zaidi, zoezi la mabadiliko ya uongozi ndani ya TANROADS yamekuwa yakipingwa na wabunge hususani Bunge la 9 kwa sababu hizohizo za kujenga barabara wakati barabara nyingi ni bomu................hii yaashiria Regional Engineers na watendaji ndani ya TANROADS wana sauti kubwa kuliko hata Bodi yao ya wakurugenzi katika kuchelewesha mabadiliko ya uongozi ndani ya TANROADS kwa masilahi yao binafsi tu......Kwa mwelekeo huu usitegemee jipya kutoka kwa Magufuli........aonekana ni mchovu sana kifikra na sasa ategemea jina kuisukuma Wizara hii atakako..........

Magufuli alishakaa kwenye wizara hiyo na of course ndiyo iliyompatia umaarufu mkubwa. Miye na-assume kwamba anaujua udhaifu wa TANROAD vizuri sana. Sina hakika kama utakumbuka, lakini kuna wakati Magufuli alimkoromea sana Chief wa TANESCO wakati akiwa jamaa mmoja kama sikosei alikuwa ni Mghana. Alichomkoromea Magufuli ilikuwa ni matumizi makubwa ya fedha za walipa kodi kwa mambo yasiyo na tija. Kwenye tukio hilo, alisitisha ununuzi wa jengo moja Jijini Mwanza ambalo TANROAD walikuwa mbioni kununua. Baada ya mkwala huo, TANROAD walifanya kazi na walibanwa mbavu kila kona na matokeo yake ndiyo hayo tunayoyaona hata leo. Barabara nyingi na bora zilijengwa.

Kwa hiyo, ninachoweza kusema hapa ni kwamba ebu tumwache Magufuli aiongoze wizara ambayo amepewa dhamana na rais na tumpe muda tuone mambo atakayofanya. Uzalendo wa Mhe. Magufuli kwa taifa lake siutilii shaka hata chembe.
 
Chadema? CUF si ndiyo walikabidhi ilani yao wakidhani CCM itawasaidia kuitekeleza ...

...Halafu, wengine zao ndio zinatekelezwa. Ingawa walisusa.

...Kero zikiwa halisi, haijalishi nani ametoa ilani kuzitafutia mkakati wa kuziondoa. Zinashughulikiwa tu.
 
Napendekeza

Mhe. Dr. John Pombe Magufuli apewe ulinzi madhubuti. Please JK if you real need him. Yes I DO!

Naungana nawe mkuu. Mkapa kwa kujua utendaji kazi wa huyu jamaa, maadui wengi waliibuka na alimwekea ulinzi wa ziada.
 
Unawajua TANROADS kwa rushwa? mbona umetoa judgement haraka sana, magufuli at least tumpe muda ni mchapakazi, i said atleast, sasa
mm ni CDM, TANROADS is the worst acha awapige full stop kuajiri, ndio maana nasema unawajua vizuri TANROADS? nikutahadharishe tu RUSHWA kubwa sana duniani kote ipo sekta ya ujenzi, barabara, reli, bandari, airports, magorofa nk ( INFRASTRUCTURE)

Source please! TANROADS KWA RUSHWA? Isije ikawa hisia tu kama vile tulivyozoea kwa watu wa KAZITAMU (Customs)!
 
Mi sipo kwenye kusifiana bado nalia na nyumba za serikali tuu zilizouzwa bei chee
 
Mi sipo kwenye kusifiana bado nalia na nyumba za serikali tuu zilizouzwa bei chee

Angalau nyumba ziliuzwa kwa wazawa na Mkapa ndio aliesema lifanyike hilo. Magufuli couldnt do shit and he never will be able to on this issue. Ikienda mahakamani, ma jaji wote waliuziwa, ikienda cabinet, mawaziri kibao.. This will never be reversed and if it is, the compensation level and subsequent law suits would be in the courts for 30 years.. costing the government God knows.... ITS DONE!
 
Taarifa ya habari ya saa moja jioni ya leo ya TBC1, Waziri wa Miundo mbinu Dr. Magufuli amesambaza Ilani ya uchaguzi za CCM kwa watendaji Wizarani kwake katika hali inayoonyesha anachapa siasa zaidi na kuwataka watendaji wote kwenye Wizara yake kuisoma, kuielewa na kuifuata..................au vinginevyo waache kazi au wataondolewa.....................

