Mh. Rais kwanza nakupongeza kwa kazi nzuri na iliyotukuka, na hongera kwa kampeni ya kisayansi, kampeni imenoga na watanzania tunakukubali. Mh. Rais kuna jambo yawezekana ukawa unalifahamu ila kwa kuelezwa na wahusika kinafiki ili kufunika kombe, juu ya huduma zitolewazo na mfuko wa bima ya afya NHIF ya kufanya maamuzi ya kuondoa baadhi ya huduma za matibabu pasipo kuwajulisha wachangiaji.
Kuna dawa muhimu ambazo zinatufanya sisi wachangiaji kuzitumia ili tuelendee kuishi na kulitumikia taifa, na kuchangia pesa ziendelee kununulia madawa, wameamua kuzitoa makusudi. Unapoandikwa na daktari wako aina ya dawa hizo ukifika pharmacy za pale MOI unaambiwa zimeondolewa. Kitendo hiki kimewafanya wachangiaji na wategemezi wachukie na kuwafanya waugue mara tatu zaidi maana dawa hizo zinauzwa ghali sana.
Kuna wategemezi wetu, watoto na wazazi, wameondolewa kwenye bima. Ndiyo mtoto kafikisha miaka 18, lakini bado wanafunzi wanamuondoa kwenye huduma hizo za matibabu, wanadai walipiwe elfu 50,000/= sasa huo mchango kazi yake ni nini. Kwanini watoto wasiwaache wafikishe angalau kati ya miaka 24-25. Hiyo ndiyo miaka ya watoto wa kitanzania kumaliza elimu ya juu.
Kwa hili Mh. Magufuli wafanyakazi wanaumizwa, hao viongozi wa NHIF wanakuchonganisha nao. Nakuomba kwa kuwa wewe Bado ni RAIS na tutakuongezea mingine 5. Tunaomba suala hili waliangalie upya ili kutupunguzia machungu ya matibabu na maisha kwa kurudisha dawa zote zilizokuwepo hapo awali, kuwarudisha wategemezi wetu kwa huduma hii ya matibabu.
Mh. Rais ni hayo tu, najua nisiposema nitazidi kuumia japo kura yangu ni yako. CCM OYEEEEEEE