Mageuzi 10 ndani ya Serikali ya Rais Samia yanayo badili sura ya Tanzania Kimataifa

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
420
220
Historia inaonyesha kuwa orodha ya viongozi mashuhuri Duniani imejawa na watu wanaopenda kufanya mageuzi chanya yenye kuleta mabadiliko. Rais Samia naye ameonyesha kwa vitendo kuwa aina ya kiongozi mwenye kariba hiyo.

Haya ni baadhi ya mageuzi yanayotekelezwa kwa weledi mkubwa;

1. Mageuzi katika utekelezaji wa sera ya mambo ya nje hususani katika kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Mataifa mengine.

2. Mageuzi katika uhuru wa Habari na kujieleza hususani sheria zinazosimamia vyombo vya Habari na mitandao ya kijamii.

3. Mageuzi katika uchumi na sera isiyoipa serikali nafasi ya kuhodhi maamuzi ya kibiashara na kuimarisha mazingira ya kuvutia wawekezaji.
4. Mageuzi katika ustahimilivu wa kisiasa na kuimarisha umoja wa kitaifa kama msingi na tunu za Taifa.

5. Mageuzi katika uwazi na uwajibikaji wa Serikali hususani katika mikopo, madeni na mipango ya muda mrefu yenye kugusa maisha ya wananchi.

6. Mageuzi katika dhana ya ustawi wa maisha ya Mwananchi mmoja mmoja na uhuru kamili wa kiuchumi.

7. Mageuzi katika huduma za Jamii, kuhamasisha ubora na unafuu wa gharama za huduma muhimu kama vile Elimu, Afya, Maji, na Miundombinu.

8. Mageuzi katika teknolojia hususani katika kuhimiza na kuwawezesha vijana kuwa sehemu ya jamii inayonufaika na mapinduzi ya nne ya viwanda (4IR).

9. Mageuzi katika dhana na sera za Kodi hususani katika kuwashirikisha wadau muhimu kwenye maamuzi ya mabadiliko ya Sheria mbalimbali za kodi.

10. Mageuzi ya kiutendaji katika Taasisi za umma. Katika hili tumeona maeneo muhimu kama Jeshi la Polisi yakifanyiwa mabadiliko lakini pia mashirika ya Umma kama vile MSD, TTCL ambayo yanalazimika sasa kujiendesha kisasa na kwa faida.

Haya ni baadhi ya Mageuzi yanayoweza kumfanya Rais Samia Suluhu Hassan hata kuweza kupewa tuzo ya Amani ya Nobel.

Unaweza kuchagua kubisha lakini ukweli unabaki kuwa kama ulivyo. Rais Samia ni mwanamageuzi wa kweli.
 
balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
6,728
11,529
Mkuu umesahau namba ya Simu
Ni muhimu hasa unapoandika thread za mlengo huu
Utakuja kunishukuru kiongozi
Weka bamba yako ya simu
 
Adlo

Member
Jul 15, 2022
28
18
We Ni chawa, unatafuta teuzi, Hamna la maanaa alilofanya,Nchi hii viongoz walioleta mageuzi Ni wawili tu,Mzee mwinyi na Hayat Mh.Mkapa only.
 
Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
420
220
We Ni chawa, unatafuta teuzi, Hamna la maanaa alilofanya,Nchi hii viongoz walioleta mageuzi Ni wawili tu,Mzee mwinyi na Hayat Mh.Mkapa only.
Mama kaleta mageuzi makubwa sana tena katika masuala yanayomlenga direct mwananchi
Lakini kwakua mmeshazoea kupinga kila kitu sishangai
 
NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
4,913
8,598
Mageuzi yasiyoleta mageuzi ya uchumi wa watanzania ni mageuzi mfu yasiyo na Maana kabisa!!

Hali ni mbaya Sana

Ndio màana tunalia na Katiba Mpya

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"
 
Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
420
220
Misukule ya mwendazake haipendi kuona mama akifagiliwa kwa kuupiga mwingi...
Mama anawanyoosha maana kila siku tunaona Tanzania inaendelea hasa katika sekta muhimu za afya, elimu, kilimo
pia ameboresha miundombinu

Fcmn3pAWIAIs0UO.jpg
 
Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
420
220
Mageuzi yasiyoleta mageuzi ya uchumi wa watanzania ni mageuzi mfu yasiyo na Maana kabisa!!

