JOHNGERVAS
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 1,011
- 1,681
Tafakuri Jadidi:
Ninapotafakari Alichosema Mzee Warioba?
Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba jana ameongea mbele ya Wahariri wa Vyombo Vya Habari.
Nimemsikiliza kwa makini Mzee Warioba. Huyu ni mmoja wa Viongozi Wastaafu wenye busara na hekima. Ni wenye kuheshimika sana.
Kwetu Wachambuzi, Mzee Warioba ni aina ya Viongozi unayepaswa kumsikiliza kwa kituo, kwa kila tungo inayotoka kinywani mwake. Kila tungo yake yumkini huacha tafsiri pana.
Kwa kumsikiliza, ni dhahiri Mzee Warioba alikuwa na bungo limemkwama kooni kwa muda mrefu. Kwamba alitaka kulitema. Hata hivyo, kuna niliyojiuliza;
Je, Mzee Warioba alilenga kufikisha ujumbe wake kwa Wananchi au Serikali? Au, hilo la mwisho kupitia la kwanza?
Kama ni hilo la mwisho, kwanini Mzee Warioba , kama anavyosema mwenyewe, ni mwenye kuongea na wengi bila mipaka, achague njia hiyo?
Si raia wengi wa Jamhuri ya Muungano wenye kuweza kufunguliwa milango wakati wote kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri, au kupokelewa simu zao wakati wowote wakiwa na jambo kubwa.
Naamini Mzee Warioba ni mmoja wa raia wachache hao wenye nafasi hiyo. Ni kwanini Mzee Warioba alitumia njia ya kwanza kufikisha ujumbe wake kwa Serikali?
Je, njia hiyo itasaidia kuimarisha umoja, upendo, amani na mshikamano wetu?
Maswali?
Na swali la kwanza Kwa Mzee Warioba likatoka kwa Mhariri na mwanahabari mwandamizi Deodatus Balile
Huyu alikuwa na mawili; la idadi ndogo ya wagombea wa upinzani kwenye Serikali za Mitaa na vurugu na vitendo vya mauaji bila kujali ni wafuasi wa vyama gani.
Balile anaulizia lilipo tatizo kama nafasi zilikuwa 64,000 na wapinzani waliweka wagombea 14,000.
Tafsiri yangu:
Inahusu uhaba wa wagombea wa upinzani. Hivyo, je, tudhani pia ni nakisi ya demokrasia?
Je, tudhani pia tatizo la uhaba wa wagombea wa upinzani ni CCM?
Wajibu wa polisi?
Mzee Warioba amewalaumu polisi, na zaidi Serikali kuwaingiza polisi kwenye siasa.
Jambo jema ni kuwa, Mzee Warioba hakusema wala kupendekeza jeshi hilo lifutwe.
Maana, ni kweli Jeshi la Polisi lina mapungufu yake na linahitaji kujengewa uwezo zaidi, lakini, hakuna mbadala wake na nchi ikatulia.
Kama taasisi, polisi ina wachache wasio na uadilifu, lakini, tuna polisi wengi nchi hii wanaojitoa mhanga kwa ajili ya kulinda raia na mali zao.
Ni polisi hao hao, moja ya majukumu yao waliopangiwa, ni kuwalinda viongozi wetu wakiwemo wastaafu.
Mzee Warioba ni mmoja wa wastaafu hao wanaolindwa saa 24 na Jeshi la Polisi. Ni kwa sheria na amri za kijeshi, bila kujali polisi hao ni wapenzi wa vyama gani.
Ni Tafakuri Jadidi.
Maggid Mjengwa.
Pia soma

- Jaji Warioba afunguka kasoro za Uchaguzi Serikali za Mitaa, atahadharisha vyombo vya usalama kujihusisha na Siasa
- LGE2024 - Jaji Warioba: Tusidanganyike kuamini walioenguliwa hawakufuata masharti
- Kuelekea 2025 - Jaji Warioba: Jeshi la Polisi limeingizwa kwenye Siasa, linatoa matamko ya Kisiasa, liachwe lifanye kazi yake
- Kuelekea 2025 - Jaji Warioba: Tusipochukua hatua, uchaguzi mkuu utakuwa kama huu wa Serikali za Mitaa
- LGE2024 - Jaji Warioba: Wapinzani Waliniambia Wangeweza Kupata Ushindi Kwa 25% tu