Magufuli a amemng’arisha Kikwete miundo mbinu,akiwa rais kung’ara zaidi kero ya barabara kuisha nchi

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
Miongoni mwa Sekta amabazo zimfanya rais Kikwete kukumbuka ni sekta ya miundo mbinu ambayo ipo chini ya waziri wake Dr. John Pombe Magufuli pia ni mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia kwa tiketi ya chama cha mapinduzi, katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne, Serikaliimepata mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara namadaraja nchini. Katika kipindi hicho, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa17,762 zimekuwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji ambapo barabara zenyeurefu wa jumla ya kilometa 5,568 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.

Aidha, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 3,873 zinaendelea kujengwakwa kiwango cha lami, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 4,965 zimefanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na Serikali inatafuta fedha za kuzijenga kwa kiwango cha lami. Vilevile, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara zenye jumla ya kilometa 3,356 unaendelea.

Pia serikali ya rais Jakaya Kikwete, chini ya waziri wake wa ujenzi dr. Magufuli itakumbukwa kwa ujenzi ujenzi na ukarabati wa madaraja, hakuna asiyejua kuwa miaka ya nyuma ilikuwa ikifika wakati wa masika kuna wilaya mbali mbali zilikuwa zinakosa mawasiliano na mikoa pmoja na miji mikubwa mpaka hali ya mvua zinapopungu hali hii ilikuwa inawakera sana wananchi kwa kuwa shughuli nyingi za maendelo zilikuwa zinasimama.

Serikali ya awamu ya nne ililiona hilo na ikadiliki kulivali njuga kwa fedha zetu za ndani bila kusubiri wafadhili, katika hili hata kama wapinzani watapinga lakini wanancjhi wanajua ukweli wa hili n hata kama utafunga safari uende katika maeneo ambayo yalikuwa na tata katika madaraja utapa majibu yake. Tumeshudia jumla ya madaraja makubwa 30 yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Kati ya hayo, madaraja makubwa 12 yamekamilika kujengwa, ambayo ni Rusumo (Kagera), Umoja (Mtwara), Mwanhuzi (Simiyu), Kikwete (Kigoma), Nangoo (Mtwara), Ruhekei (Ruvuma), Mbutu (Tabora), Mwatisi (Morogoro), Ruvu (Pwani), Nanganga (Mtwara), Maligisu (Mwanza) na daraja la waenda kwa miguula Mabatini (Mwanza).

Aidha, madaraja makubwa 6 yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi, ambayo ni Kigamboni (Dsm), Kilombero (Morogoro), Kavuu (Katavi), Sibiti (Singida), Ruvu Chini (Pwani) na Lukuledi II (Mtwara). Madaraja makubwa 12 yako kwenye maandalizi ya kujengwa ambayo ni Momba (mpakani mwa Rukwa na Mbeya), Mwiti (Mtwara), Simiyu (Mwanza), Wami (Pwani), Ruhuhu (Ruvuma), Ubungo Interchange (Dar es Salaam), TAZARA Flover (Dar es Salaam), Selander (Dar es Salaam), Daraja jipya la Wami Chini (Pwani), Pangani (Tanga), Kirumi (Mara) na daraja la waenda kwa miguu la Furahisha (Mwanza).

Sambamba na ujenzi wa madaraja makubwa, madaraja madogo madogo zaidi ya 7,200 yamejengwa na kukamilika. katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015 Serikali pia imeimarisha Mfuko wa Barabara ambapo mapato ya Mfuko yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 73.08 katika mwaka wa fedha 2005/06 hadi Shilingi bilioni 751.7 katika mwaka wa fedha 2014/15 ikiwa ni ongezeko la asilimia 928.6. ni ajabu sana pale kina Mbowe, Lipumba pamoja na Mbatia wanavyojifanya vipofu katika mafaniko haya ya awamu ya nne ambayo tangu uhuru yalikuwa kero kubwa kwa wananchi.

wakati Serikali ya Awamu ya Nne inaingia madarakani mwaka 2005, vivuko vya Serikali vilivyokuwa vinatoa huduma vilikuwa kumi na tano (15) tu. Hadi kufikia Aprili, 2015, idadi ya vivuko vya Serikali vinavyotoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini imeongezeka na kufikia ishirini na nane (28).

kwa upande wa nyumba na majengo ya Wizara ya Ujenzi chini ya Dr. Magufuli kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ilijenga nyumba 173 za makazi ya Viongozi wa Umma na kuanza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 za Watumishi wa Umma ambapo nyumba 643 zilikamilika katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015 na nyum,ba 270 zinaendelea kujengwa.

