Mageuzi Tanzania Hayawezi Kuletwa na Mtu alie zaliwa Kabla ya Uhuru... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mageuzi Tanzania Hayawezi Kuletwa na Mtu alie zaliwa Kabla ya Uhuru...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dr.Who, Sep 30, 2012.

 1. D

  Dr.Who Senior Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM walikuwa wakisema: vijana ni taifa la kesho, sasahivi msemo huu wameuondoa kwa sababu naamini wameona umuhimu wa vijana ku-speed up maendeleo ya taifa

  Ktk dunia hii ya technologia, mabadiliko ya kasi ya kisiasa na uchumi, naamini kabisa mzee kama Kingunge hawezi kabisa ku-cope na kasi na mabadiliko yanayotokea duniani.

  Mwana siasa aliyezaliwa miaka ya 50 hadi sasa atakuwa na miaka zaidi ya 65, anatakiwa astahafu kazi, kwanza atakuwa amechoka kimwili, akili na piority zake ni za kizamani na atakuwa na fikra mgando na mawazo ya karne ya 19

  Dr. Slaa ni mfano wa wazee waliozaliwa wakati wa ukoloni, zidhani kama anajua kutumia computer, ukimuangalia kwenye mfuko wake wa shati umetuna makaratasi na kalamu kubwa ya Biki, hafahamu kabisa kuwa niwakati wa kutumia Hi-pod, laptop nk....

  Maelezo ya Zito kuwa wazee wa namna hiyo hawawezi kuleta mabadiliko, nilazima yajadiliwe kitaalam bila jazba, ni kwanini bado tuamini kuwa wazee kama kina Slaa na kingunge watatuletea chamaana kuliko vijana kama Mbowe,Zitto nk....??????
   
 2. vena

  vena JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nsha kushtukia wewe umetumwa kutugombanisha wana chadema......ondoka zako
   
 3. m

  mzee wandimu JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 441
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Ndio nini hapa kwenye nyekundu?
  mtajibeba na zito wenu! nakwambaia ZITTO hawezi kuwa raisi wa TZ!
  naona wapambe wake mmekaba mpaka MATE TUKITEMA MNAFUKIA!
   
 4. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja huwezi ukakuta Zitto akizozana na mbowe Manake ni vijana wanaoshabiana na hata Kama upo ni mdogo ukitofautisha na Babu Slaa Kwani kuna mambo mengi ya kimtizamo watatofautiana.Kwangu mimi Mbowe na Zitto ndo roho ya chadema ndo watakaokisaidia hichi chama kusonga mbele.
   
 5. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Huo ni ukweli kabisaa. Maraisi wote wanaotamba hapa duniani wamezaliwa kuwanzia mwaka 1961 kuja juu. Tazama marekani Uingereza , Mexico, senegal na Congo DR. Kweli slaa umri wake umesonga sana na antakiwa ampigie debe kijana wa 1960's. Kabwe ni mzuri sana ila simpendi kwa sababu moja tuu , yeye ni mshabiki mkubwa sana wa ukomunisti.

  Ukomunisti ni siasa za kishetani. kumfanya binadamu mwenzako mtumwa na kumnyima haki za kibinadamu halafu kumfanya awe ana imba kwaya za kumsifia kiongozi aliye madarakani , hata kama anapelekeka watu operesheni vijiji.

  Kikwete ni chaguo letu. Tazama alivyojari maisha ya vijana wake. Karudisha hati miliki na wan bongo flavor wanatanua. Tazaman sinema zinavyowapa vijana ajira. Tazama soka haswa Yanga, Simba na Azam zinavyotoa ajira kwa vija wetu.

  maraisi vijana b ndiyo wajenzi wa nchi na sio wazee ambao wao hukumbushia ya zamani tuu.
   
