makologoto
Member
- Sep 21, 2013
- 38
- 27
Ndugu yangu Maggid Mjengwa nimeona tangazo lako la uzinduzi wa kitabu unachodai umekiandika au umekitafsiri na kukiita jina la "SIMULIZI ZA MZEE MADIBA". Simulizi hizi kwa asilimia zote umezitohoa au umezidurufu kutoka kitabu cha Mzee Mandela kiitwacho "LONG WALK TO FREEDOM" cha mwaka 1995 kilichochapwa na Kampuni ya Abacus. Lakini katika tangazo lako hujasema kama umepata kibali cha kutafsiri kazi ya marehemu Nelson Mandela kabla hajafa, kutoka kwake mwenyewe, au kutoka kwa wanafamilia ama wachapishaji, au mwenye kushikiria haki miliki (kampuni au mtu binafsi).
Assurance ya haki miliki ni swala muhimu sana kwa sasa ili kulinda kazi za wabunifu, ili kazi zao zisidurufiwe (copied) au kutafsiriwa hovyo hovyo kwa ajili ya kuwanufaisha watu wengine nje ya mbunifu/wabunifu au mwenye haki miliki. Sasa najiuliza hivi mauzo ya kitabu ulichokichapisha cha "Simulizi za mzee Madiba" utawafikishia wanafamilia wa mzee Mandela au unakusudia kufanyia nini mapato yatakayotokana na kazi ya marehemu Nelson Mandela ambayo sasa wewe umetumia uwezo wako wa kuihamisha kwa namna kutoka kiingereza hadi kwenye kiswahili? Nitapenda nipate uwazi wa dukuduku zangu hapo juu ili hata kama nahudhuria uzinduzi wako nakuja kwa moyo mweupe, ili nisije kuendeleza plagiarism au copyright violation!!!