Mageuzi makubwa kufanyika katika Klabu ya Atletico Madrid ya Uhispania

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
18,913
28,522
21.jpg

Hii ni timu iliyobeba ubingwa wa La Liga 2013/14. Mchezaji pekee aliyesalia mpaka sasa ni Kiungo Koke Resurrecion ambaye ndio atakuwa nahodha rasmi kuanzia July 1.


Kufuatia kuondoka kwa wachezaji kadhaa muhimu wa Atletico Madrid msimu huu sasa ni rasmi wanaingia kwenye kizazi kipya ukizingatia wachezaji wao wakongwe kama nahodha Diego Godin,Felipe Luis na Juanfran ambao mikataba yao imeisha na umri kuwatupa mkono hivyo kuondoka mwezi huu.

Pia staa wao mkuu Griezmann ametangaza kuhama mwezi ujao na kuelekea Barca,PSG au Man utd. Huku Kiungo kisiki Rodrigo Hernandez akitarajiwa kujiunga na Man city kwa dau la €70 Million.

waliosajiliwa msimu huu lakini hawakufua dafu akiwemo Gelson martins na Nikola kalinic wataondoka pia dirisha hili.

Mchezaji mtukutu Diego costa pia anatarajiwa kuondoka kuelekea China baada ya kutofautiana na uongozi wa klabu akiwalaumu kutomtetea alipofungiwa mechi 8 kwa kumtukana refa.

Kwa mabadiliko haya ina maana Atletico madrid italazimika kusajili wachezaji zaidi ya 7 ili kuziba mapengo ya wanaoondoka dirisha hili.

Beki Lucas hernandez alishatimkia Fc bayern toka mwezi march kwa dau la €80 Million hivyo Atletico imebaki na mabeki 3 pekee katika list ya mabeki 8 ilionao!! Yaani Savic,Arias na Gimenez.
images (5).jpg


Mabadiliko (Beki)
Atletico tayari imemsajili beki wa kati kutoka FC porto kuziba pengo la Godin yaani Felipe Kwa €20 Million. Pia inatarajiwa kumsajili Mario Hermoso kutoka Espanyol kuziba pengo la lucas. Huku Alex Telles (Fc porto) na Ben Chilwell (Leicester) ama Alonso wa (chelsea) wakitazamiwa kuziba pengo la beki za kushoto. Pia kati ya Trippier(Spurs),Samedo(Barca) ama Aiden Hysaj( Napoli) anatarajiwa kuziba pengo la Juanfran na Santiago Arias.

Viungo
Kuziba pengo klabu inakaribia kumsajili Hector herrera (Fc porto) anayekuja bure. Pia Kama Rodri ataondoka Marcos Llorente (Real Madrid) ataziba pengo.

Washambuliaji
Dybala ama kinda machachari wa Benfica Joao felix ndio wanatazamiwa kurithi nafasi hiyo ya Griezmann. Pia kama Costa akiondoka pengo linatarajiwa kuzibwa na Edinson Cavani wa PSG.

PS: Atletico itakuwa na uwezo wa kufanya sajili zote hizi maana kabla hata ya kupewa fungu na utawala tayari Simeone atakuwa na takribani €250+ Million kwa mauzo ya wachezaji 3 tu yaani Rodri,Griezmann na Lucas. Na kama Oblak ataelekea PSG basi fungu litafika €370+ Million.

#Aupa Atleti #Los Colchoneros

UPDATE
15609433942447.jpg

Atletico yamsajili kiungo mkabaji Marcos Llorente kutoka Real Madrid kwa thamani ya €40 Million kwa mkataba wa miaka 5. Na amewasili ili kuziba pengo la Rodri Hernandez anayetimkia Man city

UPDATE 2
Atletico Madrid tayari imewasilisha Dau la €126 Million kwa klabu ya Benfica kwa ajili ya kinda mwenye kipaji Joao Felix hivyo inasubiriwa mpaka wiki ijayo atangazwe rasmi katika viunga vya Wanda Metropolitano.
D9XYMxSXoAEwvK8.jpg
 
UPDATE 3
Sasa rasmi kiungo mkabaji Rodri kuondoka Atletico Madrid na kuelekea Man city kwa dau la €70 Million. Hilo limewekwa wazi leo hii baada ya mchezaji mpya Marcos Llorente kukabidhiwa jezi #14 ambayo inavaliwa na Rodri.
15617163229494.jpg
 
I will miss godin mpira siku zote ni ushetani lazima watu wacheke,wanune kocha Simeone na josee morihnyo walifanya mpira uchangamke ,muda wote wamesimama wanaongea kwa madaha yote ndiyo ladha ya mpira inavyotakiwa sisi ambao tulimshuhudia refa Bora kuwahikutokea duniani Mzee CORINA ukisikia UEFA inachezwa lazima uulize je Corina yupo!!maana uwepo wake unafurahi hatareee sasa wewe unayesema timu ya bange umeangalia mechi ngapi ?
 
tores alinusurika kufa hajarudigi??
alishastaafu baada ya fainali ya Europa 2018 ambayo ATL walibeba ndoo!
Hajastaafu rasmi ila amestaafu soka la ushindani maana kwa sasa anachezea timu ya Japan.

Aliondoka Atletico baada ya kutimiza ndoto yake ya kubeba ndoo na hii timu yake ya utotoni. Ila siku ya kuaga aliahidi akistaafu atarudi katika nafasi ya uongozi... Inategemewa ndio atakuja kuwa mrithi wa Simeone.
 
Atletico madrid imewatambulisha rasmi wiki iliopita wachezaji wao wapya Renan Lodi aliyetokea Atletico Paranaense ya Brazil kwa dau la €20 Million pamoja na kiungo wa kati kutoka timu ya Fc Porto Hector Herrera aliyekuja BURE kutokana na mkataba wake kuisha. Wachezaji hawa wanakuja kuziba pengo la kuondoka kwa Felipe Luis na Rodri Hernandez.
D-5k0AoXoAI8Q0v.jpg
D-j9VF7XsAA6cNH.jpg
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom