Magufuli 2015-2020: Matarajio ya uchumi na changamoto zake | Page 10 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli 2015-2020: Matarajio ya uchumi na changamoto zake

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mchambuzi, May 12, 2016.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2016
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Utangulizi

  Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais J.P.Magufuli (CCM) imeanza kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha (2015-2020) kwa mujibu wa katiba ya JMT(1977).

  Vipaumbele vikuu vya serikali ya awamu ya tano ni pamoja na:

  ·Kurudisha nidhamu katika mfumo wa fedha za umma
  ·Kuziba mianya ya ukwepaji kodi na
  .Kubana matumizi ya fedha za umma.

  Sambamba na haya, serikali pia (kupitia waziri wa Fedha, Uchumi na Mipango, Dr. Mpango), imewasilisha sura ya bajeti ya mwaka 2016-17 pamoja na mapendekezo ya Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano (2016/2017 – 2020/2021).

  Tutajadili matarajio ya kiuchumi chini ya Rais Magufuli na Changamoto zake kwa kipindi cha 2015-2020. Tutafanya hivyo kwa muktadha wa dhana ya “Mabadiliko” tarajiwa ya Wananchi wengi, hasa maisha yao KIUCHUMI.

  Wananchi wengi (hasa maskini) wanatumaini Uchaguzi wa TANO wa Vyama Vingi (2015) katika dhana ya ''mabadiliko'' utaondoa mfumo unaoshadidia mambo YALE YALE kufanywa kwa namna ILE ILE na yenye matokeo YALE YALE kwa maisha yao kwa miaka zaidi ya Hamsini ya uhuru.

  Mjadala wetu umegawanyika katika sehemu kuu SITA:

  Sehemu ya Kwanza

  Tutajadili Matarajio ya wananchi Kiuchumi tukiyangalia katika maeneo makuu mawili:

  (1) Sura ya Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano (2016-17) na Mapendekezo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano (2016/17-2020-2021).

  (2) Tutajadili matarajio ya wananchi kwa undani juu ya yanayopaswa kuwa ‘Majukumu ya Serikali” katika Uchumi wa Taifa.

  Sehemu ya Pili
  Tutajadili ngazi kuu za Serikali – (i) Serikali Kuu” na (ii)Serikali za Halmahauri.

  Hapa tutaangalia kwa undani mgawanyo wa majukumu wa ngazi hizi mbili za Serikali katika kuleta ufanisi na matokea chanya kisiasa (demokrasia), kiuchumi na kijamii, kwa faida ya wananchi walio wengi.

  Sehemu ya Tatu
  Tutajadili Mamlaka ya Kodi na Mapato [“Taxation and Revenue powers”] katika ngazi mbili kuu za serikali – Serikali Kuu na Serikali Za Halmashauri.

  Tutatazama urali “Fiscal Imbalances” katika ngazi za Halmashauri na jinsi gani changamoto zake zinapaswa kutatuliwa kwa ushirikiano baina ya ngazi mbili kuu hizi za Serikali.

  Pia tutaangalia aina mbalimbali za Kodi:

  – Kodi zipi zinapaswa kusimamiwa na serikali kuu;

  - Kodi zipi zinapaswa kusimamiwa na Serikali ngazi za halmashauri; na

  - Kodi zipi zinaweza kusimamiwa kwa kushirikisha ngazi kuu mbili.

  Lengo kuu hapa ni kuleta ufanisi wenye matokeo chanya kwa maisha ya wananchi walio wengi - Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa(demokrasia)

  Sehemu ya Nne
  Tutajadili hali ya “Deni la Taifa” na changamoto (zitokanazo) kwa Serikali ya awamu ya Tano katika utekelezaji wa mipango yake mbalimbali ya kibajeti na kimaendeleo.

  Sehemu ya Tano

  Tutajadili hali ya baadae ya uchumi katika muktadha wa deni la NJE, kwa kufanya tathmini ya mwenendo wa deni la nje.

  Pamoja na mengineyo, tutajadili:


  · Historia fupi ya deni la nje.

  · Matumizi (kisekta) ya deni la nje.

  · Athari (impact) ya mikopo ya nje katika maendeleo ya uchumi na jamii.

