Mageuzi ya Kisiasa hayawezi kuleta mageuzi ya kimaendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mageuzi ya Kisiasa hayawezi kuleta mageuzi ya kimaendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Apr 9, 2012.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Watanzania baada ya miaka 50 wamechoka na kasi ndogo ya maendeleo ya taifa lao. Ukiachilia mbali matatizo sugu ya afya na elimu, miundo mbinu isiyokidhi haja, kuzidi kuongezeka kwa tofauti ya kipato, kukithiri kwa rushwa na ukosefu wa ajira, utendaji wa serikali na sarakasi za kisiasa zisizo na tija vimeongeza zaidi hamu ya mageuzi ya kisiasa nchini.

  Tukiwa na msukumo mkubwa wa mageuzi ya kisiasa inabidi tujiulize na tufikiri kama haya mageuzi yatatatua matatizo yetu ya kimaendeleo na kiuchumi kwa ujumla. Kwani sisi kama binadamu na jamii tunahitaji kuishi kwa matarajio yaliyo na uhalisi vinginevyo tutapoteza hata nguvu ya kutumaini na kutarajia chochote.

  Sasa mageuzi ya kisiasa hayakwepeki, lakini je ni mageuzi gani ya kiuchumi na kimaendeleo tutachuma/tutavuna kutokana na haya ya kisiasa?

  Serikali ya kimageuzi ikiingia madarakani itarithi mikataba mibovu ya kinyonyaji inayolindwa na sheria za kimataifa ambayo tanzania ni mshiriki, kuna swala la madeni ya nje ya kitaifa, kuna suala la maamuzi ya taasisi za kimataifa za kifedha za nje.

  Kupingana na yote haya ni sawa na kujipiga risasi kwenye mguu. ili kuongeza kipato serikali inahitaji ufanisi wa hali ya juu sekta ya kilimo, sekta ya madini, utalii, na viwanda na biashara (sekta ya mabenki na soko la fedha na bidhaa).

  Kipato cha serikali ni kidogo kuweza kuwekeza kwenye sekta ya kilimo sawa sawa na hivyo kuinua sekta hii iliyo kubwa nchini, hapo hapo tunatakiwa kulipa madeni ili tupate misaada ya hapa na pale ambayo ni sehemu kubwa ya bajeti yetu, tukijinga na soko la dunia ili viwanda vyetu vikue ili tuweze kukusanya kodi na kuongeza kipato na ajira nchini tunapewa adhabu na hawa WB na IMF. Sekta ya biashara (mabenki na soko la bidhaa) haiwezi kukua bila kuongezeka kwa kipato cha taifa yaani cha serikali na wananchi kwa ujumla na kipato cha taifa kinaletwa na uzalishaji kwenye sekta nilizozitaja ambazo zinahitaji mkono mkubwa wa serikali (ambayo itakua imefungwa na mikataba, mahusiano ya kimataifa nk).

  Serikali ya kimageuzi itapata shida hapa na pato la taifa halitaongezeka vile wengi tunavyotarajia. wanamageuzi wataongeza ufanisi wa serikali, watapunguza ufisadi kwa kiwango kikubwa, watapunguza ukubwa na hivyo gharama za serikali, lakini hayo yote yatakua na athari za kawaida sana kwenye ujumla wa pato la taifa na hivyo kero zetu za elimu duni, afya duni, ajira, nk hazitapungua kama tunavyotarajia wengi wetu.

  wanamageuzi angalau wataleta hari mpya, nguvu mpya na hamasa ya kujivunia tanzania yetu tena.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ​Sio lazima Mageuzi ya Kisiasa yalete Mageuzi ya Maendeleo ile, by any means necessary tunahitaji Mageuzi ya Kisiasa kama tunaitaka Nchi yetu na Mali zetu period.
   
 3. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ni kweli lakini Mageuzi ya kisiasa yatasaidia kurekebisha Nguzo moja kubwa ya Umasikini Tanzania "RUSWA". Ruswa ni tatizo la kwanza kabisa Tanzania kuanzia kwenye mikataba, uchaguzi, mishahara, umeme, kodi, uningizaji wa vitu na kama tulivyoona sheria!.   
 4. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,861
  Likes Received: 2,786
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo wewe unashaurije? Mageuzi ya kisiasa hayakwepeki. Unasemaje kama sera za chama kilichopo madarakani zitashindwa kuwakomboa wananchi? Hapo hatuwezidai mageuzi ya kisiasa? Ni lazima tuelewe kuwa siasa na maendeleo ni sawa na kuku na yai. Hivyo kuwa na mageuzi ya kimaendeleo lazima kwanza tuwe na mageuzi ya kisiasa.
   
 5. m

  mharakati JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ninachosema mageuzi ya kimaendeleo kwa maana halisi ni kubadilisha hali iliyopo kabisa kiuchumi na hivyo kuondoa au kupunguza kwa kiasi kikubwa kerso zetu nyingi. lakini kwa hali ilivyo nchini kimfumo, kimazingira na kimuundo uchumi wetu hautapata mageuzi hata kama mageuzi ya kisiasa yakifika na wanamageuzi kujaribu kuleta hayo mageuzi ya kiuchumi. Nafikiri mfano mzuri ni South Africa, mageuzi ya kisiasa yameshindwa kwa kiasi kikubwa kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa wazawa walio wengi kutokana na serikali kushikwa mikono na mikataba mbali mbali na mahusiano ya kimataifa.
   
 6. m

  mharakati JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe Rushwa inarudisha maendeleo kwa kuwanyima fursa sawa wananchi na kuzuia utawala wa sheria..lakini rushwa sijui kama inaongeza pato la taifa moja kwa moja sema tu inalilinda pato lilolopo lisipochezewa na kupotea. Tukizuia rushwa tutaokoa pesa nyingi katika pato lililopo na kuwekeza sehemu nyingine za kimaendeleo.
   
Loading...