Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,299
- 33,080
Je, unajua historia ya magonjwa ya familia yako? Pengine unajua tu kuhusu mambo makubwa. Usishangae kwa mfano, kugundua kuwa nyanyako mkuu na dada zake watatu wote walikufa kutokana na saratani ya matiti, ingawa ugonjwa huu haukujitokeza kwa mama yako. Ama pengine unajua kuwa babako na ndugu zake wana ugonjwa wa Shinikizo la Damu mwilini na hujui iwapo ni la juu au la chini ama namna ugonjwa huu ulivyowaathiri.
Saratani ya Matiti
Wanawake walio hatarini kuupata ugonjwa huu ni:
- Ajuza
- Wenye asili ya kihindi au kizungu
- Wanawake ambao washaugua saratani ya matiti mbeleni
- Walio na jamaa wa karibu ( mama,dada,binti) ambao washawahi kuuguwa ugonjwa huu
- Wanawake wenye hitilafu ya kinasaba kutoka kwa mzazi aliyeugua ugonjwa huu
- Wanawake tasa au waliowapata watoto baada ya umri wa miaka 30.
- Wanawake waliopata damu yao ya hedhi wakiwa na umri mdogo kabla miaka 12.
- Wanawake waliokatika hedhi wakiwa wamechelewa baada ya miaka 50.
- Wanawake wenye matiti makubwa(daktari anaweza kukuelezea baada ya uchunguzi wa mammogram)
- Wanawake waliotumia tembe za uzazi,waliokosa kunyonyesha, wanaokunywa pombe kila siku,wanaonenepa sana baada ya kukatika hedhi,wanaomeza vidonge vya kubadilisha nasaba,na wale ambao hawakunyonyesha.
- Uvimbe kwenye matiti au kwapa
- Mabadiliko katika umbo la matiti
- Chuchu kutoa usaa ama titi kuwa nyororo
- Chuchu kupotelea ndani ya matiti badala ya kujitokeza nje
- Madutamaduta kwenye matiti kama yale ya maganda ya machungwa
- Kubadilika kwa ngozi ya matiti na chuchu kuonekana zimefura
Fanyiwa uchunguzi wa matiti mapema ili kutambua saratani ya matiti mapema.Kujichunguza kila mwezi na kufanyiwa uchunguzi wa mammograms mara moja kwa mwaka hasa wanaozidi miaka 40 in bora.