magonjwa ni ishara za mwili kupungukiwa maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

magonjwa ni ishara za mwili kupungukiwa maji

Discussion in 'JF Doctor' started by Fadhili Paulo, May 25, 2012.

 1. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135


  IJUWE KIU


  Unasubiri KIU ndipo unywe maji? Na je kiu ni?:  NAMNA MPYA YA KUITAMBUA KIU:


  Ikiwa 'mdomo uliokauka au kiu' siyo kiashiria kikuu cha mwili kuhitaji maji, ni vipi hasa viashiria vya mwanzo na sahihi vya mwili kupungukiwa maji?.


  kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj na maoni ya kisayansi, kuna mafungu ya aina mbili tofauti ya hisia, yanayotoa ishara ya kiu ya eneo moja au mwili mzima.


  Mafungu haya yanajumuisha; Maono ya jumla ya kimawazo na zile ishara kubwa zaidi za dharura za sehemu moja au za jumla za kupungukiwa maji.


  Ishara za kimawazo zinajumuisha baadhi ya viashiria vifuatavyo ambavyo vimepewa majina kama 'matatizo ya kisaikolojia'. Ishara za mwanzo za mwili kuanza kupungukiwa maji:  • Kujisikia umechoka (uchovu): Sababu maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu.

  • Hasira bila sababu: maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu cha ubongo, mwili unapopungukiwa maji, ubongo unakosa nguvu kushughurika na hali mpya, mawazo na vitendo. Hasira inatokea kuwa ndiyo namna ya ubongo kujibu hali mpya zinazohitaji majibu, "Siwezi kufanya jambo hili”, sababu hauna nguvu za kutosha.

  • Woga na aibu: dr.Batmanghelidj amepata barua ya ushuhuda toka kwa mtu aliyekuwa akisumbuliwa na woga na aibu (agoraphobic) aliyejitibu kwa tiba ya maji.

  • Kujisikia umetengwa na usiyemkamilifu - huwezi kutimiza yale uyatakayo.

  • Kujisikia unaonewa.

  • Kichwa kizito uamkapo asubuhi: hakuna nguvu za kutosha kufungua mifumo ya mishipa ya fahamu.

  • Kukosa mantiki au sababu za maana unapoongea au kujibu na kukosa uvumilivu.

  • Kukosa usikivu na ufuatiriaji hasa kwa watoto na vijana; 'Uwezo wa akili wa mwanafunzi unapungua wakati kiasi cha maji mwilini kinakuwa chini ya wastani, kushuka kwa asilimia 2 tu ya uzito wa mwili sababu ya upungufu wa maji, kunapelekea matatizo ya usikivu na ufuatiriaji na uwezo mdogo wa kumbukumbu miongoni mwa wanafunzi'.

  • Kukosa usingizi mororo na kuota ndoto za kuogofya (nightmares).
  • Pumzi fupi, hatua za mwanzo za pumu, inashauriwa pia kunywa maji kabla ya michezo au mazoezi.

  • Utegemezi kwa vinywaji vya viwandani na vilevi (conditional reflex).
  • Kukata tamaa na hasira, ubongo hauna nguvu za kutosha kushughurika na matatizo mapya na unataka kuachana na mada (wacha lipite bwana, liwalo na liwe), ndiyo maana wahenga walipomwona mtu ana hasira, watampa glasi ya maji hata kiasi kidogo cha chumvi.

  Utakuwa umegunduwa sasa ni kiasi gani mwili wako umejihangaisha wenyewe kwa kujibana katika matumizi ya maji kiasi cha kukusababishia moja au yote kati ya matatizo yaliyorodheshwa hapo juu ambayo yangeondoka tu kirahisi kwa wewe kuamua kunywa maji kwa mtindo wa kutosubiri kiu ili kunywa maji au kusubiri kuona ishara za kupungukiwa maji.  Kabla upungufu wa maji (dehydration) haujakudhuru kufikia hatua ya umaututi, Mwili utazitoa moja kati ya ishara hizi za pili kubwa na za dharura (emergency calls) za uhitaji wa maji mwilini zifuatazo; vidonda vya tumbo, tumbo kunyonga, kiungulia, mafuta yaliyozidi, kansa ya utumbo mdogo, kukinaishwa na chakula, na ernia.


  Ishara zingine ni; Kansa, kisukari, kifua kikuu (TB), shinikizo la damu (BP), mfadhaiko (stress), matatizo ya moyo na kuzimia, magonjwa ya tumbo, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya Ini, pumu (Asthima), mzio (Allergy), chunusi, homa, kupunguwa nguvu na kinga ya mwili, matatizo ya kina mama, magonjwa mengine ni pamoja na homa ya uti wa mgongo, kansa ya kizazi, kikohozi, kuharisha, kikundu, nyongo, matatizo ya tumbo, kupungua uzito, upungufu wa damu (anaemia), vichomi, utipwatipwa na uzito kupita kiasi, kuzeeka mapema, na ishara nyingine nyingi.
   
 2. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #2
  May 26, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135

  KAZI ZA MAJI MWILINI


  BAADHI YA SABABU KWANINI UNAHITAJI MAJI KILA SIKU:

