Magonjwa ya Zinaa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,297
33,082
Aina za magonjwa ya zinaa, ishara na dalili zake

STDs ni magonjwa ya zinaa, pia hujulikana kama maambukizo ya zinaa (STIs). Kwa maneno mengine ni maaambukizo yanayopitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia ngono. STIs husababishwa na bakteria na virusi.

STIs za kawaida ambazo husababishwa na bakteria zinajumuisha; Kaswende, Kisonono na Klamidia. Magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na virusi yanajumuisha; Ukimwi na Genital Herpes. Genital Herpes ni ugonjwa wa malengelenge ya neva ngozini unaoathiri viungo vya uzazi.

Unaweza kuathirika na magonjwa ya zinaa zaidi ya moja kwa wakati mmoja na mara kwa mara ikiwa umepatikana kuwa na ambukizo moja, unahitajika kupimwa ikiwa una magonjwa mengine ya zinaa ukijumuisha HIV.

Ni muhimu kufahamu ya kwamba mtu aliye na magonjwa ya zinaa yuko katika hatari kubwa ya kuambukizwa na HIV, kwa sababu STI hufungulia virusi njia ya kuingia mwilini. Ikiwa umepatikana na STI, unafaa kupimwa ikiwa una HIV. Wale ambao wameathirika na STI na HIV pia husambaza HIV kwa haraka kwa watu wengine. Kwa hivyo ni muhimu watibiwe haraka iwezekanavyo.
 
Kaswende

Mtu anapoambukizwa ugonjwa wa kaswende, mwanzoni huwa haonyeshi dalili zozote. Baada ya wiki mbili atapata kidonda ambacho hakina uchungu katika sehemu nyeti. Kwa sababu kidonda huwa hakina uchungu, watu wengi hawatakibaini kwa urahisi na kitapotea baada ya majuma 4-6.

Mara nyingine baada ya kidonda, kaswende huingia kwenye msururu wa damu na huleta homa, kuumwa na mwili na vidonda kwenye mdomo na sehemu nyeti. Wakati huu, mtu huwa na bakteria nyingi kwenye damu na anaweza kumuambukiza mtu mwingine kwa urahisi ikiwa watashiriki ngono. Ikiwa watu hawa hawatatibiwa, kaswende itabakia mwilini na inaweza kuleta matatizo kwenye ubongo ama kwenye moyo baada ya miaka kadhaa.

Kaswende inaweza kutibiwa kwa kutumia kiua vijasumu au Antibiotics kwa Kiingereza. Matibabu haya huua bakteria zinazosababisha kaswende. Ni muhimu kumaliza kiwango chako chote cha dawa ili kuhakikisha ya kwamba umepona vizuri. Ikiwa mama mja mzito ameambukizwa kisonono, mtoto ambaye hajazaliwa anaweza pia kuambukizwa. Wanawake wote waja wazito hupimwa ikiwa wana kisonono katika kliniki ili watibiwe mapema na kumlinda mtoto dhidi ya kuambukizwa.
 
Kisonono

Huu ni ugonjwa wa zinaa ambao ni wa kawaida na huathiri wanawake na wanaume kwa njia tofauti. Katika wanaume, dalili hutokea baada ya siku 2-5 baada ya kufanya mapenzi. Dalili dhahiri ni utetelezi ama usa mzito wa manjano kutoka kwenye uume. Hili husababisha hali ya kuchomeka na uchungu wakati unapokojoa. Uume unaweza kuwa mwekundu, kuvimba na huhisi uchungu unapoguzwa.Wanaume wachache huwa hawaonyeshi dalili zozote. Ikiwa hautatibiwa, unaweza kuharibu uume na kuzuia kupita kwa mkojo na manii.

Katika wanawake, dalili huwa sio dhahiri. Nusu ya wanawake ambao wameathiriwa na kisonono huwa hawaonyeshi dalili zozote na kwa hivyo huwa hawatibiwi. Wao huzidi kuambukiza watu wengine na mara kwa mara huathirika na matatizo ya vifuko vilivyo jifunga, ugumba na uchungu unaojirudia rudia katika sehemu ya chini ya tumbo (chronic pelvic pain). Wale ambao wana dalili hizi hupata homa, huhisi uchungu wanapokojoa na hutoa usaha kutoka kwenye uke baada ya siku 2-5.