  · Hatari (risk) iliyopo mbeleni ya nchi kuingia katika mgogoro mkubwa kiuchumi na hivyo kutoweza kukopesheka. Katika hili, tutafanya tathmini ya masuala makuu mawili:


  - Kwanza ni tathimini ya Mapato ya kodi kwa kuangalia iwapo katika kipindi cha 2016-2021, mapato haya yatatosha kuiwezesha serikali kulipa madeni ya nje bila ya kuathiri majukumu ya serikali ya kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.

  - Pili, ni tathmini ya Mapato ya Fedha za Kigeni kupitia mazao ya kibiashara nje ya nchi kwa kipindi cha 2016-2021, na kuangalia iwapo mapato haya yatatosha kuiwezesha serikali kulipa madeni ya nje bila ya kuathiri uwezo wake wa kuwajibika kwa wananchi.


  Sehemu ya Sita

  Sehemu ya Siita itakuwa ni hitimisho la mjadala.


  Bandiko linalofuata litaanza na sehemu ya kwanza:

  (1) Sura ya Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano (2016-17) na Mapendekezo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano (2016/17-2020-2021).

  (2) Tutajadili matarajio ya wananchi kwa undani juu ya yanayopaswa kuwa ‘Majukumu ya Serikali” katika Uchumi wa Taifa.
   
 2. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #181
  Jan 4, 2017
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Takwimu zako ni zile zile ambazo i have questioned na kujaribu sana kukuamsha kutoka kwenye usingizi pono wa msukule kwamba thats not the 'absolute truth'. Swali lako kuhusu national reserve ya chakula linaonyesha jinsi gani you are ignorant on these issues but also jinsi gani unatumika kama msukule kusafisha visivyo safishika.

  Majibu kwa swali lako lipo mdomoni mwa Waziri mwenye dhamana ya Kilimo (Chizeba) ambaye juzi ametamka rasmi kwamba akiba ya chakula iliyopo inaweza lisha taifa kwa siku saba tu incase of emergency? Sasa with your ignorance, endelea kupiga mahesabu ya 61 days, 91 days as if we are here to discuss maturity of treasury bills. Bei reflects supply and demand, i hope your ignorance self will realise that by now. You are definitely confused. Usiwe unaparamia mambo tu kuhalalisha ujira wako. Nenda kule jukwaa la siasa kwa akina MsemajiUkweli, Ritz, Lizaboni, na viongozi wako wengine humu mkapige siasa. GT sio jukwaa la siasa.

  Anachosema Waziri Chiseza is very much in line with my earlier concern kwamba takwimu kuhusu akiba ya taifa ya chakula na hata food inflation zimejaa ulakini kuliko ukweli. Natarajia urudi na spinning juu ya alichokisema Waziri. Mtumbueni maana anasema ukweli ambao always ni mchungu kwa genge lililopo Lumumba.

  Kwa mtu ambae anafuatilia mjadala huu objectively, taarifa ya Waziri kwa kiasi kikubwa inafanya sehemu kubwa ya takwimu zako na mijadala yako yote ielekee nyumbani kwake - kwenye choo cha shimo. The fact remains kwamba theres food insecurity inayonyemelea taifa, na muda sio mrefu uhalisia utajitokeza katika mfumuko mkubwa wa bei za vyakula (of which i have always maintained kwamba takwimu released haziakisi uhalisia). Muda sio mrefu wananchi wengi wataanza kufa njaa, lakini kwa vile CCM has always survived kwa exploitation ya mkulima kwa mfumo ule ule wa kikoloni, you will care less.