  Baada ya oksijeni, Maji ndicho kitu pekee ili kuishi. Chini utasoma baadhi ya sababu 41 za umhimu wa maji mwilini:  • Bila maji hakuna kinachoishi. Wakati wowote unapopungukiwa maji, seli zako hufa.
  • Panapotokea upungufu wa maji, kitu kimoja lazima kipotee, baadhi ya kazi za seli hufa.
  • Maji ndicho chanzo kikuu cha nguvu, maji ndiyo hela ya mwili, bila kunywa maji ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.
  • Maji hutumika kama moja ya malighafi katika usanifu na ujenzi wa seli, huziweka seli pamoja.
  • Maji hukinga uharibifu wa vinasaba (DNA), Vinasaba vichache visivyo vya kawaida huzarishwa.
  • Maji kwa uwezo mkubwa yanaongeza uwezo, nguvu na kinga ya mwili, ujuzi huu wote unahusisha pia dhidi ya kansa.
  • Maji ni wakala mhimu katika mmeng'enyo wa vyakula karibu vyote, vitamini na madini.
  • Maji yanatumika kusafirisha vitu vyote mwilini, maji yanapoifikia seli, huipa pia oksijeni na kuchukuwa hewa chafu hadi kwenye mapafu ili kutolewa nje ya mwili.
  • Maji huzisomba taka chafu toka sehemu mbalimbali za mwili hadi kwenye Ini na Figo ili kutolewa nje.
  • Maji ni mhimu ili kulainisha sehemu zote za mwili, hivyo kuzuia kufunga choo.
  • Maji huzuia shambulio la moyo na mshituko.
  • Maji ni mhimu katika kuupooza na kuupa mwili joto.
  • Nguvu za kiumeme katika maji hutupa nguvu za kufikiri, kufikiri kunahitaji nguvu, hivyo kuhitaji maji.
  • Maji ndicho kiamusho au kichangamusho (pick-me-up) pekee bora cha miili yetu kuliko kinywaji kingine chochote duniani, bila madhara.
  • Maji yatakurudishia usingizi wa kawaida na mororo, kila tuotapo ndoto mbaya au za kutisha (nightmares), mwili huwa unatuamusha kwenda kunywa maji. jaribu hii, siku yeyote ukiota ndoto ya kutisha, amka na kunywa glasi moja ya maji kisha rudi kulala.
  • Maji huzuia uchovu, huwapa vijana nguvu. Fikiri: unapokuwa na uchovu na ukaamua kuoga, baada ya kuoga sehemu kubwa ya uchovu hupotea. Hapo umeoga tu, je ukiyanywa maji yenyewe?!!.
  • Maji hutengeneza ngozi nyororo hivyo kuzuia kuzeeka mapema.
  • Maji yatausawazisha katika hali yake ya kawaida mfumo wa uzarishaji damu kwenye mifupa, hivyo kuzuia Leukemia na Anaemia.
  • Maji yatapunguza maumivu ya ishara za kutokea kwa hedhi.
  • Upungufu wa maji mwilini huzuia uzarishwaji wa homoni za kiume na kike, hii ndiyo sababu ya kwanza ya uhanithi (impotence) na kukosa hamu ya tendo la ndoa (negative sex libido).
  • Kunywa maji kutakutofautishia hisia za njaa na kiu ya maji, kunywa maji kwa muda na upunguze uzito na unene bila kuacha kula (dieting).
  • Maji yatazuia homa za asubuhi kwa mama mjamzito.
  • Maji yataunganisha mawazo na kazi za mwili, yataongeza uwezo katika kutambua malengo na nia.
  • Maji yatageuza utegemezi kwa vilevi ikiwa ni pamoja na pombe, kafeina na baadhi ya madawa ya kulevya.
  • Maji huzarisha nguvu za kiumeme na nguvu za kisumaku katika kila seli ya mwili - nguvu za kuishi. Nguvu za kiumeme zinafanya kazi kama nguvu za kisumaku na kuvipanga vitu anuwai kama sumaku hivyo kutoa uwepo wake sahihi na kujihusisha na matendo ya kikemikali.
  • Maji yanatumika katika kuvikatakata vyakula kuwa vipande vidogovidogo na hatimaye umetaboli wake.
  • Maji yatakiongezea nguvu chakula (transfoma chocheo ya chakula) na hatimaye chakula kutoa nguvu kwa mwili wakati wa umeng'enywaji wake.
  • Maji yataongeza uchukuwaji wa viini lishe mhimu vilivyomo kwenye chakula.
  • Maji ni kilainishi kikuu kwenye maeneo ya maungio (joints) na hivyo kuzuia ugonjwa wa yabisi na kupooza.
  • Maji hutumika kwenye 'diski' za uti wa mgongo kuzifanya zigongane na kufyonza maji.
  • Maji huzuia kuzibika (clogging) kwa ateri kwenye moyo.
  • Maji huzuia kupunguwa kwa umakini na usikivu kwa watoto na watu wazima (Attention deficit disorder - ADD).
  • Maji huongeza ufanisi katika kazi.
  • Maji yatazuia mfadhaiko, pupa na kukata tamaa.
  • Maji huzuia ugonjwa wa Glakoma.
  • Maji yataiyeyusha damu na kuizuia isigande wakati wa mzunguko wake.
  • Upungufu wa maji unavihifadhi vijidudu nyemelezi (free radicals) mwilini, na maji ndiye muondoaji mkuu wa vijidudu hivi nyemelezi.
  • Maji hutoa nuru na mng'aro kwa macho na kuhimili kuona kwa sababu kushughulika na taarifa za mwanga kunahitaji nguvu nyingi katika kusafirisha taarifa toka mfumo mmoja katika jicho kwenda katika mfumo mwingine kwenye ubongo ili kutafusiriwa.
  • Maji na mapigo ya moyo vinatengeneza muyeyuko na mawimbi ili kuzuia vitu visivyotakiwa kubaki kwenye mkondo wa damu.
  • Mwili wa binadamu hauna hifadhi (store) ya maji, ndiyo maana unatakiwa kuyanywa kila siku
  • Kunywa maji halisi, safi na salama kwa kanuni sahihi, kunausafisha mwili, maji yanaiacha sehemu ya chini ya utumbo mkubwa (colon) kuwa na uwezo zaidi wa kutengeneza damu mpya (fresh blood) ijulikanayo katika lugha ya kitaalamu kama 'Haematopaises', kwamba difu la utumbo mkubwa na utumbo mdogo (mucousal fold) huamushwa upya kwa njia hii.

  Ifike mahala tuache mazoea ya kuipa miili yetu maji ya mgawo (yaani tunapokunywa maji baada ya kusikia kiu).
   
 3. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  JITIBU KWA KUTUMIA MAJI

  MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA TIBA KWA KUTUMIA MAJI:  Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya maji ni; kunywa nusu ya uzito wako katika aunsi (ounces) ugawe mara mfululizo utakaoufuata kwa siku nzima. Kiasi kidogo chini au juu ya hiki, kinakubalika. Aunsi 1 = miligramu 31.25


  Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya chumvi ni, Robo tatu gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji, nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji.


  Pengine umeshageuza kichwa na kunisema, "Wewe ni kichaa.....hicho ni kiasi kingi sana cha maji". Ukweli ni kuwa, ni rahisi kunywa hivyo hasa tukitumia sentensi, ''Glasi 1 ya maji mara 8 kwa siku''.


