Magonjwa ya akili ya ngono.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
Huenda tumewaona wengi wao kama mashujaa, vijana wa kisasa au hata dada zetu wanaokwenda na wakati, kumbe ni wagonjwa wa akili.
Unasikiliza taarifa ya habari jioni. Unasikia kuwa, mwanamume amembaka mtoto wa miezi mitatu. Unaihoji nafsi yako… ni jambo gani lililosababisha akafanya ukatili huo? Je, ni tamaa kali ya ngono?

Wengine hudhani ni kisasi au imani za kishirikina na kwamba wahusika wametumwa.

Huu ni upotoshaji, lakini ukweli ni kuwa hayo ni magonjwa ya akili ya ngono ambayo yanawakumba asilimia 35 au zaidi ya Watanzania wote.

Watanzania hawa wanaugua magonjwa haya kwa wakati mmoja na kusababisha madhara mbalimbali kijamii, kiuchumi na migogoro katika familia na katika uhusiano.

Watu wenye magonjwa haya, si lazima watembee wakiokota makopo, kuvua nguo au kuwa na nywele ambazo hazijachanwa.

Hawa ni watu wa kawaida ambao tunafanya nao kazi, wenye uwezo mkubwa katika taaluma au pengine ni wazazi au hata walezi.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili na mtaalamu wa waathirika wa dawa za kulevya, Augustine Godman anasema, magonjwa ya akili kwa ujumla wake yanaweza kuzidi 1,886 lakini yapo yale ya ngono ambayo pengine yana changamoto lukuki kwa mwanadamu hasa Watanzania wasiofahamu kuwa ni magonjwa ya akili.

Dk Godman anafafanua kuwa magonjwa ya akili ya ngono kuwa ni yale yanayohusisha athari , upungufu au mparaganyiko au vitu visivyo vya kawaida katika tendo la ngono.

“Mtu anaweza kuwa na matatizo ya kihisia au ya kisaikolojia au vya kitabia katika suala la ngono na huweza kusababisha madhara au kutopata mafanikio,” anasema Dk Godman

Daktari huyu ambaye amewahi pia kufundisha Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (Muhas), kitengo cha magonjwa ya akili anasema watu wengi wana magonjwa ya akili ya ngono, lakini hawajui kama ni magonjwa na wanaendelea kuishi hivyo hivyo wakidhani ndivyo walivyo na baadhi wakipata matatizo katika jamii, wengine kufungwa jela au kupigwa kutokana na tabia hizo.

Mara nyingi tumekuwa tukiona wanawake wanavaa mavazi ya nusu uchi, wakizianika nje sehemu kubwa za miili yao.

 
shikamoo mzizi mkavu.ni P.M nikutumie zawadi ya Xmass.ili gonjwa baya sana linanisumbua sana ebu nisaidie Dr. nifanye nini ? nile nini? tusaidiane dokta wa ukweli.hii ndio thread nyinginezo mafotokopi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom