Magonjwa ya akili: Tukutane humu kama una mtu wa karibu mwenye ugonjwa wa akili

Curvyminx

Senior Member
Nov 29, 2016
179
220
Habari Wadau,

Wazo tu lilinijia majuzi kuanzisha hii thread. Unajua Waafrika hatuongelei hii issue sana kuhusu Afya ya Akili yaani Mental health issues. Na ikitokea kwenye familia basi tunashikana mashati kuwa ndugu yetu kalogwa, laana, katolewa kafara na suluhisho mara nyingi huwa ni kwenda kwa mganga au kuzunguka makanisa yoooote aombewe.

Chakusikitisha ni kwamba magonjwa ya akili yapo mengi from depression, bi-polar, schizophrenia etc na suluhisho izo mbili nilizotaja hazisaidii! Suluhisho ni kumuona daktari, apate ufumbuzi na kuanza kunywa dawa pamoja na kuahudhuria therapy, inategemea na diagnosis ya daktari.

Nina mzazi ambaye ni mgonjwa kiakili na hakuna maombezi yoyote yaliyosaidia na yuko na maradhi haya miaka mingi sana. Ilituchukua miaka 10 kuelewa kuwa ni ugonjwa na tunashukuru Mungu kuwa akizingatia dawa anakuwa salama anafanya shughuli zake kama kawaida ila asipozingatia dawa inakuwa hatari sana tunakuwa na hofu juu yake na sisi tunaomzunguka.

Tulivoanza therapy, nikagundua kuwa kuna wagonjwa wengi kama yeye, in a selfish way, nilifarijika kusikia kuwa si mzazi wangu tu mwenye tatizo kama lake, maana magonjwa haya tumezoea kuyasikia kwenye tv kama vile ni ya wazungu tu.

Mara nyingi, huwa najisikia vibaya sana anapoumwa, natamani angekuwa tu kama wazazi wengine, aliacha biashara zake kwasababu hakuweza kuitumikia 100%, hatakiwi kuwa na stress aina yoyote, anaweza kusema maneno makali sana asikumbuke, akikumbuka alichofanya analia kwa uchungu sana. Huwa anaomba msamaha kwa vitu alivyofanya au sema hata miaka 10 iliyopita, huwa najisikia vibaya sana japokuwa sisi tumezoea.

Nina uhakika kuna wengine mlioko kwenye situation kama hii, naomba tu share experiences zetu, breathe, exhale, najua ni ngumu sana. Naomba mchukue fursa hii kuongelea juu ya magonjwa ya kiakili, ni tatizo gumu sana kulitamka katika jamii yetu na mara nyingi tunayaficha.

Labda hapa ni sehemu nzuri kuongelea bila kuwa judged sababu ni maradhi yanatokea tu kutegemea na maisha ya mtu aliyokulia, lelewa, pamoja na mlundikano wa mawazo na kadhalika.

You are not alone!
 
mimi huwa silielewi kabisa hiyo neno 'ugonjwa wa akili' kwa nini uitwe hivyo, na te a bahati mbaya sana wagonjwa hawa huwa hawafanyiwi vipimo mbadala kama CT scan ya ubongo au MRI kujua kuna shida gani kichwani, na hivyo kupelekea hata watu wasio na mental disorders kuonekana wanazo. Unakua kuna vitu vingi sana vinaweza kupelekea mental changes kwa mtu, hata vimbe mbalimbali kwenye ubongo zinaweza pelekea hii kitu, au unakuta mtu alipata ajali damu ikavujia ndani kwa ndani akapata hili tatizo halafu unakuta watu wanaridhika kabisa na hiyo hali wakati vitu kama hivyo vinatibika kabisa.

Kuna umuhimu wa waTz kubadilika kidogo, tuwe na mazoea ya kufanya vipimo bila kuhofu gharama, hata kama huna tatizo fanya tu as check up kujua usalama wa miili yetu.