  -Tayari Longido (ITV news @8PM, 3/1/2017) tumesikia wananchi hawana chakula na badala yake wameamua kubadilishana mbuzi la beberu kwa debe moja la mahindi. Lakini pamoja na kupata hayo mahindi, bado wanakosa fedha za kwenda kusaga wapate sembe kwa ajili ya kusonga ugali kwa sababu hakuna fedha katika mzunguko.
  -Nadhani pia umesikia kuna mikoa wananchi wameanza kushindia wadudu kama mlo.
  -Pia huko Morogoro ambapo ni moja ya food baskets za taifa, leo ukibeba mfuko wa mahindi kurudi nao mjini baada ya Xmas na Mwaka mpya, njia nzima unakodolewa macho.
  -Pia nadhani unakumbuka Rais alilazimika kutembelea magereza mwezi November Mwaka jana na moja ya concerns zake ni kwamba food reserve ya taifa inakuputika and his estimation, wafungwa ndio wanaomaliza akiba hiyo, wanadoea vya bure, wafanye kazi ya kuzalisha chakula chao wenyewe. Inasemekana wafungwa wengi wanaachiwa huru kama njia ya kutanua national food reserve. What a deficit in policy making!
  -Mwisho nadhani unakumbuka wakuu wa wilaya (makada wenu Lumumba) walionywa kwamba asisikike hata mmoja akilalamika wananchi wake wana njaa. Kwa vile wapo kutetea matumbo yao, most likely wengi watakuwa na taarifa juu ya njaa na pengine hata vifo vitokanavyo ba uhaba wa chakula lakini hawawezi kusema ukweli kuogopa kutumbuliwa, na badala yake kuwaletea vitakwimu ambavyo mnatembea navyo humu and elsewhere vifua mbele kwamba thats the absolute truth.

  Inasikitisha sana.
   
 3. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #182
  Jan 4, 2017
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Siyo takwimu zangu, nimekuwekea mpaka video za watu wakihojiwa mitaani kuhusyu bei za mazao, na wanavyosema ni sawa na takwimu hizo. Na nimekupa mpaka link ya habari.
  Najua hapo umeshaelewa.

  mimi nakupa sehemu ya hiyo habari,


  Jan 04, 2017

  "Wakati Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe akidai kuwa hali ya chakula nchini siyo nzuri kutokana na uhifadhi mbaya, Serikali imesema hali ni shwari licha ya baadhi ya maeneo kutopata mvua za wastani.

  Zitto alidai jana kuwa Ghala la Taifa la Chakula (SGR) lina hifadhi ya chakula kinachotosha kwa siku nane tu wakati Novemba 2015 kulikuwa na chakula cha kutosha miezi miwili.


  Kwa mujibu wa Zitto, taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya Novemba inaonyesha kuwa Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula (NFRA), imebaki na tani 90,476 tu za chakula ambacho amedai ni cha kutosholeza siku nane.


  Hata hivyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba alijibu madai hayo ya Zitto akisema nchi ina chakula cha kutosha wala siyo cha siku nane wala mwezi pekee, bali zaidi.

  Dk Tizeba alisema NFRA inakuwa na akiba ndogo kwa kuwa mwaka 2016 ndiyo ambao nchi ilipata mavuno makubwa ya tani milioni 16 ambazo hazikuwahi kutokea, hivyo maghala ya watu bado yana akiba kubwa ya chakula hivyo wakala haukununua chakula kingi."

  Sasa wewe si utuwekee aliposema siku saba?


  Kwanini uuze mbuzi kwa debe la mahindi? Hiyo ni akili kweli? Kwanini unaona habari kama hizi zinal maana?

  Labda mwenzetu hujui bei za vyakula Tanzania. Haijawahi kutokea Morogoro ikawa na bei pungufu ya mahindi Zaidi ya Dar. Muulize mfanyabiashara yeyote. Morogoro mahindi ni expensive siku zote.
  Na hayo mambo ya kukodolewa macho njia nzima inaonyesha jinsi ulivyo looney.


  Kutembelea magereza au ziara ya kushtukiza UKONGA? Na akawapa 10bn za kujenga flats na zimeshaanza kujengwa?
  Mbona unapenda ku-exagerrate mambo? Nakuwekea video ya aliyoyasema na hakuna mahali aliposema food reserve inapukutika. Inasemekana na nani kuwa wafungwa wanaachiwa? Acha uongo!  Hehe, hizo taarifa si zingetolewa?
  Labda nikwambie tu kuwa uhaba wa chakula si jambo geni na linaweza kutokea popote duniani wakati wowote. Na ukiamua kuilaumu serikali Fulani, kuhusu uhaba wa chakula uwe na sababu.

  Nimekuonyesha kuwa takwimu hizi ndiyo prophets of doom wenzako kama Zitto Kabwe huzitumia. Kwani yeye ametumia takwimu gani kama siyo za BOT? Na wewe mwenyewe umenasa kwenye ulimbo na kuzitumia hizohizo na kuleta habari zako za vijiwe vya kangara talking about eight days.