Vile vile amesimamisha zoezi la ajira mpya TANROADS katika hali inayoonyesha mwingiliano kati ya Bodi ya Wakurugenzi na Wizara Mama.............Kiutaratibu Wizara Mama haipaswi kujiingiza katika shughuli za kiutendaji za TANROADS..........Hayo ni majukumu ya Bodi na Menejimenti.......

La kusikitisha zaidi ni sababu alizozitumia katika kuhalalisha Uongozi wa Wizara kuingilia zoezi la ajira mpya za Wahandisi wa Mikoa wa TANROADS............alidai wao wanataka barabara zijengwe tu..........kama vile waliopo kazi hiyo huifanya kwa ufanisi wakati sivyo hata kidogo..................

Magufuli anashindwa kuelewa ya kuwa ni sera ya TANROADS ili kuimarisha ufanisi ajira ni za mikataba na kama watendaji wataelewa ajira ni za kudumu hawatakuwa na motisha wa kuongeza ufanisi...............................Pia TANROADS ina kashfa nyingi za matengenezo bomu ya barabara ikilinganishwa na fedha ambazo serikali hutumiwa kwenye shughuli hizo zikiongeza kasi ya umuhimu wa kuubadilisha uongozi mzima wa TANROADS....................

Mbaya zaidi, zoezi la mabadiliko ya uongozi ndani ya TANROADS yamekuwa yakipingwa na wabunge hususani Bunge la 9 kwa sababu hizohizo za kujenga barabara wakati barabara nyingi ni bomu................hii yaashiria Regional Engineers na watendaji ndani ya TANROADS wana sauti kubwa kuliko hata Bodi yao ya wakurugenzi katika kuchelewesha mabadiliko ya uongozi ndani ya TANROADS kwa masilahi yao binafsi tu......Kwa mwelekeo huu usitegemee jipya kutoka kwa Magufuli........aonekana ni mchovu sana kifikra na sasa ategemea jina kuisukuma Wizara hii atakako..........

Tumepata maoni yako kuhusu Dr Magufuli na Wizara ya Ujenzi.
Hebu tupe pia maoni yako kuhusu Shukuru Kawambwa na Wizara aliyokuwa (Miundombinu)...
 
Kama ni mori, basi huu umeanzia kileleni. Natumai nguvu hii iliyooneshwa asubuhi hii itaendelea mchana hadi jioni. Hadi atakapochoka, atakuwa ametiisha adabu kidogo na heshima kurudi mahala pake.

Magufuli baba, lianzishe tu, barabara michosho zishatukifu, majengo yanayoanguka hovyo, sasa basi!

Bofya kifute hapo umsikilize kiduuuchu kilichorekodiwa kupitia TBC one. Taarifa ya maandishi inafuatia...

Siku moja tu baada ya kuapishwa, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na naibu wake Dk. Harrison Mwakyembe wamefanya kikao na Watumishi wa Wizara na kutoa maagizo kadha wa kadha.

Magufuli vs TanRoads vs Mrema

Mojawapo ya maagizo makuu, Waziri Magufuli alitengua maamuzi ya Mkurugenzi Wakala wa Barabara nchini (TanRoads), Ephraim Mrema na kuagiza mameneja wa mikoa waelezwe mara moja kuwa wamerudishwa kazini isipokuwa kwa nafasi ya Dodoma tu ambayo meneja wake hayupo. "Futeni hiyo mara moja, mameneja wa sasa waliopo nasema waendelee na kazi, maamuzi mliyochukua hayafai," akamwagiza Mrema kutoa tangazo haraka kuanzia leo katika vyombo vya habari, kusitisha tangazo lake la awali la kuwasimamisha kazi mameneja wa TanRoads mikoani kwa kuwa hatua aliyoichukua inaonekana ni ya kulipizana visasi. "Nimesoma katika gazeti moja wiki hii, umetangaza nafasi za kazi…kuna utaratibu kwa kazi zozote zinapotangazwa, hivyo waandikie vyombo vyahabari kuwa umefuta nafasi hizo..." "Nakuagiza Mrema, uandike katika vyombo vya habari kuwa umefuta tangazo hilo na mengine yatafuatia.” alisema na kukamtaka Mrema asifanye kazi kama mtu anayeondoka kesho, bali atekeleze majukumu yake kama atafanya kazi hiyo kwa miaka 100 ijayo.

“TanRoads jipangeni sawasawa, blaablaa ziishe, wewe Mkurugenzi uliona nafasi yako inatangazwa na wewe ukaamua kutangaza za mameneja wa mikoa ili kuchomeana na kila kitu kisimamishwe, kwanini ulitangaza kwamba waliopo hawachapi kazi?” alihoji Dk. Magufuli.

