Maghorofa mjini Dar na ujio wa Magufuli!

leipzig

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
2,766
1,707
Jana tukiwa kijiweni tukitafakari muonekano wa jiji la Dar,ni ukweli mtupu kwa kipindi cha urais wa Mh.Dr. Kikwete tumeshuhudia ujenzi wa Maghorofa ya ukweli ingawa kuna machache yaliyo mabovu na kuhatarisha usalama wa wakazi wa jiji.

Je katika kipindi hiki cha awamu ya 5 tutaendelea kushudia ujenzi huu mkubw kiasi hiki?
 
Je katika kipindi hiki cha awamu ya 5 tutaendelea kushudia ujenzi huu mkubw kiasi hiki?

Labda uulize yale ambayo hayajaisha kweli watafanikiwa kuyamaliza!
Fanya utafiti kuanzia leo! Pesa itakuwa ngumu maana pesa zingine/nyingi za hizo maujenzi ni madili /majipu yanayotumbuliwa sasa !
 
Kama watu wanaibia serikali/umma ndo wanajenga hayo maghorofa hayana maana hata kidogo. Kama ilikua halali yataendelea kujengwa ila kama yalikua yamadili hayatajengwa na wala watanzania tulio wengi hatuyaitaji. Truth will prevail
 
Hata hayo ya mashirika ya umma ukifuatilia ujenzi wake influence kubwa iko kwenye 10% na hata makampuni yanayopewa hizo tenda au subcontracts ni ya wanasiasa hao hao.
Kwa maana hiyo ni kiasi cha kuamua kuwa tujenge uchumi wa namna hiyo ya 'money laundring' au tuangalie kurasimisha shuguli za mtu wa kawaida ili ziwe na tija pamoja mazao ya kilimo ili kupunguza ushiriki wa madalali. Fikiria mkulima wa kyela angelipata sh. 150,000/- kwenye gunia la viazi au mlima korosho mtwara ingekuwa vipi!?
 
Back
Top Bottom