  You are funny dude!
   
 4. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #183
  Jan 4, 2017
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Uliyoyasema hapo Bw. Mchunguzi ni kweli iliyoandikwa kwa wino wa dhahabu!
   
 5. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #184
  Jan 4, 2017
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Kobello,
  Unanikumbusha Kobello wa kwenye gazeti la sani, alikuwa haishi vituko.

  Ni sababu kama hizi ndio zinanifanya nirudie tena na tena kwamba you lack intellectual humility. Let me explain what you are expected of as an intellectual kabla sijajadili hoja zako:

  Ungekuwa mtu makini na unayejituma mwenywe kutafuta ukweli badala ya kusubiri upandikiziwe ukweli kichwani kama njia ya kulipatia tumbo lako mileage, mjadala wetu ungekuwa na manufaa sana sio kwetu sisi tu bali kwa wale wote wanaofuatilia. Mtu yoyote mwenye akili timamu anaona kwa uwazi kabisa kwamba katika sakata hili, Serikali inaacha maswali mengi kuliko majibu.

  Hoja kwamba akiba iliyopo NFRA inatosha kwa siku saba should have stimulated you intellectually, hasa iwapo ungekuwa unatazama mambo kwa lensi ya utaifa, ‘over and beyond partisan politics’. Unachofanya sasa ni kinyume. Na mbaya zaidi, bila ya kujijua, unashabikia maafa na njaa inayotunyemelea. Pengine haujui kwamba janga la njaa huwa halichagui dini, kabila, wala itikadi za kisiasa. Njaa huwa linalikumba ‘taifa’. Ni muhimu ukalielewa hili.

  I had always assumed that you are an intellectual only to learn later that you belong to a hybrid of jesters, demagogues and ideologues.

  · As an intellectual you were supposed to tell your society how it looks like at this juncture – is it CROOKED? Is it UGLY? You are stuck with ‘HANDSOMENESS’ of the regime.

  · As an intellectual you were supposed to articulate the fears and hopes in your society and in the process, warn it of the impending dangers and parade it into action.

  · As an intellectual, you were supposed to help your society give meaning to and read meaning into what may look as routine, obvious, and innocuous. You waste time on routine things, danganya watu kwamba yaliyopo is the absolite truth ambayo ni dhambi to question.

  You have definitely failed to play that role and obviously it’s out of both – fear, selfishness, arrogance and ignorance. Taifa linaangamia, nyinyi mnatembea vifua mbele. Kwa kweli hakuna tofauti na ugonjwa wa akili!

  Had you played your role as an intellectual, ungekuwa una hoji badala ya kuishi mazingira ambayo Lumumba trains you not to question even common sense issues, not allowed to analyze beyond the absolute truth inayoratibiwa vyema na Lumumba.

  Tuje kwenye hoja ya Waziri:
  Based on the above and based on the conclusion reached on the basis of evidence and reasoning, kimsingi Waziri Chizeba hana tatizo na hoja ya Zitto kwamba tani 90,000 zilizopo NFRA katika hali ya sasa ni kiasi kidogo mno and warrants our concern including Zitto’s. By the way, iwapo ungekuwa makini, ungekuwa na kumbukumbu kwamba suala la food insecurity, famine and food inflation looming nilijadili, way before Zitto emerged nalo. Hoja yako kwamba Zitto ndio kaniamsha ni utaratibu wako ule ule wa kutafuta kila upenyo Lumumba waone umefanikiwa kuharibu huu uzi. Trust me, unaunogesha zaidi kwa sababu hauna hoja consistent and coherent. Huu uzi haujajengwa na bandiko moja, ni muendelezo wa so many issues raised about policy deficit iliyopo katika Nyanja mbalimbali pamoja na athari zake kwa taifa. If you are not holistic in discussing the issues raised, your atomistic approach will only render you aibu.

