Magu, Mwanza: Mwalimu mkuu ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuomba rushwa ya 50,000

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Magu iliyoko Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Prosper Kagombolo amehukumiwa na Mahakama ya wilaya hiyo kwenda jela miaka mitatu ama kulipa faini isiyopungua laki tano kwa kosa la kuomba rushwa kwa mwanafunzi wake ili aweze kumpatia cheti chake cha kuhitimu darasa la saba.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo, Edmund Kente baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa ulalamikaji wakati walipokuwa wakieleza Mahakama mazingira ya tukio. Mshtakiwa alipelekwa jela baada ya kushindwa kulipa faini.

Mashahidi hao walieleza namna mwalimu huyo alivyomuomba mwanafunzi wake rushwa ya Sh 50,000 ili aweze kumsaidia kupata cheti chake huku akijua ni kinyume na taratibu za nchi kupitia kifungu cha sheria namba 15 (1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.

Hakimu huyo aliiambia Mahakama kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ipo katika kuwatendea haki watu wanyonge, hivyo watumishi wa serikali wasijione kuwa wako juu ya sheria kuliko watu wengine na wanaweza kuvunja sheria na wasichukuliwe hatua kwa kuogopwa kuwa ni watumishi wa serikali.

Aidha Kente aliwapongeza maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa jinsi wanavyojitaidi kupambana na watu wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi za utumishi wa umma.

Akitoa ushahidi kwenye Mahakama hiyo ya Wilaya, Mwendesha Mashitaka wa Takukuru Maximiliani Kyabona alisema kuwa walipata taarifa za mwalimu huyo kuomba kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mwanafunzi wake aliyemfundisha miaka ya nyuma mara baada ya mwanafunzi huyo kwenda shuleni hapo kuomba cheti chake.

“Mwalimu alimuomba kijana huyo kiasi cha Sh 50,000 kwa lengo la kutaka kumsaidia, ndipo mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) alifika ofisini kwetu kuomba msaada juu ya jambo huilo,” alisema.

Chanzo: Habari Leo
 
hapo ndo utawajua mahakimu wetu maskin anachezea adhabu kubwa...fisadi anaachwa kiulain...au maskin huwa wanabeba adhabu za wenye pesa
 
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Magu iliyoko Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Prosper Kagombolo amehukumiwa na Mahakama ya wilaya hiyo kwenda jela miaka mitatu ama kulipa faini isiyopungua laki tano kwa kosa la kuomba rushwa kwa mwanafunzi wake ili aweze kumpatia cheti chake cha kuhitimu darasa la saba.

Huyu mwalimu naye kweli hamnazo!!!
 
Hakimu huyo aliiambia Mahakama kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ipo katika kuwatendea haki watu wanyonge, hivyo watumishi wa serikali wasijione kuwa wako juu ya sheria kuliko watu wengine na wanaweza kuvunja sheria na wasichukuliwe hatua kwa kuogopwa kuwa ni watumishi wa serikali.

Hakimu anazinanga awamu zilizotangulia
 
Aidha Kente aliwapongeza maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa jinsi wanavyojitaidi kupambana na watu wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi za utumishi wa umma

Mbona wale wa kofia nyeupe njiani hawaguswi wakati nao wanapokea rushwa waziwazi
 
Elfu 50 miaka 5

Wa pesa ndefu na dhamana wanapewa na furaha maana hawarudi tena mahakamani kuendelea.. naamini kama huyo mwalimu angekuwa na pesa ya kuwaonga hasingefungwa miaka yote hiyo angekuwa sasa hivi anakenua meno kuwacheka walimpeleka mahakamani.

Hii inachekesha.. kwanza inasikitisha sana sana

Hata wanaopokea rushwa kwenye kazi zingine za serikali hawapati kifungo hiki.. wapo wanatanua na kuachia mabawa yao..

Sheria ya nchi hii inasikitisha sana sana sana..

Wizara husika inabidi waweke wazi sheria kwenye mtandao wao tujisomee yote juu ya makosa nchini kwetu hapa..
 
Na wakati huo huo Wabunge wote wa MACCM waliopokea rushwa ya milioni 10 kila mmoja toka kwa aliyesukumiziwa Ikulu ili wapitishe muswaada uchwara wa kuminya uhuru wa habari nchini wako huru na uchunguzi uliokuwa ukifanywa na Takukuru haujulikani umeishia wapi!!!

Back
Top Bottom