  Mfano, kwa mtu mwenye uzito wa kilogramu 75:
  • Badili kilogramu kwenda aunsi kwa kuzidisha mara 2.2. Hivyo, 75x2.2 = aunsi 165.
  • Tafuta nusu ya aunsi kwa kugawa aunsi na 2. Hivyo, aunsi 165/2 = aunsi 82.5.
  • Gawanya mara mfululizo utakaoamua kuufuata kwa siku nzima, mfano mara 8 kwa siku. Kwa hiyo aunsi 82.5/8 = aunsi 10.3.
  • Badili aunsi kuwa miligramu za maji. Aunsi 1 = miligramu 31.25. Kwa hiyo aunsi 10.3x31.25 = miligramu 322.


  Kwa hiyo itampasa mtu huyo mwenye uzito kilo 75, kunywa ml 322 za maji mara nane kwa siku.


  Namna anavyopaswa kufuata hiyo ratiba mara 8 kwa siku:


  1) Akiamka tu (mfano saa 12 kamili asubuhi), cha kwanza atakunywa maji ml 322. ataendelea na shughuli zake za asubuhi


  2) Nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi (yaani saa 12:30 asubuhi), atakunywa maji ml 322. atasubiri nusu saa ipite ndipo atapata chakula chake cha asubuhi (itakuwa saa 1 kamili asubuhi).


  3) Kisha kula chakula cha asubuhi, atahesabu masaa 2 na nusu ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 3 na nusu asubuhi).


  4) Atahesabu masaa 2 tena ndipo atakunywa tena ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha mchana (itakuwa saa 6 mchana) kwa hiyo nusu saa baadaye atakula chakula cha mchana (yaani saa 6 na nusu mchana).


  5) Atahesabu yapite masaa 2 na nusu baada ya chakula cha mchana ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 9 kamili alasiri).


  6) Atahesabu masaa 2 na nusu yapite ndipo atakunywa maji ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha jioni (itakuwa saa 11 na nusu jioni). Nusu saa baadaye atakula chakula cha jioni (itakuwa saa 12 kamili jioni).


  7) Kisha kula chakula cha jioni, atahesabu masaa 2 na nusu tena ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 2 na nusu usiku).


  Muda wowote atakapokwenda kulala kuanzia saa 4 usiku atakunywa tena maji ml 322 kumalizia mara 8 zake kwa siku.


  Huyo alikuwa na kilo 75, sasa na wewe andika uzito wako na utumie fomula hiyo hapo juu ujuwe ni kiasi gani cha maji unahitaji kwa siku na kisha ufuate mara hizo 8 kama zilivyopendekezwa hapo juu. Kwa staili hii ndipo maji huwa ni zaidi ya dawa.


  Kumbuka, Kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ni kiasi cha chini kabisa, lakini mahala pazuri pa kuanzia, ikiwa ni mtu unayejishughurisha zaidi na mazoezi au unaishi katika mazingira ya joto zaidi, utahitaji zaidi ya hapo.


  Sasa, hutakubali kuwa kunywa maji kwa protokali hii ni kazi rahisi?.


  Ikiwa haunywi kiasi hiki cha maji kwa sasa, unapaswa kuanza kuongeza kiasi cha ziada kwa taratibu sana. Hii itaupa nafasi mwili kujirekebisha kuendana na kiasi ulichoanza kukiongeza, na ikiwa hautaupa mwili muda wa kujirekebisha, basi maji yatakuwa kama dawa ya kukojosha (diuretic), yakisukuma madini na vitamini za mhimu nje ya mwili, pengine na kukusababishia madhara zaidi kuliko faida.


  Watu wazee sana na watoto wadogo wanatakiwa kuanza kuongeza maji kufikia mahitaji yao kwa taratibu zaidi.


  Kwa kutumia mfano wa uzito hapo juu, itakupasa kuanza na glasi 3 siku ya kwanza huku ukiongeza glasi moja zaidi kila siku inayofuata mpaka ufikie glasi zote 8.


  Kumbuka kuwa, kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi na kula chumvi robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji, ni kanuni ya kimakisio tu. Baadhi ya wengine watahitaji maji zaidi wakati wengine watahitaji chumvi zaidi. Baada ya muda, mahitaji ya mwili kwa maji na chumvi yanaweza kuongezeka kidogo zaidi sababu ya mazingira ya joto, mazingira ya baridi au mazoezi ya viungo.


  Kila mmoja lazima apate kujua kiasi cha mahitaji ya mwili wake kwa maji kuanzia sasa.


  Kamwe usinywe zaidi ya aunsi 33.8 (lita moja) za maji kwa wakati mmoja ukiwa umekaa au umesimama.


  Watoto wadogo kuanzia miaka 2 mpaka 12, hasa wale wepesi kujishughulisha na mazoezi wanahitaji asilimia 75 mpaka 100 za aunsi za maji katika uzito wao kwa sababu miili yao inakua muda wote na kila seli katika miili yao inayokua inayahitaji maji haya ya ziada (mytosis).


  Tiba hii ya maji haitumiki kwa watoto chini ya miaka 2.


  Chumvi ya kawaida ya mezani iliyoongezwa madini ya iodini, itakusaidia kidogo, chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi sababu ya madini mengine mengi ya ziada zaidi ya 80 yaliyomo ndani yake. Chumvi ya baharini pia huwa na radha nzuri, nyeupe na umajimaji kidogo.


  Namna bora za kula chumvi:


  Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.

  Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.

  Ukiona viwiko, vidole, miguu, mikono au kope za macho zinavimba (kuvimba kusikotokana na ajali au jeraha), au unaharisha zaidi, usitumie chumvi kwa siku 2 mpaka 3, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena, lakini ichukuliwe taratibu. Kamwe usitumie chumvi zaidi ya robo tatu gramu kwa kila nusu lita ya maji.


  Kumbuka chumvi ikizidi hupelekea kuharisha.


  Dr.Batmanghelidj anasema, kunywa maji matupu kunaweza pelekea mwili kupoteza baadhi ya madini na vitamini zake mhimu nje ya mwili na hivyo kutozipa seli muda wa kutosha kuyatumia maji. Inashauriwa kutumia vidonge vyenye vitamini nyingi kwa pamoja (multivitamins) katika kila mlo wako ili kurudishia kile kitakachokuwa kimepotea (hasa ikiwa haufanyi mazoezi na kula kiasi kingi cha mboga za majani).