  Turudi kwa Waziri Chizeba:
  Anashosimamia Waziri wa Kilimo na Chakula ni the “UNKOWN”, lakini kwa vile you lack that capacity intellectually, hauwezi kuona hilo. The unknown factor anayosimamia Waziri ni kwamba kuna Food Reserve available over and beyond kuta za NFRA – kwamba kuna chakula kingi kwenye maghala binafsi. Its only based on this ‘unknown stock’ ndio anapingana na hoja ya Zitto. He doesn’t get into details na hoja ya 90,000 tons and seven days kwa sababu kimsingi anakubaliana nayo. Anazidi kuharibu pale anapojenga hoja kwamba – had the government known of the outcome, basi ingekusanya stock from private warehouses. Haikufanya hivyo kwa sababu serikali haikuona maana. Kauli hii ilitosha kumfukuzisha kazi mara moja. And trust me, this statement will come back hard on the government down the road.

  Kingine cha ajabu ni pale Waziri anaposema kwamba kuna mahindi yanachepukia Kiteto sijui wapi wakati ushahidi upo wazi kwamba mahindi kule yamekauka. Wananchi bado hatuna uhakika iwapo hali ni shwari (food security), na ni kwa kwa sababu zipi za kuridhisha. Je:

  - Ni kwa sababu kuna akiba ya kutosha katika maghala binafsi ya chakula?
  - Je ni kwa sababu mahindi yameanza kuchepuka na serikali inasubiri kuyavuna hayo to replenish the stock at NFRA? Iwapo kweli yapo, itayanunua kwa utaratibu ule ule wa kunyonya wakulima - hati garani with fixed amount ambayo thamani by the time wanalipwa pesa inakuwa imeshaliwa na inflation kama mchwa?

  Kama mkakati ni kwenda kununua stock kutoka hayo maghala binafsi, mbona serikali haisemi yapo wapi, kiasi gani, itaenda lini na imetenga kiasi gani kwa ajili ya zoezi hilo?

  Serikali inasubiri nini kufanya hivyo and do away with the mounting fear across the nation?

  Tumeona Waziri Mkuu leo ameenda kutembelea NFRA, lakini kwa akili zenu hili mtaeleza wananchi kwamba its ‘routine’ (again against whats expected of intellectuals). Tumezoea serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu kufanya kazi kweli kweli – lini Waziri Mkuu ataenda kuyatembelea maghala binafsi kama alivyofanya leo kule NFRA? Kwanini asingeanza na hayo maghala binafsi na badala yake akaenda NFRA? Ina maana kila siku hapati taarifa za kiusalama including state of food security?

  Waziri wa Kilimo na Chakula kasema pia kwamba – “Japo siwezi taja kiasi cha chakula kilichopo kwa sababu za kiusalama…”. Hapo hapo anasema kipo chakula cha kutosha kulisha taifa kwa muda mrefu. Sasa kama kuna uhakika wa chakula/food security, hizo sababu za kiusalama za kutolifahamisha taifa ni zipi? Hakuna mantiki. Ni ushahidi tosha kwamba hakuna chakula over and beyond kuta za NFRA. That’s the bottom line.

  Nizungumzie kidogo kuhusu akiba ya chakula ya siku saba:
  Given all the above, as an intellectual unatakiwa uwe na mtazamo huu – iwapo taifa litakumbwa na dharura (kitaifa), iwe ni man-made, natural disasters, or combined, maana yake ni kwamba uzalishaji, uvunaji na usambazaji wa mazao ya chakula utaathirika kwa kiwango kikubwa. As an intellectual (rejea roles of intellectuals katika jamii) kuna tatizo gani kuhoji:

  · Hizi 90,000 tons na ushee zitatosha kulisha taifa kwa muda gani katika mazingira husika? Hivi unajua daily food consumption ya taifa ni kiasi gani?

  Nimalizie kwa kukuelimisha tu kwamba, linapokuja suala la food security katika taifa, factors kuu tatu come to play:

  1. Food Availability: upatikanaji wa chakula au the amount of food that actually exists (local production and other sources).

  2. Food Production Stability: absence of instability in food production as well as income caused by crop failures, loss of employment (fall of disposable income), import bottlenecks, lack of exchange etc.

  3. Food Accessibility i.e. of food supplies and it includes physical, social and economic access over time.

  As intellectuals we were supposed to utilize such frameworks kuchambua mambo and inform the society accordingly. You definitely not endowed with such capacity.
   
 6. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #185
  Jan 4, 2017
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Mimi nakupa facts, na natumia takwimu ambazo wewe mwenyewe unazitumia. Publications unazotumia wewe ndiyo mimi nazitumia na nimeshakupa mifano jinsi unavyojibana mwenyewe kwa kutumia takwimu unazosema zipo cooked. Why do you use them?