Hali ni mbaya Sana

Ndio màana tunalia na Katiba Mpya

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"
Mama aliahidi kufanyia kazi suala la katiba mpya na kuusu suala la uchumi Tanzania tunaendelea kupanda kiuchumi maana Rais Samia Suluhu amefanikisha kuleta wawekezaji wengi nchini na ametoa fursa nyingi za vijana kujiajiri na kuajiriwa kupitia mikopo ya mashart nafuu inayotolewa na serikali
 
Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,612
2,787
Historia inaonyesha kuwa orodha ya viongozi mashuhuri Duniani imejawa na watu wanaopenda kufanya mageuzi chanya yenye kuleta mabadiliko. Rais Samia naye ameonyesha kwa vitendo kuwa aina ya kiongozi mwenye kariba hiyo.

Haya ni baadhi ya mageuzi yanayotekelezwa kwa weledi mkubwa;

1. Mageuzi katika utekelezaji wa sera ya mambo ya nje hususani katika kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Mataifa mengine.

2. Mageuzi katika uhuru wa Habari na kujieleza hususani sheria zinazosimamia vyombo vya Habari na mitandao ya kijamii.

3. Mageuzi katika uchumi na sera isiyoipa serikali nafasi ya kuhodhi maamuzi ya kibiashara na kuimarisha mazingira ya kuvutia wawekezaji.
4. Mageuzi katika ustahimilivu wa kisiasa na kuimarisha umoja wa kitaifa kama msingi na tunu za Taifa.

5. Mageuzi katika uwazi na uwajibikaji wa Serikali hususani katika mikopo, madeni na mipango ya muda mrefu yenye kugusa maisha ya wananchi.

6. Mageuzi katika dhana ya ustawi wa maisha ya Mwananchi mmoja mmoja na uhuru kamili wa kiuchumi.

7. Mageuzi katika huduma za Jamii, kuhamasisha ubora na unafuu wa gharama za huduma muhimu kama vile Elimu, Afya, Maji, na Miundombinu.

8. Mageuzi katika teknolojia hususani katika kuhimiza na kuwawezesha vijana kuwa sehemu ya jamii inayonufaika na mapinduzi ya nne ya viwanda (4IR).

9. Mageuzi katika dhana na sera za Kodi hususani katika kuwashirikisha wadau muhimu kwenye maamuzi ya mabadiliko ya Sheria mbalimbali za kodi.

10. Mageuzi ya kiutendaji katika Taasisi za umma. Katika hili tumeona maeneo muhimu kama Jeshi la Polisi yakifanyiwa mabadiliko lakini pia mashirika ya Umma kama vile MSD, TTCL ambayo yanalazimika sasa kujiendesha kisasa na kwa faida.

Haya ni baadhi ya Mageuzi yanayoweza kumfanya Rais Samia Suluhu Hassan hata kuweza kupewa tuzo ya Amani ya Nobel.

Unaweza kuchagua kubisha lakini ukweli unabaki kuwa kama ulivyo. Rais Samia ni mwanamageuzi wa kweli.
Mageuzi yoyote huongozwa na mageuzi ya sheria na sera. Nje ya hapo inakuwa ni porojo.

Ni sheria zipi mpaka sasa zimebadilishwa ili tuweze kusema kuwa kuna mageuzi makubwa.

Tofautisha mageuzi na hulka ya mtu. Nitaamini kuwa ni mwanamageuzi baada ya kuona sheria zilizobadilishwa, na zaidi upatikanaji wa katiba mpya.

Sasa hivi kilichopo ni kwamba Rais Samia ana ubinadamu na mheshimu utu kuliko mtangulizi wake, lakini hajagusa kabisa mageuzi ya msingi.
 
NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
4,913
8,598
Mama aliahidi kufanyia kazi suala la katiba mpya na kuusu suala la uchumi Tanzania tunaendelea kupanda kiuchumi maana Rais Samia Suluhu amefanikisha kuleta wawekezaji wengi nchini na ametoa fursa nyingi za vijana kujiajiri na kuajiriwa kupitia mikopo ya mashart nafuu inayotolewa na serikali
Hali ya Maisha ya watanzania kiuchumi yakoje!!
 
Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
420
220
Mageuzi yoyote huongozwa na mageuzi ya sheria na sera. Nje ya hapo inakuwa ni porojo.

Ni sheria zipi mpaka sasa zimebadilishwa ili tuweze kusema kuwa kuna mageuzi makubwa.

Tofautisha mageuzi na hulka ya mtu. Nitaamini kuwa ni mwanamageuzi baada ya kuona sheria zilizobadilishwa, na zaidi upatikanaji wa katiba mpya.

Sasa hivi kilichopo ni kwamba Rais Samia ana ubinadamu na mheshimu utu kuliko mtangulizi wake, lakini hajagusa kabisa mageuzi ya msingi.
Rais Samia Suluhu ni mzalemdo hata kama hajabadilisha sheria lakini anasimamia izo sheria zilizopo na anasimamia haki za nchi na wananchi na kuusu suala la katiba mpya alisema atalifanyia kazi kwaiyo ipo onprocess
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Top Bottom