  Uvimbe utakapokuwa umepotea au umeacha kuharisha, unaweza kuendelea na mpango wako wa kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ingawa mara hii utayachukua kwa kiasi kidogo.


  Kwa siku nzima, anza kuongeza kiasi cha unywaji wako wa maji mpaka ufikie tena nusu ya uzito wako katika aunsi, anza pia kuchukua chumvi pamoja na maji. Unatakiwa kuhakikisha kuwa unapata gramu 150 za madini ya iodine kwenye "multivitamins" zako kila siku mpaka gramu 450 kwa siku.

  Ili maji yaweze kukutibu na kukukinga kwa kila ugonjwa, ni lazima....


  Kisha kunywa maji, maji yanapaswa kubaki ndani ya mwili masaa 2 mpaka 2 na nusu ili kuupa mwili muda wa kutosha kuyatumia maji hayo vizuri.


  Ikiwa inakulazimu kukojoa (peeing) chini ya muda wa masaa 2 tangu unywe maji, utalazimika:


  a) Kuacha kunywa maji matupu, jaribu kunywa juisi (uliyotengeneza mwenyewe) ya chungwa, ya limau, ya embe, ya papai, ya parachichi, ya zabibu, juisi ya matunda mchanganyiko, au juisi nyingine yeyote isipokuwa kwa watu wanaosumbuliwa na pumu (asthma) ambao hawatakiwi kunywa juisi ya chungwa. Kumbuka usizidishe kiasi chako cha ujazo unaopaswa kunywa kwa wakati mmoja kwa sababu tu ni tamu.


  Wakati huo huo mhimu kukumbuka kuongeza robo tatu gramu za chumvi katika kila nusu lita ya juisi yako.


  b) Ikiwa kunywa juisi hakutasaidia kupunguza kwenda bafuni kila mara, jaribu kunywa maji huku ukila mkate. Unaweza kuongeza krimu ya siagi au jamu kwenye mkate wako (the magic bagel).


  Kisha kutumia mkate siku moja au mbili unaweza kupunguza sasa kiasi cha mkate mpaka nusu yake, robo yake na mwisho juisi pekee pamoja na mlo wako.


  Utapaswa kurudi taratibu tena kutoka kunywa maji juisi mpaka kunywa maji matupu tena, baada ya siku kadhaa itakupasa kujaribu aunsi 2 za maji matupu nusu saa kabla ya chakula, kesho yake aunsi 4, siku inayofuata itakuwa aunsi 6 kisha 8 na kuendelea mpaka ufikie kiasi chako unachotakiwa.


  c) Ikiwa kunywa maji pamoja na kula mkate au katika juisi hakukusaidii kupunguza kwenda bafuni, Glasi ya maji (ml 250) matupu ikiongezwa na kijiko (kijiko cha chakula) kimoja cha asali au sukari halisi au walau sukari nyeupe kutakutatulia tatizo hili ukiongeza na chumvi 1/8 ya kijiko cha chai , tikisa na kisha kunywa mchanganyiko huo.


  d) Hakikisha unakunywa maji kwa mjibu wa kipimo chako kulingana na uzito wako. kunywa maji mengi zaidi ya kiwango chako husababisha maji kutoka nje ya mwili mapema kabla hayajatumiwa na mwili.


  e) Acha kwanza kinywaji chochote cha kutengenezwa kiwandani, acha chai ya rangi na kahawa. vinywaji hivi ni mawakala vikojoshi (diuretics), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili mapema kabla mwili haujayatumia. utarudi kunywa chochote ikiwa utavihitaji tena vinywaji hivyo mara utakapokuwa supa tena kiafya. Acha pia uvutaji wowote wa sigara na alkoholi.


  Bilashaka umewahi kusikia msemo, "Kwa sehemu kubwa tumetokana na maji", hii ndiyo sababu zaidi ya asilimia 94 ya damu yetu ni maji, zaidi ya asilimia 85 ya ubongo wetu ni maji, huku zaidi ya asilimia 75 ya sisi ni maji.

  Kwanini unywe maji glasi 1, robo saa kabla ya kula, au glasi 2, nusu saa kabla ya kula?:


  Wanyama wote hunywa maji halisi (plain water). Ikiwa utawachunguza paka na mbwa, mara zote hunywa maji na kusubiri wastani wa nusu saa kabla ya kula. Ratiba inabadilika wanapokuwa wanatibiwa, hapa hunywa na kisha hula papo hapo ama baadaye.


  Mfululizo huu ni mhimu ili kubaki na afya bora.


  Unapokunywa maji na kusubiri nusu saa kabla ya kula, maji yanaenda tumboni na kuziamsha tezi kutoa kemikali (homoni) kuzifunika kuta za tumbo ili kuzirinda dhidi ya haidrokloriki asidi ambayo huzarishwa wakati chakula kinawekwa mdomoni.


  Maji na kemikali hizo kisha huenda kwenye utumbo mdogo ambako kemikali hizi hukaa kusubiri chakula kitakachokuwa kinakuja baadaye. Maji hayo huru, yanauacha utumbo mdogo na kwenda katika seli zote za mwili na kuzijaza (kuzinyweshea) maji kama vile unavyonywesha bustani. Baada ya seli kuwa zimenyeshewa, maji yanayobaki kisha yanasukumwa tena kwenda tumboni ili kunyeshea chakula kilichofika.


  Nguvu zetu hazitokani na vyakula tunavyokula, bali zinatoka katika MAJI ambayo huiweka atomu ya haidrojeni katika chakula.


  Tunatembea katika haidrojeni.


  Vyakula tulavyo hutupatia vitamini na madini tunayoyahitaji ili kubaki katika afya.


  Ikiwa haunywi maji halisi (glasi 1 au 2) kabla ya kula chakula na kusubiri (robo saa au nusu saa), basi mwili lazima ujikope maji wenyewe.


  Kama mwili utakopa maji toka katika damu, basi ateri lazima zipunguze vipenyo vyake na moyo lazima utumie nguvu nyingi ili kusukuma damu ambayo ni nene (nyingi), kitendo hiki tunakiita 'shinikizo la damu' (BP).


  Ikiwa mwili utajikopa maji toka katika ubongo, utapatwa na 'kichwa kizito' au kichwa kuuma ambacho kinaweza pelekea maumivu ya kichwa.