  Mimi najua Tanzania ni nchi masikini. I live and work in a very big economy, very rich and complicated economy, so I know what it takes to sustain such a big economy for a long time.Tanzania is nothing, it's not even fair to compare the two. Even my city's budget is bigger than Tanzania. Average budget per school kid is 11,000$ vs 30$ in Tanzania.

  There is nothing new that you have said, nothing to me. Ila unatumia takwimu na kuzitafsiri kisiasa na kipropaganda na mimi sitakuacha. That is my contribution.

  Sitakuacha kamwe na usitegemee hilo.Nimekuexpose Kamba zako nyingi tu na sasa hivi unayeyusha umehamisha magoli mpaka kufikia mjadala wa Food reserve. Hutoki hapa you are just tip-toeing.

  Unaweza kuwa na hoja kwamba Kagame ni mrefu kuliko Mwinyi na ukaishia hapo. Au ukawa mnafiki na muongo na kusema kuwa Kagame ni mrefu mara sita ya Mwinyi. Hapo watu makini watakuona wewe ni muongo na una exaggerate mambo kwa nia Fulani. Hapo ndipo patapokukosesha heshima. Especially usipoelezea kwanini umesema hivyo.

  Kwa hiyo hapo ulipopigia mstari hapana maana yeyote ile.

  Umeteleza ulipokadiria bajeti za sekta za elimu, afya na kilimo kwa kudhani kuwa bajeti za wizara ndiyo matumizi yote ya serikali kwenye sekta hizo. Je, ulitaka tunyamaze tu?

  Umeteleza kwenye deni la taifa uliposema deni la nje limeongezeka mara saba kati ya 2010 - 2016 (Rejea post #21). Je ulitaka tunyamaze?

  Ulisema hivi:

  Deni halikuongezeka mara saba katika kipindi hicho (according to BOT).

  Umeteleza kama mlenda uliposema kuwa NBS inapika data za inflation, tukasema tutafute inflation ya zao moja la mahindi na nikakupa mifano, wewe ukabaki tu kubwabwaja. Ulitaka tunyamaze? Katika hilihili umeteleza kwani ni wewe yuleyule uliyetumia inflation data za NBS kuonyesha kuna double digit inflation kwenye chakula (11%) na leo unasema 6% ni ya kupikwa? (rejea post #10)
  Mmmmmh! really?

  Ila food inflation at that time was 11%, so you were happy with (Y'all love double digit inflation, what a bunch of cowards!) So, this is what you said,


  Ukashauri hivi:  Sasa mbona hutupi mrejesho wa hayo maswali kuhusu takwimu zako? I can go on and on ...


  Mazingira husika yapi? Inawezekana ikawa hata siku moja. Wewe tuonyeshe aliposema ni ya siku saba, usiyeyushe.

  Are you?
   
 7. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #186
  Jan 6, 2017
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Sasa kama "unknown" ni sehemu ya total NFRA stocks, kwanini Waziri Tizeba angalau asitupe basi hiyo exact gross sum? Na pia atueleze hiyo gross quantity is sufficient to cover how many days/weeks/months.

  Mwenyezi Mungu atunusuru tu maana kauli za Dk Tizeba ni hatari mno, hasa aliposema haya maneno hapa chini...

  Ukiangalia movements za Serikali miezi ya karibuni zinaashiria wazi kuwa kuna tatizo kubwa mahali fulani :-

  1) PM Majaliwa kutembelea NFRA MICHUZI BLOG: MAJALIWA AKAGUA MAGAHALA YA HIFADHI YA CHAKULA CHANG'OMBE DAR ES SALAAM

  2) Dk Tizeba na majibu ya alichosema Zitto ambacho kwa uhalisia alinukuu sehemu ya ripoti ya BOT ya Novemba 2016. Zitto, Dk Tizeba wapingana hali ya chakula nchini

  3) Reshuffles mfano Waziri Tizeba amemwagiza Katibu Mkuu... - Ministry Of Agriculture Livestock and Fisheries | Facebook

  4) Taarifa na Ripoti mbalimbali za hali ya mavuno na chakula nchini kwa mwaka 2016/17
  Watelekeza familia kwa njaa
  http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/14565-wakulima-sasa-kupumua-kuuza-nafaka-nje-kwa-vibali
  Vihunzi vipya kwa JPM vyaibuka | Gazeti la Rai
   
 8. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #187
  Jan 6, 2017
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Tusubiri mpaka MARCH 1, 2017 Tuone kama bei ya unga wa mahindi haijapungua.
   