 6. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  You mean Ipad? Kwa kiasi fulani nakubaliana na wewe kuwa sasa wazee watupishe vijana wao tuchape kazi kwani wakati wao umeshapita na hata wao walianza kuitumikia serikali wakiwa vijana sana tu.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nikufungue kidogo hoja uliyoleta ukiweka Dr. Slaa kama kielelezo:
  1. Kwa taarifa yako Dr. Slaa ndiye amekuwa wa kwanza Tanzania kuagiza big truck for load and unload makontena bandari ya Dar es Salaam wakati akiwa Katibu Mkuu TEC. Ilikuwa ni miaka ya 1980th, hakukuwa hata kampuni au watu binafsi waliothubutu kufanya hivyo. Baadaye makampuni yakabembeleza wauziwe gari ile, ndipo Barala La maaskofu likawauzia.
  2. Kwa mara ya kwanza baraza la Maaskofu Tanzania lilipoanza kuwa na matumizi ya computer ikiwepo ofisi yake kama katibu Mkuu, na taasisi za upashanaji habari ikiwa ni pamoja na:

  • Gazeti la kiongozi kuanza kutumia mfumo wa computer katika idara ya set up
  • TMP (Tanganyika Mission Press) Kipalapala idara ya uchapishaji (printing).
  • TMP Book deparment Tabora mjini) idara ya maduka ya vitabu na usambazaji vitabu
  • TAPRI idara ya tungo za mawasiliano vitabu TEC ambayo.
  Idara hizo zilikuwa na matumizi ya computer na software amazo kwa wakati huo kwa graphic design ilikuwa kitu kigeni bado tanzania ukitilia maanani wakati huo tulikuwa na chuo kimoja tu cha ardhi kule Tabora kabla ya Ardhi Dar haijaanza kukamilika.

  Dr. Slaa atakumbukwa sana kwa makubwa aliyofanya kujenga na kuikuza TEC

  1. Makao makuu ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) tunayoona siku hizi ni matunda ya ubunifu wa Dr. Slaa alipokuwa Katibu Mkuu pale. Jengo la awali ni lile lililo upande wa mbele zinapotumika ofisi siku hizi ambapo yalikuwa madarasa ya shule ya sekondari ya Masisita Tanzania, ambayo baadaye ilihamishiwa Bigwa Morogoro kupisha kiwanja hicho kuwa makao ya Maaskofu Katoliki Tanzania, awali yalikuwa pale ofisi za St. Joseph, Dar es Salaam.
  2. Kaone maendeleo na majengo katika jimbo la Mbulu ni jitihada za Dr. Slaa na Fr. Narda ambao kwa pamoja walifanya makubwa.
  3. Kaangalie jimboni kwake huduma za kijamii ambazo amezifanya, utachoka mwenyewe kiasi ambacho CCM imekimbiwa kabisa huko sababu utendaji wa Slaa huko na CCM ni sawa na kulinganisha mlima na kichuguu.

  Chadema yaimarika baada ya Dr. Slaa kuwa mgombea urasi uchaguzi Mkuu uliopita.

  Siyo siri Chadema hakikuwa na nguvu tunayoona sasa hivi licha ya kuwa na sera nzuri, lakini leo tunaona nguvu ya Chadema inayoogopewa mno na CCM ni kutokana na Chadema katika dakika za majeruhi kuamua kumwangukia Dr. Slaa agombee urasi ambao Samweli Sitta aliingia mitini baada ya makubaliano nao. Tangu hapo Chadema imekuwa na nguvu ya ajabu.

  Je, vijana hao waliokuwemo ndani ya Chadema kabla ya Dr. Slaa kugombea Urais kwa nini hawakuipaisha juu Chadema kama sasa? Baada ya Dr. Slaa kuipaisha Chadema juu sasa tunakuja na kauli mbiu ya kubeza makubwa yaliyofanywa na hawa mnaowaita kizazi cha kabla ya uhuru.

  Ubunifu wa Chadema viongozi wakiwa mojawapo waliozaliwa kabla ya Uhuru Dr Slaa na Kamanda Mbowe:
  • Chadema wakiwemo hao unaoona walizaliwa kabla ya uhuru wamebuni mapya katika shughuli na kampeni za uchaguzi tanzania kuwa zenye mvuo kuanzia mkuktano wa ufunguzi wa kampeni uchaguzi Mkuu uliopita ulifanyika Kidongo Chekundu baada ya Dr. Slaa kushusha makumbora mazitomazito kuituhumu serikali, watendaji wa serikali na CCM, tuhuma ambazo CCM wanazidi kubabaika kuwanyoshea kidole wahusika kisha kuwakumbatia tena hivi karibuni kule Dodoma.
  • Utumiaji wa chopper kufikia maeneo magumu kufikika kwa magari na kurahisisha kazi ya kampeni, CCM wakaiga.
  • Kuwa na magari yanayotumika kama majukwaa ya mikutano badala ya kupoteza gharama na muda kujenga majukwaa yatakayotumika kwa dakika chache.