Kutokana na umuhimu wa usimamizi wa ujenzi wa barabara, Akamtaka Mkurugenzi huyo wa TanRoads, kufanya kazi kwa ushirikiano na kwamba kama Waziri na Naibu wake Dk. Harrison Mwakyembe watauliza jambo lolote, wajibiwe haraka, la sivyo itakuwa ni dharau. Mkurugenzi huyo wa TanRoads inadaiwa kuwa kipindi chake cha kuongoza wakala huo kimemalizika kwa mujibu wa mkataba wake wa kazi, lakini ameendelea kukalia ofisi hiyo.

Kunyang'anywa nyumba na kufikishwa mahakamani

Waziri Magufuli ameagiza wote waliouziwa nyumba za serikali ambao hawajamaliza madeni yao kufikishwa mahakamani pamoja na kunyangíanywa nyumba hizo. "Muwaandikie barua wote walipe au muwapeleke mahakamani na wasipolipa wanyangíanywe," alisema Magufuli na kushangaa kwa nini Wizara inahangaika suala la uhaba wa nyumba za watumishi wakati kuna pesa nyingine nje. Akasema kwa kawaida, hana lugha ya kidiplomasia na amewataka wenye madeni kuyalipa mara moja.

Magufuli vs Rushwa na Mizani

Dk. Magufuli alisema kasi ya ujenzi wa barabara na viwanja vya ndege imepungua kwa kiasi kikubwa, huku wafanyakazi wengi wakijihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwapa kazi makandarasi wababaishaji ambao lengo lao ni kuchuma. Waziri Magufuli aliahidi kupanda lori lililozidisha uzito na kutoa rushwa na akasema akikamilisha kazi hiyo watakaohusika watamtambua. Aliwataka watendaji wa mizani kusimamia sheria, kukamata magari na kupiga faini na kuteremsha mizigo bila kujali mmiliki wa gari au mzigo.

"Ukienda barabara ya Mandela, hujui kama kuna mkandarasi kwenye eneo lile ujenzi wa barabara nyingi kasi yake si nzuri, kama mkandarasi wa Mandela rafiki yako hafanyi kazi vizuri fukuza. Lazima niwaambiwe ukweli, mtu asiyetaka kuambiwa ukweli ajiandae kuondoka...," "...wananchi wamechoka kuona ubabaishaji huo, na kuanzia ni barabara ya Mandela, nataka taarifa ya ujenzi ndani ya mwezi mmoja, kwa maana mkandarasi sijui ni rafiki yenu au ni ndugu yenu kwani, hata kituo cha kazi hayupo sasa nataka ripoti yake alipofikia..." alisema Magufuli.

Akasema Watanzania wamechoshwa na maneno ya kubabaishwa na wataka barabara. "Maisha bora ni pamoja na barabara nzuri, nawapa mwezi mmoja mtafakari tuanze kujenga barabara za juu, tunaweza," alisema Magufuli.Alisema hakuna haja ya kuwasumbua askari wa usalama barabarani kuongoza msongamano wa magari, huku wakazi wa jiji wakilia na kulalamikia kero hiyo wakati nchi imesheheni wahandisi wa kutosha. Akasema kama maghorofa yanaweza kujengwa kipindi kifupi, iweje ishindikane kwa barabara za juu. “Hata barabara za juu zinawezekana, hivyo kazi ya matrafiki ibakie kukaa na kutulindia nguzo zetu na kukamata magari yanayofanya makosa,” aliweka wazi.

Waziri Magufuli alitoa maelekezo kwa bodi ya makandarasi kuwafutia vibali na kuwafukuza wale ambao wameweka zaidi maslahi kuliko kazi walizoomba. "Tutatumia sheria, lazima tuzihurumie fedha za Watanzania," alisema na kuongeza kuwa "...Serikali haiwezi kuendelea kuona kila kukicha makandarasi wanapanga bei wanazotaka," alisema.