  Ikiwa unakunywa alikoholi (pombe) na inavuta maji toka kwenye ubongo, utapatwa na kutokujisikia vizuri au uchovu (hangover).


  Watu wanaoishi katika nchi za baridi huweka alikoholi kwenye tenki zao za gesi ili kuvuta maji ndani ya gesi na hivyo kuifanya gesi isigande.


  Kokote katika ogani au tishu mwili utakakokopa maji, lazima ogani au tishu hiyo iachiwe madhara na hivyo kusababisha maumivu ama ufanyaji kazi wa ogani au tishu hiyo usio wa kawaida kama vile kufunga choo (constipation).


  kufunga choo au kupata choo kigumu sana kunatokea wakati mwili umekopa maji toka katika utumbo mdogo na sehemu ya chini ya utumbo mpana kunakopelekea taka za mwili kusimama kwenye kuta za utumbo mdogo na sehemu ya chini ya utumbo mpana (colon). Wakati mambo yako yanapokuwa na umajimaji, huteleza yenyewe chini bila kutumia nguvu yoyote.


  Kila tunapopumuwa hewa nje (exhale) tunapoteza maji.


  Ikiwa utahema juu ya kioo, utauona ukungu (maji). Tunapoteza glasi 4 za maji kwa kupumuwa tu kila baada ya masaa 24!!.


  kama mwili utakopa maji toka mapafuni, utapatwa na pumzi fupi itakayopelekea upatwe na pumu (asthima) na matatizo mengine yanayohusiana na mfumo wa upumuwaji.


  Mapafu na Moyo vinauhusiano wa karibu, kwa hiyo kama mwili utakopa baadhi ya maji toka katika mishipa ya moyo, utapatwa na maumivu ya moyo ambayo yanaweza kurahisisha kutokea kwa shambulio la moyo (heart attack).


  Mishipa inahitaji damu na maji wakati unafanya mazoezi, kwa hiyo kama unatakiwa kula chakula na kisha kutembea au kupandisha ngazi (za ghorofa) na una upungufu wa maji (dehydrated), unaweza ukapatwa na pumzi fupi, shambulio la pumu, utapatwa na maumivu ya moyo (angina) au kukakamaa kwa mishipa (cramps).


  Ndiyo maana wanasema; kamwe usiende kuogelea mara tu baada ya kumaliza kula kwa sababu mishipa itakakamaa.


  Mwili unapokuwa katika kazi yake ya umeng'enyaji chakula, huielekeza (diverts) damu toka katika mikono na miguu kwenda katika utumbo mdogo ili kusaidia umeng'enyaji wa chakula.


  Baadhi ya vyakula ni rahisi kumeng'enywa na vinawezeshwa na maji pekee, kama vile matunda na mboga za majani.


  Vinywaji vingine (liquid beverages) kama vile kahawa, chai, soda na juisi, siyo maji kwa mwili. Hivi ni vyakula pia kwa sababu ulimi unaipata radha ya viongezi (additives) na siyo radha ya maji halisi, na hivyo tumbo litaitowa haidrokloriki asidi. Mwili utakishughurikia kinywaji hicho kama chakula.


  Utafaidika na baadhi ya maji kama vile katika matunda na mboga za majani kwa masharti ya kinywaji hicho kutokuwa na kafeina (caffeine).


  Kafeina ni kikojoshi (diuretic), huyalazimisha maji kutoka nje ya mwili.


  Magonjwa mengine yanayoweza kuepukika kwa kunywa maji kabla ya kula ni pamoja na vidonda vya tumbo, tumbo kunyonga, kiungulia, mafuta yaliyozidi, kansa ya utumbo mdogo, kukinaishwa na chakula, na ernia.


  Kunywa maji masaa 2 au 2 na nusu baada ya chakula kunasaidia kumalizia umeng'enyaji wa chakula na kuunywesha mwili maji baada ya kukaukiwa kulikosababishwa na kazi ya umeng'enyaji wa chakula.


  kunywa maji ya kawaida katika joto la kawaida.


  Magonjwa mengineyanayotibika au kukingika kwa kutumia tiba ya maji ni; Kansa, kisukari, kifua kikuu (TB), shinikizo la damu(BP), mfadhaiko (stress), matatizo ya moyo na kuzimia, magonjwa ya tumbo, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya Ini, pumu (Asthima), mzio (Allergy), chunusi, homa, kupunguwa nguvu na kinga ya mwili, matatizo ya kina mama, magonjwa mengine ni pamoja na homa ya uti wa mgongo, kansa ya kizazi, kikohozi, kuharisha, kikundu, nyongo, matatizo ya tumbo, kupungua uzito, upungufu wa damu (anaemia), vichomi, vidonda vya tumbo, utipwatipwa, kuzeeka mapema, na magonjwa mengine mengi.


  Tiba hii ni nzuri kwa wote, wagonjwa watapona na wazima watabaki na afya bora na kujirinda dhidi ya maradhi kwa maisha yao yote.


  ''Kuna maajabu zaidi ya milioni katika glasi moja ya maji kuliko katika dawa yeyote utakayoandikiwa na muuguzi wako – dr.Batmanghelidj''.

  ANGALIZO:
  • Ikiwa hauendi chooni walau mara tatu kwa siku,unapaswa kumwona daktari kabla ya kuanza tiba hii.
  • Figo zako lazima ziwe zinafanya kazi vizuri, hii inamaanisha, kiasi cha maji unachokunywa lazima kiwe karibu sawa na unachotoa.
  • Wakati huo huo, kwenda chooni mara nyingi kwa siku kunaweza kukusababishia kupoteza vitamini mhimu, madini na elektrolaiti na kukufanya vibaya zaidi ya vizuri.
  • Unatakiwa kuwa makini sana unapoanza kuongeza uchukuaji wa maji mwilini, anza pole pole kwa kuongeza glasi 1 kila siku mpaka utakapofikia nusu ya uzito wako katika aunsi. lazima uupe mwili muda wa kujirekebisha baada ya kuzoea vinywaji kama kahawa, chai na soda, kwa kuwa vinywaji hivi huufanya mwili kujiendesha kwa namna nyingine.
  • Unaweza kuumwa na kichwa au unaweza usijisikie vizuri tu siku tatu mpaka wiki moja za kuanza tiba, usiache kunywa maji kwakuwa hayo si madhara bali ni dalili kuwa taka za sumu zimeanza kuondoka mwilini, baada ya muda utarudi katika hali yako ya kawaida.
  • Tunashauri watu wenye matatizo ya figo, Ini na moyo, kutofuata tiba hii mpaka watakapopata ruhusa ya daktari na muongozo sahihi.
  • Usinywe maji zaidi ya lita 3.78 kwa siku.
  • Usinywe maji kuanzia lita moja kwa pamoja au ukiwa umekaa katika mkao mmoja iwe kusimama au kukaa.