  Ilani ya Uchaguzi Chadema ndiyo inayotumika na yenye uzito sasa hivi:


  • Fukuto la Katiba mpya linaloendelea sasa nchini ni uzao wa ilani ya Chadema
  • Kikwete kufanya mabadiliko ya barala la mawaziri mara kadhaa ni kutokana na shinikizo la wabunge wa Chadema bungeni.
  • Serikali kubana matumizi ya ziada ili kuokoa pesa za walipa kodi

  Kuna mengi tu wachangiaji wengine watachangia, ni dhana potovu kuwa na fikra za aina hiyo na kuwabeza walioongoza nchi hii hadi kuwa na utulivu wa aina yake. Leo vijana mnaowasema yanayojilia ni amani kusambaratika na mauaji ambayo ilikuwa hadithi za kusimuliwa kutoka nchi nyingine, leo serikali ya CCM inayoongozwa na Rais kijana kuliko Rais mwingine aliyemtangulia imeshwa na aibu kubwa ya kitaifa na kimataifa ya mauaji ya raia wasio na hatia.

  Kuna nchi ambazo ni kielelezo cha vijana ambao mimi ningewaita watoto kukabidhiwa madaraka ya kuongozia nchi na kusababisha maafa makubwa kwa nchi husika kama Liberia, Ujerumani chini ya Hittler, na kinachoendela huko Zaire ya sintofahamu.

  Vijana achaneni na uroho wa madaraka, vema kubaki watumishi na watendaji wazuri serikalini na vyamani kujifunza mbinu za uongozi na kupata uzoefu katika kuongoza nchi.

  Kuongoza nchi hakuna shule wala kitabu cha kusomea au chuo. Hekima na busara ya mtu ndio kielelezo cha fanaka katika kuongoza nchi.

  • Vijana wana papara,
  • wanataka njia ya mkato,
  • pagumu wanataka kulasimisha bila busara
  • mambo yakigeuka magumu ni mabavu hutumika.
   
 8. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Hi pod?
   
 9. f

  filonos JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  HEBU HACHA JAZIBA CHANGIA HOJA KWA PONT..ndio maana NYERERE aliweka mpaka chuo cha SIASA pale kivukoni kwa ajili ya watu aina yako ww.usio jua SIASA NI NINI pole sana
   
 10. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  hata waliozaliwa baada ya uhuru lakini kwenye miaka ya 62 hadi 65 bado hawafai kwa mageuzi
   
 11. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Dah!

  Nyie ndo vijana wa sasa au? maana kama ikulu unakwenda kuonyesha uwezo wa kutumia ipod nimekubali kuwa uelewa wako upo pomoni,what we need from any leader atufikishe kwenye matarajio yetu awe na sifa ya kujua tulikotoka,tulipo na wapi tunataka kwenda,si kutumia ipod!

  Awe mchapakazi asiye zichoka shida za watz na mwenye moyo wa uzalendo kweli kweli na si mtakavitu hatotumia Ipod kwenye hili. Tunataka kiongozi mwenye nia ya kutuongoza kwa dhati na si kutugawa kwa namna yoyote ile iwe ya umri, udini, ukabila, ukanda, usomi, uchekibob wake ama vinginevyo ubaguzi kwake aukatae kwa maneno yake na matendo yake.Awe na sifa ya ubunifu yaani mwenye kutafuta suluhu haraka ktk matatizo ya nchi yetu,n.k

  Obama ni moja wa marais vijana na alikuwa mtumiaji mzuri wa njia za kisasa katika kuwa karibu na fans wake lakini alipoingia ikulu mawasiliano yale yalisitishwa coz si Ipod au BB inayotatua matatizo yetu bali akili yake hasa katika maamuzi.Napenda kukukumbusha kama kijana mwenzangu kuacha uvivu wa kufikiri na vema hasa jitambue.

  Ubaguzi uwe mwiko kwako na wengine wanaofanana wewe ili sote kwa umoja wetu tujenge tz isiyo na ufisadi,isiyo na matabaka kwa kiwango kilichopo na si ubaguzi na tupate maendeleo ya kweli,Tanzania inatuhitaji sisi zaidi kuiboresha na si kwamba kama tutatega Tanzania italeta maendeleo.

  Be good bro!
   
 12. vena

  vena JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siasa bongo....fitna na wiz wa CCM tu hakuna siasa hapo hadi tuwatoe 2015 ndo tuwaonyeshe siasa ni kitu gan
   
Loading...