Alionya wale wote wanaojihusisha na rushwa na kuwapatia ushindi wa zabuni makandarasi ambao ama hawana uzoefu au kwa kutaka pesa nyingi kutokana na gharama zao kuwa juu. "Tunajua rushwa ipo, hivi sasa makandarasi wapo katika mchakato tuache rushwa tutawaletea hata pesa za polisi...," “Magari yanazidisha uzito, ipo siku nitafanya msako wa kushtukiza kwa magari yanayozidisha uzito… nitaingia katika lori moja na kupanda halafu nitajibadilisha kwa kuvaa miwani na kofia ili nikamate wale wafanya kazi wenu wa mizani maana wanachukua rushwa sana...” “Sisi pia tutakuwa na kazi tutavamia maeneo na tukikuta mmeshindwa kufanya kazi tutafukuza mkandarasi na wewe ukifuata, hatutacheka na mtu tumekuja kufanya kazi maana barabara nyingi zilizochini ya Tanroads ndizo zenye matatizo, hivyo lazima malengo yatimizwe kipindi cha miaka mitatu,”alisema Waziri Magufuli na kuongeza kwamba kumezuka mtindo wa mtu anayetoa gharama za juu katika zabuni ndiye anapewa nafasi ya kwanza.

Ujenzi wa Daraja la Kigamboni na Uwanja wa Ndege Songwe

Kuhusu mradi sugu wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, Magufuli alionyesha kushangaza kuona ujenzi unasuasua na kutaka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuweka bayana kama hauwezi, atahakikisha linajengwa kwa fedha za serikali kwa kuomba kutoka Benki Kuu (BoT). "Kuna daraja moja refu sana kule China, urefu wake ni kwenda na kurudi Zanzibar mara tatu, walijenga kwa mwaka mmoja, sasa kwanini tunashindwa Kigamboni" alihoji. Aliitaka idara inayoshughulikia vivuko kuangalia uwezekano wa kununua vivuko vingine vinne, vitakavyokuwa vinafanya safari hadi Tegeta na Bahari Beach ili kupunguza msongamano wa magari barabarani.

"Tutasaidia wananchi badala ya kukaa kwenye foleni kwa saa nne hadi tano, sasa waweze kutumia dakika 45 kufika Tegeta," alisema na kuongeza kuwa kama serikali imenunua vivuko viwili, haishindwi kununua vingine kwa ajili ya kutoa huduma.

Kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege Songwe, alisema Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Prosper Tesha, anapaswa kuhakikisha na kusimamia kukamilika kwa uwanja huo uliopo mkoani Mbeya kutokana na mkandarasi kuchukua muda mrefu. “Lazima usimamie ukweli ni suala la kujiuliza kwanini ule uwanja haukamiliki na hauishi, inawezekana mnawabembeleza nini hao wakandarasi? naomba usimwogope mtu, fanya kazi hata siku ukifa amini utakwenda kuwa mkurugenzi mkuu wa viwanja vya ndege mbinguni,” alisema.

Kupoteza muda kwenye Majungu badala ya Kazi

Alisema baada ya kuapishwa, alikubaliana na naibu wake waanze kazi rasmi jana, kwani miaka mitano si mingi, ambapo aliwapa muda wa miaka mitatu wakurugenzi hao kuhakikisha yale yote yaliyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi yanatekelezwa ndani ya kipindi hicho.

"Hatujawaambia wote muwe CCM, ila kwa sababu wananchi wameamua, serikali iliyopo madarakani ni ya CCM, mnapaswa kuteleleza yale yote yaliyoahidiwa humu, kwa bahati mbaya sana mmeangukia katika mikono yetu, lazima mfanye kazi," alisisitiza.

Alisema wizara hiyo hivi sasa imegubikwa na majungu na rushwa, huku utendaji wa kazi ukiwa umezorota kwa hali ya juu. Alisema watendaji wazuri wamekuwa hawapewi umuhimu kwa sababu ya kuendesha majungu na kuwepo kwa makundi.

"Kuna mtu hapa amechora daraja la Umoja na lile na Mkapa, amefanya kazi nzuri sana, lakini hata siku ya ufunguzi, waliona kazi kumtambua kwa kumtaja jina tu, sasa nakurudisha kwenye madaraja endelea na kazi, najua ni fitina," alisema.

Muda wote wakati anazungumza, ukumbi ulizizima kiasi kwamba hakuna mtu yeyote aliyeweza kumnongíoneza mwenzie jambo, ambapo hata baada ya mawaziri hao kutoka, watumishi hao walikaa ndani kwa dakika kadhaa kila mmoja akisubiri nani aanze kutoka.

