Maghorofa yote marefu yakaguliwe, yatakayoonekana ni hatari yavunjwe kuepusha maafa zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maghorofa yote marefu yakaguliwe, yatakayoonekana ni hatari yavunjwe kuepusha maafa zaidi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chris Lukosi, Mar 29, 2013.

 1. Chris Lukosi

  Chris Lukosi Tanzanite Member

  #1
  Mar 29, 2013
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 4,587
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ndugu zanguni,

  Leo tumepatwa na msiba mkubwa baada ya ghorofa refu kuanguka na kufunika watu.
  Ni dhahir kuwa kuanguka kwa jengo hili kunatokana na makosa ya kiufundi kwani hakuna ripoti inayosema jengo limepigwa bomu.

  Hii inatisha sana, nimekaa nimejiuliza swali moja
  Ikiwa leo hii jengo linaanguka lenyewe , jee kesho likitokea tetemeko la ardhi ni majengo mangapi yatabaki

  Ndugu zangu tusije kuwa tunaishi kwenye time bomb.
  Naiomba serikali ifanyie ukaguzi majengo yote nchini yenye urefu wa zaidi ya ghorofa mbili na jengo lolote litakaloonekana kuwa liko kwenye hatari ya kuporomoka libomolewe kabla halijaua watu

  Mie sijasomea uhandisi lakini najua tuna civil engineers, architectures na quantity surveyors wa kutosha kufanya operesheni hii ili kuepusha majanga mengine kutokea.

  Kila mtu anajua uchakachuaji wa sementi na zana nyingine kwenye uienzi na tabia ya wamiliki wengi wenye majengo marefu kuajiri wajenzi wasio na ujuzi wala uzoefu ili kupunguza gharama za ujenzi wanasahau kuwa wakati wa kuporomoka hata wao wanaweza kuwa ndani ya hayo majengo.

  BORA LAWAMA KULIKO FEDHEHA, MAJENGO HATARI YABOMOLEWE!
   
 2. Blessed

  Blessed JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2013
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 2,456
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Jina la muanzisha Uzi kidogo linirudishe Nyuma....
  Aisee hii ni sahihi
   
 3. Chris Lukosi

  Chris Lukosi Tanzanite Member

  #3
  Mar 29, 2013
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 4,587
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Duh,
  mkuu Kumbe siku Hizi tuna kwenda kiitikadi?
   
 4. bily

  bily JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2013
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 7,738
  Likes Received: 2,712
  Trophy Points: 280
  waanze na wa UVCCM, LILE LA MAMA SALMA PALE KARIAKOO ILA ANGALIZO HAWAWEZI KUFANYA LOLOTE KWA WENYE MAJENGO KWA SABABU WANADAIWA HELA WALIZOKOPA KIPINDI CHA KAMPENI YA JK 2005 kwani vp waziri wa mazingira dr. Teresia alifikia wapi na lile zoezi lake hoteli zinazotiririsha kinyesi baharini vipi GOLDEN TULIP MASAKI,COCO BEACH VP ? JE BEACH ZINGINE SEWAGE SYSTEME IKOJE?
   
 5. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2013
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  sio kwa serikali hii ambayo inashindwa kukutekeleza mambo ambayo yameshaamuliwa...
   
 6. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2013
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,093
  Likes Received: 3,700
  Trophy Points: 280
  Mbele ya rushwa, ripoti itatoka kuwa yote yako kwenye viwango!!!
   
 7. M

  Mfikilwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2013
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 356
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hilo jengo Mey jerry Silaa aliliziia lisiendelee na ujenzi mwaka wa jana mwezi wa 10 kutokana na maelezo yake, sasa ni nani aliwapa ruhusa ya kuendelea na ujenzi, unayoyasema ni ya msingi sana, lakini kwa hapa tanzania tusahau tu, maana kila mtu ana mamraka, wewe mwenyewe ushangai mtoto wa polisi naye anajiona kama polisi, wewe ukiamua hivi anakuja mwingine aliyekuzidi anaamua vingine na si kwa kufuata sheria ni kwasababu ana madaraka zaidi yako, jaribu kushinda kituo cha polisi ata siku moja uone, anakamatwa mtuhumiwa ni simu tu inapigwa unasikia afande amesema tumuachie bila ya kufuata sheria wala nini, bila kufuata sheria hapa tanzania nakwambia tutaendelea tu kuwatafuta wachawi
   
 8. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2013
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,294
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180
  Angalizo hili lilishawahi kutolewa siku za nyuma, lakini viongozi wenzako wa nchi wakapotezea!
   
 9. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2013
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  Tatizo hapa ni corruption na haya yote ndo matunda yake ndugu zangu. kwenye rushwa hasa kama ya kweTu ilipofikia ambayo inataka kuwa ndo utamaduni katika nchi hayo majengo na hata vitu vingine vyote vitatumaliza. na ndiyo maana hata hela yetu haina thamani tena kwa kuwa inazunguka bila kufanya kazi. tegemeeni maumivu zaidi kama watawala hawataingiwa na roho mtakatifu na huyo roho mtakavitu awatoke tena mapema.
   
 10. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #10
  Mar 29, 2013
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,531
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  kuna hili la rizwan hapa karibu na stendi kubwa arusha nalo ni la kuvunjwa!
   
