Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,369
- 23,526
Kama kuna wakati mageuzi ya kweli yangeweza kutokea chini Tanzania ni katika ile miaka ya mwanzoni 1990 (early nineties). Nakumbuka 'wind of change' ilipoanza kuvuma na kuzikumba nchi za dunia ya tatu na hasa nchi za Afrika. Kwa masikitiko makubwa Tanzania pamoja na kuongoza kwenye hatua za mwanzo, ilipoteza nafasi yake katika kushika hatamu kwenye harakati za mabadiliko. Nani alisababisha kupotea kwa matumaini ya wanamageuzi Tanzania.
Kwa mara ya kwanza kijana wa Kitanzania aliweza kumwita Baba wa Taifa mufilisi kisiasa kama ilivyoripotiwa kwenye gazati la kwanza la binafsi kwa lugha ya Kiingereza "Family Mirror". Huyu Kijana, Mabere Marando, baada ya tamko hilo aliogopwa kama ukoma na alitengwa hata na baadhi ya ndugu zake. Hata hivyo yeye pamoja wanamageuzi wenzake waliweza kuteka mioyo ya wananchi kadhaa na wakisaidiwa na pressure kutoka nje, waliweza kuupiga vita ukiritimba wa CCM na kuushinda.
CCM ilipinga mageuzi kwa kutumia kila mbinu kama hofu, vitisho, ubabe, laghai na rushwa, lakini haikuweza kuzuia mabadiliko. Hata Baba wa Taifa baadaye alikiri kuwa hiyo tsunami ya mabadiliko ilikuwa haizuiliki. Tulishuhudia tena Mabere Marando akikataa uteuzi wa Rais Mwinyi kumwingiza kwenye tume ati ya kutafuna pesa nchi nzima kuwauliza wananchi kama wanaafiki vyama vingi. NCCR-Mageuzi ilizaliwa na chati yake ilianza kupanda kwa kasi iliyokuwa tishio kwa chama tawala, CCM.
CCM, kwa kutambua hatari iliyokuwa inawanyemelea, ilikuja na wazo la kupandikiza watu wake ndani ya NCCR-Mageuzi na wengine kuanzisha vyama lukuki , lengo likiwa kukisambaratisha. Mtu mmoja aliyetumiwa bila kujua anatumiwa alikuwa Augustino Mrema, mpinzani wa Mageuzi aliyekuwa msitari wa mbele kupinga mageuzi hata ikilazimu kutumia dola (FFU). Kashfa ya dhahabu uwanja wa ndege ilikuwa chachu tosha kumdhibiti Mrema na kuhakikisha anaondoka CCM na kundi la wafuasi.
Kitendo cha Mrema kuamua kuingia NCCR-mageuzi badala ya kuanzisha chama chake, kilifurahiwa na CCM kwa kuwa kiliwapunguzia kazi ya kukisambaratisha. Mapungufu ya Mrema yalijulikana hata kwa kipofu na haikuchkua muda mrefu mitafaruku ilianza kuiandama NCCR. Kitendo cha NCCR kumpokea Mrema na kumpa uongozi ndiko kuliua mageuzi ya kweli ya awali Tanzania.
Hivi sasa tuko kwenye mazingira yanayofanana na ya wakati huo. Nchi imedidimia kwenye tope la UFISADI. Kiongozi wetu ameonyesha udhaifu kama ule wa awamu ya pili na mabadilko hayazuiliki tena na ni muda tu. Tunaye kiongozi kiongozi ambaye ameonyesha kutokuogopa kusema bila woga na kuamsha hisia za wananchi wengi.
Je, safari hii tutasubiri tena pandikizi la CCM lije lituongoze katika hizi harakati. Naingiwa woga na watu wanaosubiri CCM ipasuke ndio apatikane Mrema mwingine. Hakuna mwalimu kama historia lakini tusipokuwa makini katika maamuzi HISTORIA INAWEZA IKAJIRUDIA - tusiipe nafasi.