Kauli ya Dk. Mwakyembe

Awali, akizungumza Naibu Waziri Dk. Mwakyembe alisema Wizara ya Ujenzi katika miaka ya karibuni imepoteza sifa yake ya awali ya kuwa wachapakazi pamoja na kuwepo kwa wasomi wazuri. Alisema mwanzoni wizara hiyo ilikuwa mfano wa kuigwa lakini anashangaa kuona ufanisi umepotea na sasa imekuwa sehemu ya kunyoosheana vidole bila kujua ni kirusi gani huyo aliyeingia. Alisisitiza kuwa sasa wanahitaji kuongea lugha moja na kuimba wimbo mmoja na kuifanya wizara hiyo kuwa ya mfano na kuagiza taarifa za kukinzana zisipewe nafasi kwa kuwa hawaendeshi wizara kwa majungu na umbeya. Aliwataka wafanyakazi kuwa wakweli na kufanya kazi kwa uwazi zaidi. "Mmepoteza sifa, sioni kama wizara hii ni kitovu tena cha ufanisi, nasema bila kuchakachua, uteuzi wetu hautakuwa wa maana kama tutaachia hali hii iendelee," alisema. Aliwataka wafanyakazi wote kufanya kazi kwa bidii, kwani muda ni mdogo na mambo ni mengi.

Ushirikiano "lay a strong foundation first" Mwanzo-Mwisho

Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli na Naibu wake, Dk. Harrison Mwakyembe, walikuwa na kikao rasmi jana na wakurugenzi wa idara na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo, ambapo walitangaza kuanza kazi kwa kukabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Walisema wao hawakufika katika wizara hiyo kwa ajili ya kutengua Torati, bali kuitekeleza na kwamba wanaweza kufanya kazi na yeyote na kusisitiza kuwa yaliyopita yaachwe na wafanye kazi kwa pamoja, "ndiyo maana tumeamua kufanya ibada yetu leo hapa," “Tushirikiane, tupendane, majungu yaishe, tuache rushwa kwa kuwa tutawategeshea hata fedha ya Polisi… na hivi ndio maana Rais ametuteua mimi na Naibu mwenye taaluma ya Sheria,” alisema.

Waziri alisema ujenzi wa barabara mpya kwa kiwango cha lami utaanza kutekelezwa mara moja kama ilivyoanishwa katika Ilani, na kutaka apewe taarifa ya barabara zinazoendelea kujengwa za Tunduma/Sumbawanga, Sumbawanga/Mpanda, Arusha/Namanga, Singida/Kateshi/Babati na Babati/Dodoma/ Iringa.

credit ya habari magazeti ya UhuruPublications, HabariLeo na Mwananchi

from: Oho hou! Moto wa Magufuli umeanza... aluuu! -

Ninarudia tena..........huu ni mwanzo mzuri...............KUDOS to Magufuli and Mwakyembe for that good start..............
 
..mambo aliyoyasema Magufuli ni ya msingi na ya kupongezwa.

..lakini ningemkubali zaidi kama angejitakasa kwa kurudisha serikalini nyumba aliyojiuzia kwa bei ya peremende.

..i mean, it's OK kwa Magufuli kuwashughulikia mafisadi wa Tanroads, lakini sijui nani atamshughulikia Magufuli kwa ufisadi alioufanya.
 
Hiyo nyumba alijiuzia kwa bei gani? Je ni yeye aliyeamua kujiuzia? Je, Mkapa ile nyumba iliyokuwa wa NHC alinunua bei gani? Unalinganisha vipi kati ya hizi nyumba mbili in terms of bei na location? Ikumbukwe vile vile Nyumba ya Mkapa ilifanyiwa ukarabati wa hali ya juu kabla ya kununuliwa Je, nyumba aliyonunua Magufuli ilikuwa kwa mtindo uleule? Je, kama Magufuli asingenunua hiyo nyumba Mtanzania mwingine angenunua kwa bei ile ile? Je, wale wote walionunua nyumba hizo ambao wako serikalini walilipa mpunga mwingi zaidi wa aliolipa Magufuli? i.e katika nyumba ambazo pengine ki-hadhi hazitilafiani sana.
 
Wacha1 said:

Wacha1,

..baraza la mawaziri ndilo lililoamua nyumba za serikali ziibiwe/"ziuzwe."

..nasema ziliibiwa kwasababu zote ziliuzwa kwa bei ambayo ni way below market value.

..uamuzi ulifanywa na baraza zima la mawaziri, lakini mjenga hoja ndani ya baraza, na mtetezi wa wizi huo ktk bunge na public, alikuwa John Magufuli kama waziri mwenye dhamana na nyumba zile.

..hoja zako ni za msingi sana, lakini la msingi zaidi ni kwamba kilichotokea ni WIZI na UHUJUMU WA TAIFA WA WAZIWAZI.

