Magoma wa CHADEMA ni fisadi, hafai kuwa MWANACHADEMA

makisu

New Member
Nov 26, 2012
3
1
Wanabodi
naomba niwaletee habari ya kada wa Chadema ndugu Magoma, Magoma ndio aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya arusha mjini hadi mwaka jana ambapo alijiuzulu kupinga madiwani wa chadema kufikia muafaka feki kama ambavyo anajisifu kwenye majukwaa ya kisiasa, kwamba amejiuzulu ili kuonesha uwajibikaji katika uongozi, Magoma ndiye alikuwa mpambe mkuu wa Lema kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 alitumia fedha za Makaburu wa kijerumani kufadhili kampeni za Mhe Lema, katika nyanja za kisiasa Magoma si mtu makini hata kigodo, Kwani Magoma amekuwa mtu katili sana hata kwenye uongozi wake Arusha analaumiwa kuendesha Chama kibabe na kwamba ni Dikteta hatari sana ambaye anakingiwa kifua na Freeman Mbowe na Dr Slaa, Magoma amekuwa akilaumiwa kwa kuwapiga makofi viongozi wengine wa Chadema Arusha mjini na amekuwa akipenda kujipambanua kama Hitler au Mwanaume wa mkono wa chuma, asiye ogopa magereza, polisi wala mahakama. mfano Magoma alitaka kuwapiga makofi madiwani waolifikia muafaka wa umeya wa arusha mjini ili Arusha iwe na amani.

Magoma ndio kinara wa fujo na vurugu zote zinazotokea mjini Arusha na ni mtu asiyependa kushauriwa wala kukubali kwamba amekosea, kwanini ninasema kwamba Magoma ni Fisadi,, Magoma amekuwa akimiliki mashamba makubwa ya Katani mkoani Tanga na mashamba ya Ngano Mkoani Manyara, mkoani tanga ana shamba la ukubwa wa hekati 3500, hata hivyo mashamba hayo ameyapata kwa njia siziho halali, kinachonitia uchungu ni kwamba Magoma amewaajiri watu kufanya kazi katika shamba lake la Katani/Mkonge kwa ujira wa shiling 42000 tu kwa mwezi, mbali na hela ndogo anayowalipa amekuwa akiwapiga na kuwatukana kila afikapo shambani na zaidi amekuwa akiwafanyisha kazi bila malipo zaidi ya miezi 9 kwa kizingizio yuko busy sana kwenye harakazi za kumboa nchi.

Amekuwa akivuna katani na kuuza kwa wajeruman ambao huwa yuko nao muda mwingi akija hapa shambani, sasa kama chadema na Magoma wamekuwa wakipigania usawa na kusema CCM ni mafisadi je anachofanya Magoma akiwa kwenye chama cha Chadema sio Ufisadi?? Magoma hafai hata kuwa balozi wa nyumba kumi kwa sababu ni mtu hatari sana kwa taifa hilo, Chadema mfukuzeni huyo fisadi atawaharibia Chama, Magoma alimkufuza mkata katani shambani kwake baada ya mkata katani huyo kugundua Magoma ana uhusiano wa kimapenzi na mke wa mfanyakazi huyo, Mbele ya macho ya jamii anajifanya mtu mstaarabu huku akivaa suti muda mwingi ili atambulike kwamba ni mtu mstaarabu kumbe ni mtu asiyefaa katika jamii, kwanza hizo suti amenunua baada ya kuwarusha wakulima wa katani hela zao, Magoma ni mwizi wa haki za wanyonge na ni fisadi mkubwaa. HAFAI,Chadema mfukuzeni huyo Jambazi wa haki za watu..


Asanteni
 
CHADEMA angalieni hzo tuhuma ni zina uzito mkubwa sana km ni kweli wapambanaji wa ufisadi

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
kama ungekuwa na akili zaidi ya maiti ungezipelekas taarifa hizi plisi kama waliopigwa hawakwenda polisi.acha umbea usiokuwa na msingi.kuanza kujadili personality ya mtu mmoja mmoja wakati kuna mambo mengi magumu ni upuuzi mtupu.kama huna ishu ya maana ya kpost utulie usome za wenzio.
 
hii si mada ya kisiasa ila unaeleza uhasama wako na huyu bwana Magoma!
 
Mmmhh kazi kweli kweli, kama ni kweli. Wenye kufanya msaidieni huyu jamaa
 
Ukweli ni kwamba Derick Magoma amekuwa mwiba mkali wa CCM Arusha mjini, kinachoendelea sasa ni kumchafua Magoma hawa majamaa wa agility Lema ski ukiwa ubunge na hukumu ikabaki Kama ilivyo, CCM wanadhani atakaye simamishwa na Chadema atakuwa Magoma, sasa wameona waanze kumpaka metope ili kumdhoofishwa Magoma, ninauhakika kuwa hizi ni fitna tu.
 
Mbona hapa sijaona Ufisadi?

kumiliki mashamba kihalali si Ufisadi.

Kama anawapunja wafanyakazi wake ni haki yao kudai ujira halali. kabla ya hapo wachunguze kima cha chini cha wafanyakazi mashambani ni kiasi gani ili waona wanapunjwa kiasi gani.

Kama kuna Mfanyakazi au wafanyakazi wananyanyaswa wana haki kulalamika kutumia chama chai cha wafanyakazi Au kufungua mashtaka.

mwana CHADEMA hakatazwi kumiliki mali, kampuni, mashamba, hisa kwenye kampuni au kuwa na utajiri kihalali.
 
Back
Top Bottom