Magonjwa huwa yanaletwa makusudi ili watu wafanye biashara au ni mabadiliko ya binadamu na tabia nchi?

complex31

JF-Expert Member
Jun 15, 2016
379
1,208
Kabla ya kuwapo UKIMWI magonjwa yaliokua yanasumbua ni Degedege Pepopunda na mengine ambayo hivi sasa yote yana Chanjo kama Polio.

Ukimwi ulivyoingia miaka ya 80 ndio ulikua ugonjwa tishio na jamii zetu nyingi hakukua na magonjwa mengine hata Malaria haikuepo sehem zote Tanzania.

Hivi sasa kuna magonjwa mengi yanakuja hayajulikani yametoka wapi au nani ameyaleta. UTI, Typhoid, AMOEBA sijui blood infection na mengine ambayo yamekua sugu kufanya serikali itumie pesa nyingi kuagiza dawa kutoka nje kutibu hayo magaonjwa

Swali langu ni je haya magonjwa huletwa makusudi ili hao wanaotengeneza dawa wapate biashara ya kuuza dawa?

Je, mipaka yetu hatuna maabara na ulinzi wa kisasa kuzuia magonjwa mengine mapya yasiletwe kwetu?

Kama Malaria miaka yote hua tunaagiza dawa kwanini saiv serikali isiweke nguvu kubwa kwenye kupuliza dawa na kuua mazalia ya mbu kama walivofanya Morocco leo hii Malaria ni historia kwao.

Pia tukija kwa wakulima kuna magonjwa ya mimea kama vitunguu kwa mtu alielima Igawa atakua anajua ulikua unaotesha vitunguu mpaka unauza gharama yako ni mbolea na maji ya kunyeshea. Mwaka 2016/7 kama sijakosea kuna ugonjwa ukaja unashambulia kitunguu hakikui hivo unahitaji kuingia gharama nyingine ya Dawa.

Ndugu zangu haya magonjwa magonjwa huwa yanaletwa makusudi ili watu wafanye biashara au ni mabadiliko ya binadamu na tabia nchi?
 
Mtaletewa kila aina ya ugonjwa maana serikali zenu ziko bize kula chips na mishkaki.

Dunia haina huruma. It is for the fittest to survive.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Magonjwa mengi yameletwa na sisi binadamu wenyewe.

Mengine yameletwa kama biological weapon Mf. Ukisoma kitabu kinaitwa "Behold the pale horse" kilichoandikwa na William Cooper kama sikosei, alisema virusi vya HIV vilitengenezwa kwa ajili ya kuathiri zaidi race ya Black na Latin American na vilisambazwa makusudi kwa njia ya chanjo. Anyway, Huyo mwamba (Cooper) alipigwa risasi mchana kweupe kwa sababu ya mambo yake ya kutoa siri za ndani za serikali. May his Soul R.I.P


Magonjwa mengine ni kwa ajili ya biashara tu. Mambo ya Demand & Supply. Unatengeneza tatizo then unakuja na solution unapiga hela. Kama wanavyofanya vijana wa IT, wanatengeneza computer virus/ malwares kama trojan then badae wanakuuzia anti virus kama kaspersky n.k. wanakupiga hela. Mtu anakupa ugonjwa halafu badae anajidai anakusaidia kwa kukuuzia dawa. Ndio dunia ilivyo!!

Magonjwa mengine yanatokana na hali tu ya maisha. Mtoto wa Kibopa hawezi kupata kwashiorkor, ila anaweza kupata obesity. Mambo ya kukosa lishe v/s lishe kuzidi.

Magonjwa mengine yameibuka kutokana na upuuzi wetu tu wenyewe. Kama mtu kufanya mapenzi na mnyama, kuparamia madawa ya kulevya, ulevi wa pombe uliopitiliza n.k

By the way, nimeskia pia COVID-19 imeletwa kwa ajili ya kupunguza population Duniani. Sina uhakika lakini you never know, Dunia ina siri kubwa!!
 