Aidha,Serikali kupitia TBA imeendelea kuhakikisha kwamba ujenzi wa nyumba na majengo yanayotumiwa na umma unazingatia mahitaji maalum hususan kwa watu wenye ulemavu. Suala hili limeendelea kutekelezwa kupitia miradi ya ujenzi wa majengo yote ya Serikali ambayo Wakala wa Majengo umesanifu na kusimamia kama ifuatavyo: Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara, Majengo ya Ofisi za Wakuu wa Wilaya za Bariadi, Rorya, Kilolo, Nyamagana na Mvomero. Mengine ni jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – Kitengo cha Wakimbizi,

Jengo la hospitali ya Manyara na ukumbi wa mikutano na Vituo vya Afya ya Msingi (Primary Health Centre Institutions – PHCI) – Iringa, majengo ya Ofisi za Wakuu 6 wa Mikoa ya Katavi, Njombe, Geita na Simiyu pamoja na majengo ya Ofisi za Wakuu wa Wilaya 19 za Buhigwe, Busega, Butiama, Chemba, Gairo, Ikungi, Itilima, Kalambo, Kaliua, Kakonko, Kyerwa, Mbogwe, Mkalama, Mlele, Momba Nyang`hwale, Nyasa, Uvinza na Wanging'ombe

Watanzania tunaamini kuwa sifa anazopata leo rais Kikwete kuhusu miundombinu zinatokana moja kwa moja na utendaji kazi wa waziri magufuli kuisimamia vyema sekta hiyo ya ujenzi na miundo mbinu nchini kote, tuaamini kuwa watanzania tutamuwezesha Magufuli kushinda kwa kishindo urais hapo octoba mwaka huu ili tuweze kupata lami wilaya pamoja na vijiji na vitongoji zaidi ya 14000 Tanzania nzima.
 
Ni kweli mkuu. Magufuli alisaidia sana kuifanya serikali ya Kikwete ionekane inafanya kazi. Big up magufuli. Endeleza moto ule ule. Sasa kwakuwa utakuwa rais mwenyewe sky is the limit.

Usisahau. Tengeneza timu nzur. Najua unajua hili
 
Magufuli tafta watu wenye uwezo, jasiri, wachapa kazi na wasio na tamaa wakusaidie. Tuone kama Tanzania haitosonga mbele. Safari hii uchumi wetu na hali za wananchi kiujumla usipopaa ntaamini kweli Tanzania tunagundu
 
Magufuli tafta watu wenye uwezo, jasiri, wachapa kazi na wasio na tamaa wakusaidie. Tuone kama Tanzania haitosonga mbele. Safari hii uchumi wetu na hali za wananchi kiujumla visipokaa vyema ntaamini kweli Tanzania tunagundu
 
Hivi uhai na barabara kipi ni kipaumbele zaidi?kama asilimia kubwa ya watanzania hawana uhakika wa kuiona kesho kutokana na changamoto ya ugumu wa maisha zinazowakabili...hizi barabara na madaraja tunazojenga tunatumia pesa nyingi kuzijenga ili zije kutumiwa na nani?ua wafu wanahitaji barabara?
 
Naamini atatafuta jeshi imara ambalo linaendana na falsafa yake ya kukabiliana na matatizo ya watu iwe usiku ama mchana ..
 
[video=youtube_share;1CnCjmzxOVY]http://youtu.be/1CnCjmzxOVY[/video]
Miundo mbinu ya kusadikika
 
Back
Top Bottom