 9. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #188
  Jan 6, 2017
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Sawa, at least umekiri kuwa bei ya mahindi iko juu.
   
 10. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #189
  Jan 6, 2017
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Umeuvaa ulimbo kaka!

  Bei ya mahindi huongezeka mwezi DEC na june - Aug.

  Tanzania ina seasons mbili ambazo nazo zimegawanyika makundi mawili. Unimodal ya nyanda za juu na bimodal ya Pwani na Kaskazini.
  Kwa hiyo price ya mahindi huwa determined na seasons.

  Soma nilichoandika pia, kitakusaidia usipende kukumbatia informations za aina moja. The dude is crooked but I can't lie, I've learnt something from him.

  Do the same usijinyime!
   
 11. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #190
  Jan 6, 2017
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Mkuu Kobello,
  Kwanini sehemu Kubwa ya maandishi yako unamjadili Mchambuzi badala ya hoja zake?

  Na uchambuzi ni kuonesha matatizo yaliyopo,vyanzo vya matatizo ama viashiria na pia kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo,kwako ni tofauti.

  Mimi ni msomaji mzuri na nawafuatilia kila hatua. You're missing intellectual integrity bro.

  Tusaidieni kujadili kwa Kina na mapana.
   
 12. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #191
  Jan 6, 2017
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Mgaya D.W

  Nilianza hivi:-

  Swali langu la pili, hapo bado sijajibiwa na unaweza kuangalia tarehe.
  Comment yangu ambayo ni jibu baada ya kujibiwa na Nguruvi3,

  Baada ya hapo, Mchambuzi akanijibu kwa mara ya kwanza hivi:-

  Mpaka hapo tulipofikia, je unaweza kuniambia nani alianza kumshambulia mwenzake personally?

  Hata hivyo, mimi nilimjibu hivi (kwa sababu hapa tunajadiliana).
  Hpo sasa akaendelea kunijibu hivi,
  Sasa mpaka hapo, huoni kuwa jamaa alishaanza personal attacks? Hata hivyo mimi nilimjibu hivi:-

  Lakini kabla ya hapo Mag3 alituonya na kusema hivi:-

  Naomba uniambie mpaka hapo wewe unaonaje huu mtiririko? Nani anamkashifu na kumkejeli mwenzie?

  Akaendelea kunijibu hivi:-
  Huu wote ni mtiririko wa hoja zangu na kejeli zake..... hapo wewe unaonaje? Niendelee?
   
 13. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #192
  Jan 7, 2017
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  All the same Kobello. Mwezi March 2017 sio mbali tutakukutana panapo majaaliwa.
  Ujue hata ukisogeza milingoti ya magoli hii mechi matokeo yake hayachakachuliki.
   
 14. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #193
  Jan 8, 2017
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Haha .... nitaku-beep March.
   
 15. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #194
  Mar 13, 2017
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Kobello,
  Napenda kukumbusha juu ya ahadi yako....... ukizingatia kuwa mwezi Machi 2017 ndio huu na bei za unga wa mahindi bado ziko juu.
   
 16. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #195
  Mar 13, 2017
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Vipi Machi bado kufika Mkuu?
   
 17. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #196
  Mar 13, 2017
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ndio uzuri wa JF...inatunza kumbukumbu.
   
 18. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #197
  Mar 13, 2017
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Zitapungua. Tuliza boli.
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #198
  Mar 13, 2017
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Sawa mheshimiwa, tuzidi kuvuta subira...! Kama tumeweza kuvuta kwa nusu karne, what's a month or two! In the same vein what's a year or two! How about a decade or two! Yeah, tutulize boli.
   
 20. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #199
  Mar 13, 2017
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Right....
   
 21. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #200
  Mar 13, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Si tulisema March, hii habari ya zitapungua ni mwezi gani tena mwingine?

  Umekuwa mpooole! Right.....
   
Loading...