Pia hao wagonjwa tunaowaita '...wa akili' wanapatiwa matibabu bure na hospitali ni nyingi, hivyo sio busara mtu kama una ndugu ana hayo matatizo halafu ukamuacha tu vyumbani au unazurula mitaani wakati hospitali zipo na uwekekano wa matibabu kwa asilimia kubwa upo.
 
Pia hao wagonjwa tunaowaita '...wa akili' wanapatiwa matibabu bure na hospitali ni nyingi, hivyo sio busara mtu kama una ndugu ana hayo matatizo halafu ukamuacha tu vyumbani au unazurula mitaani wakati hospitali zipo na uwekekano wa matibabu kwa asilimia kubwa upo.[/QUOTE]

ni kweli, inabidi kufanya awareness watu waelewe kuwa ni ugonjwa/state of mind na pia kuelewa msaada unapatikana wapi, kwasababu zina tiba na wakati mwingine mtu anaweza endelea na biashara zake kama kawaida
 
1 kati ya Watanzania 4 ni kichaa ..hivyo anza kuhesabu comment ya kwanza mpaka ya nne ..uchukue vichaa wako
 
Poleni sana mkuu.

Hii ni kawaida sana kuna jamaa alikuwa anafanya kazi tanesco nae alikuwa na ugonjwa wa akili wa msimu ilikuwa ukionana nae hivi huwezi jua kama ana huo ugonjwa, ilikuwa akianza kuugua wanampeleka hospital ya wagonjwa wa akili Lutindi ila sasa hivi alishatangulia mbele ya haki.
 
Some people try too hard to prove how stupid they are!

Kulikua na haja gani ya kumuinsult mleta mada?

PATHETIC!
Huyu ndie aina ya vichaa niliokuwa nawasemea
Ametukanwa wapi ? Hizo si takwimu zilizo tolewa

Ndio mimi mjinga ,sasa wewe mwerevu zaidi ya hicho kingereza mbuzi unajua nini ? Kiswahili hukijui mpaka uchanganye lugha ? Au ndio ule ubishoo wa ukiongea kingereza ili uonekane wa masaki sio ? Nenda Mlimani City utawakuta wenzio sio Jf
 
Poleni sana mkuu.

Hii ni kawaida sana kuna jamaa alikuwa anafanya kazi tanesco nae alikuwa na ugonjwa wa akili wa msimu ilikuwa ukionana nae hivi huwezi jua kama ana huo ugonjwa, ilikuwa akianza kuugua wanampeleka hospital ya wagonjwa wa akili Lutindi ila sasa hivi alishatangulia mbele ya haki.

ahsante. mara nyingi mgonjwa haya akizingatia dozi anaweza kuendelea na shughuli zake kama kawaida na akaishi muda mrefu tu kwasababu sio life threatening sema tu madawa yake pia yana side effects ambazo nazo sio mbaya sana. Ilikuwaje akafariki?
 
1 kati ya Watanzania 4 ni kichaa ..hivyo anza kuhesabu comment ya kwanza mpaka ya nne ..uchukue vichaa wako

naelewa you do not have the thinking capacity to decipher this thread. But it is well with me. I wouldn't wish it to you or your enemy. Ila unatakiwa ushukuru Mungu kama wewe ni mzima kiakili, kiafya na kiroho (nahisi tu siwezi jua!)
 
naelewa you do not have the thinking capacity to decipher this thread. But it is well with me. I wouldn't wish it to you or your enemy. Ila unatakiwa ushukuru Mungu kama wewe ni mzima kiakili, kiafya na kiroho (nahisi tu siwezi jua!)
Mimi sio mzima aisee ,hiyo thinking capacity sina kabisa ,nachojua ni kuvaa suruali chini na shati juu sio vice-versa hivyo mimi inanitosha kabisa
 
Haya masuala mtu hawez kuyachukulia umakini mpaka yamkute... nina dada mwenye huo ugonjwa anatumia dawa na ana muda mrefu sana, anaendelea na kazi zake vizur ameolewa na ana watoto....!
 
Back
Top Bottom