..Magufuli kama kweli yeye ni msafi alikuwa na uwezo kabisa wa kuupinga uamuzi ule ktk baraza la mawaziri. kama ilishindikana angeweza kujiuzulu na wa-Tanzania wangemheshimu sana tu.

..kama ilishindikana kujiuzulu, basi angeweza hata yeye mwenyewe kuji-excuse katika wizi ule.

..kama hilo hapo juu limeshindikana bado ana nafasi ya KUTUBU sasa hivi na kurudisha nyumba ya WIZI serikalini.
 
Ngoja tukumbushane kidogo....

Kutoka 2006 na Charles Mullinda (TzDaima) Makala -Waziri Magufuli jibu tuhuma zako

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli, kwa wiki kadhaa sasa amekuwa akiandikwa sana katika baadhi ya vyombo vya habari nchini.
Anaandikwa kwa mambo mabaya, yasiyopendeza mbele ya jamii ya wastaarabu kama hii ya Watanzania. Magufuli anaandikwa kwa madai ya kuboronga kwenye suala la uuzaji wa nyumba za serikali wakati akiwa Waziri wa Ujenzi.
Tuhuma dhidi yake zilianza mbali. Kwanza vyombo vya habari vilianika kashfa aliyoifanya ya kupindisha ujenzi wa barabara ili ipite kijijini kwake.
Habari hii iliwashtua wengi akiwamo Magufuli mwenyewe, iliwatoa watu tongotongo kwamba madai ya baadhi ya wabunge, mawaziri wanaopendelea majimbo yao ya uchaguzi katika kugawa keki ya taifa, ni ya kweli.
Naamini taarifa hiyo ilikuwa sahihi, kwani Magufuli mwenyewe hajapinga madai hayo dhidi yake.
Hata Wizara ya Miundombinu haikuthubutu kumtetea, ilikaa kimya, dalili kwamba waliyokuwa wakifahamishwa Watanzania dhidi ya Magufuli, waziri iliyejizolea umaarufu katika serikali ya Rais Benjamin Mkapa, alikuwa hapendi wala kukubali wasaidizi wake wakosolewe, hata kwa jambo la kweli.
Nisisahau, kwamba wakati hilo likiripotiwa kwenye vyombo vya habari, Magufuli aliibuka na kudai waandishi wa habari kadhaa wamemtishia kumuua. http://www.freemedia.co.tz/daima/2006/8/26/tahariri.php
Hii ni habari ngeni katika historia ya vyombo vya habari hapa nchini. Wengi walimshangaa, vyombo vya habari hata vinavyomtetea sasa, vilimkosoa, vilimwambia 'Magufuli katika hili hapana', akawa kimya! Kimya kabisa!

Baadaye zikaja habari za Magufuli kutumia mbinu chafu kuwauzia baadhi ya ndugu na jamaa zake nyumba za serikali, kazi ambayo aliisimamia kwa nguvu zake zote, ingawa lilipingwa na baadhi ya wananchi na viongozi.
Hakuna aliyekuwa na jeuri ya kuhoji uamuzi huo wa Magufuli, hata waandishi wa habari hawakuwa na jeuri hiyo kwa sababu walikuwa wanamhofia Rais Mkapa kuwa angewakaripia. Walijua wakihoji zaidi na zaidi wataambiwa waandishi gani uchwara, wavivu, wa kufikiri, tukakaa kimya!
Magufuli aliuza nyumba zilizojengwa na Watanzania kwa ajili ya viongozi kama alivyokusudia, wengi walinyamaza kwa sababu ‘mkwara' alioutumia katika uendendeshaji wa kazi hiyo, ulikuwa mzito.
Nyumba zimekwishauzwa, Rais aliyesimamia utekelezaji wa kazi hiyo, Mkapa sasa hayupo madarakani, watu hawamwogopo tena, waandishi nao hawaogopi kutumia kalamu zao kuandika ukweli, hata ule unaowachukiza na kuwakera wakubwa. Ndipo ukweli kuhusu Magufuli ulipoanza kuanikwa.

Imeelezwa kuwa Magufuli, kwa kutumia madaraka yake, alimuuzia mdogo wake nyumba ya serikali wakati akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu, jambo ambalo ni kinyume cha taratibu.
Hatujali kama ni kontena au uwanja ama nyumba ya matope, kinachozungumzwa ni kwamba mali aliyouziwa Musa Magufuli ni ya serikali na taratibu za kuiuza zilikiukwa na kiongozi aliyekuwa akisimamia kazi hiyo, ambaye ni kaka yake.
Hilo likae pembeni. Lije hili la kimada wa Magufuli ambalo ni waandishi katika upekupeku wao wakagundua alimuuzia nyumba ya serikali kwa njia zile zile za ujanja ujanja.