  Kumbuka pia kuwa hii ni elimu tu na siyo kumuondoa daktari wako au chaguo lako la kutumia dawa, ni programu iliyopendekezwa kwa manufaa yako.
   
 4. nilkarish

  nilkarish Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante sana fadhil makala nzuri snaaaa
   
 5. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Nashukuru mkuu, baki hapa, mengine mengi yanakuja. chukua kabisa glasi yako ya maji.
   
 6. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  MAAJABU YA CHUMVI

  seasalt4.jpg

  Stori kuhusu chumvi:


  Tunapata chumvi nyingi kwenye vyakula vyetu siku hizi. Chumvi nyingi itasababisha shinikizo la damu, uvimbe, matatizo kwenye kibofu cha mkojo, matatizo ya moyo na orodha inaendelea.


  Tunaambiwa chakula chenye chumvi kidogo au kisicho na chumvi kabisa ndicho bora kwa afya zetu.


  Ukweli kuhusu chumvi:


  Mpaka zama za pili za mawe (middle stone ages), hakuna chumvi iliyokuwa mbaya. Waharifu waliuliwa gerezani kwa kupewa chakula bila chumvi, iliwasababishia kifo cha taratibu.


  Miaka 2000 iliyopita, chumvi ilitumika kama hela. Dhahabu na Chumvi vyote vilikuwa na thamani sawa. Neno 'salary' (mshahara) linatokana na neno 'salt' (chumvi).


  Hapa kwetu Tanzania, watu hutumia msemo, 'Nimekula chumvi nyingi' kumaanisha kuishi miaka mingi.


  Katika siku hizo za kale, chumvi ilitumika pia kuhifadhia vyakula. Siku hizi tunatumia rifrijereta, kwa hiyo chumvi chache inahitajiwa isipokuwa kwa matumizi machache ya kusokotea nyama.


  Wanyama wote wenye damu moto, lazima wawe na chumvi ili kuishi. Ubongo wa binadamu pamoja na uti wa mgongo, vimo katika mfuko wa maji chumvi uitwao 'cerebrospinal fluid (csf)'. Umajimaji huu huzunguka sehemu zote za ubongo na uti wa mgongo.


  Sote tulitumia miezi tisa kuishi katika mifuko ya uzazi ya mama zetu inayoelea kwenye maji chumvi (amniotic fluid).


  Machozi yetu ni chumvi na tunatokwa na jasho ambalo pia ni chumvi. Mifupa yetu ina uwazi katikati yake (uboho) ambamo seli za damu hutengenezwa. Uboho huu umefunikwa na tabaka nyingi za chumvi kalisiamu kama vile kamba inavyoshikizwa pamoja. Kowa chumvi (salt crystals) zinashikizwa pamoja na kalisiamu, na kowa hizi ndizo zinazoifanya mifupa yetu kuwa imara, na siyo kalisiamu pekee.


  Mifupa inamiliki asilimia 27 ya chumvi yote mwilini. Wakati mwili unahitaji chumvi zaidi, huikopa toka mifupani, jambo hili likitokea, kalisiamu huondolewa pamoja na chumvi na kuifanya mifupa kuwa miembamba, laini na midhaifu.


  Chumvi imeundwa kwa Sodiamu na Klorini, kwa pamoja inaitwa; 'Sodiamu Kloridi' (Na Ci).


  Sodiamu ni metali laini yenye chaji chanya (+), wakati Klorini ni gesi yenye chaji hasi (-) ambayo hubadilika kuwa katika hali ya umajimaji inapoongezewa shinikizo.


  Klorini ni gesi au umajimaji, lakini kwa namna fulani wakati dunia imeumbwa, klorini ilibadilika kuwa ngumu pamoja na sodiamu na madini mengine. Unaweza kuisaga chumvi na kuwa katika unga, klorini bado itabaki na sodiamu.


  Klorini katika hali ya ugumuugumu, huitwa Kloridi.


  Chumvi tutumiayo siku hizi inatoka katika bahari, maziwa, mito au katika migodi ya chumvi. Zaidi ya sodiamu na klorini, chumvi yote kwenye sayari yetu huja pamoja na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake!.


  Kwa hiyo tunaweza kuona ni jinsi gani madini hayo yalivyo na umhimu kwetu, la sivyo yasingeshikamanishwa na chumvi. Kwa sababu ya thamani yake kibiashara, madini hayo huondolewa ili kutengeneza faida kubwa.


  Mwili wa binadamu una uwezo wa kuienguwa klorini kutoka katika sodiamu kadiri inavyohitajika. Damu yetu huihitaji klorini kama zifanyavyo ogani zingine ndani ya miili yetu.


  Tumbo huitumia klorini kutengeneza haidrokloriki asidi inayohitajika ili kuuwezesha mfumo wa umeng'enyaji chakula kufanya kazi vizuri.


  Miili yetu pia huitumia sodiamu kloridi kama chumvi kuufanya ubongo, uti wa mgongo, machozi, mifupa, tezi za jasho, ogani na damu kufunikwa na chumvi.


  Mwili unanufaika pia kutoka katika madini mengine yaliyomo katika chumvi ili kuuweka katika hali ya ualikalini na afya.


  Ni kama na vile kwa kunywa maji kuzidi kunaweza kumuua mtu (hyponatremia), vivyo hivyo kwa kutumia chumvi kuzidi, kunaweza sababisha; uvimbe, kuharisha na kifo.


  Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto 1093. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile 'aluminium silicate' huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).


  Sodiamu iliyozidi inaweza kutokea kutokana na kula vyakula vingi vyenye viongezi (additives) vya sodiamu. Sodiamu siyo chumvi, chumvi ni sodiamu-kloridi. Sodiamu bikaboneti, sodiamu benzoeti na monosodiamu glutameti (msg) ni baadhi ya viongezi hivyo.