 11. Ablessed

  Ablessed JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2013
  Joined: Mar 19, 2013
  Messages: 4,624
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo ukaguzi ufanywe sasa kwaani hawakuwepo watu wa kufanya hivyo kabla ya ujenzi kuanza, na ulipoanza na unavyoendelea wlikua hawaoni. Yaani waende kuyakagua na kuwaambia wamiliki kua yako chini ya kiwango. Haiingii akilini kabisa mkuu. Mimi naona waliotakiwa kufanya kazi hiyo wachunguzwe kama walitimiza wajibu wao au la. Wakigundulika hawakufanya kazi yao basi wote kuanzia waziri hadi mtu wa mwisho waachie ngazi. Hii ni mara ya pilitokea nakumbuka kipindi cha waziri Mkuu Lowasa kuna jengo lilianguka , Mbona hatua madhubuti zilichukuliwa na ukaguzi wa majengo ulikua unafanyika . Sasa watuambie mchakato ule uliishia wapi. Au waziri alipoondoka aliondoka na watendaji wake.
   
 12. Chris Lukosi

  Chris Lukosi Tanzanite Member

  #12
  Mar 30, 2013
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 4,587
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Suala sio kubishana,
  Waliofanya makosa wanajulikana na wakamtwe , haya ya kukimbilia kwa waziri kujiuzuru kila kukicha sio solution.
  Majanga hutokea kila wakati kinachotakiwa kufanyika ni kukamata waliofanya uzembe uliosababisha maafa
   
 13. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2013
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 860
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  KUJIUZULU KWA MEYA,WAZIRI INGEKUWA SAHIHI,ili wawajibike kisiasa na KUFIKISHWA Mahakamani kwa injinia,architect,mwenye jengo,na contractor ni muhimu.mengine ni ya kiutawala zaidi kama kukagua yaliyokwisha jengwa.naambiwa ya Kariakoo yalikaguliwa lakini majibu yalipotea kama ripoti ya moto wa Shauritanga miaka ya 1994
   
 14. Ablessed

  Ablessed JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2013
  Joined: Mar 19, 2013
  Messages: 4,624
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mkuu huu utaratibu wa kusema majanga yanatokea kila wakati si sawa. Yapo majanga yanayoepukika, haya na hiyo tuite kazi ya Mungu kwa uzembe tu wa wahusika kutofanya kazi yao vema. Kumbuka watu wanapoteza maisha ie hapo roho imekwenda hairudi tena . Lazima tuwe tunakua serious ktk mambo yanayohusu uhai wetu kumbuka leo kwao kesho kwetu. Ni vizuri kuwachukulia hatua madhubuti viongozi wazembe tusiwe na huruma nao hata kidogo. Kufiwa na wako inauma ndugu yangu we acha tu. Kwani waziri sio wajibu wake kuhakiki mambo hayo, kama hahusiki basi sawa. Hebu uwe mwaminifu , je hii issue ya kuporomoka ghorofa ni mara ya kwanza hebu rudi nyuma hukumbuki kuna kipindi kuna ghorofa lilianguka hapohapo mjini sikumbuki upande gani. Pale pia roho zilipotea, sasa jamani tutawalea hawa wahusika hadi lini eeeeh. Hapa sizungumzii vyama mimi sio mwanasiasa.
   
 15. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2013
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Isipokuwa kama wewe ni mgeni Tz, kuna ukaguzi ulifanyika baada ya ghorofa kuporomoka Chang'ombe village...badae jingine likaporomoka Kariakoo......kisha jingine maeneo ya kisutu. kumbukumbu ya haraka hili ghorofa la nne kurudi mavumbini.

  Haya yametokea kati ya 2006 - 2013.

  sasa ndugu sijui unaiomba serikali ipi kukagua majengo haya
   
 16. Ablessed

  Ablessed JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2013
  Joined: Mar 19, 2013
  Messages: 4,624
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hivi ni lini watanzania tutafanya kazi bila rushwa jamani. Kama kuna harufu ya rushwa hatua zichukuliwe , tunaangamia jamani. Rushwa imekua ibada sasa, yaani kuna maeneo ukiwa unaona mbali hautahitaji rushwa.
   
 17. Chris Lukosi

  Chris Lukosi Tanzanite Member

  #17
  Mar 30, 2013
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 4,587
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Naona unachoongelea ni kama vile mie natetea hawa watu,
  Nimesema wahusika wote wakamatwe washitakiwe lakini bado ni kama unataka sentensi yangu isomeke kuwa wasamehemewe? Au una jambo jingine?
  Kesi kama hizi hazihitaji kuumiza kichwa, na watakaokamatwa kila mtu anajua ni nani watakamatwa .
  Kinachotakiwa sasa kufanyika ni kupita jengo moja hadi jingine kukagua yalivyojenga na lolote litakaloonekana kuwa halina kiwango likumbwe na buldozer na pia kuhakikisha watu hawajijengei maghorofa kiholea wanakodi vibarua na mafundi mangungu kupanga matofali badala ya kujenga.
  Kama huna hela ya kujenga kitaalam usijenge ghorofa FULL STOP!
   
 18. Ablessed

  Ablessed JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2013
  Joined: Mar 19, 2013
  Messages: 4,624
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Samahani kama nimekukwaza sina any hidden agenda , I am sorry about that.
   
 19. Chris Lukosi

  Chris Lukosi Tanzanite Member

  #19
  Mar 30, 2013
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 4,587
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hapana hujanikwaza , ila nimegundua hatukuelewana tu,
  Unajua isiwe tabia ya watu walio chini kufanya madudu wakitegemea waziri ndio atakaewajibika kwa madudu waliyoyafanya. Tukiendelea na utamaduni huu watu wa chini ambao ndio watendaji wakuu watakuwa wanaendeleza madudu bila kuogopa.
  Hapa ni kumuomba waziri asionyeshe huruma kwa wahusika wote ambao uzembe wao umesababisha m,aafa
   
 20. t

  tenende JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2013
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Unajua unamwaga pumba saana mkuu!!!!... sehemu nyingi ninaposoma uchangiaji wako nashindwa kuelewa kuwa ni kweli unaelimu angalau ya darasa la SABA!!!!!...
   
Loading...