Magonjwa mengi yameletwa na sisi binadamu wenyewe.

Mengine yameletwa kama biological weapon Mf. Ukisoma kitabu kinaitwa "Behold the pale horse" kilichoandikwa na William Cooper kama sikosei, alisema virusi vya HIV vilitengenezwa kwa ajili ya kuondoa race ya black na latino america kwenye uso wa dunia na vilisambazwa makusudi kwa njia ya chanjo. Anyway, Huyo mwamba (Cooper) alipigwa risasi mchana kweupe kwa sababu ya mambo yake ya kutoa siri za ndani za serikali. May his Soul R.I.P


Magonjwa mengine ni kwa ajili ya biashara. Mambo ya Demand & Supply. Unatengeneza uhitaji then unakuja na solution unapiga hela. Kama wanavyofanya vijana wa IT, wanatengeneza computer virus/ malwares kama trojan then badae wanakuuzia anti virus kama kaspersky n.k. wanakupiga hela. Mtu anakupa ugonjwa halafu badae anajidai anakusaidia kwa kukuuzia dawa. Ndio dunia ilivyo!!

Magonjwa mengine yanatokana na hali tu ya maisha. Mtoto wa Kibopa hawezi kupata kwashiorkor, ila anaweza kupata obesity. Mambo ya kukosa lishe v/s lishe kuzidi tumboni.

Magonjwa mengine yameibuka kutokana na upuuzi wetu wenyewe. Kama mtu kufanya mapenzi na wanyamapori, Kutoka maliwato halafu hunawi mikono n.k.

By the way, nimeskia pia corona imeletwa kwa ajili ya kupunguza population Duniani. Sina uhakika lakini you never know, Dunia ina siri kubwa!!
nakubali 100%
 
""Magonjwa mengi yanatokana na Makosa mengi ya binadamu" mayo clinic

Magonjwa mengi yanatokana na Tabia mbaya/dhambi za mwanadamu husika"" mayo clinic

Ugonjwa husababishwa na upungu au ongezeko la mabadiliko ktk mwili wa mwanadamu"

Mfano ukiendekeza zinaa lazma utabahatisha kaugonjwa ata ka1 kazinaa e.g VVU,Gono,Kaswende n.k

Mfano ukiendekeza ulaji holela au kukosa virutubisho flan flan lazma tu utapata kaugonjwa kama vile obesity,,presha na Malnutrition nyngne kama anaemia

Ukiendekeza kutumia simu lazma utapungua uoni wa macho,,Ukizidisha sauti earphone au maeneo ya kelele kwa mda mrefu matatzo ya kusikia yatakupata tu

Ukipenda kula sukari au chumvi au pilipili au chochote kupita kiasi Lazima tu utaambulia kaugonjwa mkuu

Ivyo basi mwili unafanya mambo kwa kukadiria,Ukizidisha-ukipunguza kupita kiasi-Usipozingatia- lazima tu utapata kaugonjwa wala ugonjwa sio 7bu ya connection ili watu wapige pesa bali Ugonjwa ni Madhambi yetu tu

Mayo clinic
 
Its all about business...

Kuna kipindi kimoja kipo CBS reality hua wanaonyesha border control, nchi kama Australia hawaruhusu uingize mmea wowote ule na wako serious sasa hapa kwetu kwanini kusiwe na border control ya vitu kama hivo mfano TMDA wawe na ofisi pale airport ya kupiga marufuku kuingizwa kwa vitu vya hatari nchini kwetu
 
Malaria ikiisha hapa Tanzania kuna watu watafunga maduka yao ya dawa

Mimi naamini Malaria haijatushinda kuitokomeza, miaka zaidi 20 bado tunaimbiwa malaria inaua kwanini Serikali isiwe na mpango mkakati wa kuafanya fumigation na kupunguza kununua madawa nje
 
Back
Top Bottom