  Sodiamu, potasiamu na kloridi ni elektrolaiti (madini maalumu) ambayo huyeyuka katika maji na kubeba chaji za kiumeme na kuzipeleka sehemu zozote za mwili kuliko na maji. Madini haya yenye chaji za kiumeme yana uwezo wa kuingia na kutoka ndani ya seli kwa uhuru wote, huku yakipeleka lishe ndani na kubeba nje taka na maji yaliyozidi ili kuiacha seli katika hali yake ya usawa (balanced cell).


  Wakati huo huo, kadiri elektrolaiti hizi zikitembea ndani na nje ya seli na kufanya mabadiliko yake, usawa maalumu wa Potasiamu ndani ya seli lazima utunzwe kwa kiasi maalumu cha sodiamu na kloridi ili kuishikilia potasiamu ndani katikati ya seli.


  Elektrolaiti zinapatikana kwenye majimaji yote mwilini na hubeba mapigo (impulses) kwenye neva zetu. Kitendo hiki huusaidia moyo na kiwambo cha moyo (diaphragm) kusinyaa na kulegea.


  Elektrolaiti hubeba Glukozi (damu yenye sukari) na kuipeleka ndani ya seli baada ya Insulini kufungua milango kwa ajili ya sukari kuchukuliwa.


  Elektrolaiti pia huwasha pampu za kuzarishia nguvu ziitwazo kwa kitaalamu 'Cation pumps' ambazo huzarisha umeme ambao huifadhiwa kwenye beteri zijulikanazo kwa kitaalamu kama 'mg Adenosine Triphosphate (mgATP)' na 'mg Guanosine Triphosphate (mgGTP)' za mwili.


  Ikiwa mtu atapungukiwa kwa kiasi kingi cha Elektrolaiti hizi kutokana na kuharisha au kwa sababu ya dawa za kukojosha (diuretics), anaweza kuwa mgonjwa sana na itamlazimu kwenda hospitali kupewa elektrolaiti hizi katika mfumo wa dripu (intraveneous fluid, IV), kama vile; maji chumvi (saline solution), maji sukari (dextrose fluid) na madini.


  Siku hizi vinywaji vyetu vingi baridi vinaongezwa kafeina ambayo ni kikojoshi kinachoyalazimisha maji kutoka ndani ya mwili na kutusababishia upungufu wa maji mwilini (dehydration).


  Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, hakuna kinywaji ambacho ni mubadala wa maji.


  Wanasayansi na madaktari bado hawaelewi ni kwa jinsi gani chumvi huyeyuka ndani ya maji au ni kwa vipi iwezavyo kuendelea kuwa na hali ya uchumvi na uchumvi. Wanasayansi na wanakemia wana baadhi za nadharia, lakini bado hawajaweza kuzithibitisha. Bado imebaki kuwa ni fumbo (mystery).


  BAADHI YA KAZI ZINGINE MHIMU ZA CHUMVI MWILINI:

  • Chumvi huyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli. Inarekebisha uwiano sawa wa kiasi cha maji yaliyopo nje ya seli. kuna bahari mbili za maji ndani ya mwili, bahari moja imejishikiza NDANIya seli, na bahari nyingine ya pili imejishikiza NJE ya seli. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa ujazo wa maji uliopo baina ya bahari hizi mbili, na usawa huu unawezeshwa pekee na chumvi, chumvi ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi.
  • Chumvi husaidia kuondoa dalili za mfadhaiko (stress).
  • Figo hazitaweza kufanya kazi zake vizuri bila chumvi.
  • Kukata tamaa na matatizo ya kisaikolojia, vitaondolewa kwa kuchukuwa chumvi zaidi, kula mlo kamili na kufanya mazoezi ya kutembea.
  • Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida yanaweza kurudishwa katika hali yake ya kawaida kwa kuchukuwa kipande cha chumvi na kukiweka mwishoni mwa ulimi na kukifanya kiyeyuke.
  • Mifupa inapata uimara wake toka katika chumvi, na siyo katika kalisiamu pekee.
  • Je wewe ni mwanaume na unashindwa kuhimili kusimama? unahitaji chumvi zaidi na kunywa maji halisi zaidi.
  • Kuichukuwa chumvi na kunywa maji kabla ya mazoezi, kutakusaidia kupumua vizuri na kutokwa na jasho chache.
  • Matatizo ya kibofu cha mkojo na upotevu wa mkojo wa makusudi, vingeweza kurekebishwa kwa kuongeza chumvi zaidi kwenye mlo wako.
  • Dalili za maumivu ya jongo (Gout) zinaweza kuzuiwa kwa kutumia chumvi.
  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia kuvimba kwa mishipa na vena kwenye miguu.
  • Kwa sababu tunapata potasiamu karibu katika kila chakula tunachokula, chumvi inatakiwa kuongezwa katika milo yetu, hii itairuhusu miili yetu kuhimili usawa sahihi wa maji kati ya bahari ya ndani na ile ya nje ya seli.
  • Chumvi ni mhimu ili kuondoa asidi iliyozidi kwenye seli, hasa seli za ubongo.
  • Chumvi ni mhimu kwa ajili ya kusawazisha kiasi cha sukari kwenye damu, hivyo kuzuia ugonjwa wa kisukari.
  • Chumvi ni mhimu katika uzarishaji wa nguvu umeme itokanayo na maji katika seli zote za mwili.
  • Chumvi ni mhimu katika mawasiliano ya neva na ufanikishwaji wa taarifa wakati wote seli za ubongo zinapofanya kazi tangu kuzaliwa hadi kufa.
  • Chumvi ni mhimu katika umeng'enywaji wa chakula na madini kwenye utumbo mdogo (intestinal tract).
  • Chumvi ni mdhibiti madhubuti dhidi ya histamini.
  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia mikakamao ya mishipa (cramps).
  • Chumvi ni mhimu katika kusafisha makohozi na kubana kwa kifua.
  • Chumvi ni mhimu ili kuzuia uzarishaji wa kuzidi wa mate katika kiwango kwamba yanatoka nje ya mdomo wakati umelala, kitendo hiki cha kutoa mate (udenda) wakati umelala ni dalili ya upungufu wa chumvi mwilini.
  • Chumvi ina umhimu mubwa katika uimarishaji wa mifupa. Ugonjwa wa mifupa (osteoporosis) kwa sehemu kubwa, ni matokeo ya upungufu wa chumvi na maji mwilini.
  • Chumvi ni mhimu katika usafishaji wa makohozi mapafuni na maji yaliyogandamana hasa kwa watu wenye pumu, ikiwa inakulazimu kusafisha koo kila wakati, ni dalili kuwa umepungukiwa chumvi.