Hata hivyo wanaomtetea Magufuli vikiwamo nyombo kadhaa vya habari, wanadai anaandamwa ili jina lake lichafuliwe mbele ya jamii, kiasi kwamba asiwe na jeuri ya kuthubutu kuwania urais mwaka 2010, madai ya ajabu ambayo kwa namna yoyote hayaingii akilini.

Janet Magufuli, ambaye ni mkewe, naye amekaririwa na vyombo vya habari akimtetea mumewe kuwa ni jambo la ajabu kwa watu wasiohusika kumpaka matope mumewe kwa kumhusisha na kimada.
Janet ni Magufuli na Magufuli ni Janet, kwa maana ya wanandoa, Magufuli kama Magufuli ni kweli anamuhusu yeye tu.
Lakini Janet ni lazima aelewe kuwa Magufuli kama waziri katika serikali ya Watanzania anawahusu Watanzania wote, hivyo ni sahihi kumjadili, kumsuta, kumkosoa na kumsifia kulingana na matendo yake.
Kwa wanaosema Magufuli dhidi ya tuhuma zinazomwandama, nitakubaliana nao iwapo Magufuli mwenyewe amewatuma wawe wasemaji wake, lakini kama si hivyo, hawa nao wanapaswa kujadiliwa kuwa ni vipi wanathubutu kuusemea moyo.
Mimi ninaamini kuwa kauli kwamba kuna kundi ambalo malengo yake bado hayajawekwa bayana, ambalo lilijipanga kwa ajili ya kumshambulia Magufuli ili asiwania urais baada ya Rais Kikwete, ni sahihi.
Ni kweli kuwa wapo watu ambao kwao kuwapotosha wenzao ili wapingane na ukweli badala ya kuukili ni kazi inayowapatia riziki.
Kuwachonganisha viongozi badala ya kuwaambia ukweli hata kama ni wa kuwakosoa kwa faida ya jamii na mienendo yao katika uongozi, ambao ni dhamana tu waliyopewa na wananchi, ndiyo kazi inayowaweka mjini, wanakula kwa kazi hiyo.
Hawa ni watu hatari wanaopaswa kuogopwa kama ukoma, wawe wanasiasa, madaktari au watu wa fani yoyote!
Kwa John Pombe Magufuli, kwanza ninampa pole, ninatambua uchapajikazi wake, ingawa kwa sasa nyota yake imechafuka, lakini ninayo machache ya kumuusia.
Mosi anapaswa kutambua kuwa tuhuma zinazomkabili ni nzito, zinatia doa, kwanza kwake yeye mwenyewe kama mtu makini aliyetokea kuvuma sana pengine kuliko mawaziri wote wa Serikali ya Awamu ya Tatu.

Pili tuhuma hizi zinaitia doa serikali ya mzee Mkapa ambayo alikuwa mfano wa kuigwa kwa uchapajikazi wake, tatu Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Kikwete ambaye amemwamini na kumbakisha katika moja ya viti vya uwaziri bila kujali kama alikuwa mmoja wa wapinzani wake katika mbio zake ndefu za kuwania urais au la.
Magufuli ibuka kutoka mafichoni uliko, ueleze umma wa Watanzania kama tuhuma zinazokuandama ni za kweli au zinania ya kukuchafua tu.
Kama kuna jambo ulilokosea, usione aibu kukiri na kuomba msamaha kwa sababu hiyo ni sifa ya uungawana. Lakini sikushauri ujiuzulu kwa sababu sitaki nieleweke vibaya kuwa nina wivu na cheo ulichonacho.
Na kama tuhuma hizo si za kweli, Magufuli ukanushe, kukaa kimya ni dalili ya kukubali kuwa yanayodaiwa dhidi yako ni kweli.

Hivi na ile issue ya Rose Garden iliishia wapi ? Mara ya mwisho nakumbuka madiwani walikua wanalalamika kwa nini Magufuli alliwapa Rose G hati miliki.

Mimi nasema, magufuli ni mchapa kazi sawa! lakini hainizui kuuliza mambo mengine ya msingi na kama kweli kafanya ufisadi then hana tofauti na mafisadi wengine...
 
