Mageuzi ya kisiasa 2010 vijana mpo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mageuzi ya kisiasa 2010 vijana mpo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by houseboy, Jul 10, 2009.

 1. h

  houseboy Member

  #1
  Jul 10, 2009
  Joined: Jul 22, 2007
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani naomba tuanze kampeni rasmi kwa ajiri ya uchaguzi ujao nchini Tanzania bila ya kujali chama.kuna mwamko mkubwa sana duniani kwa kufanya vijana wawe viongozi wa leo.kwa kuanzia ni lazima kuanza kuweka viongozi wapa kabisa kwani viongozi walewale wameshidwa kufanya kazi.Tanzania inakaribia kufikisha miaka 50 tangu tupate uhuru,zaidi ya mashirika na tasisi 500 za taifa zimeuzwa kwa bei ya ubwete kabisa na baada ya kuuza kila kitu hakuna dili tena kwani zamani walikuwa wanapata pesa kutoka kwenye mashirika ya umma na sasa wengi wa viongozi hao baada ya kuuza kila kitu wanafanya ufisadi wa kwa njia ya TENDA,MIKATABA YA ULAGHAI na mambo mengine ya kiufisadi,fisadi.
  Uchaguzi unaokuja ni kuwaondoa viongozi wote tukianzia na wabunge waliokaa madalakani muda zaidi ya miaka 10 kwani wabunge ndio wanakua mawaziri baada ya uchaguzi,tuchague vujana bila ya kujali chama,na slogan yetu iwe VIJANA TAIFA LA LEO NA SI KESHO.Ananteni naomba mniunge mkono kuanzisha rasmi kampeni kabambe ya kuondoa VIGOGO WOTE
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kwanza, Tanganyika na Zanzibar ndiyo zilizo pata uhuru. Labda kama unaongelea muungano.
  Pili, weka wazi nini haswa unataka kifanyika na huo mpango utatekelezwaje? Maana sielewi hizo kampeni unazo ongelea bila kuangalia chama ni zipi maana kila mgombea anatoka chama fulani na kufuata itikadi za chama fulani. Tueleze vizuri.
   
 3. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2009
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Naanza
  Zito kabwe(Kigoma kaskazini) Nape Nauye(kinondoni),Said Kubenea (mafia),Husein Bashe (Nzega) ,Jerry Slaa (UKONGA) ,Amos Makala (Mvomero) ,John Nchimbi (Kigamboni) Sango Kasera (Rorya) ,Dr Emanuel Nchimbi (Songea mjini), Martin Shigela (Kishapu) Denis Msacky (VUNJO), Alima Mdee(kawe) ,John Mnyika (ubungo),Tom Mwangonda(MBEYA mJINI
  Greece Zinazohitajika
  Phielemon Ndesamburo,Dr Mwakyembe ,Ole Sendeka ,Dr SLAA.Samwel SITA ,mama Kilango,
  NB,tunakaribisha majina mengine
   
 4. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii imekaa vizuri sana ila sasa vyama wanavyotoka wengine ndio taabu sasa ndio maana tunatofautiana hapa
   
 5. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Houseboy, kwa uzoefu wangu Vijana ndio wapenda 'dili' wakubwa. Sidhani kwamba ujana ndio kigezo sahihi cha uadilifu. Utatuhakikishaje kwamba vijana wakiingia madarakani hawatachonga 'dili' mpya?

  Maelezo yako ni ya jumla jumla mno. Viongozi unaowazungumzia wa Mashirika ya Umma enzi hizo ni wachache sana ambao wako kwenye uongozi hivi sasa. Kama bado wako hai basi watakuwa na umri wa miaka 70 kwenda juu na wamechoka mbaya maana hata pensheni hawana! "Vigogo" waliopo madarakani wengi ni wapya hata hao Wazee waliouza mashirika ya Umma ukiwauliza watakwambia hawawajui na hawajui viongozi wa sasa wametokea wapi maana hata ndani ya Chama cha CCM hawakuwa na nafasi yoyote ukiacha 'makada' wachache kama Rais Kikwete, Waziri Chiligati na watu kama Mkuchika.

  Kama una nia ya kweli ya kutaka kuigeuza nchi iwe ya neema inayostahili, kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla, anza kampeni ya kufufua 'uadilifu' ndani ya vijana kabla hujawahamasisha kuwapindua 'vigogo' waliopo madarakani.
   
Loading...