  CHUMVI KIASI GANI?:

  Dr.Batmanghelidj anashauri; ¾ (robotatu) gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji (16 ounces), au nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji, au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji tunayokunywa. Hiki ni kiasi kizuri kwa kuanzia na siyo kanuni, tafadhari tumia aina ya kijiko kilichotajwa hapo juu kwa vipimo sahihi.


  Ukiona viwiko, vidole au kope za macho zinavimba, usitumie chumvi kwa siku 2, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena.


  NAMNA ZA KULA CHUMVI:


  Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.


  Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.


  Unaweza pia kunywa nusu ya maji unayotaka kunywa, kisha utamung'unya taratibu chumvi mdomoni kama ulavyo pipi, na kisha umalizie nusu ya maji iliyobaki.


  kuichanganya chumvi pamoja na maji ya kunywa si wazo zuri sana.


  Mhimu: Tumesema chumvi ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi sababu ya madini madini mengine zaidi ya 80 yaliyomo ndani yake, lakini hatuwezi kubeza umhimu wa madini joto (iodine) kwa afya ya mwili, ikiwa ni hivyo basi, tunashauri kwa wale ambao hawana vyanzo vingine vya madini hayo ya joto kutumia chumvi zote mbili yaani robo tatu ya matumizi yawe chumvi ambayo haijasafishwa na robo nyingine iwe ile iliyosafishwa ili kuepuka kupungukiwa madini hayo mhimu. Tunasisitiza katika chumvi hiyo iliyosafishwa hakuna kingine kilicho mhimu zaidi ya madini hayo joto ambayo yanaweza kupatikana pia kwa kula vyakula vingi vya baharini (sea foods).


  Mchungaji Stan Moore wa kanisa la Woods of life fellowship la Pembrook Florida nchini Marekani anasema aliuona ukweli kuhusu tiba kwa kutumia maji aliposoma biblia wafalme wa pili 2:19-22.


  Je Chumvi husababisha shinikizo la damu/BP? http://maajabuyamaji.net/maajabu/shinikizo-la-damubp/
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mkuu unatisha bonge la makala kuhusu maji.
   
 8. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #8
  May 29, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Nashukuru mkuu. pamoja
   
 9. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135

  DUNIA YETU, SAYARI YETU

  "Hauumwi, Una kiu. Usiitibu kiu na madawa. Dr F. Batmanghelidj''


  Maisha yetu, dunia yetu.

  Zaidi ya asilimia 70 ya uso wa dunia ni maji. Hata hivyo, zaidi ya asilimia 98 ya maji hayo ni maji chumvi. Asilimia 2 tu ya maji yote ya dunia ni maji safi kwamba tunaweza kunywa, na sehemu kubwa ya maji hayo yamejitega katika barafu.

  Ulivyo si tu ulavyo, bali ulivyo ni nini unakunywa.


  Hii ndiyo sababu kwanini maji ni muhimu sana kwa afya yako.


  Ninatoa tu ufahamu na habari huru katika kukupa urahisi kuelewa kisayansi maelezo juu ya kwa nini majini muhimu kwa ustawi wako.


  Tunaamini kutangaza "maji kwa ajili ya afya, kwa ajili ya uponyaji, kwa ajili ya maisha" ni ujumbe wenye mchango mkubwa sana katika afya ya jamii. Sisi sote tunaweza kubadilisha namna tunavyokunywa maji kwa kunywa; maji safi, na ya asili ambayo ni mazuri kwa afya zetu, mifuko yetu, na mazingira yetu.


  Siyo miujiza hii. Ni akili ya kawaida tu (common sense) kama inavyoungwa mkono na dr. F.Batmaghelidj katika miaka yake mingi ya utafiti na uchunguzi wa namna maji yawezavyo kufanya kazi hiyo vizuri katika kutunza afya zetu na kutufanya kuishi bila maumivu bure. Maji yanaweza pia kumtibu mtu aliyeanguka katika magonjwa.


  Maji ni msingi wa maisha yote ikijumuisha na maisha yako. Misuli yako ambayo ndiyo hukuwezesha kusogea kutoka sehemu moja au nyingine asilimia 75% yake ni maji, damu yako ambayo ndiyo husafirisha viinilishe vyote katika sehemu zote za mwili wako asilimia 94% yake ni maji, mapafu yako ambayo hukuwezesha kutumia oksijeni asilimia 90% yake ni maji; ubongo wako ambao ni kituo kikuu cha udhibiti wa mwili wako asilimia 82% yake ni maji, hata mifupa yako asilimia zaidi ya 27% yake ni maji.


  Afya zetu kusema ukweli zinategemea ubora na kiasi cha maji ambacho sisi hunywa kila siku.


  Dr Batmanghelidj mwasisi wa tiba kwa kutumia maji anasema upungufu sugu wa wa muda mrefu wa kutokujuwa wa kiasi cha maji mwilini (unintentional chronic dehydrationi - UCD) huchangia kuleta maumivu na magonjwa katika miili yetu, magonjwa ambayo mengi yanaweza kuzuiliwa na kutibiwa kwa kuongeza unywaji maji wa mara kwa mara.


  Kama wewe ni mtu unayeipenda afya ya mwili wako, fanya tabia ya kunywa maji ya kutosha ya asili kuwa tabia katika maisha yako. Haitachukuwa muda muda mrefu kwa wewe kuona faida zake.


  Ni uwekezaji wa bure kwa ajili ya afya yako ya muda mrefu.
   
 10. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2013
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Asante mkuu. Maisha ya kisasa yanatuangamiza wenyewe kila kukicha.
   
 11. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #11
  Feb 2, 2013
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Mbaya zaidi watu wanaogopa kuishi maisha ya kizamani mfano kula ugali wa dona badala ya sembe iliyozoeleka sasa kwa kuogopa kuitwa ni washamba. Ni lazima tukubali kuna aina fulani ya maisha ya kale bado yana umhimu mkubwa kwa afya zetu.

   
Loading...