Magufuli alishakaa kwenye wizara hiyo na of course ndiyo iliyompatia umaarufu mkubwa. Miye na-assume kwamba anaujua udhaifu wa TANROAD vizuri sana. Sina hakika kama utakumbuka, lakini kuna wakati Magufuli alimkoromea sana Chief wa TANESCO wakati akiwa jamaa mmoja kama sikosei alikuwa ni Mghana. Alichomkoromea Magufuli ilikuwa ni matumizi makubwa ya fedha za walipa kodi kwa mambo yasiyo na tija. Kwenye tukio hilo, alisitisha ununuzi wa jengo moja Jijini Mwanza ambalo TANROAD walikuwa mbioni kununua. Baada ya mkwala huo, TANROAD walifanya kazi na walibanwa mbavu kila kona na matokeo yake ndiyo hayo tunayoyaona hata leo. Barabara nyingi na bora zilijengwa.

Kwa hiyo, ninachoweza kusema hapa ni kwamba ebu tumwache Magufuli aiongoze wizara ambayo amepewa dhamana na rais na tumpe muda tuone mambo atakayofanya. Uzalendo wa Mhe. Magufuli kwa taifa lake siutilii shaka hata chembe.[/

Nakubaliana na wewe ila rekebisha hapo
 
Kuna tofauti gani kati ya MAGUFULI wenu na LOWASA? Hawa jamaa ni watumiaji wazuri wa Media na hasa TV basi. Kwa nje mnawaona hivo lakini kwa ndani acheni tu.
 
Wacha1,

..baraza la mawaziri ndilo lililoamua nyumba za serikali ziibiwe/"ziuzwe."

Kiongozi wa baraza la mawaziri alikuwa nani?

..nasema ziliibiwa kwasababu zote ziliuzwa kwa bei ambayo ni way below market value.

Kila Tom, Dick and Harry knows that!

..uamuzi ulifanywa na baraza zima la mawaziri, lakini mjenga hoja ndani ya baraza, na mtetezi wa wizi huo ktk bunge na public, alikuwa John Magufuli kama waziri mwenye dhamana na nyumba zile.

Si anaelekezwa cha kufanya na mshika mpini? i.e. rais. .... ..... Je, Wabunge wote nao walikubali kudanganywa na Magufuli pamoja na rais wao? Kama ikibidi hivyo kumbe huyu jamaaa ni smart sana au vipi? Yaani Wabunge walibaki kuwa mabwege na kukubali huu ulongo?

..hoja zako ni za msingi sana, lakini la msingi zaidi ni kwamba kilichotokea ni WIZI na UHUJUMU WA TAIFA WA WAZIWAZI.

..Magufuli kama kweli yeye ni msafi alikuwa na uwezo kabisa wa kuupinga uamuzi ule ktk baraza la mawaziri. kama ilishindikana angeweza kujiuzulu na wa-Tanzania wangemheshimu sana tu.

Yeye tu na sio wabunge, mawaziri wala rais? Wengine wote hao ni sawa ila yeye tu .... ...kazi kweli kweli ....

BTW ... ..... Ili akae wapi? Mkuu kwenye Nguchiro hata kenge wapo

..kama ilishindikana kujiuzulu, basi angeweza hata yeye mwenyewe kuji-excuse katika wizi ule.

Nani mtetezi mkuu wa wizi kama huu kama sio Rais? Pengine tuhamie nchi ya kusadikika au kama vile Robinson Cruso vile au Alladin na taa yake ya ajabu.

..kama hilo hapo juu limeshindikana bado ana nafasi ya KUTUBU sasa hivi na kurudisha nyumba ya WIZI serikalini.

Naona hapa unaongopa kwa nini hili shinikizo asipewe Mwizi wa kura au rais aliyekuwa madarakani?

Mkuu ulikosa nyumba nini? Au Magufuli alikukwaza mahali flani, atubu yeye tu wengine waendelee kupeta? Be serious tuongelee hasa mambo ambayo yatalisadia taifa na tuwe wakweli. hakuna mtu perfect lakini kwenye ukweli kama mtu anafanya kilicho chema kwa maslahi ya WTZ ni lazima tukubali tusipotoshe ukweli. Us as citizens kama kweli tunataka maendeleo ya Tanzania lazima tukemee kwa nguvu zote WIZI uliofanywa kwenye kuhesabu kura na mikingamo yake. Chama Cha Majambazi kimeonyesha kwamba kweli hadithi za Pwagu na Pwaguzi zinawezekana Tanzania
 
Back
Top Bottom