Kisonono hutibiwa kwa urahisi haswa ikiwa matibabu yataanza mapema. Mtu huhitaji tu kutumia kiua vijasumu (antibiotics) kwa siku 7-10 ili apone. Mtoto anayezaliwa na mama ambaye hajatibiwa kisonono anaweza kupata ambukizo hatari la macho wakati wa kuzaliwa. Hili litahitaji matibabu na matone ya macho ya kiua vijasumu (antibiotics).
 
Klamidia

Huu unaweza kuwa ugonjwa wa zinaa ulio wa kawaida kuliko ugonjwa mwingine wowote wa zinaa unaoathiri wanaume na wanawake. Ugonjwa huu una dalili ambazo zinafanana na zile za kisonono lakini katika wanawake na wanaume, mara nyingi huwa hakuna dalili zozote.

Klamidia ni ambukizo ambalo huja na maambukizo mengine kama kaswende,kisonono na HIV. Ukiwa hautatibiwa, vifuko vya wanawake na wanaume vinaweza kijifunga na hivyo kusababisha ugumba (hali ya kutoweza kupata watoto). Ugonjwa huu hutibiwa kwa urahisi kwa kutumia kiua vijasumu.
 
UKIMWI

Huu ni ugonjwa wa zinaa ulio hatari zaidi kwa binadamu. Unasababishwa na kirusi kinacho sambazwa kwa urahisi wakati unapofanya mapenzi. Pia huambukiza watoto ambao hawajazaliwa wakati wa kuzaliwa na wanaponyonyeshwa. Hakuna tiba ya HIV na hivi sasa zaidi ya watu milioni 30 wameambukizwa kote ulimwenguni. Wengi wa watu walioambukizwa huishi katika nchi za Afrika zilizoko chini ya jangwa la Sahara na Wakenya 700 hufariki kila siku kutokana na Ukimwi.

Virusi huingia mwilini na kuharibu seli za ulinzi katika mwilini (kinga ya mwili). Pindi tu kinga ya mwili imedhoofika, mwili huathirika na maambukizo mengine mengi ambayo husababisha kuharisha, kutapika, kuumwa na kichwa, homa ya uti wa mgongo (menengitis), maambukizo ya ngozi na nimonia na hatimaye mtu hufariki kutokana na moja ya maambukizi hayo.

Kuna madawa yanayopatikana katika hospitali za wilaya ambazo hupunguza kiwango cha ukuaji wa virusi katika mwili. Madawa haya kwa hivyo yataendeleza afya ya mtu na kurefusha maisha yake. Hata hivyo hii sio tiba na virusi vitabakia mwilini. Mtu aliyeathirika anaweza kumuambukiza mtu mwengine na mbaya zaidi anaweza kujiambukiza tena mara tena. Na kwa kila ambukizo, kinga ya mwili hudhoofika na afya ya mtu hudhoofika.
 
k ya hawara yangu inakuwa inanuka afu inatoa ute mzito asubuhi, yaani ute ule wingi wake ni kama shahawa za mabao mawili...hata siku zile ambazo nilipumzika sikumduuu manake kama sivyo ningesema shahawa zangu ndo zinatoka...huo ni ugonjwa gani? na hapohapo anaumwa figo na zinakuwa kama zinamsumbua.
 
k ya hawara yangu inakuwa inanuka afu inatoa ute mzito asubuhi, yaani ute ule wingi wake ni kama shahawa za mabao mawili...hata siku zile ambazo nilipumzika sikumduuu manake kama sivyo ningesema shahawa zangu ndo zinatoka...huo ni ugonjwa gani? na hapohapo anaumwa figo na zinakuwa kama zinamsumbua.

Mshauri aende hospital
 
Back
Top Bottom