domokaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2010
- 3,545
- 1,719
Katika segment yao ya kupaka rangi katika Morning Magic watangazaji Horace Kawawu, Mkambala na Maria wa MAGIC FM wamemtolea uvivu Rais Magufuli kwa kumwambia asifikirie kama wananchi watafuata sharia wakati yeye mwenyewe amekuwa mstari wa mbele wa kuvunja sheria. Wakatoa mfano wa Rais Magufuli kutoheshimu katiba kwa kuzuia mikutano na shughuli za siasa lakini hawakusema Rais Magufuli kavunja kifungu gani cha katiba.
Wakaendelea kusema kuwa watu wamesomea siasa, wakatoa mfano wa Mrema na Mnyika wa CHADEMA, wakasema wao waliosomea siasa kazi yao ni siasa sasa iweje rais awazuie watu waliosomea fani yao kuitumikia?
Wakazidi kusema kuwa si jambo la ajabu kwa binadamu kukosea, kwani ubinadamu haukamiliki mpaka binadamu awe na mapungufu, inawezekana kabisa rais ana mapungufu, basi hana budi kulifahamu tatizo hilo na ikiwezekana akae chini na wenzake kujadiliana nao au atolee ufafanuzi kauli yake kwani ni wazi kuwa amekosea.
Kuhusu udikteta, wamesema rais Magufuli hajafikia kiwango kikubwa cha udikteta, ni kama vile ndio umeanza anza haupo katika hatua za chini kiasi kwamba kuna hata nafasi ya yeye kukosolewa.
Inawezekana kabisa Magic FM wanasema kweli lakini swali linakuja je wana mamlaka ya kuyazungumza hayo wanayoyazungumza? Wana haki ya kukosoa na kuhukumu pasipo kusema ni kifungukipi cha katiba au kifungu kipi cha sharia kilichovunjwa? Nani amewapa Magic FM wajibu wa kutafsiri sharia na kusema nani kapatia na nani kakosea?
Hata kama ni ukweli lakini huu ndio utaratibu unaovitaka vyombo vya habari kuuwakilisha namna hii tena kuruhusu watu watume ujumbe wao na kuchangia hayo waliyoyaongea? Wachangiaji wengine wametumia lugha kali na mbaya na bado sms zao zikasomwa hewani.
Weledi uko wapi?
Jamani angalau weledi wa fani mlizosomea!